BIASHARA YA MGAHAWA WA CHAKULA, MCHANGANUO NA MTAJI MDOGO WA KUANZA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

BIASHARA YA MGAHAWA WA CHAKULA, MCHANGANUO NA MTAJI MDOGO WA KUANZA

BIASHARA YA MGAHAWA WA CHAKULA
Bila shaka yeyote ile, chakula ndilo hitaji la msingi la binadamu lililokuwa muhimu pengine kushinda mahitaji mengine yote duniani. Hii ina maanisha kwamba, pasipo kujali hali yeyote ile iwe ni ya kisiasa ama ya kichumi watu ni lazima wale kusudi waendelee kuishi. Kunaweza kukawa na vita au mdororo mkubwa sana wa kiuchumi, lakini haiwezekani watu kuishi bila kula.

Ingawa biashara ya chakula ina ushindani mkali sana, lakini ni biashara yenye faida nono mno endapo itafanywa kwa usahihi unaotakiwa. Zipo hoteli nyingi na migahawa, achilia mbali mama na baba lishe au kwa jina maarufu mama ntilie na baba ntilie, lakini bado mahitaji ya chakula hasahasa katika miji mikubwa kama Dar es salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha ni makubwa kupita kiasi.

Kama mtaji wako ni kidogo, huna mtaji wa kutosha kukodisha jengo au eneo la kufungua mgahawa wako, unaweza ukaamua kuanzisha biashara hii ya chakula nyumbani kwako na hata ikiwa nyumbani siyo eneo zuri wateja wanaloweza kuja na kulia pale, basi njia nyingine mbadala unaweza ukawa unawapelekea wateja wa chakula kule wanakopatikana kwa mfano katika maeneo yao ya kazi, majumbani au katika maeneo ya vyuo na shule.

Vyovyote vile iwe unao mtaji wa kutosha kufanya kila kitu wakati wa kuanza ama iwe huna mtaji wa kutosha kufanya kila kitu lakini hatua za kufuata ili kufungua biashara ya chakula au mgahawa ni zilezile hazitofautiani.

Zifuatazo hapa chini ni hatua au dondoo muhimu anazotakiwa kuzingatia  mtu yeyote anayeanzisha biashara ya chakula au mgahawa wa chakula;

1. Soko lako lengwa ni lipi?
Kabla hata haujatumbukiza senti yako moja ya mtaji kwenye biashara hii ya chakula, hakikisha unawafahamu vizuri wateja wako(soko utakalouza) Elewa tabia zao, wanapendelea kitu gani, umri wao na hata huwa wanakula mara ngapi kwa siku. Mambo hayo yote utayajua kupitia utafiti wa soko au kwa jina jingine upembuzi yakinifu (Jinsi ya kufanya utafiti wa soko ni somo lililopo ndani ya kitabu cha “MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI” na limefafanuliwa kila kitu pamoja na mifano)


2. Ainisha ni aina gani ya vyakula utakavyouza.
Bado hapa utategemea sana taarifa utakazozipata kutokana na utafiti wako wa soko(market survey) Kumbuka utafiti wa soko siyo lazima uufanye kitaalamu sana, zipo njia nyepesi na zimeainishwa vizuri tu katika kitabu cha Michanganuo ya biashara na Ujasiriamali. Ni lazima aina za vyakula utakavyouza ziendane na aina za vyakula wateja wako walengwa wanavyopendelea.

3. Andika Mchanganuo/mpango wa biashara yako ya mgahawa
Mpango wa biashara siyo dude kuuubwa!, linalotisha, kwa kifupi tu unaweza ukaorodhesha katika karatasi pointi zile muhimu zote zinazoihusu biashara yako kuanzia wazo la biashara, mtaji mpaka faida unayotarajia kupata kwa makisio mepesi, wala huhitaji kuwa sahihi kwa asilimia kubwa.

4. Tafuta mtaji.
Sasa umeshajua makadirio ya mtaji kutokana na mchanganuo mdogo uliofanya. Mtaji itategemea, unaweza ukatumia fedha zako mwenyewe kama unazo, au unaweza ukaenda kukopa kutoka kwa ndugu, jamaa, marafiki, saccos au taasisi nyingine yeyote ile itakayokubali kukukopesha. Unaweza pia ukauza mali yako ya thamani kama vito au kuweka rehani vyombo nk.ili kupata mtaji wa kuanzishia biashara yako ya chakula.


Kumbuka haiwezekani ukaendesha biashara ya mgahawa au chakula pasipo kuwa na fedha za kugharamia vitu kama, kodi ya jengo utakalofanyia biashara, malighafi(vyakula vibichi, matunda na mbogamboga), mishahara ya wafanyakazi, bima(kwani kitu kama moto unaweza ukazuka ghafla na kama huna bima ukala hasara kubwa) na gharama za masoko au matangazo.

5. Chagua eneo zuri.
Wakati unachagua eneo la kuweka biashara yako, zingatia sana vitu kama, wingi wa watu eneo hilo, sheria kutoka mamlaka za serikali za mitaa, kufikika kwa urahisi na wateja ikiwemo na parking ya magari, pango la nyumba na historia kwa ujumla ya eneo husika. Hii hasa ni kwa wale waliokuwa na mtaji mkubwa wa kutosha lakini kwa upande wa wale wenye mtaji kidogo kama nilivyotangulia kusema, wanaweza biashara hii wakaifanyia nyumbani na kusambaza vyakula kwenda maeneo ya jirani au maofisini na katika biashara za watu.

6. Tengeneza mandhari ya kuvutia ya mgahawa wako
Tenga maeneo mbalimbali kama vile, sehemu ya jiko, sehemu ya kulia chakula “dinning” stoo, sehemu ya kunawia mikono nk. Hakikisha madhari nzima ya biashara yako inakuwa ni yenye kuvutia.
MGAHAWA WENYE MANDHARI NZURI YA KUVUTIA
Mandhari ya kuvutia ya mgahawa.
7. Hakikisha unazingatia usalama kwa kuweka vifaa vya usalama kama vile vya kuzuia moto pamoja na bima. Kuwa pia na mwanasheria kwa ajili ya maswala yahusuyo sheria.

8. Kuwa na wasambazaji maalumu wa vifaa kama vyakula na matunda na mbogamboga, utakaowekeana nao mikataba ya kukusambazia vitu hivyo na uhakikishe bei watakazokuuzia ni za chini kwa kadiri inavyowezekana kusudi usipate hasara.

9. Nunua vyombo muhimu kama vile mafriji,viti, meza, majiko, oven, vifaa vya chipsi, sahani, bakuli, vijiko, sufuria nk.

10. Ajiri na kuwapa mafunzo wafanyakazi.
Ajiri meneja na wafanyakazi, wape mafunzo pamoja na kuwapangia kila mmoja jukumu lake sambamba na kupatana nao malipo kabla hawajaanza kazi.

11. Tangaza mgahawa wako.
Usipowajulisha watu, hamna mtu atakayefika kuja kula mgahawani kwako. Kuna njia nyingi unazoweza ukazitumia kutangaza kama vile, kusambaza vipeperushi kwa majirani, lakini ni vyema pia ukatengeneza mpango mkakati wa biashara au masoko utakaotumika wakati wa kutangaza biashara yako(Kitabu cha MICHANGANUO NA UJASIRIAMALI kimefafanua vizuri jinsi ya kuandika mpango mkakati wa biashara pamoja na mfano wa mpango mkakati wenyewe halisi)

Unaweza pia ukawatangazia majirani kwamba siku rasmi ya ufunguzi kutakuwa na chakula bure bila malipo, ukawagawia kila mmoja kuponi atakayokuja nayo kula. Wakisha kula watakwenda kuitangaza biashara yako vizuri sana kwa watu wengine.

12. Tanua biashara yako.
Wakati ukifika sasa wateja wameshakuwa wengi, hakikisha unakuwa na leseni na vibali vyote vinavyohitajika kwa ajili ya biashara ya mkahawa kwani sasa serikali itakuwa imeshaanza kutambua uwepo wako. Kama ulikuwa unafanyia nyumbani, ni wakati sasa wa kwenda kukodi jengo eneo kubwa au hata ikiwezekana unaweza ukabadilisha mgahawa wako kuwa hoteli.

………………………………………………………………….

Ndugu msomaji, kama wewe ni mpenzi wa biashara hii ya chakula, hususani mgahawa au hoteli, basi nakushauri usikose kujipatia kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NAUJASIRIAMALI ili usome kwa kina mchanganuo wa biashara ya mgahawa uitwao, JANE FAST FOOD. Agiza kitabu hicho kutoka kwangu kupitia namba za simu, 0712 202244  au  0765 553030 jina ni Peter Augustino Tarimo, na utaletewa kitabu cha karatasi mpaka pale ulipo kama unaishi Dar es salaam.

Kama upo Mkoani, mkoa wowote ule, tuma pesa shilingi 20,000/= pamoja na gharama za usafirishaji kupitia namba hizo hapo juu na nitakutumia kitabu kupitia basi linalofika kule ulipo.

Pia kitabu hiki kipo katika mfumo wa softcopy na naweza nikakutumia kwa njia ya E-mail. Chakufanya tuma pesa shilingi 10,000/= kwenye namba za simu zilizotajwa pale juu pamoja na anuani yako ya e-mail kwa meseji, kisha na mimi nitakurushia kitabu hiki kupitia email yako kama PDF. Kwa vitabu vingine zaidi na Michanganuo ya Biashara tembelea duka letu mtandaoni liitwalo SMART BOOKS TZ


BUSINESS PLANS / MICHANGANUO YA BIASHARA


Karibu, Tunaandika mpango wa biashara yeyote ile kwa ajili ya kuombea mkopo, kuwasilisha kwa wabia, wawekezaji na hata kwa ajili ya uendeshaji wenye tija wa biashara. Gharama zetu ni nafuu sana na tunakamilisha kazi kwa muda muafaka.

Ikiwa pia unapenda uandike mwenyewe na huna materials za kukusaidia tunavyo vitabu vizuri cha kiswahili na kiingereza, Templates/vielezo, Seminars na Samples au Michanganuo kamili iliyokuwa tayari unayoweza kufuatisha baadhi ya vitu wakati ukiandika wa kwako. Gharama ya package nzima ni rahisi sana na tunatuma kwa njia ya email kama softcopy

Kupata moja kati ya huduma hizo 2 za Michanganuo wasiliana nasi kwa namba, Whatsapp/call: 0765553030 au Simu/sms: 07122022446 Responses to "BIASHARA YA MGAHAWA WA CHAKULA, MCHANGANUO NA MTAJI MDOGO WA KUANZA"