JINSI GANI NAWEZA KUTENGENEZA PESA KWENYE MRADI WA MASHINE YA KUKAMUA MAFUTA YA ALIZETI? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JINSI GANI NAWEZA KUTENGENEZA PESA KWENYE MRADI WA MASHINE YA KUKAMUA MAFUTA YA ALIZETI?

ushauri, biashara ya kukamua mafuta ya alizeti
Kwenye kipengele hiki cha Ongea na mshauri wa biashara, leo kuna msomaji mmja ambaye kama nilivyoahidi siwezi kutaja jina lake lakini huwa swali na majibu nayaweka hapa katika blogu ya jifunzeujasiriamali kusudi na wajasiriamali wengine nao waweze kunufaika na majibu ya swali hilo.

Msomaji wetu huyo aliuliza hivi; 

"Ni jinsi gani nitaweza kutengeneza pesa kwenye mradi wa mashine ya kukamua mafuta ya alizeti?"

Majibu.
Ngugu( ….), mradi wowote ule wa kiuchumi unaotengeneza faida ni biashara, na biashara zote duniani ni lazima zipitie mchakato utakaohusisha vipengele mbalimbali kama vile hatua ya wazo, utafiti kujua ikiwa wazo linalipa au la, mtaji na vyanzo vyake, kuanza biashara yenyewe, soko, ushindani, timu itakayofanya kazi na uongozi, maswala ya fedha nk.

Hatua zote hizo kwa kifupi mtu unaweza ukazielezea kwenye kitu kinachoitwa mchanganuo au mpango wa biashara, lakini pia kabla ya mpango wenyewe wa biashara ni lazima ufanye utafiti wa soko lako na maswala yote yanayohusika na biashara hiyo ili kuifahamu vizuri kabla haujaianza. 

Na katika hatua hiyo ya mwanzo kabisa kabla hata haujaandika mpango wa biashara, unaweza kufanya tathmini nyepesi iitwayo, Mauzo yanayorudisha gharama zote(Brea even Analysis) inayokuwezesha kujua ikiwa mradi unaweza kukurudishia gharama utakazoweka na katika muda gani. 


Kufanya utafiti wa soko lako na kuandika mpango wa biashara kutakusaidia kupunguza hatari ya kuja kufeli kwa biashara kwani utagundua makosa mengi kabla hata hujaanza ikiwa ni pamoja na kujua ikiwa biashara itaweza kuleta faida ama la.

Kwa hiyo ndugu yangu (….), mimi siwezi nikakutabiria ikiwa utapata faida au hutapata kwani sijafanya utafiti wa biashara hiyo, ila ninaloweza kukuambia ni kwamba sekta ya kilimo na hususani ukamuaji wa mafuta ya alizeti kama ulivyosema ni sekta ambayo ina fursa kubwa bado na bila shaka ni biashara yenye faida. Mwelekeo wa jamii(trend) kiujumla ni watu kupenda mafuta au vyakula visivyokuwa na lehemu au mafuta ya mgando, wanahitaji mno mafuta ya mimea kama alizeti. Cha msingi hapo ni wewe kuingia kwenye utafiti na hatimaye uandike mchanganuo hata ikiwa siyo mchanganuo rasmi sana.


Na mchanganuo wenyewe siyo lazima uuandike kwenye makaratasi au kompyuta, unaweza tu kuuhifadhi katika kichwa chako, au pia kuna ‘option’ zingine kama vile kuandika kitu kinachoitwa, MPANGO WA BIASHARA WA DAKIKA 15, au kwa jina jingine UKURASA MMOJA WA MCHANGANUO.

Ikiwa utapenda kufahamu zaidi namna ya kufanya utafiti wa biashara na jinsi ya kuandika mchanganuo wa biashara iwe ni mchanganuo sanifu uliokamilika kila kitu au hata ni ule 'simple' tu, kurasa moja au mbili kwa ajili ya kuthibitisha wazo la biashara yako kama ni zuri au halifai, basi nakushauri kupata angalao moja kati ya huduma zetu zifuatazo;

1. KUJIUNGA NA SEMINA YA MICHANGANUO SH. 10,000/= AMBAPO UTAPEWA NA KITABU CHA BURE(SOFTCOPY) CHA MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI NA VITU VINGINE VINGI KAMA TEMPLATES UTAKAZODOWNLOAD KUTOKA KWENYE BLOGU HII YA MICHANGANUO(itafunguka baada tu ya kulipia na kuunganishwa).

2. KUNUNUA KITABU CHA MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI CHA KARATASI HARDCOPY SH. 20,000/= AMBAPO UTALETEWA KITABU MPAKA ULIPO MOJA KWA MOJA KAMA UPO DAR ES SALAAM NA KAMA UPO MIKOANI TUTAKUTUMIA KWA BASI

3. KUNUNUA KITABU CHA MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI KATIKA MFUMO WA E-MAIL(PDF)  SH. 10,000/= NA TUNAKUTUMIA HARAKA KWA EMAIL BAADA YA KUTUMA PESA NA ANUANI YAKO YA EMAIL KATIKA NAMBA, 0712202244  AU  0765553030 ,JINA PETER AUGUSTINO

Ndugu yangu(…..)nadhani mpaka hapo nitakuwa nimejitahidi kukupa majibu ya swali lako na ikiwa utakuwa bado na maswali mengine unaweza kutuma kwa email, jifunzeujasiriamali@gmail.com

ASANTE
Peter A. Tarimo



0 Response to "JINSI GANI NAWEZA KUTENGENEZA PESA KWENYE MRADI WA MASHINE YA KUKAMUA MAFUTA YA ALIZETI?"

Post a Comment