CHANGAMKIA FURSA HII MPYA YA MAZAO YA TIKITI MAHINDI, MAHARAGE NYANYA NA MBOGAMBOGA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

CHANGAMKIA FURSA HII MPYA YA MAZAO YA TIKITI MAHINDI, MAHARAGE NYANYA NA MBOGAMBOGA


TANGAZO.
Muda mchache uliopita leo hii nimepigiwa simu na mkazi mmoja kutoka Mkoani Njombe Wilaya ya Wanging’ombe aitwaye  Lameck Lupaya na kunijulisha kwamba yeye amenipata kupitia mtandaoni, bila shaka namba aliiona kwemye blogu hii.

zao la mahindi
Mazao ya mahindi mabichi
Lameck alinijulisha juu ya fursa kubwa na nzuri iliyopo Mkoani Njombe hususan ya mazao ya kilimo kama matikiti maji, mahindi, maharage, nyanya, na mboga za majani zikiwemo pilipili hoho. Alisema lakini wakulima wa huko wana changamoto kubwa ya soko la mazao yao na akasema zao kwa mfano la tikiti ni zao linalokua haraka sana hivyo kuwa na fursa kubwa mno.

Alinidokeza haja yake ya kutafuta washirika hata ikiwezekana watakaoungana naye katika kutafuta masoko maeneo mengine kama jiji la Dar es salaam na kisha kuwatafutia wakulima masoko ya mazao yao katika maeneo yenye uhakika wa masoko ambapo wakulima hao watatoa kamisheni fulani, kama sikosei bila shaka alikuwa akimaanisha yeye na hao washirika ‘kuact’ kama watu wa kati.
 
tunda la matikiti
Tunda la tikiti maji shambani.
Mimi binafsi nilimjibu kwamba hilo ni wazo zuri sana na ninachoweza kufanya kama mhamasishaji wa maswala ya biashara na ujasiriamali kwa sasa ni kuhakikisha ujumbe wake naufikisha kwa wadau wengine kupitia blogu hii ya jifunze ujasiriamali kama tangazo. Vile vile mjasiriamali huyu alinipa na namba zake za simu ambazo pia naziweka hapa ili kama kuna mtu yeyote mwenye ‘interest’ na fursa hii basi wawasiliane, 0679325541 na  0756425541 .

…………………………………………………………………
Aidha blogu hii haihusiki wala haiwajibiki kwa matangazo yanayowekwa humu, unapofanya biashara na mtu yeyote aliyeweka tangazo humu hakikisha mnapitia taratibu zote muhimu za kibiashara.


0 Response to "CHANGAMKIA FURSA HII MPYA YA MAZAO YA TIKITI MAHINDI, MAHARAGE NYANYA NA MBOGAMBOGA"

Post a Comment