SEMINA 12 ZA KUANDIKA MICHANGANUO YA BIASHARA ZA KIPEKEE ZENYE FURSA KUBWA YA KUTENGENEZA FAIDA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SEMINA 12 ZA KUANDIKA MICHANGANUO YA BIASHARA ZA KIPEKEE ZENYE FURSA KUBWA YA KUTENGENEZA FAIDA


Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa wahi kiti chako hapo! Ndiyo leo ninavyoanza ndugu msomaji wangu nikitaka kukujulisha kule tulikotokea na tunakoelekea nusu hii ya 2 ya mwaka huu wa 2018. 

Tangu mwaka huu uanze tumekuwa tukitangaza na kuhubiri semina za michanganuo ya biashara zile zilizokuwa na fursa kubwa ya kutengeneza faida, tukasema kwamba kila mwezi tungekuwa na semina moja huku masomo ya mzunguko wa pesa yakitolewa kila siku, hayo ndiyo yaliyokuwa malengo yetu ya mwaka 2018.

SOMA: Mzunguko mzuri wa fedha ndiyo njia bora zaidi ya kufikia malengo yako mwaka 2018 

Kwa yule anayetufuatilia kwa karibu hususani wateja wetu waliojiunga na GROUP LA WATSAP LA MICHANGANUO ONLINE kwa kweli wanaweza wakafikiri labda tuliwahadaa kwa kuwatangazia kitu ambacho hatuwezi kukitekeleza. Lakini naomba nichukue nafasi hii kwa heshima na taadhima kuwaomba kwamba, wasikasirike kwani sasa nusu hii ya pili ya mwaka 2019 tunakwenda kumalizia kila kitu tulichoahidi kama Mwenyezi Mungu atatupa uzima, nasema hivyo kwani kama ujuavyo ‘Mipango si matumizi’ japo haiepukiki ni lazima binadamu tupange karibu kila kitu tunachokifanya ili kiweze kwenda vizuri.

SOMA: Ratiba ya masomo ya semina hii hapa.

Nashukuru kwa upande wa masomo ya siku, tulijitahidi sana japo pia siku chachechache hatukuweza kutimiza. Programu yetu kwa mwaka huu ijulikanayo kama MZUNGUKO WA FEDHA NDIYO NJIA BORA ZAIDI YA KUFIKIA MALENGO YAKO MWAKA 2018 ilianza rasmi hapo mwezi Februari mwaka huu na itamalizika rasmi mwakani mwezi Februari 2019. Kampeni ya mwaka jana iliyokuwa imeitangulia hii ilijulikana kama, MAKE YOUR SELF GREAT AGAIN au JIRUDISHIE UKUU WAKO TENA na nakumbuka ilikuwa nzuri sana na watu wengi walihamasika mno nayo.

SOMA: Ni mwaka wa kujirudishia ukuu wako tena(MAKEYOURSELF GREAT AGAIN)

Ninachotaka hasa kusema leo ni kwamba, kama tulivyokuwa tumeahidi wakati kampeni hii inaanza, Michanganuo bunifu 12 mwaka huu ni lazima wale wote waliojiunga na Group letu Whatsap na wale wanaoendelea kujiunga sasa hivi mpaka itakapofika hiyo Februari, wajifunze na kuipata ili kuwa nayo yote 12.

Tutaandika nao hatua kwa hatua kama tulivyoanza pale mwanzoni. Kumbuka tayari tulikwishaandika Michanganuo mingine 3 ya Kuku wa mayai, kuku wa nyama na kuku wa kienyeji. Yote hiyo kwa aliyewahi kuisoma siyo michanganuo ya kawaida tu kama ilivyozoeleka bali ni michanganuo YA BIASHARA BUNIFU ZENYE UWEZO WA KUZALISHA FAIDA KUBWA NA YA HARAKA.

Siku ya Alhamisi ya tarehe 9 August, 2018 tutakwenda kuwa na semina yetu ya tatu 3 na Jina la biashara bado lipo kapuni halijatajwa, tutalizindua rasmi siku hiyo hiyo kwa wale washiriki wa semina. Ni biashara ambayo kila mtu atatamani kuifanya. Wanasema wazo la biashara haliigwi, ni kweli, lakini tusidanganyane bwana kama biashara inalipa kwanini mtu usiige na kuongeza maboresho?

SOMA: Ukibuni kitu kizuri ni kwanini watu lazima wakopi?

Ni nani anayependa kuuza kitu ambacho kutwa kucha haoni mteja wakati wenzake wanapiga hela kila dakika?  Nani wa kufa njaa usawa huu ulivyokuwa mgumu, ni lazima tukubali kuwa wabunifu lakini pia tuangalie na vile vitu ‘hot cake’ vinavyotoka chapchap kama tunapenda kutoka haraka kimaisha.

Semina yetu ni ya siku 3 na itaanza rasmi saa 4 asubuhi mpaka saa 8 mchana kila siku kwa siku hizo 3 mpaka Jumamosi.

Kwa masaa hayo manne wakufunzi wako tutakuwa macho muda wote hewani(online) tukifuatilia darasa kwa karibu kabisa huku tukiwa tayari kwa swali lolote lile kutoka kwa mshiriki yeyote atakalouliza. Siyo semina ya kitoto kabisa kwani tumepata uzoefu mkubwa kutokana na semina zilizopita huko nyuma, tunaelewa wateja wetu wanataka kitu gani na tunawapatia kile wanachokitaka vilevile bila kupunguza chochote, zaidi tunawaongezea.

SOMA: Utambulisho rasmi wa semina ya kuandaa mpango wa biashara.

Baada ya semina hii ya Alhamisi, tutakuwa na mfululizo wa semina nyingine karibukaribu ili kutimiza azma yetu ya kuwa na semina 12 itakapofika tamati ya kampeni yetu hii mwezi wa 2 mwakani. Unajua bwana, mpango wa biashara kuna watu hubeza kwamba eti, oo.. mipango si matumizi…, utapangaje wakati mambo hubadilika kila mara kwa kasi ya ajabu….., mpango wa biashara ni kupoteza muda bure……., na bla bla nyingine kibao. Lakini mimi napenda tu kuwaeleza hao rafiki zangu kwamba, hebu waache kuwadanganya watu kwani  hakuna asiyepanga mipango kichwani mwake hata kama anataka kuanzisha genge sembuse biashara ya mamilioni ya shilingi.

Utakuta mtu anaponda mipango wakati yeye biashara zake zinamuendea vizuri kutokana na mipango mizuri anayoandaa kabla ya kutekeleza biashara zake. Siri moja niliyogundua ni kwamba watu wengi hasa sisi Waafrika ni wazuri sana kupanga vichwani mwetu kuliko kwenye kipande cha karatasi. Wenzetu wazungu unajua ni kwanini karibu kila sekta wametuzidi?......... Njoo kwenye group bwana mambo haya tuje tuyadiscuss pamoja naona hapa muda hautoshi.

Mimi rafiki yako Peter Augustino Tarimo, nakuthamini sana msomaji wangu, uwe unasoma makala kwenye blogu ya jifunzeujasiriamali, uwe ni kwenye makala ninazotuma kwa njia ya email au hata katika mitandao mingine ya kijamii ninakopost post makala zangu. Lakini naomba nikuambie kwamba Binadamu hata uwe na ufanisi wa kiasi gani ndugu yangu kamwe huwezi ukamridhisha kila mtu hapa duniani. Makala zangu hata zingekuwa nzuri kiasi gani, bado kuna watu watakaoziponda na kuziona hazina maana. Kwahiyo kuna njia moja tu hapa duniani mtu unaweza ukawapa zaidi wale wanaochagua kukufuata au kuthamini zaidi kile unachotoa.

SOMA: Ingawa mipango si matumizi lakini haiepukiki kwenye maisha na biashara.

FOCUS, sijui niliweke vipi neno hili kwa Kiswahili lakini nadhani ni kuamua kuchagua vitu vichache vyenye ufanisi zaidi utakavyodili navyo. Sina maana kwamba basi nisithamini tena wasomaji wangu wa blogu ya jifunzeujasiriamali hapana, bali niwe na kipande maalumu “Segment” ambayo nitawapatia kile watakachoniambia wenyewe niwape bila mimi kuwasukuma au kuwakazania. Hii ndiyo sababu kubwa ya kuanzisha GROUP LA WATSAP LA MICHANGANUO ONLINE.

Group ni la wasap lakini siyo lazima uwe unatumia wasap ndipo uweze kupata masomo na semina zinazotolewa hapana, tunatuma pia masomo hayo kwa njia ya Email na hata tuna blogu maalumu ya private tunakoyaweka masomo yote na semina tunazozitoa. Halikadhalika ndiyo maana tukawa na email list ambayo kwa mtu kujiunga/kusubscribe, basi mtu huyo anaonyesha kile unachokitoa anakithamini zaidi na hivyo huna budi pia kuongeza umakini wako kwake kwa kuhakikisha hata huduma zako kwake zinakuwa tofauti na za kipekee pia.

Kwahiyo niseme tu kwamba wewe unayesoma Blogu ya jifunzeujasiriamali na wewe unayepokea makala kwa email, kuna fursa nyingine zaidi ambayo mimi na wewe tunaweza tukawa karibu zaidi na nakuhakikishia hapa ndipo ninakoweka maarifa yangu yote ninayohangaika kuyatafuta kila siku kwani mimi nimejitolea kufanya kazi hiyo sawasawa tu na jinsi wewe mwenyewe ulivyojitolea kuifanya ile kazi unayoifanya kila siku.

Kwahiyo sioni sababu kwanini uhangaike kutafuta maarifa ya ujasiriamali hususani namna ya kupanga biashara zako wakati tayari mimi nipo. NJOO JIUNGE LEO NA GROUP LETU KWA ADA YA SHILINGI ELFU 10 TU, TUJIFUNZE MPAKA MWAKANI NA BAADA YA HAPO TUTAANZISHA KAMPENI NYINGINE.

Ili kujiunga, lipia kiingilio chako sh. Elfu 10(10,000/=) kupitia namba za simu 0712202244  au 0765553030  na jina litakalotokea ni Peter Augustino Tarimo. Kisha tuma kwa meseji anuani yako ya barua pepe/email pamoja na namba unayotumia WASAP kama unatumia lakini, ikiwa hutumii wasap Email inatosha. Kisha tuma ujumbe usemao; “NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO”

Baada ya hatua hizo, nitakuunganisha mara moja na group muda huohuo pamoja na kukutumia masomo yote yaliyopita, semina, vitabu na michanganuo tuliyokwishachanganua katika semina zilizopita. Hatujawahi na wala hatutakaa tumwangushe mtu, fedha yako inapofika kwetu tunaithamini kwani tunafahamu fika fedha haijawahi kuwa rahisi kupatikana hata siku moja. Tutakupa pia thamani ya fedha yako na zaidi yake.

KARIBU SANA RAFIKI YANGU KAMATA KITI CHAKO HAPO USICHELEWE ILI TUWEZE KUWA PAMOJA ‘LIVE’ KWENYE HIZO SEMINA, KUNA UZURI WAKE NA FAIDA NYINGI KUWA PALEPALE WAKATI SEMINA ZIKIENDELEA.




0 Response to "SEMINA 12 ZA KUANDIKA MICHANGANUO YA BIASHARA ZA KIPEKEE ZENYE FURSA KUBWA YA KUTENGENEZA FAIDA"

Post a Comment