Mpenzi
msomaji wa blogu hii, Heri ya mwaka mpya wa 2024
Bila
shaka utakuwa na shauku ya kutaka kufahamu ni mbinu zipi hizo mtu anazoweza
akabadilisha siku yenye masaa 24 na badala yake yakawa masaa 25 au hata zaidi
ya hapo.
Lakini
nataka nikueleze kwamba hamna lisilowezekana chini ya jua. Mwenyezi Mungu
amemjalia Mwanadamu uwezo mkubwa sana wa akili kiasi kwamba Dunia sasa hivi
inahaha kuzuia janga kubwa la binadamu mwenyewe kwa kutumia akili hizohizo
alizopewa na Mwenyezi Mungu kutaka kuunda kitu chenye akili kumzidi hata yeye mwenyewe binadamu (Artificial Intelligence)
au (AI). Kwani akili bandia ni nini?
SOMA: Njia mpya za kufanya mambo, dunia, biashara, ajira vinabadilika kwa kasi ya ajabu
Kwa
maneno mengine ni Midubwana inayotumia akili bandia kufanya mambo sawasawa na
yale tufanyayo sisi binadamu na hata wakati mwingine kutuzidi. Midubwana hiyo
hutumia teknolojia hii hii ya kompyuta za kawaida lakini katika kiwango cha
hali ya juu sana cha uwezo wa kimahesabu/kukokotoa, ndiposa tunapata vitu kama ChatGPT, mithili ya zile sauti za mashine
unazojibiwa ukipiga simu huduma kwa wateja lakini hizi zimeboreshwa zaidi na
hujibu chochote unachouliza, magari na ndege zinazojiendesha zenyewe, huduma
kama za UBER nk. Ni maajabu haya mpendwa!
Sasa
hebu fikiria ikiwa upeo wa mwanadamu unaweza kufikia hatua kama hiyo ni kwanini
wengine tushindwe hata kuwa na uhakika wa mlo wa siku? Duniani kuna mbinu
nyingi za kurahisisha mambo tusiyoyajua
au tusiyojishughulisha tu kuyajua ambapo yangeweza kutufikisha viwango vingine
kabisa. Ipo dhana moja kwamba binadamu tunatumia asilimia ndogo sana ya uwezo
wa akili zetu. Tungeongeza matumizi ya uwezo huo japo sehemu ndogo tu,
tungefanya mambo ya kutisha sana.
Mwaka
huu wa 2024 Jifunzeujasiriamali blog tumeamua kuja tofauti kabisa, tumeamua
kuleta suluhisho la kutokupiga hatua kwa wajasiriamali (Startups). Biashara
nyingi zinaanza lakini hata baada ya miaka 10 kupita zinaendelea tu kuitwa changa
hazikui. Tatizo ukiuliza unaambiwa Ooo… mitaji ni kidogo haitoshelezi mahitaji.
Sasa tunaleta suluhisho gani?
SOMA: Kuendesha biashara bila mtaji ni sawa na kulima kwa jembe lisilokuwa na mpini
Hakuna
njia ya mkato lakini inawezekana kuondoa tatizo hili kabisa kwa kutumia njia na
mbinu za kiubunifu ikiwemo akili bandia (AI). Ni njia hizihizi zilizotumiwa na
watu wa Amerika, Ulaya na hata baadhi ya nchi za Asia wakaweza kufanya mambo makubwa mno katika nyanja
mbalimbali ikiwemo teknolojia. Akili bandia haina maana yeyote zaidi tu ya
ubunifu na ubunifu unaweza ukafanyika katika kila eneo ikiwemo biashara pia.
Tumeandaa
masomo mengi yenye maudhui yanayolenga kusisimua akili ili iweze kubuni njia za
kurahisisha biashara na kuzifanya ziweze kuzalisha faida kubwa haraka
itakayosaidia kukabiliana na mahitaji yetu makubwa ya kila siku bila ya
kuathiri ukuaji wake. Ndio maana tukaja na Kaulimbiu isemayo; “UBUNIFU
NA AKILI BANDIA, VITUMIE KUBOOST BIASHARA YAKO VIWANGO VINGINE”
Kwa
mfano somo hili la Mbinu za kuifanya siku yako iwe na masaa 25 badala ya 24
litatolewa leo hii tarehe 1/1/2024 katika Mastermind group letu la Michanganuo-online
usiku saa 3 na ni kila siku tunakuwa na somo moja linalochochea ubunifu katika
kuongeza mzunguiko wa fedha kwenye biashara zetu. Tunayo masomo zaidi ya 100
yaliyo tayari na huwezi ukayapata kwingine kokote.
SOMA: Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado
Aidha
tutakuwa na Michanganuo ya biashara mbalimbali kila mara kwa lengo hilohilo la
kuchohchea ubunifu. Ikiwa kina Mo, Diamond, Mark
Zuckerberg na Elon Musk wameweza hata wengine wengi wanaweza ni suala tu
la kuongeza ubunifu na ujasiriamali kwenye shughuli za biashara tunazofanya
Kujiunga
na group letu hili jipya kwa mwaka 2024 upate na OFFA ya vitabu na Michanganuo
jumla vitu 14, lipia ada yako ya mwaka sh. 10,000/= kwa namba zetu
0712202244 AU 0765553030 jina ni Peter
Augustino Tarimo. Offa ni ya muda mfupi!
VITU
14 VYA OFFA NI HIVI HAPA CHINI:
1.
KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu
za BIASHARA, jinsi ya kuandaa
michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika
kila kitu. – kwa Kiswahili
2. KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango
wa biashara-dakika 30 tu - kwa kiswahili
3. KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili
4. KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS
PLAN ni maarufu sana duniani, hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza
5. KITABU: Siri za upishi wa chapati laini-UPENDO CAFE pamoja na
Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili
6.
COMPILLATION: Masomo 30 ya fedha
usiyoweza kuyapata popote, mengine 70 utayapata kwenye group kila siku - kwa Kiswahili
7. MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili
8. MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza
9. MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili
10. MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji- kwa kiswahili
11. MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini
Broilers –kwa kiingereza
12. MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini
Broilers –kwa kiswahili
13. MCHANGANUO: Kiwanda cha mvinyo na juisi ya Rosella –Choya Investment – kwa kiswahili
14. MCHANGANUO: Kilimo cha Tikiti maji:- Kibada Watermelon Fruits – kwa kiswahili
0 Response to "JINSI YA KUIFANYA SIKU YAKO IWE NA MASAA 25 BADALA YA 24"
Post a Comment