WAZO LA BIASHARA IPI YENYE HATARI KIDOGO NAWEZA KUFANYA KWA MTAJI WA MILIONI 5?: MWAJIRIWA SERIKALINI

MWAJIRIWA SERIKALINI
Bado tunaendelea na mfululizo wa majibu ya maswali kutoka kwa wasomaji na wadau mbalimbali wanaofuatilia masomo yetu hapa katika blogu ya jifunzeujasiriamali, katika Mastermind group la MICHANGANUO-ONLINE na pia katika mitandao mingine ya kijamii tunakopatikana. Leo hii nayaweka maswali mawili yaliyoulizwa na wadau wawili katika Group na nimeona si vibaya nikayashirikisha hapa. Kila swali nitaliweka katika makala yake na la kwanza ni hili lifuatalo bila ya kuongeza wala kupunguza kitu kama alivyouliza;

Jaman I have 5m,and I don't have any  business idea”

MAJIBU:
Kwa kweli hatari(risk) ndiyo kitu kikubwa huwaogopesha zaidi wafanyakazi  kuanzisha biashara na hili ni ukweli hawaogopi bure kwani biashara bila ya kuwepo mfumo imara wa usimamizi ni bora kuacha kabisa.

Mimi binafsi kwa upande wangu nina maoni yafuatayo;

Kwa kuwa hata ukisema usubiri mpaka muda wa kustaafu ndipo uje uanzishe mradi sidhani kama ni uamuzi bora. Vyovyote vile iwavyo ukitaka kuja kuepusha stress baada ya kustaafu ni lazima sasa ujifunze biashara au miradi iliyokuwa na risk(hatari) kidogo ili uwekeze humo hizo pesa zako.

Najua tayari kuna mipango ambayo imeshawekwa na mwajiri kama vile mifuko ya mafao lakini bado inatakiwa kujaribu aina nyinginezo za uwekezaji utakaokulipa zaidi.


Mbali ya kuwepo baadhi ya biashara zenye hatari kidogo lakini pia hatari ya mradi au biashara yeyote ile hupungua kadiri mtu anavyokuwa na uelewa au kujifunza zaidi juu ya biashara husika wala haijalishi ni biashara ya aina gani, yaweza kuwa ni biashara ya duka, biashara ya mazao, biashara ya kusafiri au kuagiza bidhaa nje ya nchi, biashara ya mtandao nk.

Baadhi ya biashara zilizo na kiwango cha chini cha hatari ni kama vile,

Uwekezaji kwenye hisa.

Akiba ya kudumu ya benki(fixed deposit account)

Uwekezaji kwenye ardhi na majengo(unaweza ukanunua pagala ukalikarabati na kuweka wapangaji)

Kuna biashara pia kama hizi za mitandaoni unazoweza kuziendesha bila kutegemea msaidizi, msaidizi wako anakuwa ni teknolojia pekee ambayo haiwezi kukudokolea.

Mwisho ni kwamba unaweza kuanzisha biashara yeyote hata zile zenye risk kubwa lakini hapa ukawa mjanja 'kutokutumbukiza mayai yako yote katika kapu moja.


Anza kidogo kabisa huku ukilenga hapo baadae kukua taratibu kadiri siku zinavyosogea. Mfano Kama ukianzisha mgahawa basi uwe mdogo kabisa kusudi iwe rahisi wewe kujua kwa urahisi kila kitu kinavyoendelea, iwe ni kama vile mahali pako pa kujifunzia(field) na sio kujali unapata faida kubwa hapana.

Kwakuwa unakuwa umewekeza kiasi kidogo sana cha mtaji, hata itokee riski gani haitakuumiza kichwa sana na itakuwa moja ya funzo kwako ili baadae ukijikita kisawasawa katika biashara usijekukwama. Utakuwa umekwishajifunza mbinu za biashara husika.

Ni biashara gani uanze, hiyo ni lazima itakuwa kichwani mwako tu, hamna binadamu asiyekuwa na vitu anavyovipenda au ujuzi fulani, hobi, passion na vitu Kama hivyo. Ikishindikana kabisa wewe fikiria tu ni hitaji gani watu wanaokuzunguka linawasumbua hawalipati vizuri au hawalipati kabisa na wangetamani kulipata.


Ukisubiri watu wengine wakupe mawazo ya biashara yaliyo vichwani mwao hayataweza kufanya kazi.

By the way usikirupuke ukapoteza milioni 5 zako bure. Tulia ufikirie kwa umakini na ukipata wazo la biashara lianze kwanza kwa kiwango cha chini kabisa pasipo kuathiri kabisa muda wa ajira yako inayokuweka mjini kwa Sasa. Zipo biashara mpaka za mtaji wa laki moja(natolea mfano) unazoweza ukaanzisha hatimaye ukaweza kupata uzoefu.

.....................................................................


Programu zetu zote kubwa zinaendelea kama kawaida na usisite kuagiza PACKAGE inayokufaa muda wowote ule utakaohitaji zikiwa bado kwenye offa zake kwani ukifika muda muafaka bei zitabadilika na kupanda au OFFA husika kutokuwepo tena.

KIFURUSHI(PACKAGE) YA 1 (18,000/=  au 37,000/=)
Vitabu 3, softcopy kwa sh. elfu 18 vyote 3 na Hardcopy sh. elfu 37

1. MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI
2. MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA
3. MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA                KUITOA
Pamoja na kuunganishwa na grupu la wasap bure ukipenda

KIFURUSHI(PACKAGE) YA 2 (10,000/=)
Tunakutumia vitabu, michanganuo na masomo yote yafuatayo kwa gharama ya shilingi elfu 10 tu.(Vyote ni softcopy); Ukitaka pia unajiunga na group bure.1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  Kitabu kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1

3.  Kitabu kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2

4.  Kitabu kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.

5.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

6.  SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

7.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

8.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza

9.  Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.

10.              Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

11.              Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

12.              Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.


13.              Ukurasa mmoja wa mchanganuo.KIFURUSHI(PACKAGE) YA 3 (20,000/=)
Semina maalumu ya jinsi ya kufanya hesabu za mpango wa biashara(Advanced Business Plan Financials) Bei yake ni shilingi elfu 20 na tunatuma kama softcopy kwa email.

0 Response to "WAZO LA BIASHARA IPI YENYE HATARI KIDOGO NAWEZA KUFANYA KWA MTAJI WA MILIONI 5?: MWAJIRIWA SERIKALINI"

Post a Comment