KUTUMIA NYUMBA KIWANJA AU ARDHI KAMA REHANI KUOMBA MKOPO NI SAHIHI? NAOMBA USHAURI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KUTUMIA NYUMBA KIWANJA AU ARDHI KAMA REHANI KUOMBA MKOPO NI SAHIHI? NAOMBA USHAURI


Msomaji wa blogu hii kutoka Songea Mkoani Ruvuma ameuliza maswali yake matatu, pia kuna maswali mengine kadhaa ya wasomaji wengine ambayo yote kwa pamoja nitayajibu kwa mfululizo katika makala zinazoanza leo mpaka pale maswali yote yatakapomalizika. Swali lake la kwanza kutoka Songea aliuliza  hivi;

SOMA: Kufungua kiwanda kidogo cha kusindika & kufungasha nafaka. naomba ushauri.

“Hivi kuweka rehani kiwanja, nyumba au ardhi kwa ujumla ili kupata mkopo ni sahihi na inawezekana?”

JIBU:
Ndugu msomaji, umenikumbusha mbali sana ulivyotaja kuwa unatokea Songea, Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla una fursa nyingi sana na nzuri za kiuchumi hasa katika shughuli za biashara ya mazao ya chakula na hata biashara nyinginezo, nasema hivyo kwani niliwahi kuishi mkoani humo na nilijihusisha na kilimo cha mbogamboga na matunda kama nyanya pale Ruhuwiko japo kwa kiasi kidogo, najua jinsi mazao mengi yanavyostawi huko hasa mahindi mihogo na mazao mengine yote, kwa ujumla Songea kila zao hustawi.


Kuhusu iwapo ni jambo zuri kuweka rehani rasilimali zako kama dhamana ya mkopo, hilo ni jambo sahihi kabisa na duniani kote mikopo hasa ile ya mabenki mkopaji huwezi ukapewa mkopo pasipo kuonyesha kwanza hati miliki ya dhamana iwe ni nyumba, kiwanja, ardhi au mali nyingine yeyote itakayokuwa kama ulinzi endapo ikatokea ukashindwa kulipa mkopo utakaopewa. Ni ukweli mchungu kwamba hakuna mkopo rahisi popote pake ila tu urahisi wa kupata au kuomba mkopo utategemea vigezo mbalimbali vikiwemo, ukubwa wa mkopo unaoomba, aina ya taasisi unayoiomba mkopo, aina ya dhamana unazotumia kuombea huo mkopo nk.

Pia ni lazima ukumbuke ya kwamba hakuna mkopo usiokuwa na dhamana. Hata ile mikopo ya vikundi dhamana yake kubwa ni ile wakopaji kuwa katika vikundi vya watu kadhaa marafiki wanaofahamiana vizuri na kuaminiana. Kwa mtindo huo benki au taasisi inayokopesha hujiridhisha kuwa mmoja wao atakaposhindwa kulipa marejesho ya mkopo basi wenzake ndio watakaowajibika kumlipia au kukata akiba zao.


Unapoomba mkopo tuseme labda benki, ukapewa fomu ya maombi ya mkopo,(loan application form), kuna mahali utahitajika kujaza dhamana utakazoweka, kisha afisa anayehusika atakwenda kuzikagua ili kuzitathmini kama zinalingana na kiasi cha mkopo unaoomba kupatiwa. Ikiwa vigezo vyote utatimiza matokeo yake ni kupewa mkopo ambao utaingiziwa katika akaunti yako ya mkopo. Zipo aina mbili za hatimiliki za mali, hatimiliki ya serikali na hatimiliki za kimila

Kuna masharti katika sheria ya rehani yanayohusiana na dhamana ya mkopo kwa pande zote mbili yaani Mkopaji na mkopeshaji ambayo yanahitajika na sheria ya ardhi ya Tanzania ya mwaka 1999 sura ya 334 kifungu cha 24 mpaka cha 30 kama vile mkopaji kuhakikisha anamhusisha mwanandoa ikiwa dhamana ni mali ya familia na kutokupangisha au kuuza dhamana kabla ya kumaliza kulipa mkopo bila idhini ya maandishi kutoka kwa mkopeshaji.


Kwa upande wa mkopeshaji naye anatakiwa kutoa taarifa ya siku (60) kwa umma endapo kutakuwa na ucheleweshwaji wa marejesho au uvunjifu wa masharti kwa mkopaji kabla ya hatua ya kuuza mali iliyowekwa rehani. Baada ya hizo siku 60 nyumba au mali hupigwa mnada kwa kutoa taarifa au notisi ya siku 10 kwa wale wanaoishi ndani ya nyumba hiyo au mmiliki. Mkopeshaji pia haruhusiwi kununua mali iliyowekwa dhamana labda kwa kibali maalumu cha mahakama. Watu wengine hudhani benki au taasisi ya fedha kutangaza mnada wa mali wanazoweka rehani siyo huduma nzuri kwa mteja(bad customer care) lakini kumbuka sheria ya nchi inawataka kufanya hivyo.

Kuweka rehani hatimiliki ya mali yako ili kujipatia mkopo siyo jambo baya na wala hakuwezi kukupa madhara yeyote endapo utazingati masharti yote yanayotakiwa ikiwa ni pamoja na kuwa na nidhamu nzuri ya pesa ili kuhakikisha fedha unazokopa zinafanya ile shughuli uliyokusudia tu na wala siyo kwenda kufanyia starehe au matumizi ya kawaida ya kifamilia ambayo mishowe fedha hupotea na huwezi tena kuzipata ili urejeshe kule ulikozikopa.


Matumizi mazuri ya fedha za mkopo ni kwenda kuziwekeza katika mradi uliokusudia au katika vyanzo vingine vya uhakika vya mapato ambavyo hatimaye vitakuletea faida kifedha utakayoitumia kurejesha mkopo wa watu, riba yake na mahitaji yako mengine ya kila siku.

Huo ndio mwisho wa majibu ya swali la kwanza kutoka kwa msomaji wetu wa Songea Ruvuma, tukutane tena katika makala itakayofuata baada ya hii kwa ajili ya majibu ya swali lake la pili.

NJIA RAHISI ZAIDI YA KUPATA VITABU VYA SELF HELP BOOKS TANZANIA NI KUPITIA EMAIL YAKO, SOFTCOPY NI BEI RAHISI, HUKUFIKIA HARAKA, NA KWA UHAKIKA.


UNACHOTAKIWA KUFANYA TU NI KULIPIA KITABU/VITABU UNAVYOTAKA KUPITIA SIMU YAKO KWA NAMBA 0712202244  AU  0765553030 JINA PETER AUGUSTINO TARIMO, TUMA NA ANUANI YAKO YA EMAIL KWA MESEJI, HALAFU TUNAKUTUMIA KITABU/VITABU MUDA HUOHUO BILA KUCHELEWA UNADOWNLOAD.

Bei: 10,000/= softcopy


Bei: 5,000/= softcopy




Bei: 10,000/= softcopy

0 Response to "KUTUMIA NYUMBA KIWANJA AU ARDHI KAMA REHANI KUOMBA MKOPO NI SAHIHI? NAOMBA USHAURI"

Post a Comment