NJIA 6 ZA KUONDOA WOGA NA STRESS ZA FEDHA KATIKA MAISHA YAKO. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NJIA 6 ZA KUONDOA WOGA NA STRESS ZA FEDHA KATIKA MAISHA YAKO.

mawazo na wasiwasi wa pesa
Katika mfululizo wa masomo ya mzunguko wa fedha kwenye group la whatsap la MICHANGANUO-ONLINE mwaka huu wa 2018 unaomalizika sasa niliwahi kutoa somo jingine  lililosema. Stress za fedha zinavyoweza kuzima kabisa ndoto zako na hatua za kuchukua haraka. Somo hilo la aina yake na lililopendwa sana na watu linaweza kushabihiana kidogo na hili la leo lakini ni masomo 2 tofauti kabisa.

Kabla hatujakwenda kuona kipekee kabisa, njia hizo 6 zenye nguvu zinazoweza kukuondolea kwa asilimia kubwa woga na stress zinazoambatana na matatizo kifedha, ningependa kwanza kuzungumzia kwa ujumla (in general) jinsi ya kukabiliana na tatizo hili nikiwa namaanisha Utambuzi katika maswala ya fedha(money consciousness).

Uelewa katika maswala mbalimbali muhimu yahusianayo na fedha bila shaka ndiyo njia kubwa ya jumla ya kupunguza stress na wasiwasi kifedha ingawa pia mtu unatakiwa kuzama ndani zaidi na kufahamu kwa kina ufanye kipi na kuacha kipi kama tutakavyoelezea katika njia hizo 6 leo hii.

SOMA: Njia 7 halali na nzuri za kupata mafanikio & utajiri wa haraka

Utambuzi wa masuala ya pesa ndiyo chanzo cha wewe leo hii kuwa unasoma somo hili hapa, pia ndiyo sababu kubwa ya wataalamu wa biashara, makocha na walimu mbalimbali wa ujasiriamali na uchumi duniani kufungua madarasa, kuanzisha blogs na tovuti, magroup ya wasap na facebook, vyote vikiwa na lengo moja tu la kuelimisha watu juu ya PESA. Ndiyo hata iliyonisukuma na mimi kuanzisha Group mahsusi la stori na masomo yanayohusu pesa kama hili unalosoma sasa. Kwa mwaka huu wa 2018 wote tangia mwezi Januari tumekuwa tukijifunza masomo mengi sana ya mzunguko wa fedha na ambayo tayari tumekwishayatengenezea vitabu vizuri 3.

Kujitambua kifedha huhusisha mambo mengi na kwa asilimia kubwa tulishayajadili katika masomo yaliyopita kuanzia kubajeti fedha zako, kujua unatumia kiasi gani cha fedha kila siku, kufahamu unamiliki mali kiasi gani(your networth), kulijua vizuri soko lako pale bei inapopanda na kushuka pamoja, kujiamini zaidi wakati unapofanya maamuzi makubwa kifedha pamoja na kila kitu mtu unachoweza kufanya kila siku kuhusiana na pesa.

SOMA: Wasomi na watu waliofanikiwa hawaachi kujifunza.

Zijue sura mbili za pesa, upande wa mahesabu(namba) na upande wa Saikolojia.
Uelewa katika masuala ya fedha umegawanyika katika sehemu kuu 2, namba na saikolojia. Kuwa na uelewa wa pesa kisaikolojia ni muhimu hata kushinda kuwa na uelewa wa pesa kimahesabu(namba), ingawa mtu unapaswa kuwa na uelewa wa msingi katika pande zote mbili, saikolojia na namba.

Ingelikuwa uelewa wa pesa unategemea namba tu peke yake kama vile kukokotoa faida na hasara, majedwali na chati basi watu wengi wangeliogopa sana pesa na wasomi tu peke yao ndio ungekuta wanamiliki utajiri mkubwa kote duniani. Lakini hapana haiku hivyo kwani hata wale wanaotoa elimu ya pesa kama mimi hapa bado nao kila siku tunanastruggle kusaka pesa. Donald Trump, Warren Buffet, Robert Kiyosaki, Reginald Mengi na wengine kibao bado utakuta wanaendelea kutafuta pesa hawabweteki na katika safari yao kuna mahali hupata hasara au biashara kutoenda vizuri.

SOMA: Siri ya matajiri na watu waliofanikiwa kimaisha.

Ni nini basi wanachokifanya kila siku pamoja na kwamba tayari wamebobea kwenye upande wa namba au mahesabu ya pesa? Jibu ni, HUJIPATIA UTAMBUZI WA KIFEDHA KILA SIKU HASA KATIKA UPANDE ULE WA KISAIKOLOJIA. Kasome kitabu cha Dr. Reginald Mengi, I CAN I MUST I WILL utaelewa vizuri ninachotaka kukizungumzia hapa au kitabu chochote kingine kinachoelezea namna ya kufanikiwa kifedha kama vile OUTLIER cha Malcolm Gladwell, THINK AND GROW RICH cha Napoleo Hill, SECRETS OF THE MILLIONAIRE MIND cha Harv Eker na vingine vingi.

Wasiwasi na Stress za pesa hutokana na nini?
Jibu rahisi ni Kukosa tu utambuzi kifedha, basi.

Unapokosa utambuzi wa kutosha wa kifedha wasiwasi na stress havikuishi kamwe. Muda wako mwingi utajikuta ukiutumia katika kuogopa kusikokuwa na mashiko. Utakuwa ukihofia kila mara kukumbwa na matatizo ya fedha mengine wala hayana mpango wa kutokea.

SOMA: Usiogope, mabadiliko ya maisha ni kama plasta ikishabanduka kidonda hupona chenyewe.

Unaweza kukaa mahali ghafla ukaanza kuwaza ugumu utakaoupata ikiwa utapatwa na ugonjwa unaohitaji fedha nyingi kuutibu, kwa kuwa kipato chako ni cha wasiwasi basi na akili yako haiishi wasiwasi. Utafikiria ni kwa namna gani utaweza kulipa gharama mbalimbali kama ada za watoto za shule wakati hata pengine watoto wenyewe hawajaanza shule. Utalipa vipi pango la nyumba, utakula nini nk. Na unawaza tu pasipokuwa na njia yeyote mbadala ya kukabiliana na wasiwasi huo.

Lakini kumbuka kuwa muda huo mwingi unaoutumia kufikiria ungeweza kuutumia katika kufanya shughuli chanya za kukuingizia kipato cha kutatua matatizo yako. Inasemekana katika tafiti kuwa masikini tunatumia muda mwingi zaidi katika stress na wasiwasi kuliko muda ule tunaoutumia kuzalisha mali.

SOMA: Kwanini vitabu vya elimu ya pesa na mafanikio haviwasaidii watu wengi?

Kujifunza elimu ya pesa na kuweka vizuri mipango yako ya baadae ya fedha pasipo jukumu hilo kumpa mtu mwingine yeyote hata ikiwa ni mtaalamu vipi ndio njia muafaka zaidi ya kupunguza na hatimaye kuondoa kabisa wasiwasi na stress za fedha ingawa wakati unajifunza unaweza kuhitaji wataalamu, mamentor na hata makundi kama hili la kwetu la MICHANGANUO-ONLINE na mengine mengi.

Ndio maana katika group letu tunasisitiza kwamba wasiwasi katika maswala ya kifedha kila mtu huwa nao ila woga huo usiuruhusu kuchukua muda wako mwingi, upe angalao dakika 2 mpaka 5 kisha muda mwingi uliobakia wewe CHAPA KAZI!


NJIA ZENYEWE 6  ZA KUONDOA WOGA NA STRESS ZA FEDHA KATIKA MAISHA YAKO.

Njia hizi 6 tunazokwenda kujifunza hapa zote ni za kivitendo siyo tu za mtindo wa, "usifanye hivi au fanya vile" hapana, ni njia zinazokutaka uchukue hatua fulani za kivitendo(action plans) na utakapotekeleza vitendo hivyo kweli utaona ukiachana na waiwasi na stress zilizokuwa zikikutesa juu ya fedha.................................


Mpendwa msomaji wa blogu hii, unaweza kupata sehemu iliyobakia ya somo hili la kwanza kabisa la fedha kati ya 30 kwa mwezi huu wa 12 utakapojiunga na group la MICHANGANUO-ONLINE kwa kiingilio cha sh. Elfu 10.

Si kusudi langu kuu kukatisha masomo ninayoyaweka katika blogu hii isipokuwa tu kwa yale machache tunayoyatoa katika Group la kulipia la whatsapp kama somo hili na lengo kubwa ni kupata wale wasomaji waliokuwa  na nia ya thati ya kujifunza kwa kiwango cha juu zaidi, sina maana kuwa wengine hawana nia hapana, najua wapo wengine wenye nia lakini uwezo wa kutoa ada ya kiingilio ni changamoto kwao na ndio maana naendelea kuweka makala nyingi zisizokuwa za kulipia kwa kundi hili ili watakapopata uwezo basi waweze kujiunga.

Kuanzia leo tarehe 1 Disemba, hadi tarehe 30, tuna siku 30 mwaka 2018 umalizike. Kwa siku hizo zote 30 nimeandaa masomo 30 ya pesa, ninaposema masomo ya pesa ni masomo ya pesa kwelikweli na wala siyo ubabaishaji. Kama ulisoma vitabu 3 vya  masomo kama haya tuliyojifunza kwenye group tokea mwezi January unaweza ukaelewa namaanisha kitu gani.

Nikukumbushe tu ndugu msomaji, kama ulikuwa hujajiunga na program yetu hii itakayoisha mwezi huu mwishoni, tafadhali lipia shilingi elfu 10 ili uweze kutumiwa program yote yenye vitu(items) zaidi ya 12 vikiwemo vitabu, seminars, michanganuo na masomo mbalimbali tuliyojifunza kwa mwaka mzima ndani ya group. Kumbuka offa hii itadumu siku 30 tu na baada ya hapo haitakuwepo tena, tutaanza programu mpya ya mwaka 2019

Ikiwa hutumii wasap hamna tatizo kwani unaweza ukatumiwa masomo yote kupitia email yako. Vilevile faida utakayopata ukilipia kipindi hiki ni kwamba unajihakikishia nafasi ya kushiriki masomo yote ya mwaka 2019 kwani idadi ya wana group karibu itafikia ukomo wake, group huchukua wastani wa watu 250 tu na hatutakuwa na muda wa kuendesha magroup 2 kwa wakati mmoja. Nitakuwa nakukumbusha kila siku kwa siku zote 30, kusudi usijekusema hukujua

Namba za kulipia ni, 0712202244  au  0765553030

Unaweza pia kupata vitabu vyetu mbalimbali, fungua ukurasa huu hapa, Smart books tz

0 Response to "NJIA 6 ZA KUONDOA WOGA NA STRESS ZA FEDHA KATIKA MAISHA YAKO."

Post a Comment