KUKU NI UTAJIRI: ANGALIA MCHANGANUO JINSI KUKU WA MAYAI WANAVYOWEZA KUKUTAJIRISHA HARAKA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KUKU NI UTAJIRI: ANGALIA MCHANGANUO JINSI KUKU WA MAYAI WANAVYOWEZA KUKUTAJIRISHA HARAKA


Kuku wa mayai, hakuna shaka yeyote kuwa wanaweza katika kipindi kifupi sana wakabadilisha maisha ya mtu yeyote yule kiuchumi licha ya woga wa watu wengi ya kwamba kuku wa kisasa na hususani wale wanaofugwa kwa ajili ya uzalishaji wa mayai wana hatari na changamoto nyingi.

Lakini kuna kitu kimoja ambacho watu wengi hawakifahamu na pindi tu mfugaji yeyote yule wa kuku anapokijua basi  huo ndio utakaokuwa mwanzo wa neema kwake na akiwa mchoyo hawezi kabisa kumdokeza mtu mwingine kwa dhana ileile potofu kuwa akimjulisha na mwingine soko litapungua kumbe kitaalamu wala siyo kweli.


Siri kubwa katika shughuli hii ya ufugaji wa kuku na hasa wale wa mayai si nyingine bali ni, kufahamu kwa undani taratibu na miiko ya ufugaji wa kuku wenyewe wa mayai likiwamo pia na suala zima la mahitataji na gharama za ufugaji wa kuku hao wa mayai kwa njia ya kisasa kabisa. Huwezi kufuga kuku tuseme labda kuku 20 wakati fedha za kuwahudumia mpaka wiki watakayoanza kutaga huna, matokeo yake utawalisha ‘kinjaanjaa’ jambo litakalosababisha wakupe hasara badala ya faida

Kote katika jamii kumejaa elimu hii ya ufugaji wa kuku, kuna majukwaa mbalimbali kuanzia kwenye mitandao ya kijamii, vitabu, majarida na hata semina mbalimbali inakotolewa elimu ya ufugaji bora  wa kuku wa aina zote, iwe ni wale wa mayai, kuku wa nyama, kuku wa kienyeji na aina zingine zote za ndege wafugwao. Kwa kifupi leo hii siyo vigumu hata kidogo kwa mtu kupata elimu ya ufugaji wa kuku kitaalamu.

Katika makala haya nilipenda ufahamu, ni kwa jinsi gani unavyoweza kuwa milionea kwa kazi ya kufuga kuku wa mayai tu, tena wala pasipo kupoteza miaka mingi. Tena mamilioni hayo ya fedha unaweza ukayakisia wewe mwenyewe ni shilingi ngapi  kabla hata haujaanza mradi wenyewe na huo ndio uzuri wa kufuga kuku wa mayai.

Hakuna biashara iliyokuwa nzuri kama ile ambayo unakuwa na uwezo wa kutabiri kwa dhati kabisa baada ya muda tuseme miezi 22 na nusu kama ilivyokuwa kwa kuku wa mayai unaweza ukashika kiasi gani cha pesa kulingana na idadi ya kuku wako ulioanza nao.


Ikiwa utafuata taratibu zote kama inavyopendekezwa na wataalamu ikiwa ni pamoja na kanuni zote za msingi, makisio au utabiri wako unakuwa na uhakika wa asilimia zaidi ya 85%. Ina maana kuwa ikiwa utafuga kuku wa mayai wapatao 1000 basi  una uhakika wa kuwa na kuku zaidi ya 850 watakaokuwa wakitaga utakapofika muda muafaka wa kutaga ambao ni wiki kuanzia ya 18 tangia siku ya kwanzauingize vifaranga wa kuku wa mayai bandani kwako.
 
Kuku ni utajiri:Ufugaji wa kuku bora na wa kisasa wa mayai(kuku 1000)
Haya maneno si kama nayatunga kama hadidhi hapana, ni matokeo ya tafiti za kweli ukiwemo utafiti nilioufanya mimi mwenyewe binafsi kama mfugaji wa kuku wa mayai. Ikiwa utapenda kusoma Mchanganuo  kamili wa biashara hii ya ufugaji wa kuku wa kisasa wa mayai ili uweze kuamini kama ni kweli kuku wa mayai wanaweza kukuletea utajiri, tazama mpango wa biashara huu hapa, jinsi biashara yaufugaji wa kuku wa mayai inavyoweza kumtoa mtu haraka katika umasikini.

Mchanganuo huo unaelezea kila kitu kuanzia gharama za kuanzia kwa mtu anayefuga kuku wa mayai 1000, mbinu na mikakati mbalimbali inayotumika katika uendeshaji wa mradi huu, gharama za uendeshaji,  mapato na faida pamoja na timu nzima ya watu wanaohitajika kuhudumia mradi huo.
 ..................................................................................................


Usikose kujiunga hapa darasa la Michanganuo ya Biashara, kupata mambo mengi usiyoyapata mahali pengine popote pale. Pamoja na kuwa mwanakikundi cha kushauriana mambo mbalimbali ya kiuchumi na ujasiriamali. 

Tafadhali niwaombe wasomaji radhi, kuna watu walinitumia ujumbe kutaka kujiunga na darasa lakini kwa bahati mbaya sikuwajibu kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu, sasa nimerudi na kila kitu kitakwenda kama kilivyokuwa kimepangwa. Asanteni sana wadau wangu wapendwa.

Tembelea pia na SMART BOOKS TZ kujipatia vitabu vyako vya ujasiriamali kwa lugha ya kiswahili.

0 Response to "KUKU NI UTAJIRI: ANGALIA MCHANGANUO JINSI KUKU WA MAYAI WANAVYOWEZA KUKUTAJIRISHA HARAKA"

Post a Comment