KANUNI ZA KUGUNDUA UWEKEZAJI UNAOLIPA PESA NYINGI ZAIDI UKITUMIA VIGEZO VYA FAIDA, HATARI & UOEVU WA MRADI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KANUNI ZA KUGUNDUA UWEKEZAJI UNAOLIPA PESA NYINGI ZAIDI UKITUMIA VIGEZO VYA FAIDA, HATARI & UOEVU WA MRADI

Mradi wa  uwekezaji katika kuku
Kwa mwekezaji mchanga anayeanza inaweza kuwa mtihani kwake kuamua ni uwekezaji gani aanze nao kati ya miradi mbalimbali ya uwekezaji iliyopo. Mtu anaweza akafikiria na kujiuliza, Sijui niwekeze kwenye hisa?, ninunue dhahabu na kuziweka, ninunue vipande(UTT), nifungue akaunti ya amana ya kudumu(fixed deposit), ninunue mazao nihifadhi, Nifungue akaunti ya akiba benki, nikalime matikiti, nifuge kuku,  ninunue maturubai na viti nikodishe  Au nianzishe biashara ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo?




Yote hiyo ni miradi mtu anayoweza akatumia fedha zake kuwekeza kwa lengo la kupata faida. Lakini miradi hiyo kila moja hutofautiana na mwingine kutegemeana na vigezo mbalimbali hasa vigezo vitatu ambavyo ndivyo tutakavyokwenda kuviona katia somo hili la leo. Katika kuwekeza fedha zako kuna vitu vitatu muhimu sana,

1.  Hatari ya kupoteza fedha zako(Risk)
2.  Uoevu(Liquidity)
3.  Kiwango cha Faida utakayopata(Returns)

Nitaelezea kila kimoja kisha tutaenda kuona kila uwekezaji au mradi ni kwa jinsi ganii unavyoweza kuamua kuwekeza ukizingatia athari za vitu hivyo. Tutachambua na kuainisha vigezo hivyo kwa biashara zipatazo 8 hivi, kisha tutahitimisha kwa ushauri wa ni nini cha kufanya kama mwekezaji anayeanza.

1.HATARI
Hatari ni uwezekano wa kupotea kwa fedha zako utakazowekeza, kuna miradi yenye uwezekano mkubwa zaidi wa fedha kupotea na mingine hata isiyokuwa na hatari kabisa.

2.UOEVU
Uoevu maana yake ni ile hali au wepesi wa mwekezaji kuweza kubadilisha uwekezaji wake kuwa pesa taslimu. Kupata pesa chapchap unapozihitaji, kuna uwekezaji mwingine ukishatumbukiza fedha zako tu hivi unaweza hata ukafa njaa ikiwa huna njia nyingine ya kujipatia fedha, mingine ukihitaji pesa fasta unapata.

3.FAIDA.
Faida ni hali ya kulipa kwa uwekezaji au mradi wako, kuna uwekezaji mwingine unalipa faida kubwa zaidi na mingine kulipa kwake ni kwa hali ya chini sana au  hailipi chochote.

  
Sasa pasipo kupoteza muda mwingi hebu tuanze kuona ni kwa namna gani vigezo hivi 3 vinavyotegemeana na kuzidi kwa kimoja kunavyoweza kukafanya kingine kipungue, nitaanza kuelezea mifano michache lakini unaweza ukaongeza miradi mingi kadiri mtu unavyoweza.

1.UWEKEZAJI KATIKA HISA.
HATARI - Ni kubwa kutokana na sababu kwamba hazitabiriki muda wowote bei ya hisa inaweza ikaporomoka au kupanda.

UOEVU - Ni kidogo sana kwani itakulazimu usubirie muda mrefu kama utataka ikulipe, ooevu utakuwa mkubwa ukitaka kuziuza harakaharaka

FAIDA - Faida ni kubwa  ikiwa utazishikilia hisa zako kwa kipindi kirefu.

2.UNUNUZI WA NAFAKA NA KUJA KUUZA BAADAE
HATARI – Ni kubwa kutokana na kutokutabirika kwa bei, hali ya hewa na wadudu waharibifu.

UOEVU – Ni wa wastani kutokana na kuwepo na uwezekano wa kuuza mazao yako muda wowote.

FAIDA – Faida ni kubwa


3.AKAUNTI YA AMANA(FIXED DEPOSITS ACCOUNT)
HATARI – Hatari ya uwekezaji huu ni ndogo sana, hakuna uwezekano wa fedha zako kupotea kiurahisi.

UOEVU – Uwezekano wa kugeuza uwekezaji kuwa pesa haraka ni mdogo sana au wakati mwingine ni wa wastani kutokana na mkataba wake kuwa ukishaweka ni mpaka muda ufike huwezi kutoa pesa kirahisirahisi tu. Ukitaka kutoa kabla ya muda kufika upapigwa penati

FAIDA – Faida ni kidogo sana mabenki mengi haifiki hata asilimia 10%

4.KUWEKA FEDHA KATIKA AKAUNTI YA AKIBA
HATARI – Hatari hakuna
UOEVU – Muda wowote unaweza kuchukua cash yako hivyo uoevu ni mkubwa sana
FAIDA – Hakuna faida au ni kidogo mno...........................................

.............................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

Somo hili zima litatolewa leo Tarehe 1/6/2023 katika Mastermind group la Michanganuo-online. Unapewa na masomo mengine yote yaliyopita tangu group lianze, kupata vitu vyote hivi jiunge na group hili kwa kulipa ada sh. elfu 10 tu kwa muda wa miezi 12

Masomo ni kila siku na tunakuwa na semina pia mara kwa mara za jinsi ya kuandika michanganuo ya Biashara zenye fursa kubwa ya kutengeneza faida  haraka.

Ukilipa nakutumia pia OFFA ya e-books na Michanganuo jumla vitu 12 muda huohuo

Kujiunga lipa kiingilio sh. 10,000/= kupitia namba zetu, 0765553030  au 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo. Ukifuatia na ujumbe wa, "NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO & OFFA YA VITU 12"

Ikiwa hutumii wasap unaweza kututumia anuani yako ya E-mail na kila kitu tukakutumia kwa email. 


 OFFA YA VITU 12 NI HII HAPA CHINI;

 

                 1.      COURSE/SEMINA: (compiled complete course) ya Jinsi ya kuandika Mchanganuo wa biashara –(Ukishindwa kuandika mchanganuo wako mwenyewe utarudishiwa pesa zako) - kwa kiswahili

                 2.       KITABUMichanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu za BIASHARA, jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika kila kitu. – kwa kiswahili

                 3.      KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili

                 4.      KITABU: Siri za upishi wa chapati laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili

                 5.       KITABUNjia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 - kwa kiswahili

                 6.       KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ni maarufu sana duniani na ndio hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza

                 7.       MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini Broilers - kwa kiswahili

                 8.      MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza

                 9.      MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji- kwa kiswahili

              10.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili

              11.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza

              12.    MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado millingkwa Kiswahili

              13.    Kuunganishwa Group la masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mwaka mzima ukitaka. (Mentorship group) (Ni hiyari yako lakini, usipotaka hatukuunganishi)

 

Karibu tukutane darasani leo usiku saa 3 tarehe 1/06/2023

Kwa vitabu, michanganuo na semina mbalimbali tembelea duka letu la vitabu SMARTBOOKSTZ

 

Somo hili limeandaliwa na:

Peter Augustino Tarimo

Mtaalamu wa Michanganuo ya biashara aina zote

Phone/Watsap: 0765553030 au 0712202244



0 Response to "KANUNI ZA KUGUNDUA UWEKEZAJI UNAOLIPA PESA NYINGI ZAIDI UKITUMIA VIGEZO VYA FAIDA, HATARI & UOEVU WA MRADI"

Post a Comment