MDUDU HATARI ANAYEWEZA KUUA BIASHARA YAKO HARAKA LICHA YA KUWA INAINGIZA FAIDA KUBWA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MDUDU HATARI ANAYEWEZA KUUA BIASHARA YAKO HARAKA LICHA YA KUWA INAINGIZA FAIDA KUBWA


Kwenye Ulimwengu wa biashara upo usemi usema, “Cash is a king” au Pesa taslimu ni kama mfalme, Usemi huu una maana kubwa sana hasa ukizingatia kwamba ili biashara iweze kuendelea vizuri inahitaji fedha taslimu kwanza za kulipia gharama mbalimbali kabla mauzo hayajafanyika, pia yanaweza yakawa ni mauzo kwa mkopo ambapo hapa biashara inakuwa bado haijaingiza pesa taslimu.

Tuchukulie mfano mmoja wa mtu aitwae Juma aliyeamua kuanzisha biashara ya kuuza kuku wa kienyeji ambao anawafuata mikoani na kisha kuja kuwauza jijini Dar es salaam. Juma baada ya kugundua kwamba biashara hii ya kuku ina faida nzuri na nono, aliamua kuanza kuifanya lakini mtaji aliokuwa nao ulikuwa ni kidogo mno, hivyo alimkopa mtu shilingi laki 3 kwa lengo la kwenda kununulia kuku wakubwa 300 kwa bei ya shilingi elfu 10 kila mmoja halafu baadae ndipo amrudishie mwenyewe pesa zake.


Alitarajia atakapowafikisha hao kuku katika masoko ya Dar es salaa angewauza kila mmoja kwa shilngi elfu 20 mpaka elfu 25 na hivyo kutengeneza jumla faida ya shuilingi laki 3 juu, tena chapchap.

Lakini ilikuwa rahisi kiasi hicho Juma kutengeneza kiasi kikubwa namna hii cha cha faida katika muda mfupi hivyo? Huu ndiyo mtego ambao wajasiriamali wengi huingia pasipo kujua na baadae kuja kujutia sana kwanini walianzisha biashara kwa msukumo tu wa faida kubwa kabla kwanza ya kutafiti au hata kuingia kidogo kwanza katika uhalisia wa mambo ulivyo ndipo waweke fedha zao nyingi.

Mdudu hatari tunayemzungumzia leo hii hapa siyo mwingine bali ni UKOSEFU WA FEDHA TASLIMU ZA UENDESHAJI KWENYE BIASHARA(WORKING CAPITAL) au kwa lugha nyingine tunaweza tukasema mzunguko mdogo wa fedha taslimu unaosababisha  biashara kushindwa kujiendesha na hatimaye kufa ingawa faida ipo nyingi tu. (Masomo kama haya na mengineyo kuhusiana na fedha kwa undani kabisa ndiyo tunayojadili kila siku usiku saa 3 katika Group la MICHANGANUO-ONLINE.)


Juma anapokwenda zake Morogoro kufuata kuku kwa fedha za mkopo shilingi laki 3 kumbuka anatakiwa pia mbali na kwenda kuwalipia hao kuku, ale chakula na maji njiani, akalale nyumba ya wageni pale Moro, alipe nauli ya basi, awalipie hao kuku usafiri kutoka hapo Moro mpaka Dar na ushuru wa soko au njiani. Akiwafikisha Dar kuna gharama za kuwalisha siku mbili tatu watakazokuwa wakisubiri wanunuzi nk.

Si hivyo tu wakati wa kuwauza wataibuka wateja wengine ambao watataka kuchukua kuku kwa mkopo na kisha kuja kulipa baada ya siku kadhaa au hata mwezi na kwa kuwa ni wateja wenye ofizi zao kama migahawa, huwezi kuwakatalia au kuhofia watakuzima pesa zako. Lakini Juma mategemeo yake ya haraharaka yalikuwa kwamba, laki 3 angenunua  hao kuku 30 atakaouza kila mmoja kwa shilingi elfu 20-25 apate faida laki 3 na ushee ndani ya siku chache tu kisha arudi tena Moro kufuata mzigo mwingine wa ‘ndege’. Kwa kifupi ni kwamba Juma mawazoni mwake alikisia umilionea kumnyemelea ndani ya miezi  michache tu ijayo.


Badala yake Juma alipofika Morogoro alitahamaki mfukoni amesaliwa na shilingi laki moja na elfu sabini tu, fedha ambazo hazikuweza tena kununulia kuku 30 kama alivyokuwa amepanga awali.Aliishia kununua kuku 25 na mfukoni akabakiwa na elfu 30 hivi. Alipokuja kwenye malori ya mizigo wakamwambia mzigo ili uweze kufika Dar es salaam walitaka shilingi elfu 50 ambazo Juma hakuwa nazo, alikuwa na elfu 30 peke yake.

Ilimbidi Juma akimbie tena kwenda kwa rafiki yake mmoja anayeuza kuku pale Morogoro na kumkopa shilingi laki moja nyingine ili atakaporudi kutoka Dar amrejeshee fedha zake, kwa bahati njema jamaa alikubali akampatia laki moja.

Juma alifanikiwa kuufikisha mzigo Dar salama na kesho yake ilimkutia pale Manzese darajani kando kando kabisa ya daraja kwenye banda la kukodi la kuuzia kuku wa kienyeji. Alitakiwa kila siku alipe shilingi elfu 5 auze asiuze, na kuku wale mpaka kuja kumalizika ilimchukua siku 5 huku akiwa amekopesha kuku 8 kwa mwenye hoteli moja pale pale Manzese.

Ingawa mzigo haukuchukua muda mrefu lakini Juma hakuwa tena  na fedha za kutosha kwenda kufuata mzigo mwingine Morogoro. Huku nyuma mdai wake aliyemkopesha laki tatu alimjia juu ile mbaya akitaka angalao amrudishie hata laki moja na nusu kwanza kiasi kingine aje kumalizia akiuza mzigo wa pili. “Si umeuza mzigo wote wewe, sasa kwanini usinipe hela yangu?”  jamaa alimfokea Juma kwa ghadhabu.


Ulikuwa ni ugomvi mkubwa. Siku hiyohiyo rafiki wa Morogoro naye aliyemkopesha laki moja alikuwa akipiga simu utadhani kapagawa vile, “Juma chondechonde nakusubiri hapa stendi nimekwama kishenzi, njoo haraka na kale kamzigo kangu”

Biashara ya Juma ya kuku kama angelikuwa na mtaji wa kuiendeshea (Working capital)  kwa kweli angeweza kutajirika haraka sana kama alivyokuwa amedhamiria mwenyewe. Lakini kwa kuwa hakuwa nao, alitegemea mtaji wa kuungaunga tena wa kukopa, sasa anazidi kujiongezea umasikini, kaingia migharama kibao wakati biashara si endelevu inaishia njiani na kubaki na mideni lukuki ambayo hata yanaweza kumsababisha ahame mji au hata kufikia hatua mbaya zaidi ya kujitoa uhai wake shauri ya madeni.

Juma alipaswa angalao kuwa na kiasi cha fedha zake mwenyewe kwanza kama shilingi laki 3 ndipo sasa akaazime nyingine tena laki 3. Hapo biashara hii yenye faina nono na nzuri ingeliweza kufanikiwa. Au pia kama ni kukopa basi alipaswa kuhakikisha anakopa kiasi kinachotosheleza mahitaji yote ya biashara hiyo na siyo tu kukubali kupokea hela ya mkopo kinjaa njaa kwa vile kaona pesa halafu anakuja kukwama na fedha za wenyewe nazo kukatikia humohumo.


Kosa la kuingia mikopo isiyokidhi mahitaji ni watu wengi hulifanya na husababishwa na watu hao kutokufanya tafiti za biashara zao kabla na kuandaa japo mpango rahisi tu unaoonyesha wanahitaji mtaji kamili kiasi gani. Wala mpango huo si lazima kuuandika, unaweza hata kuupangia ndani ya kichwa chako ingawa kuuandika kuna faida za ziada.

…………………………………………………

UKWELI KUHUSU KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA

1.  Mpango wa biashara siyo kitu cha ajabu, ni vile unavyofikiria juu ya biashara yako tu basi, hakuna cha zaidi ya hapo.

2.  Kila mtu mwenye uwezo wa kufanya biashara, moja kwa moja ‘automatically’ anao uwezo pia wa kuandaa au kuandika mpango wa biashara yake.

3.  Ushahidi kwamba mpango wa biashara kila anayefanya biashara anaweza pia kuandaa, tazama watu matajiri wengi wa zamani waliofanikia wengine hata shule hawakwenda kabisa halafu ujiulize mipango ya biashara zao waliandika wapi na lini? Kama hawakuandika sasa waliwezaje kufanikiwa?

4.  Ukweli ni kwamba watu wengi mipango ya biashara zao huipangia kichwani tu kitu ambacho ni sahihi kabisa lakini uwezo wa vichwa vya wanadamu hutofautiana na ndiyo maana mwingine anapoandika mahali mipango yake ndiyo huweza kuitekeleza na kunyooka vizuri zaidi.

5.  Ikiwa wewe uwezo wako wa kupanga kichwani tu peke yake si mkubwa jaribu pia kutumia karatasi na kalamu kuweka mipango yako. Wenzetu Wazungu kwa hili wametupita sanan na pengine ndiyo sababu kubwa ya maendeleo yao makubwa kutuzidi sisi Waafrika.

Katika GROUP LA MICHANGANUO ONLINE ambapo washiriki hujifunza kupitia WASAP na EMAIL tunajifunza masomo ya namna ya kuandaa mpango wa biashara yeyote ile kwa kichwa na pia kwa kuandika katika karatasi. Hata uwe mvivu kiasi gani kwenye mambo ya kuandika-andika, course hizi unaweza tu kujifunza kupitia kusoma michanganuo ya biashara mbalimbali na ukajijengea uwezo mkubwa wa kuandaa mpango wa biashara yako yeyote ile kichwani tu pasipo hata kuandika mahali.

KIFURUSHI (PACKAGE) CHA MASOMO YA MICHANGANUO YA BIASHARA.
Kuna kozi kamili ya kuandika mpango wa biashara yenye masomo 11, vitabu, cha kiingereza na cha Kiswahili, michanganuo halisi mbalimbali iliyokamilika kila kitu kuanzia Kasha la nje(jalada) mpaka makisio ya hesabu zote na vielelezo halafu kuna semina 12 za kuandika michanganuo yabiashara bunifu hatua kwa hatua ambazo semina ya tatu tunakwenda kuifanya siku ya Alhamisi wiki hii tarehe 9/8/2018. Nyingine zitafuata mpaka mwisho wa programu hii Februari 2019 kabla hatujaanza kampeni nyingine tena.

Ukipata package(kifurushi) hiki chote kizima unakuwa umejijengea uwezo mkubwa wa kupanga biashara yeyote ile utakayoianzisha na utakuwa vilevile umeongeza mara dufu uwezekano wa kufanikiwa biashara yeyote ile utakayoifanya kwani unakuwa umemaster ‘ABCD’ zote za biashara.

Kwa habari zaidi kuhusiana na semina ya Alhamisi tarehe 9/8/2018 fungua hapa, SEMINA 12 ZA KUANDIKA MICHANGANUO BUNIFU YA BIASHARA.


Usisahau pia kuwa leo 4/8/2018 kwenye group la ICHANGANUO-ONLINE tutakenda kujifunza somo muhimu sana la pesa lisemalo

JE, UNAIFAHAMU THAMANI YAKO HALISI KATIKA FEDHA, UTAJIRI NA MALI UNAZOMILIKI?

Usikose somo hili na ikiwa utachelewa kujiunga basi bado unayo nafasi ya kupata somo hili na mengine yote toka January mwaka huu lakini kabla ya february mwaka ujao. Simu 0712202244 na wasap ni 0765553030.


0 Response to "MDUDU HATARI ANAYEWEZA KUUA BIASHARA YAKO HARAKA LICHA YA KUWA INAINGIZA FAIDA KUBWA"

Post a Comment