MAZINGIRA YA BIASHARA KUELEKEA MIAKA 5 IJAYO YA UTAWALA WA RAIS JOHN MAGUFULI JE, UMEJIPANGA VIPI? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MAZINGIRA YA BIASHARA KUELEKEA MIAKA 5 IJAYO YA UTAWALA WA RAIS JOHN MAGUFULI JE, UMEJIPANGA VIPI?

Rais Magufuli akiapishwa awamu yake ya pili







Mazingira ya biashara ni nini?

Mazingira ya biashara ni jumla ya nguvu mbalimbali zinazobadilika muda wote kutoka ndani au nje ya biashara zinazoweza kuiathiri biashara ikashamiri au kudumaa.

 

Mazingira ya biashara ya ndani (Internal business environment)

Mazingira ya ndani ya biashara hujumuisha nguvu au mambo yote yanayohusisha maamuzi ya kila siku ya biashara na ambayo mmiliki au meneja wa biashara anao uwezo wa kuyathibiti kwa mfano; 

·       Bidhaa

·       Wateja

·       Mmiliki wa biashara

·       Uongozi

·       Mtaji

·       Wasambazaji bidhaa(suppliers)

·       Ugavi na mahitaji na

·       Vyombo vya habari

Mazingira yote haya ya ndani ya biashara yanaweza yakathibitiwa na biashara au mmiliki

  

2. Mazingira ya nje ya Biashara (External business environment)

Hizi ni nguvu au mambo ambayo yapo nje ya biashara na huwa hayawezi kuthibitiwa na uongozi wa biashara kirahisi. Kitu pekee uongozi au mmiliki wa biashara unachoweza kukifanya ni kujibadilisha wewe mwenyewe na biashara yako ili kuweza kuendana na mazingira hayo jinsi yanavyotaka huku ukitumia fursa zozote zile zinazoweza kuwepo katika mazingira hayo kwa faida ya biashara yako. Mazingira ya nje ni kama vile mazingira ya; 

·       Kiuchumi

·       Kisiasa na kisheria

·       Kijamii

·       Ushindani

·       Majanga ya asili

·       Kiteknolojia

·       Kidemografia(kitakwimu)

 

MAELEZO YAFUATAYO YENYE RANGI YA BLUU HAYAKUWA SEHEMU YA MAKALA HII TANGU AWALI NILIPOKUWA NAANDIKA HII MAKALA, NIMEYAONGEZEA LEO HII BAADA YA TATIZO LA KUTOFANYA KAZI VIZURI KWA MITANDAO YA KIJAMII KUMALIZIKA

Wakati naandika makala hii siku ya tarehe 1 NOVEMBA 2020 nilipanga kuwa ndio iwe siku ya kuipost katika blog hii lakini ilishindikana kutokana na mtandao wa intaneti kutokufanya kazi vizuri, ilinibidi tu kuituma kwenye listi yangu ya email ya watu ninaowatumia masomo kwani ni email peke yake iliyokuwa inafanya kazi tena kwa kusuasua na kwa bahati nzuri email hiyo ilikuwa tayari nimeshaingia “sign in” kabla ya tatizo la mtandao kuanza. Tatizo hili lilikuwa ni mfano dhahiri wa mazingira ya nje ya biashara (External business environment) niliyoyataja hapo juu katika makala ya awali hasa mazingira yale ya kiteknolojia kwani kama tulivyoshuhudia hakukuwa na mtu hata mmoja aliyeweza kubadilisha kitu kwenye tatizo hili zaidi ya kusubiria tu ni lini mitandao ya kijamii itafanya kazi vizuri.

 

Katika makala hii ya leo ingawa nimeyataja mazingira ya aina zote mbili, ya nje na ya ndani, lakini lengo langu kubwa lilikuwa ni mazingira ya nje ya biashara hasa hasa katika kipengele cha mazingira ya Kisiasa na kisheria.

SOMA: NUFUVI(SWOT ANALYSIS) Tathmini muhimu kabla hujaanza kuandika mchanganuo wa biashara yako

Bila shaka sote tunakumbuka kipindi cha miaka mitano iliyopita jinsi tulivyoshuhudia mabadiliko makubwa na ya haraka katika mazingira mazima ya kisiasa na kisheria ya biashara. Mabadiliko hayo ya kisiasa na kisheria yaliathiri karibu kila biashara iwe ni katika muelekeo chanya ama muelekeo hasi kulingana na vile wamiliki wa biashara hizo walivyoweza kujibadilisha ili kuendana na mazingira hayo ama kinyume chake na hivyo kusababisha kudorora au kushamiri kwa biashara zao.

 

Kubadilika kwa mazingira ya kisiasa na kisheria kulileta pia mabadiliko katika sera mbalimbali za kiuchumi za serikali ambazo zimesababisha kuwepo kwa fursa mbalimbali lakini pia Vikwazo/hatari mbalimbali. Kwa mfano sera ya serikali kuhimiza wafanyabiashara kulipa kodi halali kwa kiasi fulani imesababisha wale waliokuwa wakikwepa kodi kuwa na wakati mgumu wakati huohuo ikiwa ni fursa kwa wale waaminifu wanaolipa kodi zao kihalali kwani ushindani umepungua wa wale waliokuwa wakiibia serikali mapato.

 

Mfano mwingine wa mabadiliko ya mazingira ya biashara kisiasa na kisheria tunaweza kuuona katika suala zima la usajili wa biashara Tanzania, mnamo mwaka 2018 serikali ilianzisha utaratibu mpya wa kusajili biashara Mtandaoni kwa mfumo uitwao, Online Registration System(ORS), mfumo huu ulitamatisha ule wa zamani ambao mtu alitakiwa kwenda hadi ofisi za Brela akiwa na makaratasi yake mkononi.

 SOMA: Fursa za mafanikio kamwe hazitakaa ziishe  lakini pia hazichumwi mtini kama embe

Moja ya fursa kubwa mfumo huu uliokuja nayo kwa wamiliki wa biashara ni urahisi wa kusajili biashara zao na kufanya marekebisho ya nyaraka za usajili hata baada ya usajili wenyewe. Mtu hata uwe kule Kigoma, Kilimanjaro, Ruvuma, Kagera nk. Unao uwezo wa kufanya usajili wa biashara yako ilimradi tu uwe na kompyuta na mtandao wa intaneti

 

Lakini pia kuna vikwazo ama ugumu mabadiliko ya mazingira haya kisheria yaliyokuja nao, moja ni kwamba Mfumo wa ORS unamtaka kila anayetaka kusajili biashara/kampuni au kufanya marekebisho baada ya kusajili basi awe na namba ya Utambulisho wa Utaifa NIN wakiwemo pia wale wanahisa wote wa kampuni. Jambo hili limesababisha kutokuwepo tena na fursa ya mtu kumsajili mwanaye au ndugu yeyote wa karibu mwenye umri chini ya miaka 18.

 SOMA:Hatua zipi nifuate kuanzisha kampuni na ni jinsi gani ya kuiendesha?

Zamani mtu uliweza kuunda kampuni hata na mwanao wa miaka 2 mkiwa kama wakurugenzi. Aidha mfumo huu pia umeziba fursa ya mtu yeyote yule mgeni asiye Mtanzania kusajili jina la biashara au Ubia kwani kigezo cha kusajili majina ya biashara na ubia mtu ni lazima awe na namba ya kitambulisho cha Taifa NIN kitu ambacho wageni hawawezi kuwa nacho.

 

Mabadiliko mengine ni katika sera na taratibu za serikali kwenye sekta ya fedha, kwa mfano hapo zamani kabla ya mabadiliko hayo yaliyokuja kipindi cha awamu ya tano ya serikali, wajasiriamali wengi na wafanyabiashara walikuwa na fursa pana ya kuchukua mikopo wapendavyo.

 SOMA: Mikopo midogomidogo ya biashara: Kabla hujakimbilia kufuga ng'ombe anza angalao na kuku au bata kwanza

Mtu mmoja aliweza kuomba mikopo hata kutoka taasisi tofauti zaidi ya nne bila ya kujulikana  wala kufuatiliwa na mtu yeyote yule lakini sasa hivi serikali kupitia Benki kuu imeanzisha utaratibu wa Taasisi za kifedha hasa Mabenki kuwasilisha taarifa za wakopaji wote kusudi taasisi hizo kabla ya kumkopesha mtu kuchunguza kwanza historia yake ya ukopaji kama ni nzuri au mbaya. Utaratibu huu kwa kiasi Fulani umepunguza mzunguko wa fedha kwani umeminya fursa iliyokuwepo ya watu wasiokuwa waaminifu kupata mikopo kirahisi.

Mabadiliko hayo ya sera na taratibu za serikali kwenye sekta ya fedha pia yalisababisha taasisi mbalimbali za kifedha zilizokuwa zinafanya vizuri hapo kabla kushindwa kumudu mazingira ya biashara na hata nyingine kufikia hatua ya kufilisika na kufunga shughuli zao, kulikuwa na taasisi mfano, PRIDE Tanzania na nyinginezo ambazo zilikuwa chanzo kizuri sana cha mitaji kwa wajasiriamali wadogo kwa masharti nafuu lakini mabadiliko hayo na wamiliki wake pengine kushindwa kwenda sambamba nayo hayakuziacha salama hata kidogo

 SOMA: Elimu ya fedha na umuhimu wake, nkoo tuunganishe nguvu tuhamishe milima

Kwa ujumla kuna mambo mengi sana kutokana na mabadiliko ya Kisiasa na kisheria yameziathiri sana biashara iwe ni katika mlengo chanya au mlengo hasi lakini cha msingi zaidi hapa ni Je, mjasiriamali ni kwa namna gani unazitumia fursa zinazotokana na mabadiliko hayo na kukwepa au kupunguza hatari zilizopo?.

 

Ingawa hatuna uwezo kabisa wa kuzuia sera na kanuni za serikali lakini tunaweza kutumia kila fursa zitokanazo na sera hizo kuhakikisha biashara zetu zinashamiri na siyo kufa. Badala ya kufunga maduka kwa kuhofia kudaiwa kodi na leseni za biashara, tujifunze namna ya kuweka kumbukumbu za biashara zetu vizuri kusudi serikali iweze kukata kodi yake halali na sisi tubakie na faida tunayostahili kuipata.

SOMA: Jinsi ya kutumia maajabu yaliyopunguza corona Tanzania kuubusti uchumi wako unaosambaratika

Watanzania ndani ya miaka 5 iliyopita tumejifunza kwamba serikali hii haipendi wala kuvumilia vitendo vya mkato mkato, kwa hiyo katika awamu hii nyingine inayoanza sasa hivi ni lazima tukitaka biashara zetu kushamiri basi tuhakikishe tunafanya mambo yetu pasipo kuwa na kona kona kwani hakuna namna tunaweza kubadilisha sera na misimamo ya serikali. Serikali inapoweka sheria hizo si kwa lengo la kuwakomoa wananchi wake hapana bali lengo lake ni kuhakikisha kunakuwa na utawala wa sheria unaomlinda kila mtu na kwa maslahi ya kila mwanachi.

 

Serikali ikikubali mambo yajiendee kama kila mtu ambavyo angependa yajiendee matokeo yake ni kuvurugika kwa kila mfumo katika jamii na matokeo yake ni kuwa na Taifa lisilojali taratibu na sheria, jambo ambalo linaweza kuibua madhara makubwa mwisho wa siku. Kila mtu ataamua kujifanyia anavyotaka na mwishowe hata kila mtu kuamua kujianzishia ‘kataifa’ kake ndani ya Taifa. Kwa mantiki hiyo nchi haitakuwa tofauti na Mataifa mengine yaliyofeli kama vile Somalia, Afghanistan, Libya na Syria.

 SOMA: Kati ya Obama na Putin ni nani aliyeisaidia IS

Marekani Taifa  linaloongoza kwa wananchi wake kuishi maisha ya viwango vya hali ya juu zaidi pia ndio Taifa linaloongoza duniani kwa kuzingatia sheria na taratibu za kibiashara. Ingawa kuna nchi nyingine za Ulaya kama  vile Uswizi, Ujerumani, Norway, Sweden na nyinginezo zinazosemekana wananchi wake wanaishi maisha bora zaidi kwa kupata vipato vikubwa kupita Wamarekani lakini ni ukweli usiopingika kuwa katika nchi hizo bei za bidhaa na huduma mbalimbali zipo juu mno kushinda zile za Marekani na matokeo yake ukiwa na dola moja ya Kimarekani Uswizi utanunua vitu vichache zaidi kuliko utakavyonunua nayo ukiwa Marekani kwenyewe.

 

Wamarekani ndio watu wa kwanza duniani kuhakikisha maadili ya biashara na Ujasiriamali yanapewa uzito unaostahili na kwa Wamarekani Biashara ndiyo kigezo kikubwa kinachoamua ubora wa maisha ya watu kwa kutengeneza ajira, bidhaa mbalimbali na huduma katika jamii.

SOMA: Rais Obama: Kila mtu duniani anatakiwa apewe nafasi nyingine ya kurekebisha maisha yake

Ubora wa maisha kwa ujumla unahusiana na furaha ya mwanadamu katika vitu kama vile, viwango vya elimu, makadirio ya umri wa mtu wa kuishi, afya, usafi na muda wa burudani. Hivyo ili kujenga maisha yenye ubora wa hali ya juu ni lazima kuwe na juhudi za pamoja za Wananchi wenyewe, Serikali, Mashirika mbalimbali na wadau wengine wa nje.

 

Kama kinavyoelezea vizuri kabisa kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI toleo jipya maalumu la mwaka 2021, biashara ndio kila kitu. Uwe umeajiriwa ama huna ajira. Ikiwa umeajiriwa kuna siku tu utajikuta unafikiria kufanya biashara kwa namna moja ama nyingine na hivyo utahitaji maarifa ya kufanya biashara kama siyo leo basi kesho.

SOMA; Unajua biashara yenye faida kubwa na ya haraka mara 2 ya mtaji utakaowekeza?

Hebu fikiria baada ya kustaafu kwa mfano, utaniambia.. oo, mimi bwana nitakuwa nimeshawekeza kwenye majumba na viwanja kwahiyo biashara hainihusu kabisa, lakini kumbuka kuwa pia hizo ni aina ya biashara (Real estate business) tena ni aina ya biashara zinazohitaji mtu uwe na weledi mkubwa nazo, tazama mtu kama Donald Trump, hizi ndio biashara zilizomjengea heshima kubwa hata akaukwaa urais wa Marekani.

 

Katika toleo hili la kitabu cha Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali, mbali na mada zote zilizokuwepo katika toleo lililopita vitu vya kipekee vilivyoongezwa ni hivi vifutavyo;

 

  

1. JINSI YA KUANDIKA MPANGO RAHISI WA BIASHARA YAKO KWA MUDA MFUPI (Ndani ya nusu saa tu)

Suala la kuandika mpango wa biashara au kutokuandika limekuwa na mjadala mwingi, wajasiriamali wengi hasa wale wadogo ikiwawia vigumu kuandaa michanganuo ya biashara zao kwenye karatasi.

SOMA: Jinsi mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanikio ya biashara yako

Kwa kuwa haiwezekani mtu yeyote yule chini ya jua kuanzisha biashara bila ya kuwa na mpango wa biashara, wanachofanya wajasiriamali wengi ni kuweka mipango ya biashara zao vichwani hata pasipo wao wenyewe kujua wanafanya hivyo. Kupanga mpango wa biashara kichwani na kuuhifadhi akilini ndio njia ambayo imekuwa ikitumiwa siku zote tokea enzi na enzi, siyo jambo baya kupanga kichwani lakini katika mazingira ya sasa na hasa biashara inapokuwa kubwa mahitaji ya kuandika mpango katika karatasi yanakuwa makubwa zaidi.

 

Hata hivyo kwa mjasiriamali mdogo mdogo kuanza kuandika mchanganuo katika karatasi ni kama vile kupoteza muda wake ambao ni heri angeliutumia kuendesha biashara yake akapata faida chapchap. Kwa kulizingatia hilo, katika toleo hili maalumu la 2021 tumeongeza mada mahsusi inayoelezea namna mjasiriamali mdogo anavyoweza akayaweka mawazo yake yote ya biashara kwenye ukurasa mmoja tu wa karatasi kwa muda mfupi ajabu! Haichukui zaidi ya nusu saa kukamilisha zoezi hilo.

 SOMA: Sababu kuu tano (5) kwanini uandike mpango wa biashara yako kwanza kabla hujaianzisha biashara yenyewe

Njia hii inampa mjasiriamali faida zote za kuandika mpango wa biashara hasa umakini(Focus) wakati huohuo ikimpa muda mwingi zaidi wa kuihudumia biashara yake changa inayohitaji zaidi rasilimali ya muda kama mtaji pekee. Kumbuka mjasiriamali mdogo mtaji wa pesa kwake ni kitu adimu mno hivyo ni lazima ajitahidi kuzitumia ipasavyo rasilimali zingine rahisi kupatikana alizokuwa nazo hasahasa MUDA.

 

Maelezo hayo pamoja na mfano mzima wa mpango huo mfupi yamechukua takriban kurasa 8 kuanzia ukurasa wa 343 – 352 ikiwemo pia nukuu moja ya maneno yenye busara ambayo, acha kusoma kila kitu kinachohusiana na mpango wa biashara kwenye kitabu hiki lakini siyo hii nukuu ya busara yenye aya mbili tu iliyopo uk. Wa 352.

 

 2. JINSI YA KUSAJILI KAMPUNI/BIASHARA KWA KUTUMIA NJIA MPYA YA KISASA MTANDAONI (ORS)

 

Tangu mfumo huu uanzishwe rasmi na serikali chini ya Mamlaka ya leseni na usajili wa biashara BRELA mnamo hapo tarehe1 February 2018 bado kuna watu wengi wameendelea kupata changamoto mbalimbali kwa kutokujua tu vizuri jinsi ya kufanya usajili huo mtandaoni.

SOMA: Kuanzisha kiwanda rahisi cha juisi ya matunda, Tanzania ya viwanda yaja jiandae

Ingawa kuna watu mbalimbali na taasisi wanaotoa huduma hiyo kwa malipo lakini ikumbukwe pia kwamba kuna wajasiriamali wadogo ambao bajeti zao ni finyu, wana ada tu ya kulipia usajili Brela lakini hawana uwezo wa kupata ada ya kulipia huduma hiyo kwa “mawakala” au wawakilishi.

 

Katika maelezo yangu haya mbali na kuelezea Utaratibu wote kama ulivyo kwa lugha rahisi pia tumejaribu kutaja changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wajasiriamali wanaotaka kusajili biashara zao iwe ni majina au Kampuni kwa mfumo mpya na jinsi ya kuzitatua wenyewe bila ya msaada wa mshauri au mwakilishi yeyote.

SOMA: Jinsi ya kuuza wazo lako la biashara au ubunifu kwa wawekezaji na watu wengine  

Brela wenyewe wamejitahidi kuhakikisha taarifa zote za namna ya kusajili biashara zipo katika mtandao wao wa https://www.brela.go.tz/ lakini katika maelezo yetu haya kuna vitu vingine vingi ambayo aidha brela hawakuvifafanua kwa kirefu au hawakuviweka kabisa. Sisi siyo mawakala wa Brela isipokuwa kazi yetu ni kuhakikisha msomaji anapata taarifa kwa ajili ya kufanya maamuzi sahihi. 

 

Maelezo yetu haya ya kipekee usiyoweza kuyapata mahali kwingine kokote yanalenga hasa kumsaidia mjasiriamali asiyekuwa na bajeti ya kutosha ya kumlipa mshauri kumsaidia katika mchakato huu, kwa walio na bajeti zao napendekeza maelezo haya hayawahusu kwani kumlipa mshauri ni njia fupi na ya haraka zaidi.

SOMA: Nataka kufungua duka la rejareja la mahitaji ya kila siku katika jamii, ni mbinu gani naweza kuitumia ili kufanikisha?

Aidha pia maelezo haya yamelenga kuwasaidia wale wajasiriamali ambao mchakato wa kufanya jambo lao muhimu kama hili la kusajili biashara zao za kwanza kabisa, kama tu lilivyokuwa tukio la kuoa mke, mume au kupata mchumba linakuwa ni la kwao binafsi pasipo kuwashirikisha watu wengine wa pembeni. Maelezo ya mchakato mzima pamoja na mawaidha mbalimbali yamechukua takriban kurasa 7 yameanzia ukurasa wa 354 – 362.

 

Ikiwa unayo shauku ya kujua vyema jinsi ya kusajili biashara yako kwa njia ya kisasa mtandaoni ORS basi unaweza kujipatia nakala yako ya kitabu hiki na moja kwa moja ukafungua ukurasa huo uliotajwa tu hata kama huna shida na mambo mengine yaliyoko ndani ya kitabu. Maelezo ni mafupi na yaliyolenga zaidi utatuzi wa changamoto zile zinazowasumbua zaidi wajasiriamali katika mchakato huu wa kusajili kampuni na majina ya biashara mtandaoni.

 

Toleo hili jipya maalumu (New Special Edition) ingawa litatoka rasmi hapo January 2021 lakini kwa sasa hivi lipo tayari na kwa wale wateja watakaowahi kabla ya muda huo wataweza kukipata kwa njia ya nakala tete(Softcopy).

 

Tumetoa pia OFFA ya wiki moja kuanzia leo Jumapili tarehe 1/11/2020 mpaka Jumamosi tarehe 7/11/2020 (Kutokana na tatizo la mtandao tumeongeza tena wiki moja mpaka tarehe 14/11/2021) kwa kila atakayenunua kitabu hiki kupewa vitabu na michanganuo ya biashara ifuatayo pale chini, pia kuunganishwa na Group la Whatsap la MICHANGANUO-ONLINE kwa muda wa miezi 3. Group hili linaendesha masomo ya kila siku ya fedha na Ujasiriamali pamoja na semina za mara kwa mara kuhusiana na Uandishi wa Michanganuo ya biashara zinazolipa.

 

OFFA HIYO YA WIKI MOJA NI HII HAPA CHINI;

1.  KITABU cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI (New special edition 2021) –kwa kiswahili

 

2.  KITABU mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.-kwa kiingereza

 

3.  Semina ya siku 7 na mpango kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –unga wa dona(USADO Milling))-kwakiswahili

 

4.  Kifurushicha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS) kuku wamayai, kuku wanyamana kuku wakienyeji-zote kwa kiswahili

 

5.  Mchanganuo kamili wa kilimo cha Matikitimaji (KIBADA WATERMELON BUSINESS PLAN)-kwa kiswahili

 

6.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) –kwa Kiswahili & kiingereza

 

7.  Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili

 

8.  Mchanganuo kamili wa BiasharayaChipsi (AMANI CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili

 

9.  Somomaalumu la Mzunguko chanya wa fedha kwako binafsi na kwabiashara yako-kwa kiswahili

 

10.              Vielezo(Templates)zamichanganuo ya biashara vinayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. Kwa Kiswahili & kiingereza

 

 

11.              Mchanganuo mfupi wa biashara ya Steshenari(One page Business plan) (NEEMA STESHENARY) -kwa Kiswahili

 

12.              Vipengele / (Outlines) vya Mpango wowote ule wa Biashara kwa kiswahili na kwakiingereza. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika business plan unaweza kuvifuatisha ukaandika.

 

13.              Kuungwa group la Michanganuo la mentorship miezi 3 (michanganuo-online) unaweza kuuliza swali lolote lile muda wowote kuhusu michanganuo na ujasiramali kwaujumla

Siku za nyuma tumekuwa tukitoa offa kama hii ingawa kila offa huja na vitu tofauti na nyingine, na kwa wale waliokuwa wakitufuatilia ni mashahidi, huwa tunaposema ni ya wiki moja ni ya wiki moja kweli hatutanii, na ikishapita imepita hakuna tena namna unaweza kuja kuipata labda ije nyingine ambayo itakuwa na vitu vingine tofauti.

 

Kupata toleo hili jipya la kitabu cha MICHANGANUO NA UJASIRIAMALI-new special edition pamoja na OFFA zake zote 12, lipia sh. Elfu 10 tu kwa namba zetu, 0765553030  au  0712202244 jina ni Peter AugustinoTarimo

 

Kisha tuma ujumbe wa Watsap au Sms ya kawaida usemao, “NITUMIE OFFA YA MWISHO 2020 YA VITU 12” Ukihitaji na group la mentoship basi ongeza “…NA GROUP LA MICHANGANUO” kwenye ujumbe wako. Unaweza pia kutuma kwa Telegram namba ni 0765553030

 

Ikiwa hutumii watsap wala telegram usijali, unaweza kututumia anuani yako ya email kwani masomo, vitabu na michanganuo vyote tunatuma pia kwa njia ya email. Vilevile kwa kipindi hiki mitandao ya kijamii ipo chini sana, watsap haifanyi kazi maeneo mengi hivyo email inaweza kufaa zaidi. Wahi offa hii kabla wiki haijakwisha. ASANTE SANA.

 

HATA HIVYO OFFA HII ITAONGEZEWA TENA WIKI MOJA MPAKA JUMAMOSI IJAYO YA TAREHE 14/11/2020 KUTOKANA NA SABABU KUBWA KWAMBA TAARIFA HII HAIKUWEZA KUWAFIKIA WATU WENGI SHAURI YA TATIZO LA KITEKNOLOJIA LA MTANDAO WA INTANETI LILILOSABABISHA PIA MITANDAO YA KIJAMII NCHINI TANZANIA KUWA CHINI MNO KIASI CHA KUTOKUFUNGUKA KWA URAHISI 

0 Response to "MAZINGIRA YA BIASHARA KUELEKEA MIAKA 5 IJAYO YA UTAWALA WA RAIS JOHN MAGUFULI JE, UMEJIPANGA VIPI?"

Post a Comment