MAFANIKIO MAKUBWA YA HENRY FORD YALIANZA PALE ALIPOANZA USHIRIKIANO NA MATAJIRI WENGINE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MAFANIKIO MAKUBWA YA HENRY FORD YALIANZA PALE ALIPOANZA USHIRIKIANO NA MATAJIRI WENGINE


FIKIRI UTAJIRIKE THINK AND GROW RICH SEHEMU YA II
Nishati ndiyo msingi wa asili, ambao kutoka kwake asili hutengeneza kila kitu kilichopo Ulimwenguni, akiwemo binadamu na kila aina ya wanyama na maisha ya mimea. Kupitia mchakato wa asili ambao ni asili tu inayoufahamu kikamilifu unaigeuza nishati kuwa maada.

Viasili vya uumbaji hupatikana kwetu katika nishati inayohusika katika kufikiria. Ubongo unaweza ukafananishwa na betri ya umeme. Hunyonya nishati kutoka angani, ambayo husambaa katika kila atomu ya maada na na kujaza Ulimwengu mzima. Kundi la betri za umeme zitatoa nishati kulingana na idadi na uwezo wa seli zilizokuwa nazo. Ubongo hufanya kazi kwa namna inayofanana.

Hii ni sababu ya baadhi ya ubongo(akili) kuwa na ufanisi kushinda nyingine, na kusababisha kauli hii muhimu – kundi la akili(ubongo) zilizoratibiwa(au kuunganishwa) katika roho ya masikilizano litatoa nishati nyingi zaidi ya mawazo kuliko ubongo mmoja kama tu ilivyo kwa kundi la betri za umeme zitakavyotoa nishati zaidi kushinda betri moja. Kupitia huu mfano mara moja inakuwa dhahiri kwamba kanuni ya ushirika hubeba kanuni ya nguvu iliyotwaliwa na watu ambao hujihusisha wenyewe na watu wenye akili.

Inafuata sasa kauli nyingine ambayo itaongoza bado karibu na uelewa wa kiroho wa ushirika: Kundi la akili za watu linaporatibiwa na kufanya kazi kwa masikilizano, nishati ya ziada inayotengenezwa kupitia ushirika huo hupatikana katika kila ubongo(akili) ya mtu mmojammoja ndani ya kundi hilo.

Henry Ford alianza biashara yake akiwa na kilema cha umasikini, kutokuwa na elimu na ujinga. Ndani ya kipindi kifupi kisichofikirika cha miaka 10 Bwana Ford alivishinda vilema hivi vitatu, na ndani ya miaka 25 aliweza mwenyewe kuwa mmoja wa watu matajiri zaidi Marekani. Unganisha na ukweli huu ujuzi wa ziada kwamba, hatua za haraka alizopiga Bwana Ford zilianza kuonekana tokea muda alipoanza urafiki na Thomas A. Edison na utaanza kutambua athari ambazo ubongo mmoja unaweza ukawa nazo dhidi ya mwingine.

Nenda hatua moja zaidi na zingatia ukweli kwamba, mafanikio makubwa ya Bwana Ford yalianza tokea muda alipoanza kufahamiana na Henry Fireston, John Burroughs na Luther Burbank(kila mmoja akiwa ni mtu wa akili yenye uwezo mkubwa) na utakuwa na ushahidi zaidi kuwa nguvu hiyo inaweza ikapatikana kupitia ushirikiano wa kirafiki wa ubongo(akili). 

Itaendelea......

 UKITAKA KUSOMA SEHEMU NA SURA ZILIZOPITA FUNGUA HAPA





Usikose somo la leo 20/8/2019 usiku saa3 katika Group letu la Whatsap na mada itakuwa ni;


“KUFIKIA NDOTO NA MALENGO YAKO, HIZI HAPA NI HATUA 3 ZA KUTENGENEZA BAJETI YA JAMBO LOLOTE  MAISHANI”

Masomo ni kila siku, kujiunga namba ya wasap ni 0765553030 *kuna kiingilio sh. 10,000/-*

0 Response to "MAFANIKIO MAKUBWA YA HENRY FORD YALIANZA PALE ALIPOANZA USHIRIKIANO NA MATAJIRI WENGINE"

Post a Comment