Nimewahi mara nyingi kuulizwa swali hili na Wanafunzi hasa
wale wa vyuo na sekondari wakati mwingine wakiomba ushauri ni biashara zipi
wanaweza wakazifanya wangali wakiwa bado wanasoma. Kwa kweli hili swali
nimelijibu mara nyingi katika post na makala zangu ndani ya blogu hii mtu
yeyote anaweza akazifuatilia humo.
Kimsingi katika majibu yangu hayo sijawahi kuwashauri
wanafunzi kufanya biashara wakiwa wanasoma bali kujitengenezea mazingira fulani
mazuri ya kiujasiriamali yatakayokuja kuwasaidia katika biashara na miradi yao
hapo baadae pindi watakapohitimu masomo au course zao.
SOMA: Biashara nzuri 4 mwanachuo anaweza kufanya na mtaji wa laki 2 huku akisoma
Lakini pia kuna mazingira mwanafunzi anaweza akalazimika
kufanya biashara angali chuoni au shuleni na ikiwa ni lazima basi mwanafunzi
afanye biashara, inawezekana lakini ni lazima mwanafunzi huyo azingatie vigezo
na masharti fulani fulani niliyoyaainisha kwenye hizo makala ili kuhakikisha
hapotezi malengo yake ya kielimu ambayo ndiyo msingi na focus yake
kwa sasa.
Leo nitazungumzia jinsi ya kutengeneza au kumtengenezea
mwanafunzi/mtoto wako mazingira mazuri
ya kiuwekezaji na biashara au kwa maneno mengine unaweza ukasema roho ya
kijasiriamali tangu pale anapoanza masomo yeke iwe ni chekechea, darasa la
kwanza, kidato cha kwanza, cha tano, chuo na hata chuo kikuu. Hujachelewa
unaweza kuanzia darasa lolote lile kwani wengine huanza hata pale mtoto
anapozaliwa siku ya kwanza.
Ingawa siku hizi karibu kila mtoto anayezaliwa hupata
fursa ya kusoma shule, siyo watoto wote hufanikiwa kupata bahati ya kuajiriwa
iwe serikalini ama hata sekta binafsi. Kwanza ieleweke wazi kwamba watoto wengi
huishia ngazi za chini za elimu, mfano kidato cha nne, sita na hata vyuo vya
kati vya elimu, ni wachache wanaohitimu shahada zenye soko zuri katika vyuo
vikuu na kupata uhakika wa ajira.
Kusema ule ukweli ni vigumu mtu kukosa kabisa ajira
endapo atasoma kikamilifu na kuhitimu course yenye soko inayohitajika mno katika
jamii, tena isitoshe watu kila siku wanazeeka na kustaafu hivyo ajira
zitaendelea kuwepo tu siku zote lakini kwa wachache waliosoma na kuhitimu
vizuri kozi zenye uhitaji.
SOMA: Kuanzisha biashara nikiwa chuoni nasoma nipe ushauri nina wakati mgumu
Hebu tuachane kwanza na ajira, mimi nitajikita zaidi kwenye
kundi lile la wengi wanaoishia ngazi za chini au hata elimu ya juu lakini
hawajabahatika kusoma course zilizokuwa na soko la haraka. Ukiwa katika kundi
hili bila shaka utakubaliana nami kwamba, ni lazima ujiingize kwenye
ujasiriamali na hata ikiwa kama umefanikiwa kuajiriwa kipato chako kinaweza
kisikidhi mahitaji ukashindwa kubadilisha maisha yako. Ujasiriamali utaweza
kukupa kila kitu unachohitaji kiuchumi ukiufanya inavyotakiwa.
Jinsi
ya Kutengeneza Roho ya Ujasiriamali
Mwanafunzi hata yule anayekwenda kuanza darasa la kwanza
au shule ya vidudu Januari anapaswa kuanza kufanyiwa maandalizi ya kujengewa
uwezo wa kijasiriamali na kiuwekezaji katika umri wake huo mdogo. Mlezi au
mzazi ikiwa unataka mwanao umjengee msingi imara anzia hapa hapa na kuna vitu
vingi tu unaweza ukavifanya kama nitakavyoeleza huko mbele kwenye hii makala.
Kwa upande wa mwanafunzi mwenyewe ikiwa tayari
amekwishajielewa pengine ndiyo anakwenda kuanza kidato cha kwanza, kidato cha
tano au chuo, kuna mambo kadha wa kadha anayoweza akayafanya katika kujenga
mustakabali wake mwema kiuchumi hata ikiwa kama hatafanya biashara moja kwa
moja au uwekezaji mkubwa. Hebu sasa tukaone ni mbinu zipi mzazi/mlezi au hata
mwanafunzi mwenyewe anaweza akazitumia ili kujenga msingi bora wa ujasiriamali
hapo baadae akimaliza masomo yake.
SOMA: Maana halisi ya ujasiriamali, ulikotoka, ulipo na unakoelekea duniani
Watu wazima waliokwishapita umri wa kawaida wa shule, wengi
leo hii wanajutia sana ni kwanini hawakuzijua mbinu kama hizi au wazazi wao
hawakujishughulisha kuwaandaa mapema kwani wasingelikuwa na hali za kiuchumi
walizokuwa nazo sasa.
Kwa
Mzazi/Mlezi
Hata ikiwa mwanao unamwanzisha chekechea/ day-care ,
hakikisha unamfanyia kitu cha kuja kumsaidia huko mbele maishani mwake. Kumbuka
kumpatia mtoto elimu tu peke yake hakutoshi, mjengee kitegauchumi/akiba
itakayoweza kuja kuwa kama nyenzo kwake (backup)
endapo lolote litaweza kuja kutokea hasa ikiwa kama huna uwezo mkubwa kiuchumi
unaoweza kuja kuwahakikishia wanao ulinzi wa kutosha kiuchumi. Hatuombei mabaya
lakini leo mzazi upo, na kesho inawezekana ukawa haupo tena duniani, itamsaidia sana.
Mfungulie mtoto akaunti ya akiba benki kama zawadi ya
kuanza masomo yake au bima ambapo zipo za aina mbalimbali kulingana na
utakavyopenda mwenyewe. Hivi vitu ni vidogovidogo na unafanya polepole sana
lakini vinaweza kuja kuwa na athari chanya
kubwa kwa maisha ya mtoto siku za mbeleni. Au unaweza kuamua kuanzisha uwekezaji wowote
ule wa muda mrefu kwa niaba yake ambao mapato yake utahakikisha yanawekwa
mahali salama na huyagusi.
SOMA: Elimu ya fedha na umuhimu wake 2024 njoo tuunganishe nguvu tuhamishe milima!
Kwa wazazi wanaoishi vijijini au pembezoni mwa miji
kidogo wanaweza wakaamua kuanzisha miradi mfano shamba dogo la miti kwa ajili
ya mtoto, huu ni uwekezaji rahisi utakaochukua muda mrefu lakini una uhakika
utakuja kumnufaisha mtoto moja kwa moja kiuchumi baadae.
Miradi si lazima iwe ya maelfu ya shilingi hapana,
unaweza kwa mfano kuamua mwanao umuanzishie miradi midogomidogo mfano wa ile
nitakayokwenda kuelezea hapo chini kwenye kipengele kinachomhusu
mtoto/mwanafunzi mwenyewe.
Jambo jingine la msingi sana unaloweza kulifanya kwa
mwanao ni kumfundisha stadi mbalimbali za ujasiriamali kama vile kujiwekea
akiba hata kile kidogo sana anachokipata, kutumia muda vizuri, uaminifu,
uvumilivu, msimamo na kuwa na kiasi mara zote. Mfundishe pia mtoto kwa vitendo
kazi za kuingiza kipato unazozifanya wewe mwenyewe kipindi awapo likizo .
Usisahau pia kumpa usaidizi na mentorship katika usimamizi wa miradi yake
midogomidogo atakayoanzisha akiwa anasoma kama tutakavyoona hapo chini, mtie
moyo.
Kwa
Mwanafunzi / Mtoto mwenyewe
Hasahasa hapa inawahusu wale wa vyuo, kidato cha tano na
sita, kidato cha kwanza –cha nne na hata waliomaliza darasa la 7 kwakuwa
wameshaanza kujitambua tayari. Huwa siwahamasishi kabisa wanafunzi kufanya
biashara yeyote ile labda mara chache kwa wale wa vyuo na vyuo vikuu kwenye
baadhi tu ya biashara tena kwa mahesabu makubwa wasije wakajikuta wanahujumu
muda wao wa course au masomo darasani.
Kabla
sijaendelea kwanza kumbuka kwamba kinachowakwamisha sana vijana wengi katika
kuanzisha shughuli za ujasiriamali pindi wanapokuwa wamehitimu masomo yao ni
suala zima la mitaji na rasilimali za kuanzisha miradi/biashara hizo. Somo hili
nalenga hasa kuchochea wazazi, walezi na wanafunzi wenyewe kutengeneza mbinu zitakazomsaidia
mtoto kuja kuwa na uwezo wa kuanzisha biashara ikitokea hakupata ajira na mzazi
/mlezi wakati huo pengine hana uwezo wa kumpatia hizo rasilimali.
Ikiwa bado hujapata ajira ni lazima ujiajiri na kujiajiri
kunahitaji nyenzo (mtaji). Mtaji hata kama ni kidogo namna gani hauwezi kuupata
kirahisi kama huko nyuma hukujiwekea akiba au kufanya matayarisho yeyote yale
ya maana. Hakikisha kwa namna yeyote ile kile kidogo unachokipata unaweka
sehemu ndogo kama akiba, akiba haijali kama wewe ni mwanafunzi au ni nani bali
kanuni inasema tenga sehemu fulani ya kile upatacho iwe ni zawadi, ruzuku,
kipato au hata pocket money unayopewa na mzazi/mlezi
SOMA: Kuanzisha biashara bila mtaji, hivi inawezekana au ni kutiana moyo tu?
Kumbuka sasa hivi wewe bado upo chini ya uangalizi wa
wazazi/walezi au hata serikali inakupatia mkopo wa masomo, tumia fursa hiyohiyo
kujiwekea akiba kidogokidogo.
Kama ni lazima ufanye biashara basi wekeza katika miradi
midogomidogo isiyohitaji muda au uwepo wako wala kuingilia ratiba zako za
masomo. Katika miradi hiyo, epuka miradi yenye hatari kubwa na pia usilenge
kupata faida kubwa bali lenga zaidi kutunza fedha zako au na faida kidogo sana
kwani huhitaji kuishi kwa kuitegemea hiyo biashara.
Unaweza ukaanza kununua hisa kidogokidogo kwa fedha za
ziada unazozipata au biashara nyingine yeyote ile inayoendana na vigezo nilivyovitaja
hapo juu kulingana na mazingira uliyopo baada ya kufanya utafiti wa kutosha.
Ikiwa unaishi kijijini au nje kidogo ya mji unaweza kuanzisha ufugaji wa kuku
wa kienyeji, nunua kuku wachache hata 3
tu. Mradi kama huu ni rahisi kuendesha
kwani gharama ni banda la kulalia kuku usiku tu na kutagia pia chanjo mara
chache hasa mdondo na dawa ya minyoo .
Chakula waache wajitafutie wenyewe na mtu yeyote ndani ya
familia asichinje kuku wala kula mayai kiholela pasipo kulipa. Mapato yote
yatokanayo na mradi huo yaweke katika akaunti maalumu ya benki kama akiba pasipo
kuzitumia kwa jambo jingine lolote lile.
Mradi mwingine rahisi sana ni ufugaji wa ndege aina ya
njiwa. Unaweza ukafuga njiwa wa kawaida kwa ajili ya nyama au njiwa wa mapambo.
Uzuri wa njiwa ni kwamba hawahitaji gharama kubwa wala muda mwingi wa kuwaangalia.
SOMA: Utajuaje kama biashara yako ya kuku itakupa faida?
Ukishawazoesha njiwa kwenye banda lao dogo wataingia humo
kila siku jioni na kutoka asubuhi huku wakizaliana kwa kipindi kifupi sana.
Soko lao lipo kwani watoto wengine wengi mtaani watahitaji kuja kununua na
kwenda kufuga pia. Mapato fanya kama nilivyoeleza kwenye kuku hapo juu.
Kuku na njiwa wa kienyeji hawana gharama za chakula
kabisa labda tu mabaki ya vyakula na kazi kubwa ni kufunga na kuwafungulia
mlango asubuhi na jioni, kazi ambayo mwanafamilia yeyote anaweza akaifanya
pamoja na usafi wa banda mara chache kwa wiki. Ikiwa upo boarding waachie
wazazi/walezi wakuangalizie mradi wako mpaka muda wa likizo utakaporudi
nyumbani. Mlezi mwenye mapenzi mema hawezi kuacha mradi ufe kizembe ilihali na
wewe mtoto unaonyesha tabia njema, utii na shauku ya mafanikio.
Nimechagua miradi hiyo 2 ya kuku na njiwa wa kienyeji
makusudi ili kuonyesha umuhimu wa mwanafunzi kuchagua miradi isiyoweza
kuingiliana na muda wake wa masomo wala kumpa stress za kupata hasara kwa
urahisi, na hata ikitokea hasara uwekezaji wake ni mdogo mno kiasi cha kumpa
mwanafunzi msongo wa mawazo ashindwe kuzingatia vizuri masomo yake. Unaweza kubuni miradi mingine rahisi kulingana
na mazingira yako uliyopo.
Kitu kingine mwanafunzi anachoweza kukifanya angali
shuleni ni kutengeneza mtandao wa mawasiliano mazuri (networking) na watu
mbalimbali wanaoweza kuwa msaada kwake siku za baadae. Nasema mawasiliano
mazuri kwani kuna mawasiliano au mahusiano mengine ni haramu kwa mwanafunzi na
yanayoweza kumtumbukiza kwenye majanga mfano mapenzi nk.
SOMA: Ushauri kwa mwanafunzi aliyehitimu chuo/masomo anayetaka kuanza maisha
Mfano nakumbuka tulipokuwa sekondari kuna rafiki yangu
mmoja alikuwa anapenda sana kuandikiana barua na marafiki wa nje ya nchi
(ughaibuni) wengine walimtumia zawadi mbalimbali mpaka wakati mwingine fedha za
malipo ya ada. Mwishowe alipata rafiki wa kike nchini Sweden ambaye kwao
walikuwa matajiri sana akamtumia mwaliko wa kwenda kuishi na kusoma hukohuko
elimu yake ya chuo Kikuu. Alihama UDSM na kwenda Sweden ambako mpaka hivi leo anafanya
kazi hukohuko na walikuja kuoana na yule msichana.
Simaanishi wanafunzi watafute wachumba mitandaoni hapana,
bali wajenge mahusiano mazuri yenye malengo ya kuongeza zaidi uelewa wao kwa mambo
mbalimbali yanayoendelea duniani ikiwa ni pamoja na fursa za kiuchumi
wanazoweza kuja kuzifanyia kazi hapo baadae wakimaliza kusoma. Uzuri siku hizi
mtandao wa Intaneti na akili bandia vimerahisisha mno watu kuwasiliana na
kupata taarifa nyingi kwa muda mfupi
.............................................mwisho.....................................
OFFA
MPYA KWA MWAKA 2024 (VITU 14)
Kifurushi cha Offa iliyopita kilikuwa na vitu 12 tu
lakini hiki kina vitu 14, vitu vinaweza vikapunguzwa au offa kuondolewa muda
wowote ule hivyo kwa watakaowahi itakuwa bora zaidi kwao. Huu ni mchanganyiko
wa vitabu na michanganuo ya biashara mbalimbali iliyokamilika.
MALENGO
YAKE:
1.
Kifurushi hiki kinalenga kumfanya
anayekichukua kujifunza michanganuo ya biashara kwa kina kabisa ikiwa ni pamoja
na kujiandalia mwenyewe mpango wa biashara yake bila kuhitaji usaidizi wowote.
2.
Unapojua kuchanganua biashara maana yake
umejifunza biashara kwa ujumla wake kwani mchanganuo kamili wa biashara ni
jumla ya vipengele vyote vinavyoihusu biashara kuanzia bidhaa/huduma mpaka soko
na mpango mzima wa fedha.
3.
Kinalenga pia mtu yeyote mwenye ndoto ya kuwa
mtaalamu aliyebobea katika uandaaji wa michanganuo ya biashara kwa
wafanyabiashara wengine kama ilivyokuwa mimi mwenyewe, tazama hapa >KAZI ZETU , baadhi ya
michanganuo niliyokwishawaandikia makampuni na biashara binafsi za watu mbalimbali
VIGEZO
NA MASHARTI YA KUKIPATA KIFURUSHI HIKI:
· Unalipia
shilingi elfu 10 tu badala ya shilingi elfu 90 ukinunua kimoja kimoja na
utatumiwa papo hapo kila kitu katika simu au kompyuta yako
· Unapata
fursa ya kuunganishwa Mastermind group la whatsap kwa ajili ya mentorship na
masomo yenye maudhui ya fedha yasiyopatikana mahali pengine popote. Tuna masomo
zaidi ya 100 na mwanachama utahakikisha unayapata yote 100 kabla ya muda wa
group kuisha (miezi 12). Masomo haya humpa mtu uelewa mpana wa suala la fedha
na saikolojia nzima inayolizunguka katika kuondoa na kuvunja imani potofu
zinazomfanya mtu kutokusonga mbele
· Ndani
ya group kutakuwa na semina za kuandika michanganuo mifupi ya biashara zenye
ubunifu wa hali ya juu kwa ajili ya kutengeneza na kukuza mitaji haraka kwa
wajasiriamali wale wasiokuwa na sifa za kukopesheka na taasisi kubwa za
kifedha.
· Kaulimbiu
yetu kwa mwaka huu wa 2024 ni; UBUNIFU NA AKILI BANDIA, VITUMIE KUBOOST
BIASHARA YAKO VIWANGO VINGINE. Kwahiyo ukiwa ndani ya kundi hili
utakuwa ukishiriki moja kwa moja katika kuhakikisha kauli hii unaitimiza kwa
vitendo ili kuondoa kabisa vikwazo vinavyokudumaza siku zote usipige hatua
ikiwemo suala zima la mtaji na rasilimali nyingine muhimu za kufanikisha
biashara Dunia ya leo.
Haiwezekani kuanzisha
biashara yeyote bila ya kuwa na mpango wa biashara hiyo kichwani au kwenye
makaratasi, njoo ujifunze mbinu za kuweka mpango wa biashara yako yeyote ile na
si lazima uandike makumi ya kurasa, unaweza kuuweka mpango wako huo kichwani tu
na ikatosha kuendesha biashara yako kwa ufanisi mkubwa.
KUFANYA MALIPO KWA OFFA HII
TUMIA MOJA KATI YA NAMBA ZETU 2 HAPA CHINI;
0712202244
AU 0765553030
Jina ni;
PETER AUGUSTINO TARIMO
VITU
14 VYA OFFA NI HIVI HAPA CHINI:
1.
KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu
za BIASHARA, jinsi ya kuandaa
michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika
kila kitu. – kwa Kiswahili
2.
KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 tu - kwa kiswahili
3.
KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri
Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili
4.
KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN ni maarufu sana duniani, hutumika
vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza
5.
KITABU: Siri za upishi wa chapati
laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili
6.
COMPILLATION: Masomo 30 ya fedha
usiyoweza kuyapata popote, mengine 70 utayapata kwenye group kila siku - kwa Kiswahili
7.
MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji
Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili
8.
MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane
Restaurant –kwa
kiingereza
9.
MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane
Restaurant –kwa Kiswahili
10. MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji- kwa kiswahili
11. MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini
Broilers –kwa kiingereza
12. MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini
Broilers –kwa kiswahili
13. MCHANGANUO: Kiwanda cha mvinyo na juisi ya Rosella –Choya Investment – kwa kiswahili
14. MCHANGANUO: Kilimo cha Tikiti maji:- Kibada Watermelon Fruits – kwa kiswahili
Simu/Whatsap:
0712202244
AU 0765553030
0 Response to "BIASHARA & UWEKEZAJI MWANAFUZI ANAWEZA KUANZA AKIWA CHUO, KIDATO CHA 5, 1, DARASA LA 1 HATA CHEKECHEA "
Post a Comment