Kufanya muujiza katika jambo lolote lile maishani
hakuhitaji mtu kuwa na kitu cha pekee sana zaidi ya kuwa na mabadilio ya
kifikra. Unapoamua kubadilisha mtazamo wako kuelekea jambo fulani basi hapo
ndiyo umeanza kutenda muujiza na jambo ambalo hapo kabla ulikuwa ukiliona ni
gumu haliwezekani kabisa sasa linawezekana.
Watu wote waliowahi kufanya miujiza wakiwemo hata Mitume
na Manabii mbalimbali, miujiza hiyo ilianzia kwenye mawazo. Nitatoa mifano
ingawa kwa leo sitatumia mifano ya mitume na manabii katika vitabu vitakatifu,
mifano hiyo tutaitafutia siku nyingine kutokana na sababu kwamba ni mingi na inabidi niweze kupitia karibu vitabu vyote
vitakatifu vya dini na madhehebu yote makubwa duniani.
Hapa tutaangalia mifano ya miujiza iliyowahi kufanywa na
wagunduzi wakubwa 3 duniani ambao vitu walivyogundua kwa hakika mpaka karne
nyingi zijazo vitabakia kuwa ndiyo vitu vilivyoibadilisha Dunia yetu hii kwa
kiasi kikubwa sana na kuonekana kama vile ilivyo sasa. Maendeleo makubwa yote
ya Kisayansi na Kiteknolojia msingi wake mkuu unatokana kwa kiasi kikubwa na
uvumbuzi wao. Sisemi mchango wa wagunduzi wengine ni mdogo hapana bali hawa
waligundua vitu vya msingi zaidi.
Thomas Edison, Alexander Graham Bell na ndugu wawili
Wright Brothers ndio nitakaozungumzia ‘miujiza’ yao leo. Thomas Edson aligundua
mamia ya vitu lakini vilivyompa umaarufu
mkubwa zaidi ni taa/balbu ya umeme tunayoitumia hadi leo, spika za redio. Sementi
ya kujengea na betri za magari za alkaline.
Alexander Bell aligundua Simu zile za waya ambazo kanuni
yake ndiyo hiyohiyo imeendelezwa mpaka kufikia hizi simu za mkononi za kisasa
tunazotumia leo, aligundua pia gramophone, kifaa kilichotumika kurekodi na
kucheza sauti/muziki, muendelezo wake umefanikisha kuwepo kwa player za
santuri, cassettes na hata teknolojia nyinginezo za kisasa za kurekodi na
kucheza sauti katika makompyuta, simu nk.
Kwa upande wa ndugu wawili Wright Brothers, Orville na
Willbur Wright au ‘watoto wa mchungaji’
kama watu walivyopenda kuwaita, wao walifanya ugunduzi wa ndege hizi
tunazosafiria kwa mara ya kwanza kabisa.
Ingawa wagunduzi hawa wote 3 walikwishafariki dunia
kitambo zaidi ya karne moja iliyopita na waliishi pia katika nyakati tofauti
lakini kuna vitu fulani wanavyoshea vinavyowafanya kufanana kikubwa kikiwa,
kwanza wote ni wagunduzi wakubwa na pili ni kwamba vitu vyote walivyogundua
kuna wakati kabla ya ugunduzi wao vilikuwa ni mawazo matupu(ndoto) katika akili
zao.
Vitu vilivyokuwa mawazo matupu akilini mwao hatimaye
vikaja kubadilika na kuwa vitu halisi, mashine zilizo na uwezo wa kumrahisishia
binadamu kazi zake kwa kiwango cha hali ya juu kabisa.
Mwanzoni
katika akili zao walianza tu na mawazo madogo wakifikiria uwezekano wa kuwepo
kwa vitu hivyo, kisha mawazo hayo yaliongezeka kidogokidogo na kugeuka kuwa imani yenye nguvu. Na hatimaye basi
Imani hizo ndizo zilizosababisha wachukue hatua mbalimbali zilizowaletea uzoefu,
hali, watu na kila kitu kilichosaida wao kukamilisha ugunduzi wao.
Njiani walikutana na vikwazo vingi, mfano Edison
alipokuwa akigundua balbu ya umeme alifeli mara 9,999 kabla hajaja kufaulu mara
ya elfu 10, lakini mara zote alizoanguka katu hakukata tamaa mpaka muujiza
ulipotimia. Vivyo hivyo na ndugu wawili waliogundua ndege mwazoni walikumbana
na vikwazo vingi kikiwemo cha kukataliwa hatimiliki na serikali ya Marekani
ikawabidi wakauze ugunduzi wao Ufaransa. Pia walipata ajali kadhaa wakati wa
majaribio ya kuruka kiasi cha kuhatarisha maisha yako kwa kiasi kikubwa.
Kwahiyo mawazo au fikra ndiyo hatua ya mwanzo kabisa ya
kufanikiwa katika kila kitu ikiwa mtu ataamini katika kile anachokifanya huku
akikifanyia kazi kwa juhudi zote bila kukata tamaa. Mwisho wazo hilo litageuka
kuwa kweli. Zawadi kubwa kulio zote Mwenyezi Mungu aliyotupatia wanadamu ni
nguvu ya ajabu ya mawazo yetu kwani mawazo ndiyo hutuwezesha kubadilisha maisha
kutoka kushindwa mpaka ushindi, kutoka huzuni mpaka kuwa na furaha, kutoka
umasikini hadi utajiri kupitia tendo dogo tu la kubadilisha mtazamo wa mawazo
yetu.
Tatizo tu ni kwamba watu wengi hawafahamu wala kuamini
kwamba nguvu hiyo kubwa wanayo na wanaweza kuidhibiti.
Mwisho.
………………………………………..
Ndugu msomaji wangu mwezi huu tunahitimisha mwaka wa 2018
na kuukaribisha 2019. Ingependeza kama tungelizitumia siku hizi 30 zilizobakia
kufanya tathmini ya yale yote tuliyofanya kwa mwaka mzima lakini kwa upande
wangu nimefikiri niendelee kutuma makala hizi pamoja na kuweka masomo katika
group la wasap nikilenga hasa wale ambao hawakupata fursa ya kujiunga na programu
yetu inayoisha ya “MZUNGUKO WA FEDHA NDIYO NJIA BORA ZAIDI YA KUTIMIZA MALENGO
YAKO 2018”.
Kwa siku hizo 30 na nimeanza jana tayari kwenye group,
tutakuwa tukitoa somo moja lenye maudhui ya pesa kila siku huku nikikukumbusha
umuhimu wa kujiunga na programu hiyo kabla ya mwisho wake itakapofika Novemba
30. Nafanya hivyo kuepuka lawama zozote mtu anazoweza kuja kunipa hasa kwa wewe
ambaye huwa unafuatilia blogu hii. Kama unapenda makala hizi basi naamini zile
ninazotuma wasap zitakuwa nzuri zaidi kwako ndio maana nachukua hatua ya
kukuhamasisha kujiunga.
Ni sababu hiyohiyo pia iliyonifanya masomo na semina zote
za tangu mwezi Januari mpaka sasa nitengeneze vitabu maalumu 3(PDF) kwa ajili
yako. Vilevile kuna michanganuo ya biashara bunifu tuliyoandika hatua kwa hatua
na wadau wa group, vitabu na sasa masomo haya makubwa 30 kuhusiana na fedha
tutakayokwenda kujifunza kwa muda wa siku 30.
Kwenye Group somo tuliloanza nalo jana katika utaratibu
huu wa masomo 30 ya siku 30 lilikuwa linasema hivi; “NJIA 5 ZA KUONDOA WOGA NA STRESS ZA FEDHA KATIKA MAISHA YAKO”
Na leo hii tarehe 2 Desemba
2018 tutakuwa na somo jingine linalosema; “AINA
ZA BIASHARA UTAKAZOFANYA ILI KUPATA UHURU KAMILI WA KIFEDHA”
Ukitaka kujiunga na masomo
haya lipia kiingilio ambacho ni sh. Elfu 10 kisha tuma ujumbe wa kawaida au wa
wasap usemao; NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE”. Namba zetu za simu
ni 0765553030 au
0712202244 WHATSAP tumia 0765553030 na jina ni Peter Augustino
Tarimo.
Kumbuka baada ya Desemba 30,
offa ya programu hii itamalizika rasmi na tutaanza nyingine ya mwaka 2019.
Masomo yote ya mwaka 2018 pamoja na semina zake hazitakuwepo tena, Pia nafasi
katika group zilizobakia ni chache kufikia watu 250 hivyo nakusihi sana msomaji
wangu, usikose fursa hii adimu kama wewe ni mpenzi wa masomo haya.
0 Response to "HIVI UNAJUA UNAWEZA KUFANYA MIUJIZA HAPA DUNIANI UKIAMUA?"
Post a Comment