SEHEMU NGUMU KULIKO ZOTE UNAPOANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SEHEMU NGUMU KULIKO ZOTE UNAPOANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA

Mahesabu au namba za mchanganuo wa biashara

Watu wengi husema kwamba sehemu ngumu zaidi wakati wa kuandika mpango wa biashara ni sehemu au kipengele cha fedha. Hili linaweza likawa na ukweli lakini mimi nasema inategemea na vile mtu anavyochukulia suala zima la mahesabu kwani kwa mfano kuna baadhi ya watu wengine hata mashuleni au vyuoni wao wakati wengine wakisema hesabu ni ngumu kwao huona ni kitu rahisi. Hivyo hata mahesabu kwenye mchanganuo wa biashara unapokuwa umezishika kanuni zake vizuri basi wala siyo kitu kigumu vile wengi tunavyoamini.

Kama tulivyokwisha kuona katika semina yetu ya michanganuo ya biashara ndani  ya blogu ya darasa la semina, hesabu au namba katika mpango wa biashara ni makisio siyo hesabu halisi hivyo hesabu za mwanzo kabisa ambazo ni makisio ya mahitaji na vyanzo ya mahitaji, wengine kwa lugha rahisi ya kawaida huita mtaji wa kuanzia. Na mahitaji au mtaji wa kuanzia hasa ni kwa biashara mpya kabisa lakini kwa biashara ya zamani ni hesabu za kipindi cha nyuma ndizo zinazoangaliwa kuamua ikiwa biashara ina kiasi gani cha fedha zitakazoendesha biashara kwa kipindi kingine tena.

Hayo yote bila shaka yapo ndani ya yake masomo yetu 11 ya semina kwenye blogu ya darasa la semina. Lakini ili kuweza kuzishika vizuri kanuni za mahesabu ya kwenye mchanganuo wa biashara mtu hauna budi kuyafahamu maana ya maneno kadhaa ambayo pia yamo ndani ya kitabu chetu tunachokitoa bure(softcopy) kwa yeyote anayelipia semina, kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NAUJASIRIAMALI. 

Kwa hardcopy analipia elfu 10 badala ya elfu 20. Kitabu hicho mbali na kuwa na kozi ya michanganuo, vilevile kimesheheni masomo yote ya biashara na ujasiriamali kuanzia, maana ya ujasiriamali wenyewe na jinsi ya kuanza biashara mpaka usimamizi wa biashara na njia wanazotumia matajiri kutajirika haraka. Unapokuwa nacho ni sawa na kuua ndege wengi kwa jiwe moja. Baadhi ya maneno hayo ninayosema ni haya yafuatayo;

Mali(Assets); ni rasilimali au vitu biashara  inavyomiliki kama  vile fedha taslimu, fedha biashara inazodai kutoka kwa wateja (wadaiwa), bidhaa zilizopo, ardhi, majengo, magari, samani(fenicha) nk.

Madeni (liabilities);  ni fedha au rasilimali zozote ambazo biashara  inadaiwa na watu au taasisi nyingine.

Mtaji (capital);  Ni fedha au mali zilizowekezwa na mmiliki/wamiliki. Ni dhamani halisi ya biashara au “fedha unazoidai biashara” kumbuka hapa biashara ni kitu kinachojitegemea tofauti na wewe mwenyewe hivyo unapoipa fedha ni sawa na umeikopesha. Ipo kanuni muhimu sana inayosema hivi;

 (Mali (Asset) = Madeni (Mikopo uliyokopa) + Mtaji (fedha zako)

Ina maana kwamba, biashara inamiliki mali ambazo zimenunuliwa kwa  fedha zilizotolewa na wale walioianzisha hiyo biashara na, au kwa fedha za mkopo. Ikiwa mwanzilishi/waanzilishi hawajatoa fedha yeyote basi itawabidi wakope ili biashara  iweze kuwa na mali (Asset) .Vile vile biashara inaweza ikawa na mtaji wa waanzilishi pekee bila kukopa yaani,  Mali = Mtaji.

Mauzo (sales); Kubadilishana bidhaa kwa fedha. Mauzo yanaweza yakawa katika fedha taslimu au mkopo.

Gharama  za mauzo (Cost  of sales);  ni zile gharama  za moja  kwa moja zinazosababisha bidhaa/huduma kuzalishwa au kununuliwa, kwa mfano;  unaponunua  embe ili ukaliuze  basi gharama ya mauzo ni kile kiasi ulicholipa kununua lile embe pamoja na nauli  uliyolipa kulisafirisha.

Faida ghafi(Gross Margin); Ni faida kabla haujatoa gharama za uendeshaji, riba na kodi.Unapochukua mauzo ukatoa gharama za mauzo/uzalishaji, jibu lake ndio faida ghafi.

Gharama kudumu za uendeshaji  (operating  exprenses);  hizi ni zile gharama  ambazo hazihusiani  na bidhaa  au huduma,  tukichukua mfano wetu wa embe ni ile kodi unayolipia pango la genge/chumba cha biashara, matangazo mbalimbali unayofanya,  mshahara  wa mfanyakazi, bili za simu, na vitu vyote  biashara inavyolipa lakini haviuzwi. Hata kama hutazalisha au kuuza bidhaa/huduma hata moja gharama hizi zipo palepale.

Faida halisi (net profit); unapochukua  mauzo ukatoa gharama za mauzo halafu ukatoa tena gharama za uendeshaji jibu lake ni Faida halisi.

Hayo ni baadhi tu ya maneno machache yanayohusiana na sehemu ya fedha wakati unapokokotoa mahesabu hayo, kuyafahamu pamoja na baadhi ya kanuni zinazoambatana nazo ambazo zimefundishwa vizuri kwenye masomo ya semina ndiyo ufunguo wa kuelewa vyema sehemu hiyo ya hesabu za mchanganuo wa biashara inayosadikiwa na watu wengi kuwa ni ngumu kumbe siyo.

……………………………………………………………………..

Ndugu msomaji wangu ikiwa bado hujajiunga na semina ya michanganuo, wahi sasa hujachelewa, semina hii ni nafasi pekee ya gharama ya chini kabisa ya kujifunza namna ya kuandika mpango wa biashara, huwezi kupata masomo haya kwa kina namna hiyo katika gharama ndogo kiasi hiki, hii ni ofa ya kipekee na itakapomalizika bei haiwezi kubakia tena kama ilivyo sasa. 

Na zaidi ya hayo wakufunzi wako tumejitolea na kuacha vitu vingi kwa ajili ya kuelekeza nguvu zetu zote kwenye semina kwa ajili ya washiriki katika kipindi cha wastani wa mwezi mmoja na nusu hivi, baada ya hapo pia hata kama semina itaendelea lakini “concetration” hiyo itakuwa imepungua kidogo.

Huwezi kuamini muda wote tupo karibu na washiriki wa semina yeyote anapouliza kitu au ana shida fulani kuhusiana na semina tunamhudumia mara moja bila kuchelewa. Ikiwa unataka kujua namna ya kulipia ili kujiunga na masomo hayo fungua ukurasa huu, JINSI YAKUJIUNGA NA MASOMO YA SEMINA YA MICHANGANUO YA BIASHARA.
                           





0 Response to "SEHEMU NGUMU KULIKO ZOTE UNAPOANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA"

Post a Comment