SEHEMU YA 4: DARASA LA SEMINA YA MPANGO WA BIASHARA(MUHTASARI) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SEHEMU YA 4: DARASA LA SEMINA YA MPANGO WA BIASHARA(MUHTASARI)


1.MUHTASARI
Katika mlolongo wa sehemu au vipengele vya mpango rasmi wa biashara, Muhtasari au unaweza ukauita Muhtasari Tendaji, unahesabika kama sehemu ya kwanza ya mchanganuo wa biashara yako baada ya Jaladala nje, Jina la mchanganuo na yaliyomo. Hii ndiyo sehemu muhimu kuliko nyingine zote katika mpango wa biashara kwani ndiyo msomaji anapoanza kusoma na atapata hamasa ya kuendelea kusoma sehemu nyingine za mpango wa biashara endapo sehemu hii itamvutia. Ikiwa muhtasari wako hauwezi kumshawishi msomaji basi ujue atautupa kapuni, hivyo ni sehemu inayotakiwa umakini wa hali ya juu.

Sehemu hii hukaa mwanzoni lakini huandikwa baada ya kukamilisha sehemu nyingine zote. Aya zinazounda Muhtasari ni ufupisho kutoka katika sehemu/vipengele vingine vyote 7. Kumbuka wakati unapoanza kuandika vipengele/sehemu nyingine zote unapaswa kila sehemu uanze na ufupisho mdogo wa sehemu husika, mihutasari hiyo midogomidogo ndiyo hatimaye huja kuunda muhtasari.

Au unaweza tu ukachagua kutoka katika kila kipengele zile sentensi muhimu zilizobeba vitu muhimu ukaziunganisha pamoja na kupata Muhtasari wako ama ufupisho wa andiko lako zima la biashara.

Kama unavyoweza kuona, MUHTASARI unaweza ukabeba vitu muhimu kwa ufupi kama vile;

·       Historia ya biashara
·       Malengo ya biashara
·       Mahitaji ya wateja unayotaka kuyakidhi
·       Upekee wa biashara yako
·       Uchambuzi wa mazingira ya biashara, nguvu, udhaifi, fursa na hatari(vikwazo).
·       Utawala na wafanyakazi
·       Kiasi cha makadirio ya mtaji unaohitaji
·       Chanzo/vyanzo vya mtaji.
·       Mikakati ya kufanikisha malengo
·       Makisio ya mapato na matumizi
·       Jinsi utakavyolipa deni ikiwa utakopa.

Hata hivyo siyo sheria kwamba katika muhtasari wako ni lazima pointi zilizotajwa hapo juu ziwe ndizo zitakazounda Muhtasari wako hapana. Katika Muhtasari unaweka vile vitu ambavyo katika mchanganuo wako unaona ndivyo vyenye uzito zaidi kwasababu kila mchanganuo au tuseme kila biashara ina malengo na vipaumbele tofauti na nyingine na hivyo kusababisha hata vipengele navyo kuweza kuwa tofauti au kuwa na uzito usiolingana.

Mpenzi msomaji huu ni utangulizi tu wa somo letu la nne 4 katika semina yetu ya Darasa la Michanganuo ya biashara. Pata somo zima ndani ya blogu maalumu ya Michanganuo hapa, pamoja na kutumiwa somo hilo (PDF) katika email yako.

…………………………………………………………………….

Masomo yanawekwa  kila siku somo moja, huku washiriki wakifuatilia na kuuliza maswali. Kila mshiriki anahudumiwa kikamilifu kulingana na mahitaji na uelewa wake, ni lazima kila anayeshiriki mafunzo haya mwisho wa semina aweze kuandika mpango wa biashara na ataamua yeye mwenyewe wazo la biashara atakayoiandikia mchanganuo kisha kupewa usaidizi wowote atakaohitaji hatua kwa hatua hata ikiwezekana mkufunzi kuja mpaka eneo la biashara na kufanya naye utafiti wa baadhi ya vipengele mpaka mchanganuo umekamilika.
Ada ya semina ni shilingi elfu 10. Ukishalipa kupitia namba 0712 202244 au 0765 553030 , unatuma na email yako pia lakini iwe (GMAIL), utaunganishwa na blogu ya michanganuo ambayo 'link' yake ipo kwenye blogu hii ya jifunzeujasiriamali pale juu katika MENU, baada ya kuactivate email tutakayokutumia utaweza kusoma masomo kwenye blogu hiyo lakini pia masomo hayohayo utatumiwa kwenye email yako moja kwa moja. Unapatiwa pia na kitabu cha Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali(softcopy) bure.

Kwa yule atakayehitaji kitabu cha karatasi hardcopy, basi atalipia semina sh. 10,000/= na kitabu atapewa kwa punguzo la shilingi 10,000/= badala ya bei yake ya kawaida ya shilingi elfu 20.

Nafasi  zinazotarajiwa zikishatimia darasa litafungwa mpaka waliojiunga wamalize kwanza kutokana  nafasi na rasilimali za mkufunzi, dhamira yetu kubwa ni kuhakikisha tunaandikisha idadi ya washiriki tutakaokuwa na uwezo wa kuwafundisha barabara ili na wao wakawatangazie wengine huduma zetu. 

Kwa hiyo ni vizuri kama unahitaji semina hii ukawahi mapema kabla muda haujakwisha. Zoezi la kujiunga litaenda sambamba na semina mpaka pale idadi tarajiwa itakapotimia.


                                                              



0 Response to "SEHEMU YA 4: DARASA LA SEMINA YA MPANGO WA BIASHARA(MUHTASARI)"

Post a Comment