Sehemu ya 2 tutaandika hatua kwa hatua Sura au vipengele vikubwa viwili ambavyo ni; “Maelezo ya Bidhaa” na “Tathmini ya Soko”
Lakini kabla ya kuanza
sehemu hii naomba turudi sehemu ya kwanza kuna vitu au mambo matatu (3)
hautukuyaelezea vyakutosha ambayo ni muhimu kabla ya kusonga mbele zaidi, mambo
hayo ni;
1)
Orodha ya vipengele vyote vinavyounda
mpango wa biashara
2)
Vipengele vidogo muhimu 4 , Dhamira kuu,
Maono, Malengo na Siri za mafanikio
3)
Jedwali la Mahitaji na chanzo cha fedha
za mahitaji
Vyote hivi ni vitu tulipaswa
kuvijadili kwa kina kwenye sehemu yetu ile ya kwanza
Wakati tunaanza nilisema
kwamba baada tu ya kazi ya kufanya utafiti kukamilika sasa unaanza kuandika vipengele
vya mchanganuo wako kimoja baada ya kingine kisha nikasema tuanze na kipengele
kikubwa cha kwanza ambacho ni Muhtasari ambao tutauandika mwishoni
1. Sasa nataka kabla ya
kuanza kuchanganua vipengele niweke hapa chini mlolongo wa vipengele vyote vinavyounda
mchanganuo mzima kisha mtu unafahamu kabisa ni kipengele kipi tunaanza nacho na
kipi kitafuata kulingana na jinsi nilivyoandika.
Na huu ndio mlolongo wetu wa
vipengele vyote 9. Kwanini 9 na siyo 8? Hamna fomula maalumu, kwa mfano mimi
hapa nimeweka na kipengele cha UENDESHAJI ambacho mara nyingi watu hukiacha
kama biashara haihusishi uendeshaji. Ni biashara chache zenye shghuli za
uendeshaji mfano kiwanda au makampuni makubwa.
1.0
MUHTASARI TENDAJI
2.0
MAELEZO YA KAMPUNI / BIASHARA
2.1
Malengo
2.2
Dhamira kuu
2.3
Siri za mafanikio
2.4
Umiliki wa Biashara
2.5
Kianzio (kwa biashara mpya au historia kwa kampuni iliyokwishaanza)
2.6
Eneo la biashara na vitu vilivyopo
3.0
BIDHAA au HUDUMA
3.1
Maelezo ya bidhaa/huduma
3.2
Utofauti wa bidhaa/huduma na za washindani
3.3
Vyanzo vya malighafi/bidhaa
3.4
Kopi za matangazo
3.5
Teknolojia
3.6
Bidhaa au Huduma za baadae
4.0
TATHMINI YA SOKO
4.1
Mgawanyo wa soko
4.2
Soko lengwa
4.2.1
Mahitaji ya soko
4.2.2
Mwelekeo wa soko
4.2.3
Ukuaji wa soko
4.3
Tathmini ya sekta
4.3.1
Washiriki katika sekta
4.3.2
Usambazaji 4.3.3 Ushindani
4.3.4
Washindani wako wakubwa
5.0
MIKAKATI NA UTEKELEZAJI
5.1
Nguvu za kiushindani
5.2
Mkakati wa soko
5.2.1Kauli
ya kujipanga katika soko
5.2.2
Mkakati wa bei
5.2.3
Mkakati wa matangazo/promosheni
5.2.4
Programu za masoko
5.3
Mkakati wa mauzo
5.3.1
Makisio ya mauzo
5.3.2
Programu za mauzo
5.4
Mkakati wa ushirikiano
5.5
Vitendo na utekelezaji
6.0
UENDESHAJI
7.0
MAELEZO YA UONGOZI NA WAFANYAKAZI
6.1
Mfumo wa uongozi
6.2
Timu ya uongozi na wafanyakazi
6.3
Mpango wa mishahara
8.0
MPANGO WA FEDHA
7.1
Dhana/makisio muhimu
7.2
Tathmini ya mauzo ya kurudisha gharama (Break Even Analysis)
7.3
Makisio ya faida na hasara
7.4
Makisio ya mtiririko wa fedha
7.5
Makisio ya mali na madeni (mizania ya biashara)
7.6
Sehemu muhimu za biashara
9.0
VIELELEZO/VIAMBATANISHO
•
Taarifa za mahesabu ya fedha kwa undani
•
Mahesabu yako ya nyuma
•
Leseni, vibali ripoti za kodi, hatimiliki na alama za
biashara
•
Mikataba mbalimbali
•
Orodha ya mali na vifaa mbalimbali(Dhamana)
• CV
za viongozi na wafanyakazi muhimu
•
Kopi za matangazo ya biashara.
*Kumbuka utakapokuwa
ukiandika mpango wa biashara yeyote ile ni vizuri sana ukawa na hii listi ya
vipengele mezani kwako.
2.
Kitu cha pili nilichosema hatukukielezea ni vipengele
vidogo 3 vya mwanzo vya sura ya Kampuni/Biashara unavyoona kwenye orodha yetu
ambavyo ni; Malengo, Dhamira kuu, Maono
na Siri za mafanikio
Haya maneno 3 ya msingi kuna watu wengine huyaweka punde
tu chini ya Muhtasari na wengine huyajumuisha kwenye Sura ya Maelezo ya kampuni
kama uonavyo hapo juu
Katika mchanganuo wetu huu wa Chamazi milling niliviweka
chini ya Muhtasari na siyo kwenye maelezo ya Biashara. Lakini haijalishi popote
pale unapoviweka ni sawa tu kati ya hizo sehemu mbili.
Nitaanza kueleza nilivyoandika hivi vipengele vidogo 3
kama ifuatavyo;
Dhamira
kuu
au wengine huita Dhima, kwa kimombo Mission Statement: Maana yake ni unaandika lile lengo hasa biashara
yako inataka kulitimiza katika mtazamo mpana.
Mara nyingi watu huelezea kile kitu biashara
inachokifanya lakini Mission yako pia itategemea biashara inalenga soko gani au
ni faida zipi inatoa kwa mteja.
Kwa mfano hata dhamira nyingine hueleza malengo ya ndani
mfano kuwajali wafanyakazi nk.
Dhamira yako unapoelezea ni biashara gani unafanya jaribu
kutoa maelezo yanayojitosheleza usiminye baadhi ya shughuli zako mfano badala
ya kusema ‘dhamira yetu ni kuuza simu za
mkononi’, sema dhamira yetu ni ‘kutoa
huduma bora za mawasiliano’ , maana utakuwa unaondoa uwezekano wa kufanya
mambo mengine yahusuyo simu za mkononi mfano kuuza vocha, vifurushi na
accessories nyingine za simu za mkononi.
Pia usiseme dhamira yetu ni kutoa huduma ya usafiri wa
daladala, sema ni kutoa huduma za usafirishaji maana hujui ni lini utakuja
kununua na malori kwa ajili ya kwenda mikoani.
Kwenye Dhamira kuu ya Chamazi maize milling nilizingatia
zaidi fursa kubwa ya soko lililopo katika kata tunazozilenga kwa hiyo hii ikawa
ndiyo mission yetu kubwa itakayopelekea hatimaye kutimiza malengo yetu mengine
madogomadogo mfano kupata faida, kukua kwa biashara yetu, kuongeza biashara nk.
Niliandika hivi dhamira yetu kuu;
........................................................................................................................................................................................................................................
Maono/
Vision:
Unaeleza kile unachoota biashara yako kuwa baada ya muda
fulani kupita huko mbele, unatamani biashara yako ije iwe vipi miaka 2, 3, 5 na
kuendelea?
Sisi kwenye Chamazi Milling tuliandika hivi;-
...............................................................................................................................................
Malengo
/ Objectives
Haya ni malengo au vitu biashara imepanga kufikia au
kukamilisha, ni lazima yawe halisi yapimike, na yawe na muda maalumu wa
utekelezaji. Mfano yanaweza kuwa kiwango cha mauzo, faida, ukuaji wa soko nk.
Malengo yetu Chamazi kwa miaka 3 ni haya yafatayo;
· Ku...................................................................................................................................................................
· Ku................................................................................
· Kufikisha ....................................................................
· Kuunga ..........................................................................
Siri
za Mafanikio
Unataja mambo ambayo ni kipaumbele kwa kampuni katika
kutimiza malengo yake
Hata hivyo kwenye mchanganuo wetu huu hatukuwa na siri za
mafanikio. Lakini tungeliweza kutaja kwa mfano hata eneo la kimkakati linalokua
kwa kasi, Uzoefu wa muda mrefu wa wamiliki kwenye sekta ya mazao ya nafaka nk.
3. Kitu cha tatu nimesema tutarudia kukielezea ni lile
jedwali la namba za kuanzia kwenye kipengele kidogo cha “Kianzio”
Kimsingi jedwali la kwanza lina mahitaji ya aina tatu
ambayo ni;
· Gharama
za awali
· Rasilimali
za muda mfupi
· Rasilimali
za kudumu
Gharama za awali (Start
up expenses), niliorodhesha zile gharama ambazo........................................................................
...........................................................................................................................................................................................................
Rasilimali za muda mfupi (Short term assets) ni .........................................................................................................................................................................................................
Rasilimali za kudumu (long
term assets) Ni vifaa na mashine zote za kudumu mwaka mmoja na zaidi
unazonunua.....................................................................................................................................................................................
Jumla ya vitu vyote 3 ukijumlisha unapata mahitaji yote
kwa ajili ya kuanzisha biashara hii ambayo ni sh. milioni 29 lakini tunahesabu
zile gharama za awali sh. milioni 4 hupotea na hivyo jumla ya Rasilimali au
assets zitabakia kuwa sh. milioni 25 tu
Jedwali la Chanzo cha fedha za mahitaji nalo lina
vipengele 2, juu kuna Deni au mikopo na chini kuna Mtaji wa wawekezaji.
Jumla ya deni na Mtaji wa wawekezaji (0 +29,000,000
-4,000,000) = hulingana na jumla ya Rasilimali tulizopata kwenye jedwali la
mahitaji ya kuanzia( 11,000,000 + 14,000,000) sawa na 25,000,000
Na jumla ya mahitaji yote (4,000,000 + 11,000,000
+14,000,000 ) ni lazima yalingane na jumla ya vyanzo vyote vya fedha(29,000,000
+ 0) sawa na milioni 29
NB:Zingatia kanuni ZifuataZo;-
Mahitaji = Gharama za awali + Rasilimali za muda mfupi
+ Rasilimali ma mda mrefu
Vyanzo
vya fedha = Mtaji wa wawekezaji + Deni(mikopo)
Mtaji
jumla = Mtaji uliowekezwa – Gharama za awali zilizopotea
Baada ya kukamilisha vipengele vyote vidogo vinavyounda
sura yetu ya kwanza ya Maelezo ya Kampuni /Biashara, sasa tunachagua sentensi
muhimu kuunda muhtasari mdogo wa sura hii ambao huwekwa mwanzoni mwa sura
yenyewe na kisha kuja kuunganishwa na mihutasari mingine kuunda Muhtasari
Tendaji wa mchanganuo mzima.
Mpaka
kufikia hapo tumemaliza “Kiporo chetu” cha Sehemu ya kwanza ya mafunzo haya
labda ikiwa kama kuna swali lolote unaweza ukauliza nitakujibu. Sasa tuingie
rasmi sehemu ya pili.
SEHEMU
YA 2
· MAELEZO YA BIDHAA
· TATHMINI YA SOKO
3.0
MAELEZO YA BIDHAA
Katika mlolongo wetu wa vipengele/sura zinazounda mpango
wa biashara hii ni sura ya tatu na inaundwa pia na vipengele vidogo vifuatavyo .........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
Maelezo haya nakuwa
nimeyafahamu kupitia utafiti nilioufanya kabla ya kuandika mchanganuo huu kwani
kila kitu nilikuwa nimeshachunguza na hapa ilibaki kuandika tu. Kwa mfano....................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
Unaweza kusoma sura yako nzima kwenye mchanganuo kamili
wa Biashara hii niliokupatia na mifano mingine kwenye michanganuo mbalimbali
pia niliyokupa.
4.
TATHMINI YA SOKO
Katika sehemu hii ya pili tunajifunza pia jinsi
nilivyoandika Kipengele/Sura ya 4 ya mchanganuo huu wa Chamazi White Maize
Milling
Sura hii ni kubwa hivyo lazima ianze na muhtasari mdogo
ambao lakini huandikwa mwisho. Kumbuka pia Tathmini ya soko ndio kipengele
kinachotumia zaidi taarifa za utafiti tuliofanya kuliko vingine vyote. ..............................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
4.1
Mgawanyo wa soko
Baada ya kuacha nafasi ya kuja kuandika muhtasari mfupi
wa sura nilianza moja kwa moja kipengele hiki kidogo kwa kueleza eneo la soko
letu lengwa kuwa ni............................................. ................................................................................................................................................................................................................,
unaweza kuzisoma kwenye mchanganuo wako.
Kisha nikaonyesha jinsi nilivyogawanya soko hilo katika
makundi makuu mawili nikitumia kigezo cha ..........................................................................................................................................................................................................
4.2
Soko lengwa
Katika hayo makundi mawili nikachagua soko muhimu zaidi
kwetu kuwa ni ..............................................................................................................................................................................................................................................................................................................
4.2.1
Mahitaji ya soko
Kwa kutumia Takwimu mbalimbali nilizopata kwenye utafiti
nilioufanya nilionyesha mahitaji ya soko la unga wa mahindi kuwa yapo na hivyo
biashara hii inaweza kuleta faida.
Nilionyesha idadi ya watu ipo ya kutosha na namna watu
wengi wanavyotumia unga wa mahindi (sembe na dona). Soma takwimu hizo kwenye
mchanganuo wako na jinsi nilivyoeleza
4.2.2
Mwelekeo wa soko
Hapa nilieleza muelekeo wa soko la unga wa mahindi
nikizingatia mazingira mbalimbali kama vile mazingira ya kisiasa, hali ya hewa
na ulaji wa watu
4.2.3
Ukuaji wa soko
Hapa pia kwa kutumia takwimu mbalimbali za utafiti
nilionyesha soko la unga wa mahindi Temeke na Tanzania kwa ujumla linakua
namnagani
4.3
Tathmini ya sekta
Hapa nilianza na muhtasari mfupi wa kipengele hiki kidogo
kwa kuelezea sekta biashara hii ilipo ya usagishaji nafaka kwani ni kipengele
kidogo kinajitegemea mbali na soko lenyewe. Nilieleza historia yake kwa ufupi
tangia Uhuru pamoja na mabadiliko makubwa yaliyoikuta kipindi hicho chote
4.3.3
Ushindani
Kisha niliingia moja kwa moja kueleza ushindani ulivyo
kwenye hii sekta, halafu chini yake nikataja washindani wetu wakubwa wawili na
sifa zao, nguvu na udhaifu waliokuwa nao nikilinganisha na sisi Chamazi White
Maize Milling.
Fuatilia vizuri mchanganuo wako maelezo yanajitosheleza
hayana ugumu wowote ule kueleweka
Baada ya kumaliza vipengele vyote vidogo vya Sura hii ya
Soko sasa...................................................................................
....................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
Tumehitimisha
Sehemu ya pili ya Mafunzo yetu haya ya kuandika kwa vitendo Mchanganuo wa
Biashara ya Usagishaji nafaka ambapo tuliandika sura 2, ya maelezo ya Bidhaa na
Tathmini ya Soko.Tukutane sehemu ya tatu.
Semina
hii hapa katika blogu ya jifunzeujasiriamali tumeweka dondoo chache tu,
ukihitaji semina nzima iliyokamilika jiunge na mafunzo haya pamoja na kupata
mchanganuo wako kamili wa Chamazi white maize milling, pia zawadi ya vitabu na
michanganuo mingine mbalimbali. Mawasiliano yetu ni; 0765553030 au 0761002125
SEHEMU YA 1 SEHEMU YA 3
0 Response to "SEHEMU YA 2: MAELEZO YA BIDHAA & TATHMINI YA SOKO"
Post a Comment