KUFANIKIWA BIASHARA YA UFUGAJI WA KUKU UZINGATIE KITU GANI KATI YA MABANDA, CHAKULA, CHANJO NA DAWA? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KUFANIKIWA BIASHARA YA UFUGAJI WA KUKU UZINGATIE KITU GANI KATI YA MABANDA, CHAKULA, CHANJO NA DAWA?

Swali  la mdau: Naomba muongozo wa kujenga bada

Swali hili ameniuliza mdau wangu mmoja kupitia watsap na aliuliza hivi;

Ok, Peter, mimi bawana ni mdau nataka kuanza kufuga kuku wa kienyeji, nahitaji muongozo wa kujenge banda na mengineyo yanayohusiana na ufugaji kuku kienyeji.

 

Nami nikamjibu kama ifuatavyo;

 

Habari kiongozi,

Unajua bwana, suala la mabanda kwenye biashara ya ufugaji wa kuku siyo ishu kubwa sana ni suala tu la kuwa na mtaji wa kutosha, kuku hawahitaji mabanda spesho sana bali wanachohitaji wao ni mahali watakuwa salama, pa kuwakinga na hatari zote kama vile hali mbaya ya hewa- jua, mvua na upepo, lakini wanyama hatari walao kuku kama vicheche, paka, kunguru, fisi, mbwa, nyoka nk. bila kusahau binadamu wezi.

Kwa kuzingatia mahitaji hayo niliyoyataja mtu unaweza kumtafuta fundi yeyote yule mzoefu ukamlipa akakutengenezea banda zuri litakalokidhi mahitaji hayo na wala siyo kuhangaika sijui eti ukatafute ramani za mabanda ya ghorofa, mabanda yenye hadi siting room, dining room na makorokoro kibao kama hayo, kuku hawahitaji vitu hivyo, wawekee mabembea, vyombo vizuri vya maji na chakula, viota na nafasi iwe ya kutosha mita moja ya mraba wasizidi kuku wakubwa 6 -10, basi umemaliza

Ukitaka uone mafanikio ya faida kifedha kwenye mradi wa kufuga kuku wa aina yeyote ile iwe ni kuku wa kienyeji, kuku wa kisasa, chotara au kuku wa aina nyingine yeyote ile, zingatia sana mambo haya 3 nitakayokueleza hapa

(1) Zingatia sana kitu kinachochangia gharama kubwa kwenye hii miradi ya ufugaji wa kuku ambacho si kingine bali ni gharama za CHAKULA.

Gharama za chakula ni zaidi ya asilimia 70% ya gharama zote za mradi wowote ule wa kuku so, unapaswa ili kuona faida basi uhakikishe unapata vyakula vya kuku kwa gharama nafuu kadiri iwezekanavyo, jifunze jinsi ya kupunguza gharama za chakula kwa mradi wako wa kuku na hiki ndicho kitu kikubwa kitakachoweza kuleta tofauti kubwa kwenye mradi wako na siyo mabanda ingawa nayo ni muhimu pia.

(2) Kitu cha pili cha kuzingatia ikiwa kama kweli umedhamiria kutajirika na mradi wa kufuga kuku ni CHANJO. Ikiwa ufugaji wako siyo kwa ajili ya kitoweo cha siku za sikukuu kama Iddi, Krismasi, Pasaka na Mwakampya ambapo huna umuhimu mkubwa nao, basi ni  lazima uzingatie chanjo zote muhimu pasipokujali ikiwa unafuga kuku wa aina gani kienyeji au kisasa

Dawa nyinginezo za magojwa ni muhimu pia mfano za minyoo na kuharisha.

Achana kabisa na kasumba ya kusema eti, “Kuwalisha kuku dawa au chanjo kuna madhara kwa afya ya binadamu” wewe unafuga kibiashara na tena isitoshe binadamu tukiumwa tunachoma hizihizi chanjo na madawa antibiotics, sasa kuku kwani siyo viumbe hai kwahiyo hawastahili dawa?

(3) Jambo la tatu ni UFUGAJI WA KIWANGO KIKUBWA (Mass production). Kutokana na gharama hasa za chakula na virutubisho nilivyosema hapo juu, faida kwenye ufugaji wa kuku wachache siyo kubwa sana ikiwa utaamua kuwahudumia ipasavyo ingawa pia ni ya uhakika kama umezingatia hayo yote. Sasa kwa kuwa ni kidogo na ya uhakika, basi ili iweze kuwa kubwa na kukujengea utajiri inakupasa ufanye ufugaji wa kiwango kikubwa na siyo kuku waiwili watatu wa kitoweo nyumbani

Tatizo la wafugaji wengi wadogowadogo ni kwamba kwakuwa wanaogopa gharama basi hujikuwa wakipata hasara au kutokuona faida kwenye idadi ndogo ya kuku wanaofuga na hivyo kuogopa moja kwa moja kufuga idadi kubwa ya kuku. Hufikiria changamoto walizopata ikiwa wataingiza pesa nyingi itakuwaje? Lakini changamoto hizo dawa yake ni kuzingatia tu hayo mambo 3

Mtaji wa kufuga kuku pia haupaswi kuwa wa ‘mawazo’ hakikisha unazo pesa za kutosha kulipia gharama za mradi mzima mkononi au benki kabla hujaanza na siyo kuja kuanza kutafuta pesa wakati vifaranga wameanza kuota manyoya au matetea wanakaribia kutaga, utawaua na njaa bure

Fanyia mazoezi kwanza mradi wa kuku wachache ukishapata uzoefu na kuona idadi hiyo kuku wote wamepona na umepata faida kidogo, basi ongeza mradi wako (scale it up) na utumie mbinu zilezile ulizotumia kwenye mradi wa idadi ndogo ya kuku halafu utaona matokeo yake yatakavyokuwa makubwana ya kushangaza.

Imagine kwa mfano umefuga kuku 100 tu ukapata faida ya shilingi elfu 50, sasa ukifuga kuku 2000 piga hesabu una faida kiasi gani hapo? Tena ni kwa muda uleule uliofuga kuku 100

Kila la kheri

Peter Tarimo

0765553030 / 0761002125

Kwa mahitaji ya michanganuo ya kuku aina zote, kienyeji kisasa na chotara kwa bei rafiki, tuwasiliane.

Mchanganuo unakuwezesha kujua gharama, faida, changamoto na mahitaji yote kabla hujaanza kufuga au kufanya mradi mwingine mkubwa zaidi.



SOMA NA HIZI HAPA;

1.   Banda la kuku 100 wa kienyeji: vipimo, ramani, picha na jinsi ya kulijenga kwa ubora

2.   Muongozo kamili wa jinsi ya kufuga kuku wa nyama (broilers) kitaalamu- semina siku-3

3.   Ufugaji wa kuku wa kisasa wa mayai vs kuku wa nyama ni biashara ipi inayolipa faida zaidi?

4.   Semina: mchanganuo wa kuomba mkopo biashara ya ufugaji wa kuku 200 wa nyama

5.   Kilichokuwa nyuma ya pazia, ufugaji kuku wa kienyeji(kuku wa asili).

 

6.   Kuku wa nyama broilers: kwanini faida na gharama za ufugaji zinavunja moyo?

 

 

0 Response to "KUFANIKIWA BIASHARA YA UFUGAJI WA KUKU UZINGATIE KITU GANI KATI YA MABANDA, CHAKULA, CHANJO NA DAWA?"

Post a Comment