SABABU 5: KWANINI MASIKINI WENGI HAWAFANIKIWI KIRAHISI? (NAKOSEA WAPI PART II) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SABABU 5: KWANINI MASIKINI WENGI HAWAFANIKIWI KIRAHISI? (NAKOSEA WAPI PART II).....Nakosea wapi? SEHEMU YA II

Mpenzi msomaji wa blogu hii, katika majibu yangu kwa swali alilouliza msomaji mmoja, A.J Mbawala  kutoka kule Songea Mkoani Ruvuma katika makala iliyopita aliyeuliza,  Kwanini WENGINE HUFANIKIWA KUWA MATAJIRI, MIMI NIMESHINDWA,NAKOSEA WAPI? Wakati namalizia makala hiyo niliahidi kuendeleza majibu ya swali hilo katika makala nyingine ijayo ambayo sasa ndiyo hii unayoisoma.

Niliahidi kuzitaja sababu kubwa tano (5) ni kwanini watu wengi masikini pamoja na jitihada nyingi wanazoweka lakini bado huendelea tu kubakia kuwa masikini, je, wanapenda kuendelea kuwa hivyo au ni kitu gani? Sisemi  kwamba ni watu wote masikini wanaoshindwa kujinasua katika umasikini hapana, wapo pia baadhi wanaotoboa ila si wengi kwa idadi ulilinganisha na idadi ya wale wanaoendelea kuganda kwenye tope hili la umasikini.


Kama nilivyosema siku ile kuzijua sababu hizo na kuziondoa  ndio utakaokuwa mwanzo wa safari yako ya kuufikia utajiri ikiwa kama upo kwenye hali duni ya umasikini. Hivyo bila ya kupoteza muda mwingi zaidi naomba tukazione sababu hizo 5 ni zipi;

1.Matumizi kupita kiasi.
Unaweza ukaona ni jibu rahisi sana au kama mzaha vile, lakini huo ndio ulweli wenyewe ulivyo kwamba watu masikini hufanya matumizi kuzidi wenzao watu matajiri. Badala yake wengi wetu tunaamini kinyume na kauli hii, tunaamini kimakosa kuwa matajiri hufanya ‘matanuzi’ ya kufa mtu na masikini hujibana kupindukia jambo ambalo si kweli aslani.


Kivipi basi?
Kwa kadiri ya vipato vyao, tajiriri hutumia kidogo kushinda masikini. Kwa mfano tuchukulie mtu “A” anayeingiza shilingi milioni 3 kwa mwaka, kipato hiki siyo kidogo sana kwa mwaka lakini mtu huyu utashangaa anaweza kuendelea kuwa masikini,

Kwanini?
Mtu huyu ataendelea kubakia masikini kutokana na vile atakavyofanya matumizi ya hizo milioni 3 zake. Ikiwa atatumia shilingi milioni mbili na laki 8 kati ya milioni 3 atabakiwa na kiasi kidogo sana cha pesa(shilingi laki 2 tu) jambo litakalomfanya aendelee kubakia kuwa masikini milele.

Wakati huohuo hebu tumchukue mtu mwingine “B” ambaye kipato chake ni sawasawa na kile cha mtu “A” shilingi milioni 3 lakini ambaye anajitahidi kuondokana na hali yake ya umasikini.

Anafanyafanyaje?
Ni kwa kupitia namna anavyozitumia fedha zake kama ifuatavyo; “B” anachokifanya ni kujaribu kujiwekea akiba nyingi zaidi kutoka katika kile kipato chake cha shilingi milioni 3 kwa kupunguza matumizi yake mengine yasiyokuwa ya lazima.


Hivyo wakati mtu tajiri ama tuseme mtu aliye na mawazo ya kitajiri akiweka akiba karibu asilimia 50% ya mshahara/kipato chake (chaweza kuwa faida ya biashara au mshahara) , masikini au mtu mwenye mawazo ya kimasikini yeye hula kila kitu(kutumia) na, au kusaliwa na pesa kidogo sana ambazo nazo hata kuziweka kama akiba mwishowe hushindikana kutokana na ama kuibuka matumizi ya dharura au tu kuamua kuzitumia kwa sababu zinaonekana ni kidogo haziwezi kuja kufanyia jambo la maana.

Ijapokuwa unaweza ukamuona mtu tajiri akifanya matumizi mengi na ya mara kwa mara kuliko masikini  lakini bado anakuwa na kipato kikubwa zaidi kwa maana ya asilimia. Si ajabu asilimia ya matumizi yake yote kwenye mapato yake hayafiki hata asilimia 10%, masikini yeye anaweza hata akafanya matumizi yake ya kawaida kwa asilimia 90% ya mapato yote, akaweka akiba pengine asilimia 1% tu au 2% tu pasipo kujua kwamba hilo ni janga hatari sana kwake linaloweza kumfanya awe masikini milele.

Hitimisho ni kuwa, kuweka akiba kidogo sana au kutokuweka kabisa akiba ndio sababu kubwa ni kwanini watu wengi masikini huendelea kubakia kuwa masikini. Unapojiwekea akiba kidogo sana kutoka katika mapato yako tuseme labda asilimia 1% au 2% kama tulivyoona kwenye mfano wetu kwa mtu “A”  utaishia kukata tamaa ya kuweka akiba yenyewe na kuona ni bora tu uzitafune au uzitumie kwa mambo mengine madogomadogo.


2. Kutokujiwekea mpango wa Dharura(Tahadhari)
Wakati matajiri hupanga kabisa mipango yao kwa ajili ya dharura, masikini wao hulichukulia jambo hili kama vile ni uchuro kwao. Ni ukweli kwamba hamna mtu awezaje kutabiri kwa uhakika wa asilimia 100% kuwa ni lili jambo baya litaweza kutokea lakini tunaweza kujitayarisha kwa ajili ya jambo lolote lile la dharura linaloweza kutupata kwa kuweka pembeni kiasi cha fedha mbali na ile akiba ya kawaida kwa ajili ya dharura au kama tahadhari kwa lolote lile ambalo hatukulitegemea. Kiasi hiki inapendekezwa kiwe angalao ni mara tatu 3 ya matumizi yako ya kila mwezi, ikiwa kwa mwezi matumizi yako ni shiligi mfano laki 1 basi uwe na fedha ya dharura shilingi laki 3 mahali muda wote.

Matajiri pamoja na kuwa na fedha za dharura lakini pia hujiwekea Bima za aina mbalimbali kama vile bima ya afya, bima ya maisha, bima ya gari, bima ya maisha nk. Pesa ya dharura hushughulika tu na mambo yale bima haiwezi kushughulikia. Masikini huwa hawana kabisa mipango hii na matokeo yake hujikuta majanga au dharura zinapoibuka hugeukia kaakiba kidogo walikodunduliza na kubakia masikini milele.


3. Hujibebesha Mizigo ya Madeni.
Ingawa Matajiri uwezo wao wa kulipa madeni ni mkubwa lakini kamwe huwa hawaruhusu kuwa na madeni ya hovyohovyo, madeni yasiyokuwa na mpango siyo kitu kizuri kabisa kwao, ni utumwa badala ya uhuru wa kifedha. Masikini wengi hujikuta wakitumia zaidi ya asilimia 30% mpaka 50% ya mapato yao kulipa madeni. Kwa matajiri wao kiwango ni cha chini zaidi.

Tatizo la masikini ni kwamba, hukopa na kisha kuzitumia pesa za mkopo katika “matanuzi”(Matumizi yasiyokuwa na faida au katika starehe). Mfano utakuta mtu akinunua, samani za ndani, simu ya bei, usafiri binafsi nk. kwa kutumia fedha za mkopo. Matajiri huwa hawafanyi kitu cha namna hiyo, hutumia kwa umakini mkubwa mikopo kwa kuwekeza tu katika biashara na miradi waliyoiombea hiyo mikopo. Kama ni matumizi basi watasubiria mpaka pale miradi au biashara hizo zitakapotengeneza faida. Kabla tajiri hajanunua chochote kwa ajili ya matumizi yake binafsi hupanga kwanza, mfano akitaka kununua gari mwakani ataanza kuweka mipango leo kwa kujiwekea fedha kidogokidogo kila mwezi mpaka pale zitakapotimia ndipo anunue gari na wala siyo kukimbilia kwenda kununua gari kwa fedha za mkopo.


4.Kutokujishughulisha na elimu ya Uhuru wa kifedha.
Wakati Matajiri muda wote hujielimuisha jinsi ya kuwa huru kifedha, Masikini yeye hana muda na kujifunza chochote kuhusiana na uhuru wa kifedha na wala wengi hawafahamu ni nini maana ya uhuru wa kifedha.

Hawajui kama kuwa huru kifedha ndio hatua muhimu zaidi ya mtu kuwa tajiri. Na safari ya kuwa huru kifedha huchukua muda mrefu hivyo ni vizuri mtu kuanza mapema iwezekanavyo. Tajiri wa leo hakuanza safari yake jana au juzi, ni muda mrefu huko nyuma.

Uhuru wa kifedha unaanza hivi;

Mtu kwa kutumia kipato chake cha kawaida, iwe ni mshahara au faida ya biashara, huwekeza kwenye vitegauchumi tofautitofauti na faida inayopatikana ndio ataitumia kwenye matumizi yake ya kila siku ya kawaida, Kwa upande wa mtu masikini yeye atachukua kipato chake karibu chote au chote kabisa na kukitumia katika matumizi yake ya kila siku ya kawaida. Ikiwa kipato hicho atabakiza kiasi kidogo kama akiba basi ndio atakachowekeza hapa na pale. Kwa mtindo huo tajiri ataweza kutajirika haraka huku masikini akiendelea kukimbizana na kipato cha siku au mwezi kwa mwezi.


5. Kutokujua njia sahihi za kuwekeza fedha.
Matajiri ni wajanja sana, hawawekezi kabla kwanza ya kufanya uchunguzi, kwa upande wa masikini wengi wao wakiwekeza fedha hufuata mkumbo au pasipo kufikiria kwa kina. Mfano ni uwekezaji katika biashara ya hisa, matajiri wanajua ni muda gani wanunue hisa na muda upi waziuze kwa faida. Masikini yeye atanunua hisa ilimradi tu amenunua pasipo kujua kama zimepanda au kushuka sokoni.

Si hivyo tu, tajiri akinunua rasilimali kwa mfano kiwanja, atakiacha mpaka kiwanja  hicho kitakapopanda thamani yake ndipo akiuze au kukifanyia miradi ya faida kubwa zaidi lakini masikini anaweza akanunua kiwanja leo hii na kukiuza kesho yeke au keshokutwa kisa tu pengine hana hela ya kumlipia mwanae ada ya shule. Matajiri hununua nyumba au rasilimali nyinginezo na kisha kuzikodisha kwa watu lakini masikini ukiona kanunua rasilimali au nyumba basi ujue ni kwa ajili ya matumizi yake mwenyewe siyo uwekezaji.


Matajiri hununua dhahabu kama tahadhari endapo uchumi utadorora lakini masikini ukimkuta kwa sonara basi ujue tu ni lazima ana shughuli ya ndoa(harusi) siku ya karibuni au kuna mtu wake wa karibu katika familia/ukoo anaoa, kuozesha au kuolewa.

Hitimisho.
Mpaka hapo, kuna mengi tumeweza kujifunza kutokana na makosa wanayoyafanya watu masikini yanayowagharimu kuendelea kubakia kama walivyo milele. Njia pekee ya uhakika ya kujinnasua na hali hiyo ni kwa mtu kuchukua hatua ya kuyakwepa makosa hayo kwa nguvu zake zote.

Hapa chini nakuwekea tena kwa ufupi yale yote tuliyozungumzia leo katika makala hii(Jinsi utakavyorekebisha makosa wafanyayo masikini), ikiwa pengine utakuwa hujaweza kushika kila kitu kilichoelezwa;

1.  Kwanza kabisa jifunze namna ya kuwa huru kifedha
2.  Bajeti fedha zako, mapato na matumizi.
3.  Punguza utegemezi kwenye madeni kwa kujiwekea mipango yako kabla.
4.  Jiwekee fedha kwa ajili ya dharura itakayotosha matumizi yako yote katika miezi 3 ikiwa itatokea kwa bahati mbaya kipato chako cha mwezi kimekoma ghafla.
5.  Ongeza kipato chako cha ziada.
6.  Wekeza fedha zako kwa busara kama wafanyavyo matajiri

……………………………………………………….      

TAARIFA: KWA ANAYEHITAJI KUJIFUNZA ZAIDI
HII NI KWA YULE TU AMBAYE HAJAJIUNGA BADO NA GROUP LA (WASAP MASTERMIND GROUP) LA MICHANGANUO-ONLINE AU KUSOMA VITABU VYA SELF HELP BOOKS TZ

Najua wapo wadau ambao mmejiunga kwa email hivi karibuni na hivyo hamjapata fursa ya kufahamu Programu zetu nyingine kama wale waliotangulia, hivyo naomba kuchukua nafasi hii kidogo kuwajulisha Programu hizo.

PROGRAMU#1
SELF HELP BOOKS TANZANIA tuna vitabu mbalimbali vya ujasiriamali katika lugha ya Kiswahili na miongoni mwavyo ni hivi vikuu vitatu.
1.MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI
2.MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA
3. MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIOPENDA KUITOA.

Vitabu vyote 3 softcopy kwa njia ya email ni sh. Elfu 18 na hardcopy kama upo Dar es salaam unaletewa ulipo kwa sh. Elfu 37. Unaweza kupata kimojakimoja pia. Ukinunua vitabu vyote 3 softcopy au hardcopy unapata pia offa ya kujiunga na MASTERMIND GROUP la wasap bure pamoja na michanganuo kadhaa na vitabu vingine 4(softcopy) bila malipo yeyote.

PROGRAMU#2
MASTERMIND GROUP LA WATSAP
Tunalo group la masomo na mijadala ya kila siku WASAP ambalo tunajifunza hasa Vitu 2 kwa undani, Jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara mbalimbali zinazolipa haraka pamoja na masomo yenye maudhui ya pesa(MZUNGUKO WA FEDHA KWENYE BIASHARA ZETU). Ada ya kujiunga ni sh. Elfu 10 tu mwaka mzima na punde baada ya malipo tunakutumia kupitia wasap au email vitu vyote hivi vifuatavyo;

1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  Kitabu kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1

3.  Kitabu kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2

4.  Kitabu kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.

5.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

6.  SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

7.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

8.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza

9.  Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.

10.              Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

11.              Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

12.              Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.

13.              Ukurasa mmoja wa mchanganuo.

PROGRAMU#3
PACKAGE NZIMA(kifurushi) cha semina kubwa ya jinsi ya kuandaa hesabu za mpango wa biashara(ADVANCED BUSINESS PLAN FINANCIALS) katika mfumo wa PDF. Bei yake ni sh. 10,000(Bado ipo kwenye offa, baadae itarudia bei yake ya kawaida sh. elfu 20)

UKITAKA PROGRAMU ZOTE 3 KWA PAMOJA KATIKA SIMU, KOMPYUTA AU TABLET YAKO NI SH. ELFU 38 TU.


ASANTE SANA,
PETER A. TARIMO
Wasap:0765553030
Simu:   0712202244
self help books Tanzania


0 Response to "SABABU 5: KWANINI MASIKINI WENGI HAWAFANIKIWI KIRAHISI? (NAKOSEA WAPI PART II)"

Post a Comment