BIASHARA NZURI 4 MWANACHUO ANAWEZA KUFANYA NA MTAJI WA LAKI 2 HUKU AKISOMA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

BIASHARA NZURI 4 MWANACHUO ANAWEZA KUFANYA NA MTAJI WA LAKI 2 HUKU AKISOMA

WANACHUO, MVULANA NA MSICHANA WAKIDISCUSS MASOMO NA BIASHARA ZAO
Baada ya kujibu swali la jana kutoka kwa mdau wa group la MICHANGANUO-ONLINE kuhusiana na wazo la biashayenye hatari ndogo mwajiriwa serikalini anaweza akafanya kwa mtaji wa milioni 5, leo tutaendelea kusoma majibu ya swali la mdau mwingine tofauti, huyu ni mwanachuo na alipenda kushauriwa biashara nzuri anazoweza akafanya kwa mtaji wa laki mbili akiwa angali chuoni akisoma(Kusoma na biashara). Swali lake kama alivyouliza naliweka hapa chini kama lilivyo bila kuedit kitu;

“Habari za jioni ndugu zangu, naitaji ushauri kutoka kwenu jamani,, mm nipo chuo dodoma apa, ninataka nianzishe biashara na nina mtaji kidogo tu almost laki 2 je ni biashara gani naweza kufanya kwa mtaji huu nilio nao??”

MAJIBU YA BIASHARA UKIWA CHUONI:
Kwa kweli hebu nivae viatu vyako kidogo nikiwa na maana kwamba nitajifanya  kama vile mimi ningelikuwa ndio wewe mwana chuoni Leo hii(sasa).

Kwa kadiri ya muda wa chuo/shule ulivyokuwa mchache(miaka 2 tu au 3) na ukilinganisha na umuhimu wa malengo mtu unayokuwa nayo kimaisha ya kwenda pale chuoni, kwa kweli ningeahirisha biashara nikomae kwanza na chuo ili niweze kufaulu vizuri. 

Biashara nitaweza kuja kufanya muda wowote ule nitakao lakini sio chuo, muda wa chuo/shule kama ni mwaka 1, 2, 3 au 4 ukishapita bwana, ni kazi kwelikweli kuja kupata tena chance kama hiyo, tuulize sisi tuliopitia huko tutakueleza.


Inawezekana kufanya biashara ukiwa chuoni, kwa huo mtaji wa sh. laki 2 lakini itakulazimu kwanza uapply kitu kinachoitwa "bootstrapping" Kufunga mkanda kwa kiwango kikubwa ikiwa utataka huo mtaji usije kukata.

Sababu ni  kwamba, kwanza kiwango cha huo mtaji ni kidogo, hautaweza kununua bidhaa nyingi za kuuza labda iwe utatoa huduma.

Sipendi kuondoa uwezekano wa kufanya biashara ukiwa chuoni wala kukukatisha tamaa bali tu ninachotaka ufahamu, ni changamoto mbalimbali na ile risk ya kukosa vyote 2, elimu na biashara.


Hata hivyo bado wapo watu walioweza kumudu kufanya biashara wangali chuoni japo siyo wengi sana. Na kama nilivyosema wengi wao ilibidi wajitume sana ili waweze 'kucope' au kuendana na muda mchache waliokuwa nao. Kuna baadhi ya biashara kama vile;

Kuuza airtime, miamala ya kifedha kama tigo pesa, Mpesa, Airtel money, ezy pesa, TTCL money na Halo pesa. Unaweza ukaongeza na vitu, vifaa au huduma zinavyoendana na hivyo mfano, flash zenye ubora wa hali ya juu, kusajili laini za simu mitandao mbalimbali(uwakala wa makampuni ya simu) nk.

Kama unayo laptop, jinunulie kaprinta kako hata ka sh. laki moja, kaweke bwenini na uwatangazie wenzako kwamba unaprint kwa bei poa kuliko steshenari za jirani.

Tumia smartphone yako kuanzisha biashara yeyote ya mtandaoni mfano ya kuuza nguo, au bidhaa yeyote ile kali unayojua unaweza kwenda kutuma muda haupo kwenye masomo. Bidhaa hiyo unaweza pia hata kuwauzia wanafunzi wenzako watakaopendezwa nayo. Unaweza hata ukaamua kuuza simu.nk. 

Usijali hata ikiwa utanunua bidhaa moja tu kwa hiyo laki mbili lakini inayouzika kirahisi na yenye faida. Njia mbadala pia unaweza ukatangaza bidhaa fulani ambazo unajua pa kuzipata mjini au kokote kirahisi lakini wateja wako hawajui namna ya kuzipata. Kisha wakioda wewe ndio unakwenda kuchukua na kuwapelekea au kuwatumia. Tafuta kitu ambacho hakitakupa usumbufu wala kula muda wako mwingi

Unaweza pia ukajiunga na moja ya makampuni ya network marketing(riferral marketing) yanayoaminika na yasiyokuwa na viingilio vikubwa.


Kabla ya a kufanya biashara ukiwa chuoni, pima kwanza mazingira yako kikamilifu ukiona utaathiri kwa kiasi kikubwa matokeo yako ya mwisho, ni bora ukavumilia huku ukijifunza ujasiriamali mitandaoni kidogokidogo, utakuja kuwa na muda mwingi tu wa kutosha hapo baadae wa kufanya biashara ya ndoto yako mpaka wewe mwenyewe ukose pa kuupeleka.

MASOMO NA BIASHARA CHUONI
Wahitimu wa chuo kikuu
Uhalisia wa mambo ni kwamba, kutokana na muda kuwa mfupi mno na mambo yenyewe kuwa ni mengi, chuoni hapawezi kuwa mahali unapoweza kutimiza malengo makubwa sana ya kibiashara ila ni mahali unapoweza kujiwekea msingi wako wa kuja kufanya biashara hapo baadae kwa kufanya biashara simple kama nilizozitaja hapo juu na nyinginezo.

Lakini pia kujifunza kwa kufuatilia programu rahisi kama zilivyokuwa hizi za kwetu, Self Help Publishers ambazo zimekwishaandaliwa tayari na unaweza kujifunza ukiwa tu na muda wa ziada mbali na ule wa masomo yako ya chuo. 

Ikiwa huna muda wa kutosha unachoweza kukifanya ni kuendelea tu kuyahifadhi masomo yako hayo kwani yanahifadhika na uzuri pia tunalo group la kudumu la watsap la MICHANGANUO-ONLINE ambalo utaweza kuja kuwasiliana na admin muda wowote akutumie(program nzima) masomo yote in case labda umeyapoteza.

...............................................mwisho..........

Hakikisha hukosi vitabu vyako hivi vifuatavyo, kwa maelezo zaidi unaweza pia kutembelea; SMART BOOKS TZ

Watsap: 0765553030
Simu: 0712202244








KUJIUNGA NA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE LIPIA KIINGILIO AMBACHO NI SH. ELFU 10, KISHA TUMA UJUMBE KWA WASAP 0765553030.

0 Response to "BIASHARA NZURI 4 MWANACHUO ANAWEZA KUFANYA NA MTAJI WA LAKI 2 HUKU AKISOMA"

Post a Comment