UTAJUAJE KAMA BIASHARA YAKO YA UFUGAJI WA KUKU ITAKUPA FAIDA? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UTAJUAJE KAMA BIASHARA YAKO YA UFUGAJI WA KUKU ITAKUPA FAIDA?


UFUGAJI WA KUKU KIBIASHARA UNAOLETA FAIDA
Kabla hujaamua kwa dhati kabisa kwamba unataka kuanzisha biashara ya ufugaji wa kuku kibiashara ikuletee faida, ni lazima kwanza ufanye utafiti wa kina(upembuzi yakinifu) katika masuala yote yale yanayohusiana na aina ya biashara ya kuku unayotaka kufanya. Inawezekana unataka kufuga kuku wa nyama, kuku wa mayai, kuku wa kienyeji au hata kuku chotara aina ya kroiller nk.ilimradi umetaka kufuga kuku kama biashara vinginevyo unaweza ukawa unapoteza muda wako bure na mtaji(fedha) ulizozipata kwa tabu.


Baada ya kufanya utafiti wako, sasa utaweza kuandaa mpango wa biashara yako ya ufugaji wa kuku uliochagua kufanya na mpango wa biashara siyo lazima uandike mreefu sana hapana, unaweza tu kwa kutumia ukurasa mmoja wa karatasi ukapanga ni nini unachokusudia kukifanya, gharama zitakazohitajika ni zipi na makisio ya mapato yake na faida(kile unachotarajia kupata) ni kiasi gani.


Bila ya kupoteza muda, hebu tuone moja kwa moja ni maswali yapi unayopaswa kuyajibu unapofanya utafiti wa biashara ya ufugaji wa kuku;

VIFARANGA
1)  Gharama na upatikanaji wa vifaranga ukoje?
2)  Utanunua sehemu gani vifaranga?
3)  Bei ya kila kifaranga ni shilingi ngapi?
4)  Gharama ya usafiri kama utawatoa mbali ni kiasi gani?
5)  Je Utaanza na vifaranga wa siku moja, wiki au kuku wa muda gani?

CHAKULA
1)  Utatengeneza chakula cha kuku mwenyewe au utanunua kilichotengenezwa tayari madukani?
2)  Kuna maduka au kampuni zinazouza chakula cha kuku karibu na mradi ulipo?
3)  Bei ya mfuko mmoja wa chakula cha kuku ni shilingi ngapi?
4)  Kuna gharama zozote za usafirishaji wa chakula?

VIFAA MBALIMBALI NA BANDA
1)  Unalo banda au utakodisha?
2)  Gharama za banda ni kiasi gani?
3)  Mahitaji ya vifaa vya kulishia na maji pamoja na bei zake ni kiasi gani?
4)  Utahitaji vitalu vingapi?
5)  Gharama za vitalu ni kiasi gani?
6)  Ni wapi utapata matandazo na kwa gharama kiasi gani?
7)  Utapata wapi huduma za chanjo na dawa?


MASWALI YA SOKO
1)  Ni wapi utauza kuku/mayai?
2)  Utawauzia kina nani? Ni majirani, mashuleni, sokoni, viwandani, au katika maduka makubwa?
3)  Ni kina nani wanaofuga kuku sawa na utakaofuga wewe na bei zao huwa zikoje?
4)  Kwanini watu wanunue kutoka kwako?
5)  Bei yako itakuwa shilingi ngapi?
6)  Utakuwa na uwezo wa kuuza kiasi gani cha kuku au mayai kwa mwezi, msimu au kwa mwaka?
7)  Utajuaje kama utaweza kuuza kiasi hicho?

Maswali haya ndiyo yatakayokuwezesha kuweka mpango wa biashara yako ya ufugaji wa kuku iwe ni kuku wa mayai, kuku wa nyama, kuku wa kienyeji ama kuku chotara.

…………………………………………………

Ndugu msomaji, biashara ya ufugaji wa kuku ni moja kati ya biashara zilizo na fursa kubwa kutokana na uwezo wake wa kuzalisha faida kubwa ndani ya kipindi kifupi.Lakini ili kuweza kunufaika na fursa hii kubwa mfugaji yeyote yule hana budi kuwa na taarifa zote sahihi juu ya aina ya ufugaji kuku anaotaka kuufanya hasa hasa katika upande wa gharama mbalimbali zinazohitajika.

Tuna kifurushi cha michanganuo mitatu 3 ya ufugaji wa kuku kijulikanacho kama MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS, kuku wa mayai, kuku wa nyama na kuku wa kienyeji. Michanganuo hii inaweza kuwa msaada mkubwa kwa mtu anayetaka kufuga kuku kibiashara au hata ambaye ameshaanza kufuga tayari na angependa kuboresha mradi wake kuwa wa kisasa zaidi.

Kifurushi hiki kinapatikana kama softcopy kwa njia ya e-mail na bei yake ni shilingi elfu 10 tu. Unaponunua tunakupa na offa ya vitu vingine mbalimbali pamoja na kuwa mwanachama wa kudumu katika GROUP la masomo ya kila siku la MICHANGANUO ONLINE. Offa hiyo ni hii hapa chini;

1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  Masomo 11 ya semina kamili ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

3.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

4.  Mfululizo wa Tafsiri ya kitabu mashuhuri cha THINK & GROW RICH kwa Kiswahili.

5.  Kuunganishwa na blogu ya kulipia ya michanganuo bure.

6.  Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

7.  Masomo yote yaliyopita katika group la whatsapp la MICHANGANUO NA MZUNGUKO WA FEDHA.

8.  Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENTA SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

9.  Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.

10.      Ukurasa mmoja wa mchanganuo.

Ikiwa utahitaji kifurushi hicho unaweza kulipia moja kwa moja sh. elfu 10 kupitia namba zetu, 0712202244  au  0765553030 au WHATSAPP 0765553030 kisha tuma ujumbe kutujulisha nasisi tutakutumia kila kitu muda huohuo. Ikiwa hutumii whatsapp hamna shida kwani masomo tunatuma pia kupitia email na blogu ya private. 

0 Response to "UTAJUAJE KAMA BIASHARA YAKO YA UFUGAJI WA KUKU ITAKUPA FAIDA?"

Post a Comment