JIBU HITAJI AU TATIZO LA MSINGI WATEJA WAKO WATARAJIWA LINALOWASUMBUA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JIBU HITAJI AU TATIZO LA MSINGI WATEJA WAKO WATARAJIWA LINALOWASUMBUA

Kitu kikubwa kabisa unapotaka kuandika mpango wa biashara ni kujua kwanza ni mahitaji gani au matatizo gani wateja wanayotaka bidhaa au huduma zao ziyatatue; “Business plan, It’s all about finding what is the problem a customer needs to be solved by your service or productUlisha lifahamu hilo pamoja na kujua namna utakavyowatatulia wateja shida hiyo kwa ufanisi zaidi kuwashinda watu wengine wanaotatua shida za wateja kama wewe, basi biashara hiyo utakuwa umeibuka kidedea.

Kwa hiyo mchanganuo wa biashara kama maelezo mengi kuhusiana na biashara wakati mwingine yanaweza yasiwe na umuhimu mkubwa sana kama mtu utakuwa na haraka au kutojua namna ya kuandika mchanganuo wenyewe. Kama nilivyoandika jana juu ya njia 3 mtu anazoweza akazitumia kuifanya kazi ya kuandika mpango wa biashara kuwa nyepesi, leo hii nimeamua kuendelezea nilipoacha jana kwani njia moja niliyoahidi  sikuwa bado nimeiweka rasmi katika ile Blogu yetu ya SEMINA kwa ajili ya washiriki kuipakua.

SOMA: Kuku ni utajiri. soma mchanganuo wa kuku 1000 wa mayai

Hata washiriki wengi wakaanza kunitania, “Vipi mkufunzi mbona unaaza kuleta usanii?” lakini sasa nawajibu semina hii nimeamua kujitolea na nipo ‘serious’ kwelikweli siwezi kuwaangusha hata kidogo. Kwanza niseme tu kwamba washiriki ambao bado hawajaanza kuweka msingi wa mipango ya biashara zao za mazoezi nawaomba watafute daftari zuri au kama ni kompyuta basi wafungue ‘document’ watakayoanza kujaza vitu ndani kusudi baada ya muda waje waunganishe mipango yao kuwa mchanganuo kamili. 

Unaanza kuifikiria biashara unayoiandikia mpango, kila hatua ni vitu gani utavifanya na kisha unaandika kwenye hilo daftari au kompyuta. Mambo yako hayo utakayokuwa ukiyaandika ni lazima yatokane na utafiti kusudi yaweze kuwa na ukweli na siyo vitu vya kutunga au hadithi. Kama ni bei za bidhaa basi zioane kweli na bei za bidhaa hiyo au huduma iliyopo sokoni.

Nirudie tena kwani kauli hii nimeisema mahali pengi hasa kwenye masomo yetu yaliyopo kwenye blogu ya MICHANGANUO, “Unaposikia aina mbali mbali za michanganuo ya biashara,sijui mpango mkakati, sijui mpango wa masoko, upembuzi yakinifu, andiko la biashara, mpango wa utekelezaji na hata “UKURASA MMOJA WA MCHANGANUO” kama huu nitakaouzungumzia leo hii na ambao nimeweka mfano(sample) wake mzima kwenye blogu ya MICHANGANUO, aina zote hizo wala zisikuchanganye akili ukadhani labda kila moja ni aina ya kipekee sana ya mchanganuo. Zote ni mchanganuo wa biashara uleule ila katika sura na maumbile tofautitofauti

Utakuta kila aina ina vipengele vilevile lakini hutofautiana katika wingi wa vipengele au wingi au uchache wa maelezo tu, kwa mfano unaposema Ukurasa mmoja wa mchanganuo ni mchanganuo lakini ulioshindiliwa ili uweze kuenea katika ukursa mmoja, ni jinsi gani unavyoshindiliwa sasa inabidi uutazame ukurasa huo mmoja ukiwa kamili ndani ya blogu yako ya michanganuo.

Hapa chini nitaenda kuweka kwa kuorodhesha baadhi tu ya vipengele vichache vinavyopatikana ndani ya ukurasa mmoja wa mchanganuo, kwa kweli ni kitu kinachovutia kwani hata unaposoma ukurasa huo wote unapata picha vizuri sana ya biashara nzima itakavyokuwa au ilivyo.


SOMA: Utambulisho rasmi wa semina hii.

Kuna vile vitu vya msingi sana katika biashara kama ulivyoona kwenye kichwa cha makala hii nilivyoandika,  JIBU HITAJI AU TATIZO LA MSINGI WATEJA WAKO WATARAJIWA LINALOWASUMBUA. Vitu vya msingi kama hivyo huwezi ukavikosa katika kila aina ya michanganuo tofauti niliyoitaja nau aina zingine zozote zile hata ikiwa vitaandikwa kwa namna tofauti, Soko halikadhalika, washindani na rasilimali au nguvukazi. Nataka uanze kufahamu kwamba mpango wa biashara siyo kitu cha ajabu bali ni yaleyale mambo unayoyafanya kila siku katika mchakato mzima wa biashara yako.

UKURASA MMOJA WA MCHANGANUO

UTAMBULISHO
Ielezee biashara yako katika sentensi moja ni kitu gani unachokifanya. Kwa mfano utambulisho wa duka la nguo za wanawake unaweza kuwa hivi; “Tunauza nguo zinazomfanya mwanamke kujiamini muda wote na siyo ilimradi nguo tu”. Utambulisho wako ni kile kitu kinachokutofautisha na washindani wako.

TATIZO UNALOTATUA
Eleza hitaji au tatizo lile ambalo wateja wako watarajiwa linawasumbua. Ni kwanini wanahitaji bidhaa ama huduma zako?

SULUHISHO LAKO
Bidhaa au huduma yako ni nini? Ielezee hapa na jinsi itakavyotatua shida ya mteja.

USHINDANI
Ni bidhaa au huduma utakavyowahudumia kwa ufanisi zaidi kuwashinda washindani wako.gani wateja wako watarajiwa wanaitumia kwa sasa kukidhi mahitaji yao? Eleza……………

Nakuomba ukadownload template ya UKURASA HUO MMOJA WA MCHANGANUO uone jinsi unavyotakiwa kuwa, ni kitu gani hasa huwa ndani yake na kisha wewe mwenyewe kwa dakika 15 uandike wa kwako mwenyewe kwa ajili ya uendeshaji kwa ufanisi wa biashara yako. Lakini mpango kamili wa biashara usiache kujifunza kwani kwa kujifunza michanganuo unapanua zaidi uwezo wako wa kufikiri kibiashara na hatimaye uwezo mkubwa zaidi wa kufanya biashara yeyote ile kwa weledi kama walivyo kina Bill Gates, Warren Buffet, Donald Trump, kina Rostam Aziz, MO, Mzee Mengi na Bakhresa.

...........................................................................

TEMBELEA UKURASA WA VITABU VYAKO VYA UJASIRIAMALI NA MAENDELEO BINAFSI HAPA







0 Response to "JIBU HITAJI AU TATIZO LA MSINGI WATEJA WAKO WATARAJIWA LINALOWASUMBUA"

Post a Comment