Mimi
nilisomea ualimu na mpaka sasa hivi bado ni muajiriwa shule ya serikali lakini
kwakweli kazi ninayoipenda kutoka moyoni ni kazi ya ununuzi na ugavi (Supply
and Procurement). Hivyo wakati nikiendelea na ualimu nilichukua uamuzi wa
kwenda kusomea course ya ununuzi na ugavi chuoni na tayari nimekwisha fanya
mipango yote ya kujiunga na chuo.
Hata
hivyo wakati nikijiandaa na chuo kuna mawazo mengine yameibuka kichwani mwangu
na kunifanya niwe katika wakati mgumu sana wa kuamua. Kuna biashara nikiwa bado
mwalimu naendelea kuifanya ambayo pia nilichukua mkopo mahali kwa ajili yake na
tayari mkopo huo karibu namaliza kuurejesha.
Sasa
kinachonitatiza ni kwamba, nikaendelee na masomo ya ugavi chuoni miaka 3 au
niamue kuzama moja kwa moja kwenye biashara na kuachana kabisa na ndoto za
kuajiriwa serikalini?
Ingawa
ninao uhakika nikimaliza chuo bado naweza kuajiriwa na serikali kwani sasa hivi
pia nimeajiriwa nayo kwa kazi hii ya ualimu ila tatizo nahisi miaka 3 na 1 wa
kusubiri ajira naona kama ni muda mrefu mno, nitakuwa nimechelewa sana.
Hiyo ni changamoto anayopitia msomaji wangu mmoja kutokea
kule Mkoani Kigoma akiomba ushauri ili aweze kuondokana na mtanziko unaomkabili
juu ya kuchagua aendelee na chuo au biashara.
MAJIBU:
Katika changamoto yako nimegundua kwanza kuna mambo
makubwa matatu yanayokufanya ushindwe kuamua ni lipi sahihi unalopaswa kushika
na kuachana na mengine, lakwanza ni ualimu ambao unasema ulisomea lakini moyo
wako haukuwa kwenye ualimu, jambo la pili ni kusomea course ya manunuzi na
ugavi (Procurement and Supply) ambayo
unasema ndiyo moyo wako ulipo hasa lakini kuna jambo la tatu ambalo umesema ni
biashara uliyoanzisha tangu ukiwa mwalimu na bado unaendelea kuifanya.
Sasa unataka ama uendelee na chuo au uamue kuzama moja
kwa moja kwenye biashara yako na kuachana kabisa na mambo ya kuja kuajiriwa
serikalini iwe ni ualimu au kwenye manunuzi na ugavi
Ushauri
wangu kwako
Ushauri wangu ni kwamba, usiachane na hiyo ndoto yako ya
kuendelea na chuo kwa ajili ya masomo ya procurement and supply kisa biashara
uliyoanzisha hata kama unaona inalipa kiasi gani.
Jambo la busara ambalo unaweza kulifanya ni kuendelea
kufanya mambo yote mawili kwa wakati mmoja kama ulivyokuwa ukifanya kwenye
ualimu kwani inawezekana kabisa ukizingatia kazi ya ualimu ni lazima serikali
itakuruhusu usimame kwanza kupisha hayo masomo yako mapya chuoni.
Kwanini
nakushauri hivyo?
Fursa yeyote ile ya masomo kwa binadamu kwa kawaida ni ya muda mfupi sana
ukilinganisha na muda atakaokuja kuishi mtaani akifanya biashara au kwenye
ajira. Watu wengi waliozichezea fursa za kukaa shuleni au chuoni kwa namna moja
ama nyingine kuna nyakati katika maisha yao walikuja kuzijutia.
Kwani ukimalizia digrii (shahada) yako hiyo miaka 3 tu na
kisha ukaja kuendelea na biashara zako ukiwa umeshahitimu course kuna tatizo
gani?
Watu wengi sana siku hizi huponzwa na dhana iliyoenea
dunia nzima kwamba, matajiri wengi hasahasa baadhi ya mabilionea wa Kimarekani
na hata nchi nyinginezo mfano Uchina na Uingereza ni “drop outs” nikiwa namaanisha
walikatisha masomo yao katika vyuo na vyuo vikuu na kwenda kuanzisha biashara
ambazo hatimaye ziliwafanya wawe matajiri wa kutupa
Usahihi wa dhana hii ni mdogo sana ukizingatia hali
halisi. Kwanza hii ni bahati na sibu zaidi kuliko uhallisia wenyewe, usidhani
kila anayeacha shule/chuo basi moja kwa moja atakwenda kutoboa kwenye biashara,
si rahsi kihivyo.
Utakuta katika watu labda 1000 ni asilimia % ndogo sana
wanaoweza kufanikisha jambo hilo na hao ndio hawa kina Bill Gates, Mark Zuckerberg, Steve Jobs, Larry Ellison, Richard Branson, Jay-Z na wengineo
Kwanza ni lazima ujiulize, Je mazingira ya watu hao
kiuchumi na hata kijamii yanalingana na yale unayoishi wewe? Kwa mfano wengi wa
hao mabilionea tunaosema wa Kimarekani kwanza walikuwa ni watu waliokuwa na asili
ya utajiri tayari, wazazi wao aidha walikuwa na uwezo mkubwa kifedha au kielimu
na hivyo kuwafanya maamuzi yeyote yale ambayo wangeliyafanya yasiweze kuwa na
adhari hasi kwenye maisha yao.
Mtu kama Bill Gates tayari alikuwa na ‘exposure’ kubwa sana kwenye kompyuta
shauri wazee wake walikuwa wataalamu waliobobea kwenye fani hiyo, hivyo
aliachana na chuo kikuu pale Havard akiwa na uhakika kabisa kwamba alikuwa
anakwenda kutoboa kwenye fani ya uinjinia wa programu za kompyuta.
Kwa bahati mbaya sana Dunia haina mazoea ya
kutangaza sana hadithi za wale wanaofeli kimaisha, vinginevyo watu
tungelistaajabishwa mno na idadi kubwa ya wale waliowahi kuanguka kimaisha
baada ya kuacha masomo na kwenda kukimbilia kuanzisha ujasiriamali wakidhani
watatoboa kirahisi
Ulimwengu wa biashara umejaa vihatarishi vingi mtu
unapaswa kukabiliana navyo kabla hujatoboa rasmi na ikiwa hukujiandaa vyema au
hauna uvumilivu ni bora usijaribu kujikita huko na kuachana na fursa ya masomo
uliyokwisha itia mkononi kama yakwako.
Acha ajaribu mtu asiyekuwa na fursa hiyo ama yule
mwenye maandalizi ya kutosha na mazingira yake yanampendelea kama walivyokuwa
kina Bill Gates, Mark Zuckerberg, Steve Jobs, Larry Ellison na Richard Branson.
Unaweza sema leo unaachana na chuo na ajira ya
serikali ukafanye biashara zako kwa kuwa tu unao uhakika wa kuishi kwa mshahara
uliokuwa ukiupata kwenye ualimu, lakini kumbuka utakapoacha na mshahara wa
ualimu utakoma hivyo itakubidi uanze kutegemea faida ya biashara kwa matumizi
yako binafsi ya kila siku, je, umeshajiandaa na hilo?
Na umesema kwamba una mkopo wa biashara unamalizia,
sasa ikiwa hata biashara ilikuwa inategemea mkopo, huna mtaji toshelevu
utakapoanza kutumia faida kwa matumizi ya kila siku biashara itaweza kuhimili
hilo?. Mwaswali haya na mengine itakubidi ujiulize kwanza kabla hujafanya
maamuzi ya mwisho.Kifupi fanya upembuzi yakinifu wa maana kwanza
Siyo nia yangu kukutisha usiingie mazima kwenye
biashara ila ninachotaka tu kukuambia hapa ni kwamba, chuo kikuu siyo kama O
Level au A level, unaweza kuwa ‘flexible’
ukaendelea na course yako huku
ukifanya biashara mdogomdogo. Siku hizi fursa za biashara zisizomgharimu mtu
muda mwingi ziko tele kutokana na maendeleo makubwa ya teknolojia ya habari na
mawasiliano hasa kompyuta na mitandao ya kijamii.
Ukiwa Kigoma unaweza ukaagiza mzigo Dar es salaa
bila ya kuufuata mwenyewe, ukaletewa na kuuza pasipo kuzunguka nao mtaani wala
kuwa na fremu ya duka mahali kwa kutumia tu simu au kompyuta yako mpakato
(laptop), tena katika muda wako wa ziada wa mapumziko au ukiwa nje ya kazi za
darasani.
Ninachotaka kukueleza hapa ni kwamba, jaribu kuwa
mbunifu kidogo usikubali kirahisirahisi tu kuachia fursa hii adhimu ya kupata
ujuzi wa Manunuzi na ugavi utakaoishi na wewe milele.
Biashara ipo kila siku lakini kuja kupata ujuzi
baadae umeshapiga teke fursa uliyoipata ni jambo gumu sana, kumbuka binadamu
kadri miaka inavyosonga mbele na majukumu nayo huongezeka, leo una mtoto mmoja
lakini mwaka kesho na keshokutwa utaweza kuwa na watoto 3, 4 na kuendelea.
Familia haitakuruhusu kirahisi ukafanye digrii yako
ikiwa pengine kiuchumi hauko vizuri. Wakati huo pia sidhani kama fursa ya
udhamini wa serikali itakuwa bado ikikusubiri, watakuwa wameshaidaka vijana
wengine wapya kutoka form six nk.Hivyo ndugu yangu kabla hujafanya maamuzi yako
juu ya jambo hili, pima mara mbilimbili matokeo ya uamuzi wako.
Mwisho
Tunatoa ushauri mfupimfupi kama huu kwa yeyote
mwenye changamoto kwenye maeneo yanayogusa hasa biashara, ujasiramali na
uwekezaji. Tuma changamoto yako kupitia;
Whatsapp/sms/call: 0765553030 / 0761002125
HUDUMA ZETU MBALIMBALI, VITABU
& MICHANGANUO
(a) HUDUMA:
1. Kuandikiwa
Mpango wa Biashara yeyote ile
-Gharama zetu ni rafiki kuanzia
chini ya asilimia 0.5% ya mtaji wa biashara husika
2.
Kuandikiwa Company Profile
-Gharama za huduma hii ni kuanzia
Tsh. 50,000/=
3. Program
ya Make Yourself Great Again 2025
-Ni group la whatsap na channel ya Telegram kwa
ajili ya kujifunza jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara, Ubunifu kwenye
biashara, masomo ya fedha, mauzo na uwekezaji, Jiunge group la MAPOKEZI HAPA
kupata masomo ya bure kwanza. VIP ni Tsh. 10,000/=
4. Usomaji wa Kitabu cha
Think and Grow Rich kwa Kiswahili na kiingereza
-Ni Group maalumu na Washiriki ni wale wote
waliowahi kununua kitabu cha Fikiri & Utajirike (Think & Grow
Rich-swahili edition) cha karatasi (hardcopy) au nakala laini (softcopy)
(b) VITABU & MICHANGANUO:
1. Think & Grow Rich
Swahili Edition:
Hardcopy ukiwa Dar es salaa ni Tsh. 25,000/=
unaletewa mpaka ulipo, Mikoa mingine kwa basi ni Tsh. 32,000/= Kwa upande wa
softcopy ni Tsh. 10,000/= nunua katika App hii ya GETVALUE
kupitia kiungo hicho (bofya kununua)
2. Mafanikio ya Biashara ya
Duka la Rejareja:
Nakala ngumu Tsh. 20,000/= Dar es salaa unaletewa
ulipo, Mikoa mingine kwa basi ni sh. 30,000/= Kwa nakala laini (softcopy) ni
sh. 10,000/= tunatuma kwenye simu au kompyuta yako unapolipia kwa namba,
0761002125 au unaweza kununua katika duka letu la mtandaoni la Selar.com
kwa kubofya kiungo hicho
3. Michanganuo ya Biashara
na Ujasiriamali:
-Hardcopy ni Tsh. 25,000/= Dar es salaa, Mikoa
mingine kwa mabasi ni Tsh. 35,000/= Kwa upande wa softcopy lipia kupitia namba
0761002125 na tutakutumia kwenye simu au kompyuta yako bila kuchelewa popote
pale ulipo duniani au nunua online moja kwa moja kwa kubofya hapa>>>Selar.com
4. Kwa Vitabu zaidi na
Michanganuo ya Biashara kamili (Ready
made Business Plans)
-Ingia kwenye duka letu la mtandaoni kwa kubofya
kiungo hiki kifuatacho>>>SELF HELP BOOKS TZ
SOMA NA HIZI HAPA;
2.
Biashara nzuri 4 mwanachuo anaweza kufanya na mtaji wa laki 2
huku akisoma
3.
Kuanzisha biashara nikiwa chuoni nasoma nipeni ushauri nina
wakati mgumu
4. Maajabu ya kufikiri mambo makubwa na kwanini uweke malengo
makubwa maishani
5. Biashara ya laini na miamala ya simu kwa mwanafunzi wa chuo
kikuu, mtaji laki 3 –ushauri
0 Response to "NATAMANI KUFANYA BIASHARA BAADA YA KUACHA UALIMU NA KUSOMEA UGAVI (PROCUREMENT)"
Post a Comment