ELIMU YA FEDHA NA UMUHIMU WAKE 2019 NJOO TUUNGANISHE NGUVU TUHAMISHE MILIMA! | JIFUNZE UJASIRIAMALI

ELIMU YA FEDHA NA UMUHIMU WAKE 2019 NJOO TUUNGANISHE NGUVU TUHAMISHE MILIMA!


Elimu ya fedha ni uwezo wa kuelewa jinsi fedha zinavyofanya kazi, jinsi mtu anavyoweza kupata pesa, jinsi ya kusimamia na kutunza fedha, jinsi ya kuwekeza fedha na jinsi ya kutumia fedha. Kila mtu anapaswa kufahamu kwa undani elimu hii ya pesa namna pesa inavyofanya kazi na jinsi pesa inavyoweza kumfanyia kazi hata ikiwa amelala usiku kwa njia ya kuiwekeza katika miradi inayoweza kumzalishia faida mfano katika masoko ya hisa, masoko ya mitaji au hata kwenye miradi na biashara nyingine kama za ardhi na majengo.

Ili kuielewa vizuri pesa na namna inavyofanya kazi ni vyema mtu akafahamu kwanza kanuni zile za msingi za fedha kama vile; Malengo ya kifedha, Bajeti, Uwekezaji, Mafao ya uzeeni, Mikataba na mifumo ya ajira.

SOMA: Kama fedha haijawahi kuwa rahisi kupatikana, kwanini uchezee pesa?

Tafiti mbalimbali zilizowahi kufanyika kuhusiana na uelewa wa watu wa pesa  zimeonyesha kwamba watu wengi wakiwemo Wajasiriamali na Waajiriwa hawana elimu ya msingi ya fedha wala uelewa wa dhana mbalimbali zinazohusiana na pesa hata zile za kawaida kabisa kama vile mikopo, riba na uwekaji wa akiba, hii huwafanya wengi wao kuogopa mno kukopa kwa ajili ya kuwekeza katika miradi jambo linalowafanya wengi kufa masikini.

Aidha kwa upande wa watumiaji wa bidhaa mbalimbali za kifedha kama vile mikopo na mifuko ya mbalimbali ya hifadhi ya kijamii huwa hawajishughulishi na kutafuta taarifa za kifedha kabla hawajafanya maamuzi yao mbalimbali ya kifedha, huishia kukosa uwezo wa kuchagua na kusimamia mikopo au mafao yao kikamilifu, kutokuweza kupanga biashara zao au kushindwa kupanga maisha yao baada ya kustaafu. Wastaafu wengi hukosa taarifa kuhusiana na akiba na uwekezaji kwa ajili ya kustaafu, wanashindwa kupanga kabla  na kuamua kuchukua hatari za kifedha  pasipo kujua.

SOMA: Je, kukopa ili ukalipe deni la zamani kunawezaje kuboresha mzunguko wa fedha kwenye biashara yako?

Tatizo la madeni ni kubwa kwa watu wengi kwasababu ya kutokuwa na elimu ya fedha na kundi linalokabiliwa na tatizo hili ni vijana zaidi kuliko wale walio ana umri wa makamo au wazee. Elimu ya kutunza  fedha inaweza kuwanufaisha makundi ya watu wa rika zote na vipato. Kwa vijana ambao ndio kwanza wanaanza maisha inaweza kuwapa uwezo wa kubajeti na kujiwekea akiba itakayowawezesha kudhibiti matumizi yao na madeni.

Maarifa ya msingi ya fedha pia yanaweza kuzisaidia familia kuwa na nidhamu ya fedha itakayowawezesha kujiwekea akiba kwa ajili ya elimu ya watoto wao au maendeleo mengine ya familia. Inaweza kuwasaidia wafanyakazi wazee kuhakikisha kwamba wanakuwa na akiba ya kutosha kwa ajili ya kustaafu raha mustarehe pasipo kuhofia kikokotoo hatimaye kuchanganyikiwa bure kunakoweza kuwapa magonjwa ya moyo na kiharusi kwa kuwapa mbinu na taarifa zitakazowawezesha kuchagua uwekezaji unaofaa katika pensheni na mipango mingine ya akiba.

SOMA: Njia 6 za kuondoa woga na stress za fedha katika maisha yako.  

Elimu ya fedha inaweza ikawasaidia watu wa kipato cha chini kufanya kila linalowezekana katika kujiwekea akiba itakayowasaidia kuepukana na mikopo yenye riba kubwa inayotolewa na taasisi au watu binafsi nje ya mifumo rasmi ya kibenki.

Kiwango cha mtu cha Elimu yake kifedha huathiri kwa kiasi kikubwa ubora wa maisha yake. Huathiri uwezo wake wa kujipatia mahitaji yake lakini na ya familia yake pia, mwelekeo wake kwenye pesa na uwekezaji pamoja na mchango wake kwa ujumla kwenye jamii nzima inayomzunguka, hivyo kuipata elimu hiyo ni sawa na hazina itakayodumu daima na haiwezi kuharibiwa kirahisi.

SOMA: Download(pakua) kitabu hiki cha elimu ya pesa na mafanikio bure mtandaoni.

Uelewa wa pesa humfanya mtu afahamu ni kitu gani kinachohitajika kufanyika ili kufikia maisha endelevu yenye maadili, uwajibikaji na uhuru wa kifedha. Humsaidia mjasiriamali pia kutumia fedha za watu wengine kama nyenzo ya biashara ya kutengeneza MAUZO na FAIDA.

2019 Njoo Tuhamishe Milima!
Siri hii sikupenda kabisa kuitoa kiholela kwa kila mtu kwani nahofia sana washindani wangu kibiashara kuikopi na kuitumia, makundi mengine ya wasap na hata yale ya facebook. Si unajua tena huku mitandaoni, huwezi kuwa na hatimiliki ya mbinu uliyobuni kirahisi inayotekelezeka kivitendo. Siri hiyo ni mfumo tunaoutumia katika uendeshaji wa GROUP letu la masomo ya kila siku, mijadala na Seminars za mara kwa mara, MICHANGANUO-ONLINE.

SOMA: Semina 12 za kuandika michanganuo ya biashara za kipekee zenye fursa kubwa ya kutengeneza faida.

Tumeamua kutumia mtindo uliowahi kutumika na Mabilionea wakubwa wengi duniani(MASTERMIND GROUP), ni vigumu kukuelezea jinsi mfumo huu unavyofanya kazi kwa maneno matupu ukaelewa labda tu kama unajiunga ndiyo utaweza kunielewa kikamilifu. Ni hivi, Kwanza hatuna kocha, kiranja wala mentor yeyote ndani ya group letu, admini yupo tu kwa ajili ya kuwezesha (kufacilitate) wanaoingia na wanaotoka au wanaotaka kubadilisha namba zao. Kila mtu ana nafasi sawa ya kumuelimisha na kumshauri mwenzake.

Tunaishi kistaarabu kupita kiasi, hakuna matusi isipokuwa utani na vichekesho havizuiwi, kazi kubwa ni moja tu, kujifunza elimu ya fedha, uwekezaji, Business plans na ujasiriamali kwa ujumla. Tunashea vitu vingi vya thamani ambavyo mtu peke yako ingelikugharimu muda mwingi na hata fedha kuvipata, documents na hata vitabu mbalimbali vizuri. Wadau ni watu kutoka tasnia mbalimbali wengine wamebobea katika fani zao na hukubali kushea mambo bila uchoyo.

Maajabu haya ya kundi kushirikiana kwa kufuata kanuni nilizozitaja na nyingine ambazo siwezi kuziweka wazi kwa sababu za kibiashara, ndizo zinazotufanya kuwa group la kipekee zaidi nchini Tanzania linalooperate si tu kwenye wasap bali pia kupitia email kwani si kila mtu hutumia wasap na wote hupata masomo yote na semina tunazofanya.

SOMA: Kwanini kundi la kushauriana(Master mind group) ni muhimu kwa kila anyetafuta mafanikio?

Kushirikiana kuna faida nyingi siyo katika group kama hili tu, hebu tazama Mataifa makubwa mfano Marekani, Umoja wa Ulaya na hata Urusi kabla ya kusambaratika(Soviet Union). Marekani kwa mfano jeuri yake yote inatokana na muunganiko wa nchi zaidi ya 50(States). Tumeona Ulaya jinsi Uingereza na kiburi chake inavyoanza kutaharuki hata kabla ya BREXIT yenyewe. Unaikumbuka Usovieti? Superpower pekee iliyoweza kuitikisa Marekani ikashika adabu, zilikuwa  nchi 15.  Hatujui pengine kama Putin anaweza akarudisha Soviet nyingne kwa kuamua kuungana na Iran, Uchina na Baadhi ya mataifa mengine ya Mashariki, hatujui, muda ndio utakaoamua.

SOMA: Mafanikio makubwa ya Henry Ford yalianza pale alipoanza ushirikiano na matajiri wengine.

Nimeeleza hayo yote ili kuonyesha jinsi ambavyo ushirikiano ulivyokuwa na nguvu ya ajabu, kidole kimoja hakivunji chawa, Mnapokuwa wengi mnaweza kufanya mambo makubwa yanayoweza yakalinganishwa na mlima, hebu jaribu kufikiria jinsi mlima ulivyo, halafu uambiwe mlima huo uuhamishe ukiwa peke yako, je utaweza? itakuchukua miaka mingapi? Lakini mkiwa wengi sina shaka utahama, tena ndani ya kipindi kifupi tu. 2019 NJOO JIUNGE NASI KATIKA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE NA KWA PAMOJA TUTAHAMISHA MILIMA!

Ujumbe wangu wa mwisho kwako(ikiwa hujajiunga lakini) katika mwaka huu wa 2018 nataka nikuambie hivi;

“Ukitaka mahali sahihi zaidi utakapoweza kupata elimu ya pesa mtaani(nje ya mfumo rasmi wa shule) kwa gharama rafiki zaidi kuliko sehemu nyingine yeyote usihangaike, bali njoo Michanganuo-online, nakuhakikishia utapata kila kitu unachohitaji katika kutengeneza maisha yako upya kifedha”

Kujiunga Lipa ada yako sh. Elfu 10 kupitia namba 0765553030  au 0712202244, jina ni Peter Augustino Tarimo.

Baada ya malipo, tuma ujumbe wasap au sms usemao, “NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE”

Wasap: 0765553030

Ikiwa hutumii wasap hamna shida, tuma anuani yako ya email tutakayokutumia masomo na semina zote pamoja na updates kila zikitokea.

0 Response to "ELIMU YA FEDHA NA UMUHIMU WAKE 2019 NJOO TUUNGANISHE NGUVU TUHAMISHE MILIMA!"

Post a Comment