Wanafunzi wengi hasa wa vyuo wanatamani sana kufanya
biashara wakiwa wangali hawajamaliza course zao mfano biashara ya uwakala wa
m,itandao ya simu, na hili mara nyingi linatokana na sababu mbalimbali zikiwemo
mwamko wa vijana wengi siku hizi wa kuwa na roho ya ujasiriamali hivyo wanaona
kama vile wanachelewa kuanza ujasiriamali.
Lakini sababu nyingine kubwa ni mahitaji ya wanafunzi
wengi kutokana na fedha kidogo wanazopewa na wazazi ama walezi wao ama mkopo
kwa wanachuo kutokutosheleza mahitaji yao jambo linalosababisha maisha ya
wanachuo hao kuwa magumu na kuamua kujitafutia fedha kupitia biashara
mbalimbali halali.
Nimekuwa nikipokea maombi mengi ya ushauri toka kwa
wanachuo mbalimbali na jinsi ya kufanya biashara, mfano ni kijana mmoja kutoka
Chuo Kikuu cha TIA mwaka wa pili liyetaka kushauriwa biashara ya kufanya kwa
mtaji wa laki 3 (300,000/=)
Hapa chini nimeweka mawasiliano yangu na yeye whatsap
kama yalivyo bila ya kupunguza wala kuongeza kitu isipokuwa utambulisho wake
kamili tu;
SWALI:
MWANACHUO:
Habari za asubuh naitwa Imma..... Niko chuo kikuu TIA second year. Nina mtaji
wa laki 3 tatu naomba msaada nifanye biashara gani ili niweze kuzalisha pesa naomba
msaada wenu.. ushauri
MAJIBU:
JIFUNZEUJASIRIAMALI:
Nzuri Imma na karibu,
Biashara utakayoifanya Ni lazima iendane na mazingira
yako ya chuo isije ikaingiliana na muda wako wa masomo wala kukufanya ushindwe
kwa namna yeyote ile kutimiza majukumu yako ya chuo.
Fanya utafiti kujua Ni kipi utaweza kufanya ukilenga
wateja ambao wengi itabidi wawe ni wanachuo wenzako. Uzuri wa biashara hizi
ndogondogo za uwakala au uuzaji bidhaa wala huhitaji leseni ya biashara
Chunguza Wanachuo wana mahitaji gani makubwa ya vitu
unavyoweza kwenda kununua na kuja kuwauzia mfano simu, mavazi nk. Unaweza kuwa
wakala wa mitandao ya simu na kupata kamisheni. Cha msingi ni kujua jinsi ya
kuwa wakala na kumiliki laini za uwakala wa hayo makampuni
Lenga biashara/bidhaa zisizoharibika upesi zisijekukupa
presha ya kuuza haraka kwa bei ya chini.
Unaweza kuchagua bidhaa hata 2 tu (pc 2) zenye ubora na
za kipekee sana ukazifanyia marketing ya uhakika taratibu ukilenga kupata kila
bidhaa faida hata ya sh. Elfu 10 mpaka15 tu hivi. Mtaji wa shilingi laki tatu 3
unatosha kuendesha biashara ya bidhaa chache ikiwa hutegemei pesa yeyote ya
matumizi kutokana na hiyo biashara.
Zikiuzika unafuata nyingine hivyohivyo. Unaweza ukaamua
kudili labda na viatu, suruali, simu, mikanda mikali ya kiunoni au chochote
unachojua kuna wanafunzi wenye uwezo wa kuvilipia
Ni lazima hizi bidhaa ziwe za kipekee (unique) na siyo bidhaa mtu anaweza
kwenda kutafuta kirahisirahisi tu. Tafuta sababu kubwa itakayomsukuma mteja
wako kununua. Siku hizi kuna mpaka uwezekano wa kuagiza bidhaa toka nje mfano
China nk. kupitia mtandao wa intaneti.
Mwisho kumbuka ukiwa chuoni kipaumbele/focus yako ni
kukamilisha course yako zaidi ya kitu kingine chochote, mwaka wa chuo ni mmoja
lakini utakuwa na miaka kibao huko mbeleni kufanya biashara zozote upendazo
baada ya kuhitimu, hivyo biashara chuoni ifanye bila kuiwekea mategemeo makubwa
kupitiliza usijekujikuta baadae unavunjika moyo vibaya endapo haitafanya vile
unavyotaka ifanye.
Weka hatari kidogo kwenye hiyo biashara au risk tu kitu unachoweza kukubaliana na
matokeo yake kwa urahisi yawe mazuri au mabaya.
IMMA: Nashukuru, hapo kiukwer nipe wazo nianze na
lipi japo wengi wanajikita kwenye laini na miamala unanisaidiaje kupitia
biashara yoyote nipe plan mkuu
JIFUNZEUJASIRIAMALI:
Uamuzi Ni wakwako kulingana na mazingira ulipo hata ukiona miamala ya simu,
vocha na laini inafaa pia siyo mbaya kwani si vitu vya kuharibika na unaweza kuicontrol
kwa urahisi. Vilevile ni bidhaa wanachuo hununua kila siku kwa wingi.
Kama nilivyotangulia kusema biashara yeyote simple
inayokuhitaji wewe na begi lako tu chuoni inawezekana kufanya, kikubwa ni
kujenga jina na wanachuo wajue bidhaa ama huduma fulani inapatikana kwako tu.
Vifaa vya kielectroniki hasahasa vile kwa ajili ya mawasilianao ndiyo habari ya
mjini nyakati tulizokuwana nazo sasa kwahiyo hutakuwa umefanya uamuzi mbaya
kuchagua miamala ya simu na vifaa vyake kwa ujumla.
Nakumbuka kabla ya kuja simu za mkononi zamani mashuleni
na vyuoni wanafunzi walifanya sana biashara ya upigaji wa picha za mnato kwa
kutumia kamera aina ya YASHIKA, binafsi ninayo yakwangu mpaka hivi leo ingawa
zimepitwa na wakati hazitumiki tena. Vitu ama vifaa vinavyotrendi / kwenda na
wakati ni moja ya biashara nzuri sana ikiwa soko lako ni wanafunzi maana
wanapenda kwenda na wakati.
Asante Imma Nikutakie mafanikio katika shughuli zako zote
chuoni.
...................................................
Huduma za ushauri mfupimfupi kama huu huwa tunatoa Bure
kwa mtu yeyote mwenye changamoto au maswali yeyote kuhusiana na Biashara au
Ujasiriamali.
HUDUMA
ZETU NYINGINE
1. UANDISHI
WA MIPANGO/MICHANGANUO YA BIASHARA
Tunaandika Michanganuo ya Biashara kwa aina zote za
Biashara kubwa na ndogo, huduma au bidhaa na gharama zetu ni rafiki. Walengwa
ni mtu yeyote anayeomba nkopo kutoka katika Taasisi za fedha, kutafuta wabia na
wawekezaji, kusajili kampuni au biashara au mtu yeyote anayehitaji mpango wa
biashara yake kwa ajili ya uendeshaji mzuri wenye tija.
2.
MAFUNZO YA JINSI YA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA
Tuna kifurushi cha masomo, vitabu na Michanganuo jumla vitu 14. Kifurushi hili ukikisoma unaweza kuandaa mpango wa biashara yeyote bila usaidizi wa mtu mwingine yeyote. Bei yake ya OFFA ni shilingi elfu 10 tu na unapata nafasi ya kujiunga na group la watsap la masomo na mentorship kwa mwaka mzima.
1. 3. VITABU VYA BIASHARA NA UJASIRIAMALI
Tunavyo vitabu mbalimbali
kama ifuatavyo
1. Michanganuo
ya Biashara & Ujasiriamali = 10,000/=
2. Mafanikio
ya biashara Duka la rejareja = 6,000/=
3. Mifereji
7 ya fedha na siri Matajiri wasiyopenda kuitoa = 3,000/=
4. Think
& Grow Rich Swahili edition = 10,000/= kwenye app ya GETVALUE
5. Sayansi
& Sanaa ya Upishi wa chapatti laini = 5,000/=
Kupata Huduma yeyote hapo
juu wasiliana na sisi kwa namba zifuatazo kupitia Simu, Whatsapp au Ujumbe;
0712202244 au 0765553030
Peter Augustino Tarimo
SOMA NA HIZI HAPA:
1. Biashara nzuri 4 mwanachuo anaweza kufanya na mtaji wa laki 2
huku anasoma
2. Ushauri kwa mwanafunzi aliyehitimu chuo/masomo anayetaka kuanza
maisha
3. Kuanzisha biashara nikiwa chuoni nasoma nipe ushauri nina
wakati mgumu
4. Biashara ndogondogo zenye faida ya haraka tanzania ni hizi hapa,
zipo nne(4)
0 Response to "BIASHARA YA LAINI NA MIAMALA YA SIMU KWA MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU, MTAJI LAKI 3 –USHAURI"
Post a Comment