MAWAZO YA BIASHARA ZITAKAZOVUMA MIAKA IJAYO 2018 NA KUENDELEA MPAKA 2020 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MAWAZO YA BIASHARA ZITAKAZOVUMA MIAKA IJAYO 2018 NA KUENDELEA MPAKA 2020

Mara nyingi watu hukaa na kutafakari ni biashara zipi wanazoweza wakaanzisha ambazo zina fursa kubwa wakati ujao ukizingatia mabadiliko makubwa na ya haraka yanayotokea kila siku duniani. Biashara unayoweza kuiona leo kuwa inayo fursa nzuri ya kutengeneza faida, miaka miwili au mitatu ijayo siyo tena itakayokuwa biashara yenye kulipa vizuri.

Kama mjasiriamali makini ni lazima ujiulize hivi, “ni wazo gani la biashara linaloweza kuja kuwa na fursa kubwa baada ya miaka tuseme miwili, mitatu au hata kumi ijayo?”. Karne ya leo si kama karne zilizopita, wakati Waingereza walipoanzisha Mapinduzi ya viwanda karne ya 19, wazo la biashara au fursa kubwa iliyoonekana wakati huo kushika chati ya juu kabisa ilikuwa ni biashara ya kuunda na kuuza mitambo mbalimbali kwa ajili ya kuzalisha viwandani.


Wamarekani nao katika karne ya 20 wakiwa katika kilele cha ukuu wao, wakatawala duniani kwa wazo lao kuu la biashara ya uzalishaji na utoaji huduma mbalimbali. Leo hii karne ya 21 iliyopewa jina kuwa ni karne ya mawasiliano, tumeshuhudia wakiibuka miamba mingine kama Uchina na hata India wakiwapa ushindani mkali kwelikweli miamba wengine waliokuwa wametawala uchumi wa Dunia hii kwa kipindi kirefu.

Kinachowapa nguvu kubwa sana miamba hao wapya ni teknolojia ya mawasiliano. Leo hii Wamarekani hawaishi kulialia mitandao yao kudukuliwa na kuibiwa siri kibao kuanzia za kibiashara na hata zile nyeti kama za uchaguzi mkuu pasipo hata kuwa na nguvu kubwa ya kujitetea.

Ingawa hatuwezi kufahamu kwa uhakika mia kwa mia kuwa ni biashara gani au mawazo gani ya biashara zitakazoshika nafasi ya juu miaka michache ijayo, lakini watu tunaweza kutabiri ni biashara gani zitakazoweza kuja kushika chati katika miaka ijayo kwa kutumia vigezo mbalimbali.

Kidunia sekta zinazotabiriwa kuja kuwa tishio kwa mujibu wa taasisi iitwayo, “World Economic Forum”(WEF) ni hizi hapa chini;

*   Biashara ya simu za mkononi na teknolojia ya kuhifadhi data mtandaoni(Cloud technology)
*   Kompyuta zenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi kumbukumbu.
*   Vyanzo vipya vya nishati na teknolojia
*   Biashara ya kwenye mtandao(Intaneti)
*   Biashara ya vifaa vinavyojiendesha vyenyewe kama vile maroboti, vyombo vya usafiri kama ndege na magari yasiyokuwa na dereva nk.
*   Teknolojia za viumbehai(Biotechnology) 
  
Tukirudi katika mawazo ya biashara zinazotabiriwa na watu wengi hapa Tanzania kama biashara zinazotabiriwa kuwa na fursa kubwa miaka ijayo kuanzia mwaka 2018 na kuendelea mpaka 2020 na zaidi, tunaweza kuzitaja fursa au mawazo ya biashara hizo kuwa ni hizi hapa;

1.  Biashara ya ujenzi.
Ujenzi hasa wa nyumba za makazi, maofisi na miundombinu mbalimbali kama barabara na madaraja. Ongezeko kubwa la watu hasa mijini linaifanya fursa hii kuwa ya kipekee kabisa na itakayoshika chati kwa kipindi kirefu kijacho. Vilevile nchi kama Tanzania bado ni nchi inayoendelea hivyo ujenzi unahitajika mno. Kwa hiyo wazo la kuanzisha biashara kama ya vifaa vya ujenzi(hardware), ujenzi wa majumba(Real estate) na hata udalali wa majumba na viwanja ni mawazo muafaka ya biashara kabisa kuanzia mwaka huu, ujao na kuendelea.


Kuna mtu mmoja, mwanamke, hivi karibuni aliniacha hoi, alisema kuwa yeye sasa ameshachoka na  biashara nyingine zote, anatafuta mtaji japo kidogo tu akafungue hardware yake maeneo ya nje kidogo ya mji wanakoanza kujenga, akasema hata kama ataanza na sementi mfuko mmoja ya kupima kwa kilo, hilo halimpi wasiwasi kwani biashara ya vitu vya ujenzi ina uhakika wa wateja na bidhaa zake haziharibiki upesi. Hata usipouza mwaka huu utauza mwakani.

2.  Wazo la biashara ya kilimo cha mazao ya chakula.
Fursa ya kilimo cha mazao ya vyakula nayo inatabiriwa kuwa itakuwa na uhitaji mkubwa miaka ijayo kutokana na ongezeko kubwa la watu mijini na vijijini. Ongezeko hilo la watu linaenda sambamba na ongezeko la watu wasiopenda kazi ya kilimo, wao manapenda kuishi mijini na kufanya kazi za uchuuzi tu. Ukiwa mjanza ukakamata fursa hii utachuma senti zao kidogo wanazopata kutokana na uchuuzi kwani hakuna binadamu mwenye ujanja wa kuishi bila kula hata ikiwa anaishi London, New York au Paris.

……………………………………………………………………....

Ndugu msomaji, ungana nasi katika kampeni yetu ya “jirudishie tena ukuu wako”(Make yourself Great again) kwa kusoma makala hapa katika blogu hii kila siku. Jitahidi pia kupata kitabu cha “Kanuni ya kujifunza ELIMU YA PESA NA MAFANIKIO” tunachotoa bila malipo kwa muda mfupi na kisha kitaanza kuuzwa pindi idadi ya watu waliokusudiwa itakapotimia.

Jipatie pia moja kati ya vitabu vingine vifuatavyo au vyote ukiweza lakini napendekeza zaidi usikikose kitabu cha, MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI” kuona vitabu hivyo vyote fungua blogu hii hapa, SMART BOOKS TANZANIA


Ili tuweze kwenda sambamba zaidi, jiunge na Darasa la semina ya kujifunza jinsi ya kuandaa na kuandika mpango wa biashara yako au biashara yeyote ile utakayotaka. Kujiunga na darasa hilo fungua hapa, DARASA LA SEMINA YA MCHANGANUO WA BIASHARA. 

1 Response to "MAWAZO YA BIASHARA ZITAKAZOVUMA MIAKA IJAYO 2018 NA KUENDELEA MPAKA 2020"

  1. Nahitaji kitabu cha ELIMU YA PESA NA MAFANIKIO, je Nitaipata wapi?

    ReplyDelete