JE, KUKOPA ILI UKALIPE DENI LA ZAMANI KUNAWEZAJE KUBORESHA MZUNGUKO WA FEDHA KWENYE BIASHARA YAKO? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JE, KUKOPA ILI UKALIPE DENI LA ZAMANI KUNAWEZAJE KUBORESHA MZUNGUKO WA FEDHA KWENYE BIASHARA YAKO?


USIKOSE KITABU HIKI CHA MICHANGANUO NA UJASIRIAMALI
Suala la kukopa fedha kwa ajili ya kuendeshea biashara ni jambo la kawaida linalofanywa na wafanyabiashara wengi wakubwa kwa wadogo lakini kuna wakati mtu unaweza kuwa umekopa fedha mahali, beki au katika taasisi fulani ya fedha kisha njiani kwenye marejesho ya mkopo mzunguko wa fedha kwenye biashara ukayumba na kuwa mdogo.

Hali kama  hii inaweza kukulazimisha kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha mzunguko huo wa fedha uliodorora na baadhi ya wajasiriamali huamua kutumia njia ya kwenda kukopa tena mkopo mwingine juu ya ule aliokuwa nao mahali pengine kwa makusudi ya kuongeza mzunguko wa pesa wa biashara ikiwa ni pamoja na kuendelea kulipa deni la zamani lililokwama kulipika kukwepa kupigwa faini, kuongezeka riba ya mkopo na kuchafua sifa yake ya kukopesheka.

SOMA: Je Mtanzania unakopesheka na taasisi za fedha au benki?

Katika somo hili tutakwenda kujua iwapo hatua kama hii ni sahihi au siyo sahihi na ni kwa kiasi gani inaweza kusaidia katika kuboresha mzunguko wa fedha wa biashara. Lakini kabla hatujakwenda kuona hayo yote, hebu kwanza tujikumbushe mawili matatu kuhusiana na mikopo ya kuanzisha biashara au kukopa kwa ajili ya kuendeleza biashara kwa ujumla na hata ni nini hutokea ukikiuka masharti ya mkopo.

Kabla ya kwenda kukopa unatakiwa kufanya kitu gani?


Kabla hata ya kuinua mguu wako kuelekea benki au taasisi ya kifedha kuulizia jinsi ya kupata mkopo wa biashara yako, kitu cha kwanza unachopaswa kujiuliza ni IKIWA KAMA KWELI UNAHITAJI MKOPO. Taasisi za mikopo Tanzania zilizo nyingi wao kwa sababu wanafanya biashara hawawezi kuhangaika sana kukutafiti ili kujua kama unahitaji mkopo ama huhitaji.

SOMA: Ukisoma hapa utakaa uwalaumu tena benki na taasisi za kifedha.

Kuna mikopo rahisi na ya haraka siku hizi ikiwapo pia hata mikopo online inayotolewa mtu akiwa mtandaoni bila hata ya kuonana ana kwa ana ilimradi tu mkopeshaji ana uhakika fedha zake hazitaweza kupotea. Mikopo ya biashara ndogondogo si tatizo kubwa tena kama ilivyokuwa miaka michache iliyopita.

Katika nyakati kama hizi ambazo uchumi hautabiriki sana, gharama za vitu mara zimepanda mara zimeshuka, watu wengi huamua zaidi kulipa madeni waliyokuwa nayo kuliko kukopa na kujiongezea mizigo ya madeni zaidi. Wala haijalishi tena ikiwa mtu anavyo vigezo vya kupata mkopo vilivyokamilika.

SOMA: Kufanya biashara na mtaji kidogo ni sawa na kulima kwa jembe lisilokuwa na mpini.

Hata unaweza kuona mikopo ya magari kwa wafanyakazi wengi siku hizi imepungua sana. Katika kujiuliza kama kweli unahitaji kwenda kukopa fedha bila kujali kama ni mkopo wa haraka au ni mkopo wa riba nafuu, yapo maswali mengine madogo kadhaa utakayotakiwa kuyajibu nayo ni haya hapa chini;

·       Ni kweli unahitaji kukopa?
·       Tatizo unalotaka kukopea pesa lina umuhimu gani?
·       Hakuna njia nyingine mbadala ya kutatua tatizo hilo zaidi ya kukopa?
·       Utamudu kulipa fedha unazotarajia kukopa?

Ni kweli unahitaji kukopa?
Hebu jichunguze kwanza kama unayo tabia ya kununua au kulipia kitu kutokana na mihemko. Jipe kwanza muda usikurupuke kwani unaweza kujikuta kumbe wala huhitaji kiasi hicho kufanya hayo maamuzi yanayokusukuma ukakope.

Baadhi ya watu huenda kukopa fedha pasipo kwanza kufikiria kwa kina ni jinsi gani watakavyoweza kumudu marejesho, hudhania kwamba hawana kabisa njia nyingine mbadala zaidi ya kukopa kumbe wangeweza kabisa kuahirisha matumizi hayo au hata kuachana nayo kabisa. Hebu jaribu kujiuliza tena maswali haya mengine 3;

·       Kwani siwezi kusubiri mpaka pale nitakapomudu mwenyewe kutatua tatizo hili kwa fedha zangu pasipo  kwenda kukopa?

·       Hakuna njia mbadala ambayo naweza kuitumia kutatua tatizo hili mfano kununua kitu cha bei ya chini au hata kuomba msaada usiokuwa na masharti ya riba?

·       Sitaweza kujiwekea akiba kidogokidogo mpaka pale nitakapokuwa na uwezo wa kulitatua tatizo hili badala ya kwenda kukopa?

Badala ya kukimbilia kwenda kukopa ‘madeni mabaya’ unaweza ukaamua kujiwekea akiba kidogokidogo mpaka fedha hizo zitakapotimia kutatulia shida yako. Hii itakuepusha na mzigo wa riba ya deni na stress zitokanazo na madeni mabaya. Lakini ikiwa utaamua kukopa pesa basi hakikisha unao uhakika wa kuja kulipa deni na ujue kabisa ni kiasi gani utaweza kulipa kila mwezi au muda mliokubaliana na mkopeshaji.

SOMA: Je una madeni kama Ugiriki?


MADENI MAZURI NA MADENI MABAYA.

Yapo madeni mazuri na madeni mabaya pia, kwa mfano;
Juma anamiliki biashara ndogo ya duka la rejareja na sasa toka aianzishe ana miezi kadhaa. Kulingana na mauzo yeke ya kila siku Juma anao uhakika wa kuingiza faida ya shilingi elfu 30 kwa wiki. Aidha Juma anahitaji friji kwa ajili ya kuuzia vinywaji baridi ambalo gharama yake ni shilingi laki 3, fedha ambazo hana taslimu mfukoni na amepanga kwenda kuzikopa kutoka taasisi moja ya fedha na kulipa kila wiki shilingi elfu 20 kwa muda wa miezi 3.

Deni la juma hapo juu tuliloona ni DENI ZURI, kwanini? Kwasababu ukitazama utagundua kwamba biashara yake inao uwezo wa kuingiza kila wiki sh. Elfu 30, akitoa elfu 20 za marejesho atabakiwa na sh. Elfu 10 ambazo zitatosha kwa matumizi yake na gharama mbalimbali za biashara huku mtaji ukiendelea kuzunguka kama kawaida.

2. Aloys ni mfanyakazi katika kampuni moja ya ulinzi, anataka kukopa fedha sh. Milioni 2 kwa ajili ya kununulia pikipiki ya kumrahisishia kuwahi kazini jioni. Mshahara wake kwa mwezi ni shilingi laki moja na marejesho ya mkopo huo kila mwezi ni sh. Elfu 95.

Mkopo wa Aloys ni MKOPO MBAYA kwasababu, kwa muda wote wa miaka miwili atakuwa akikimbizana kulipa deni la pikipiki tu, hata fedha ya matumizi kama kununulia chakula cha nyumbani inawezekana asiweze kuipata kwasababu katika fedha za mshahara shilingi laki moja, ni shilingi elfu tano tu zitakazobakia baada ya kutoa za marejesho ya mkopo. Asipotafuta chanzo kingine cha fedha kuna hatari ya kuja kufilisiwa mali zake pamoja na pikipiki aliyonunua kwa fedha za mkopo.

SOMA: Mdudu hatari anayeweza kuua biashara yako haraka licha ya kuwa inaingiza faida kubwa.

Baada ya kutazama dondoo hizo chache juu ya Mikopo, sasa hebu turudi katika mada yetu ya somo la leo isemayo;

JE, KUKOPA ILI UKALIPE DENI LA ZAMANI KUNAWEZAJE KUBORESHA MZUNGUKO WA FEDHA KWENYE BIASHARA YAKO?

Ndugu msomaji wa makala hii, somo hili zima lilitolewa jana katika group la masomo ya kila siku la Whatsap la MICHANGANUO-ONLINE. Ili kupata mfululizo wa masomo haya yote tangu mwaka huu uanze tafadhali jiunge na group hilo kupitia namba 0765553030, tuna kiingilio kidogo cha shilingi elfu 10 lakini vitu unavyovipata ni vingi na vyenye thamani kubwa, Tutakutumia vitu vifuatavyo sambamba na kuunganishwa katika hilo group;

1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

3.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

4.  Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.

5.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

6.  Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

7.  Masomo yote yaliyopita katika group kuhusu MICHANGANUO NA MZUNGUKO WA FEDHA. A & B (Tumecompile katika vitabu PDF 2)

8.  Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENTA SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

9.  Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.


10.      Ukurasa mmoja wa mchanganuo.



Kupata vitabu mbalimbali katika lugha ya kiswahili kutoka self help books Tanzania tembelea ukurasa huu, >>SMART BOOKS TZ











0 Response to "JE, KUKOPA ILI UKALIPE DENI LA ZAMANI KUNAWEZAJE KUBORESHA MZUNGUKO WA FEDHA KWENYE BIASHARA YAKO?"

Post a Comment