BIASHARA YA DUKA INAVYOWEZA KUKUTOA KIMAISHA UKIWA MJANJA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

BIASHARA YA DUKA INAVYOWEZA KUKUTOA KIMAISHA UKIWA MJANJA

Duka la rejareja, kitabu kilichoandikwa na Peter Augustino Tarimo
Ni misemo iliyozoeleka katika maisha ya kila siku mitaani, utawasikia watu wakisema; “biashara ya duka bwana, kichaa kabisa hailipi”, “duka unalinda mtaji wako tu usipotee lakini hamna unachopata”, “duka ukila hapo hata pipi umekula faida yenyewe”, “duka labda ukae wewe na mkeo, wengine watalifilisi mara moja”. 

Kauli za kukatisha tamaa kuhusiana na biashara hii hasa yale maduka ya rejareja  ni nyingi mno kiasi kwamba ukizifuata unaweza uione biashara hii haifai kabisa kufanya.

Lakini cha kustaajabisha ni pale utakapokuta katika mitaa yetu kila kukicha maduka yanafunguliwa, kweli kama zilivyokuwa biashara nyingine zote duniani, siyo maduka yote yanayofunguliwa hufanikiwa hata kudumu miezi yake sita ya mwazo, lakini ni ukweli usiopingika kuwa kuna walioanzisha maduka tena ya rejareja tu wakatajirika na kufikia hatua za juu kabisa kama kumiliki nyumba nzuri, magari na hata kufungua biashara nyingine kubwa zaidi.


Kiukweli hakuna biashara yeyote ile isiyokuwa na faida, bali faida au mafanikio ya biashara yeyote ile yanatokana na jinsi biashara yenyewe itakavyoendeshwa pamoja na mazingira ya biashara hiyo. Mbali na uzushi wote huo katika mitaa yetu kila kukicha utashuhudia maduka yakimea kama uyoga, mbona hawayafungi kama hayana faida?. 

Wakati wewe ukidanganywa kuwa duka ni biashara kichaa, wapo wenzako wanaosomeshea watoto wao shule za ‘international’ na wakati huo huo wakiwa na uwezo wa kubadilisha mboga majumbani mwao watakavyo. Kitu kingine cha kutia matumaini zaidi ni kwamba duka ni rahisi mno kuanzisha na halihitaji mtaji mkubwa sana wa kuanzia ilimradi tu una vifaa muhimu na chumba kilichokuwa eneo watu wanakopita.

Asilimia kubwa ya watu kwa mfano katika miji mikubwa kama Dar es salaam, Mwanza na Arusha wanapowaza akilini mwao juu ya biashara ya kufanya, wazo la kwanza linalowajia akilini huwa ni biashara ya duka na hasa maduka yale ya rejareja kutokana na soko lake kuwa la chapchap mno, unajua hakuna binadamu asiyekuwa na mahitaji hasa yale ya kila siku kama, chumvi, majani ya chai, sukari, unga, mchele, sabuni, mafuta, dawa za maumivu kama panadol, nk. Kwa hiyo unapoanzisha duka ni lazima uuze tu.


Katika kitabu nilichoandika, SIRI YA MAFANIKIO YA BIASHARA: DUKA LA REJA REJA, nimetumia uzoefu wangu binafsi wa miaka zaidi ya 12 katika biashara hii, tangu nikiwa Msimbazi Kariakoo kwenye vibanda, Sinza, Buguruni na hata Ubungo. Kitabu hiki ni kazi ambayo najivunia kwani nimeiandika kutoka moyoni mwangu asilimia mia moja.

Kitabu cha duka toleo la 2024

Ninao ujasiri wa kutoka kifua mbele na kukuhakikishia kuwa ninacho kitu unachoweza kujifunza kutoka kwangu. Huna tena sababu za wewe kwenda kujifunza kupitia njia ngumu na ndefu kama nilivyofanya mimi kwa miaka yote hiyo 12 nikijaribu hili na lile katika kupata njia sahihi na yenye tija katika uendeshaji wa duka la rejareja. Tayari nimeshakurahisishia yote katika kitabu hiki kimoja.

Kuna anayeweza kuhoji, “Peter kama umefanya biashara hiyo kwa miaka 12 tuonyeshe mafanikio uliyoyapata” Na mimi nakujibu hivi; “hebu ‘imagine’ miaka zaidi ya 10 mtu ukiendesha maisha na familia, bila ya kukutajia mafanikio mengine niliyoyapata, nadhani wewe mwenyewe unaweza kuona ni kwa kiasi gani biashara hii inaweza kumuweka mtu mjini”.


Hata hivyo ninachokushauri kama wewe una mpango wa kuifanya biashara hii au hata tayari unayo na ungependa ikupe kile unachokitaka, basi nitafute upate kitabu hiki, ninaamini kabisa ikiwa kama utashindwa hata kujifunza mafanikio niliyoyapata kutokana na biashara hii ya duka, basi angalao utajifunza changamoto nilizokutana nazo kwa miaka 12 ili na wewe usije ukazirudia.

Kitabu kina majibu ya maswali mengi yanayowahangaisha wamiliki wachanga wa biashara za rejareja na hata wale waliokwishafikia hatua za kati lakini kikubwa zaidi ni mbinu za usimamizi wa duka au biashara ya rejareja uweze kuona faida yako 'live bila chenga'. 

Mbinu za kudhibiti udokozi wa wasaidizi kwa asilimia zaidi ya 98% pamoja na mifumo ya kuleta ufanisi mkubwa. Katika toleo hili jipya la mwaka 2024 tumeongeza Sura mpya kabisa yenye kurasa 8 kuhusu teknolojia mpya ya Akili bandia (AI) inayoleta mapinduzi makubwa kwenye tasnia ya biashara za rejareja kote duniani na Tanzania ikiwemo.

Kitabu hiki katika nakala-tete unaweza kukipata kwa njia ya E-mail kwenye kompyuta au simu (smartphone) yako na bei yake ni Tsh. elfu 6 (6,000/=) tu. Unatuma pesa shilingi elfu 6 kwenye namba 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo, kisha nakutumia kitabu muda huohuo unadownload na kusoma au unakisave katika flash/disc yako.

Ikiwa utahitaji kupata kitabu hiki nakala-ngumu na upo jijini Dar es salaam, wasiliana na mimi moja kwa moja kupitia namba hizi, 0712 202244  au  0765 553030  na utaletewa kitabu hicho mpaka pale ulipo. Bei yake ni shilingi elfu 16 tu nauli ya kukuletea ni juu yangu mwenyewe.

Na kama upo Mikoa mingine kitabu hiki unaweza kukipata kwa kutuma fedha sh. 16,000/= pamoja na gharama ya kukisafirisha ambayo ni sh. 10,000/= jumla sh. 26,000/= , kwa namba 0712 202244 au 0765 553030, Jina ni Peter Augustino Tarimo. Tupe na maelezo ya mahali/mkoa ulipo kisha tutakutumia kitabu kwa njia ya basi linalofika hapo ulipo. 

Au unaweza pia kukipata katika application ya GETVALUE kwa kujisajili kwenye website hiyo, ukishalipa kwa njia ya mtandao wa simu una-download App yao kwa simu janja kisha unapakua kitabu chako. Anuani ya kujisajili ni hii hapa, bofya haya maandishi, GETVALUE KITABU CHA DUKA LA REJAREJA


Kwa maelezo ya vitabu vingine zaidi vya maendeleo binafsi, ujasiriamali na biashara tembelea ukurasa huu hapa; SMARTBOOKSTZ.


Mwisho usisahau kuendelea kuwa nasi katika kampeni yetu ya  #jirudishietenaukuuwako au #makeyourselfgreatagain Narudia tena, hii siyo kampeni, “nguvu ya soda” bali ni kampeni itakayodumu kwa muda mrefu na kwa wale ambao Ukuu wao utarudi kipindi kampeni haijamalizika tutawaomba watoe shuhuda zao hapahapa.

Kwa wale pia walio katika Ukuu wao nao nawaomba waendelee kutufuatilia kuhakikisha wanapata mbinu sahihi zaidi za kuendelea kuushikilia ukuu huo usijewaponyoka. Ninaposema UKUU ninamaanisha hali bora kimaisha katika nyanja yeyote ile, inaweza kuwa, kiuchumi, kielimu, kiafya, kiuhusiano,  kiibada nk.


Makala hii imeandikwa na:
Peter ugustino Tarimo
Mwabdishi vitabu na Mtaalamu wa michanganuo ya biashara
simu/watsap: 0712202244 / 0765553030


2 Responses to "BIASHARA YA DUKA INAVYOWEZA KUKUTOA KIMAISHA UKIWA MJANJA"

  1. Mtaji wa sh 2.5mil.unatosha kuanzisha duka?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ubatosha itategemea wewe unataka kuanza na bidhaa zipi na vifaa vya aina gani, mchanganuo wako ndio utakaokujulisha ni mtaji kiasi gani unahitaji kulingana na vile vitu utakavyohitaji. Mwingine hata hiyo milioni 2.5 kwake ni kubwa sana na mwingine kwake ni kidogo sana. Tuchukulie mfano labda unataka kuanzisha duka aina ya supermarket, milioni 2.5 haiwezi kutosha lakini mfano unataka kuanzisha tu duka dogo lenye mzani, friji, shelfu na bidhaa muhimu tu watu wanazohitaji kwa wingi, milioni 2.5 ni zaidi ya mtaji unaohitaji.

      Delete