MFANO WA MCHANGANUO WA BIASHARA(TEMPLATE) UNAPOTAKA KUANDIKA MPANGO WAKO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MFANO WA MCHANGANUO WA BIASHARA(TEMPLATE) UNAPOTAKA KUANDIKA MPANGO WAKO

Mfano wa mpango wa biashara
Sasa wale wanachama walio na ufunguo wa kuingia katika Darasa la Michanganuo ya Biashara(Tanzanaia Online School Of BusinessPlanning) wanaweza kudownload bure mfano wa mchanganuo wa biashara(Business plan Template) ya kiswahili ambayo mtu unapotaka kuandika mpango wa biashara yeyote ile, unajaza tu taarifa zako kuhusiana na biashara hiyo pasipo kuumiza kichwa sana kufikiria ni nini cha kuandika.


Template(kielezo) hicho kina sehemu zote zinazotakiwa kujazwa ili mchanganuo wa biashara ukamilike, pamoja na maelekezo muhimu yanayokuambia ni kipi cha kuandika katika sehemu husika. Ni rahisi sana kuandika mchanganuo wa biashara na katika muda mfupi kwa kutumia njia hii hasa ikiwa wewe haujawa mzoefu vya kutosha katika utayarishaji wa mipango ya biashara.

Template(mfano) upo katika fomati ya “word template” na una sehemu nane ambazo kila moja imegawanyika vijisehemu vidogovidogo ndani huku kukiwa na maelezo kwa lugha ya kiswahili. Wewe utajaza maelezo yanayofanana na kuendana na biashara unayotaka kuiandikia mpango wa biashara na ukishamaliza kuandika kila kitu unasave, basi umemaliza.

Darasa linaendelea na wanachama/wanafunzi katika ngazi ya Ordinary Level” wanaongezeka. Kama ulikuwa hujajiunga ni wakati wako sasa kufanya hivyo ikiwa upo ‘serious’ kweli na kupanga biashara yako. Mpango wa biashara utakusaidia mambo mengi ikiwemo kuijua biashara kwa kina hata kama hupendi kwenda kuombea mkopo.

Unapoelewa mtiririko mzima wa biashara unayoifanya kuanzia mtaji mpaka faida utakayopata, akilini unakuwa umeshajijengea picha ni kitu gani unachotaka kukifanya hivyo hautakurupuka tena na kufanya vitu kwa mtindo wa zima moto.

Ni kweli kabisa siyo kila utakachopanga kitaenda vilevile ulivyopanga hapana, ndiyo maana unatakiwa mpango wa biashara yako uufanyie marekebisho mara kwa mara kulingana na hali halisi inavyokuja kujitokeza. Hata kama yatatokea matukio usiyokuwa umeyatarajia utakabiliana nayo vizuri zaidi pasipo kukuchanganya akili.


Dhana ya mipango, asijekukudanganya mtu yeyote kuwa haipo, sijui ni kupoteza muda, mara mipango siyo matumizi, ni uwongo mtupu, hakuna binadamu asiyepanga ila kinachotokea hapa ni watu kuchukia dhana ya kupanga kwa sababu ni kweli matokeo mara nyingi hayawezi kuwa sawasawa na kile ulichopanga kwa asilimia 100%. Lakini ukweli utabaki palepale kwamba kupanga kuna faida zake na ni nyingi kushinda kutokupanga kabisa.

Hebu fikiria vitu hivi vifuatavyo kama kusingelikuwa na mipango ni nini kingelitokea?,

Vita: mpaka unaona majeshi yakilipua mizinga siyo uamuzi wa siku moja kama mtu anazima moto, ni maandalizi na mikakati ya siku, miezi na hata miaka kadhaa inayohusisha bajeti, rasilimali watu na kila kitu mfano wa vile uonavyo mtu akianzisha biashara.

Harusi: Ni moja ya vitu tunavyovipenda mno, na ukitaka kujua watu ni mahodari wa kutengeneza michanganuo(plans), basi hudhuria vikao vya harusi, unaweza ukasoma makala hii hapa, Ni nini kilichokuwa nyuma ya harusi nzuri ya kupendeza?

Chakula: Hivi ni kwanini nchi au hata mtu mmoja mmoja huamua kujenga maghala kwa ajili ya kuhifadhi chakula cha ziada asisubiri mpaka njaa itakapopiga hodi ndipo aanze kukimbiakimbia kutafuta chakula? Je, kujiandaa kwa njaa kwa kujenga ghala hiyo siyo mipango?

Kuna mifano mingi, ila ninachotaka kukueleza hapa tu ni kwamba, kama unadhani kupanga ni kupoteza muda, basi jaribu kufanya mambo yako kwa mitindo ya zima moto uone matokeo yake. Tena watu wengi wanaoponda suala la mipango utakuta wao mambo yao yanakwenda vizuri kutokana na mipangilio mizuri ya shughuli zao, huku wakihubiri kupanga ni kupoteza muda.

………………………………………………………………….....…


Kujiunga na Darasala Michanganuo gharama yake ni shilingi elfu 10 tu, ambapo baada ya kulipa pesa kupitia namba 0712 202244 au 0765 553030 jina ni Peter Augustino Tarimo, unatuma na meseji yenye anuani yako ya Gmail ambayo ndiyo tutakayotumia kukuunganisha na blogu hiyo ya darasa. Tunakupa pia na kitabu cha Michanganuoya Biashara na Ujasiriamali  (softcopy) “free of charge”  


Sehemu iliyopita.                                                Ifuatayo. 

0 Response to "MFANO WA MCHANGANUO WA BIASHARA(TEMPLATE) UNAPOTAKA KUANDIKA MPANGO WAKO"

Post a Comment