Nataka kuacha kazi nianzishe biashara kwa mtaji wa milion 5 hadi10 nishauri nianze biashara ipi? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

Nataka kuacha kazi nianzishe biashara kwa mtaji wa milion 5 hadi10 nishauri nianze biashara ipi?

kuanzisha biashara ndogondogo ya mtaji mdogo baada ya ajira
Huwa najibu maswali mafupi mafupi toka kwa wasomaji wa blogu hii na wafanyabiashara ndogondogo za mtaji mdogo au wale wa kati. Ni kawaida swali likitumwa kwetu huwa hatubadilishi chochote hata speling na tunaliweka hapa kama lilivyoulizwa isipokuwa tu hatuwezi kutaja utambulisho kamili wa muulizaji pasipo kuwa na idhini yake.  Leo katika swali lililotufikia mezani ni hili lifuatalo, Nataka kuacha kazi nianzishe biashara kwa mtaji wa milion 5 hadi10: nishauri nianze biashara ipi? Kwa kirefu swali hilo linasomeka hivi;
swali la msomaji
SWALI.
Kiukweli mim kwa umri niliofikia hadi kukua kwangu sijawahi kuuza hata pipi kwahyo sina idea ya biashara wala uzoefu wowote kuhusu biashara na Nina mpango niachane na kazi ninayoifanya nianzishe biashara kwa mtaji wa wastani wa chini ya million 5 au zaid ya hiyo lakin haitazid 10, lakin hadi saiv kila nikuliza watu biashara ambazo zinaweza zikalipa wananambia biashara tofauti tofauti wengine mazao wengine duka wengine grocery sasa kwa ushauri wako kwa mtu ambae hana uzoefu kabisa na biashara unampa mwongozo gani?

MAJIBU.
Kwanza ni vizuri usichukue ghafla uamuzi wa kuachana na kazi unayoifanya kabla hujawa na uhakika na biashara utakayoifanya. 

SOMA: Je, ajira ni jambo baya, utumwa na kukosa malengo?

Cha pili ni kwamba biashara ya kuanza pamoja na kupokea maoni, ushauri na maelezo toka kwa watu mbalimbali nikiwemo na mimi, lakini uamuzi wa mwisho utoke moyoni mwako.(Akili ya kuambiwa changanya na ya kwako) Hapo ninamaanisha kwamba hakikisha ukianzisha biashara angalia ile ambayo una moja kati ya vitu vifuatavyo, au viwili au vyote ikiwezekana kuwa navyo vyote;

1.  Una mapenzi nayo.
2.  Una uzoefu nayo.
3.  Una ujuzi nayo.
4.  Ni hitaji muhimu kwa watu na wanalihitaji kwelikweli, kwa maana nyingine ni biashara yenye soko kubwa na la uhakika kwa asilimia nyingi.

Ukishachagua biashara yenye moja ya sifa nilizotaja, ianze kwa kiwango kidogo(anza biashara na mtaji mdogo kwanza), wakati bado hujaachana na kazi au shughuli unayoifanya sasa ili kupima kama ina uwezo wa kukufanya uishi kwa kuitegemea muda wote(full time) Hapa unafanya utafiti kwa vitendo na wala siyo kinadharia tena.

Baada ya hapo ukishagundua biashara hiyo ni ya uhakika angalao inaleta faida hata usipopata mshahara 'itakuweka mjini' basi ndipo uachane rasmi na kazi unayoifanya. Kuanza biashara ndogo kwa mtaji mdogo hakumaanishi kwamba biashara hiyo unalenga iwe ndogo siku zote hapana, unafanya hivyo huku maono yako yakiwa ni kuja kuifanya iwe biashara kubwa baada ya kuachana na ajira kwa kuongeza mtaji uwe mkubwa zaidi pamoja na muda wako wa kutosha.

SOMA: Maajabu ya kufikiri mambo makubwa na kwanini uweke malengo makubwa maishani.


Hata baada ya kumpa msomaji wangu huyu majibu hayo bado hakuridhika akaendelea kutaka kujua zaidi kwa kuniuliza kama ifuatavyo;

kujua faida na hasara ya biashara


“OK nimekuelewa vizuri kiongozi lakin sasa ili ujue biashara inalipa au hailipi mi najua inatakiwa uisimamie mwenyewe ili ujue faida na hasara zake halaf kama ndo unamuachia mtu umuachie huoni kama hilo swala LA kuacha kazi litakuwa na uzito ili nijue faida na hasara ya biashara nitakayoianzisha”


MAJIBU:
Ndio maana nimesema lazima kwanza ufanye utafiti wa kutosha wa kulithibitisha wazo lako la biashara kivitendo kama linalipa kabla hata haujaacha kazi kwani kuna takwimu za biashara nyingi kufa ndani ya muda mfupi mara tu baada ya kuanzishwa.

Kinachosisitizwa zaidi hapo ni ule uwezo wa kuhimili gharama za maisha wakati ukiitengeneza biashara yako ili isimame. Kumbuka kuwa ukianzisha biashara leo kuna kipindi fulani kitapita hata miezi 6 na zaidi kabla haijaanza kutengeneza faida.

SOMA: Jinsi ya kufanya utafiti wa biashara yako/upembuzi yakinifu.

Ikiwa unacho kianzio,(mtaji wa kutosha) utakaoweza kutenga hapo kiasi cha matumizi yako ya kila siku pasipo kutegemea hiyo biashara basi hamna shida sana juu ya kuachana na kazi na kuelekeza nguvu zako zote kwenye hiyo biashara.

Ila  kama mtaji wa biashara yako ni mdogo, ni bora ukafuata hiyo njia ya kuanza biashara katika levo ndogo ukiwa bado na ajira yako lengo likiwa si kutengeneza faida kubwa bali network, soko na uzoefu wa kiasi fulani ili baadae ukiacha kazi uwe unajiamini zaidi na biashara yako.

Unaweza hata ukaanza katika levo(hatua) ambayo si ya kumwajiri mtu, just unaifanya katika muda wako wa ziada na ikiwa utaweka mtu basi uhakikishe ni lazima ‘unacontrol’ mahesabu ya biashara yako kikamilifu( effectively ) muda unapokuwa nje ya ajira yako. Na kwa kuwa nimeshakuambia utaanza biashara kwa kiwango kidogo sana mwanzoni(biashara ndogo kwa mtaji kidogo), bila shaka kusimamia hesabu haitakuwa kazi ngumu sana kwako, nusu saa au lisaa kwa siku itatosha kabisa, ili mradi usipitishe hata siku moja bila kujua hesabu za biashara yako zinaendaje, ni nini kimeingia na ni nini kimetoka, nani anadai na ni nani anadaiwa.

SOMA: Jinsi ya kusimamia hesabu katika biashara ndogo unayomwachia mfanyakazi.

Kumbuka katika levo hiyo utakuwa haupotezi  chochote kwani bado unao uhakika kazini(kwenye ajira yako), na katika biashara yako pia unaendelea kupata ‘exposure’ kubwa hata kama hupati faida kivile. Lakini ‘at least una gain experience’ na kujua ni kitu gani kinachofanya kazi na kipi hakifanyi kazi.

Pia katika hatua hii ya majaribio kwenye biashara, “usicheke na kima tafadhali”, hapa kucheka na kima namaanisha kwamba usije ukamvumilia mtu yeyote atakayeonyesha daliki zozote za kuihujumu biashara yako ndogo hasa yule pengine utakayemwachia akuangalizie biashara muda haupo. Kuwa strictly sana kwani hapo ndipo palipo na mtihani mkubwa kwa mtu yeyote yule anayeanza biashara mpya.

Kwakuwa huna cha kuhofia, ajira yako ipo 'intact' hujaiacha bado, usimbembeleze sana mtu kupita kiasi, akionyesha dalili kidogo tu za kuzingua mwambie kwaheri asijekukuharibia msingi wako bure, ndio maana nimetangulia kusema kwamba katika stage hii unaweza hata kuifanya muda wako wa ziada baada ya kazi kwani lengo lako kuu hutafuti faida, bali uzoefu na uwezekano wa kupata faida baadae endapo utaamua kuifanya full time kwa mtaji na muda wa kutosha.

SOMA: Jinsi gani naweza kutengeneza pesa kwenye mradi wa mashine ya kukamua mafuta ya alizeti?

Inamaana kwamba hiyo biashara unaweza kuwekeza kiasi kidogo kwanza cha fedha kama biashara ya mtaji mdogo, mfano umesema una kama milioni 5 hivi, wekeza kwanza labda milioni 1  zingine ziweke mahali(benki) zitulie tuli.

..................................................................

Ndugu msomaji wangu kama unamiliki biashara ya rejareja hususan Duka la vyakula mtaani au una ndoto ya kuanzisha biashara ya rejareja siku moja, nakushauri usikose kupitia kitabu kifuatacho japo kurasa mbili au tatu tu za mwisho ambazo kuna Mfumo maalumu unaomwezesha mmiliki wa duka la rejareja kusimamia kwa ufanisi mkubwa biashara yake, mfumo huo uitwao, "TWO IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM" umebuniwa kitaalamu kwa ajili ya kuhakikisha msaidizi au mfanyakazi hadokoi hata senti tano huku mmiliki akifanya majukumu yake mengine bila kuumiza kichwa.


Biashara ya duka la vyakula/mfumo wa usimamizi/two in one store management system

Bei ya kitabu cha karatasi(hardcopy) ni sh. 12,000/=, tunakuletea ulipo Dar, mikoani ongeza gharama ya basi.

Bei ya kitabu(nakala tete) softcopy ni sh.5,000/=

Kwa mahitaji: Whatsapp, 0765553030  au simu, 0712202244


0 Response to "Nataka kuacha kazi nianzishe biashara kwa mtaji wa milion 5 hadi10 nishauri nianze biashara ipi?"

Post a Comment