NAMNA BORA ZAIDI YA KUBUNI WAZO LA BIASHARA ITAKAYOLIPA HARAKA BILA MSAADA WA MTU MWINGINE


WAZO LA MFUMO WA BIASHARA INAYOJIENDESHA YENYEWE
…..Namna bora zaidi ya kubuni wazo la biashara ni ipi? Na Je biashara ndogo inaweza ikajiendesha yenyewe kimfumo?

Namna ya kubuni wazo la biashara ni moja kati ya changamoto kubwa wanazokutana nazo wajasiriamali wengi wachanga wanaoanza lakini wala haipaswi kuwa hivyo. Nimekuwa napata maswali  kutoka kwa wajasiriamali na wafanyabiashara hao na swali la hivi karibuni kabisa nililipata jana kutoka kwa msomaji mmoja aliyetaka kupata wazo la biashara kupitia kitabu changu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI.

Aliuliza hivi,
“ Bwana Peter, nahitaji kitabu chako cha Michanganuo  ya biashara na Ujasiriamali, lakini kabla ya kukinunua ningependa unihakikishie kwanza kama nitaweza kupata wazo zuri la biashara itakayonifaa miongoni mwa michanganuo uliyoiweka katika kitabu hicho”

Sikutaka kumpa mjasiriamali huyu mchanga matumaini feki ili tu niuze kitabu changu kwani dhamira yangu kuu si kupata pesa bali ni kuwasaidia wajasiriamali wadogowadogo na wale wa kati kuanzisha na kukuza biashara zao kwa ufanisi mkubwa. Hivyo nilimueleza ukweli tu kwamba ikiwa shida yake ilikuwa ni kupata wazo zuri la biashara kutokana na michanganuo mbalimbali iliyokuwepo katika kitabu kile, basi kitabu hicho kisingeliweza kumsaida kitu na ni bora angeachana na uamuzi wake wa kununua kitabu hicho kwani angekuja kuniona kama vile nilimtapeli.

SOMA: Mawazo ya biashara zitakazovuma miaka ijayo 2018 na kuendelea mpaka 2020

Ingawa kitabu cha Michanganuo ya biashara na ujasiriamali katika Sura yake ya kwanza kabisa, kinaelezea vizuri sana njia mbalimbali za kubuni na kupata wazo la biashara(jinsi ya kubuni wazo la biashara) lakini wazo la biashara kwa kiasi kikubwa hutokana na Mjasiriamali mwenyewe na wala siyo kwenye kitabu au kwa mtu mwingine yeyote yule.

Ni baada tu ya mjasiriamali kwa kutumia njia na mbinu hizo mbalimbali za kupata wazo la biashara kuamua sasa wazo lake ni lipi, ndipo ataweza kusema amefanikiwa kupata wazo la biashara. Mbinu za kupata wazo la biashara zipo nyingi lakini leo hii ningependa zaidi kuizungumzia mbinu iliyokuwa kuu kuliko nyingine zote na ambayo karibu kila mtu ndiyo huitumia hata yule asiyekuwa na uelewa wowote ule katika masuala ya biashara.

SOMA: Wazo la biashara ipi yenye hatari kidogo naweza kufanya kwa mtaji wa milioni 5?: Mwajiriwa serikalini.

Njia bora zaidi ya kubuni wazo la biashara tena isiyokuwa na uwalakini wowote ule ni ile ya KUCHUNGUZA MATATIZO WALIYOKUWA NAYO WATU KATIKA JAMII INAYOKUZUNGUKA. Wataalamu wote wakubwa katika biashara na mambo ya uchumi kote Duniani wanaafikiana kitu kimoja kwamba, “Mjasiriamali/mfanyabiashara yeyote yule lengo lake kuu halipaswi kuwa ni kupata pesa, bali linatakiwa kuwa ni kutatua matatizo yanayowakabili wateja wake”. Pesa ni matokeo tu ya utatuzi wa matatizo hayo ya wateja.

Kabla hata ya kuanza kuwaza sijui utaanzisha biashara ya mtaji wa laki tano au biashara ya mtaji wa milioni moja, unachotakiwa kwanza kuanza kufikiria ni ikiwa utatatua tatizo gani linalowakabili watu fulani. Ukishapata tatizo hilo sasa ndipo unaweza kuendelea na mchakato wako katika vipengele vingine kama mtaji, timu ya watu, eneo la biashara nk.

SOMA: Sababu kuu tano (5) kwanini uandike mpango wa biashara yako kwanza kabla hujaanzisha biashara yenyewe.

Kimsingi kitabu hiki cha Michanganuo ya biashara na ujasiriamali, kina kila kitu mjasiriamali yeyote yule anachohitaji ili kuijenga biashara endelevu na inayoweza kujiendesha yenyewe mwisho wa siku endapo tu atakuwa mvumilivu na mwenye bidii. Unapozungumzia Mpango wa Biashara au  Business Plan, ni kila kitu katika BIASHARA. Maana yake kama kwa mfano ingelikuwa ni binadamu, “Unazungumzia biashara tangu ikiwa tumboni kwa mama yake mpaka inazeeka na kufa

Kuna msomaji mwingine mmoja aliniuliza ikiwa biashara ndogo unaweza ukaijengea mfumo ikajiendesha yenyewe ukiwa haupo pale, nilimjibu, ndiyo/hapana, hapo sikumpa jibu moja kamili kwani itategemea mpango wake wa biashara upoje na aina ya biashara anayoifanya pia ni ipi.

SOMA: Unajua biashara yenye faida kubwa na ya haraka mara 2 ya mtaji utakaowekeza?

Niseme tu ukweli hapa kwamba, sipendi unafiki wala kumpa mtu hamasa hewa kwani na mimi pia nimewahi kupitia uzoefu huu, biashara ndogo sana ni vigumu kidogo kujiendesha yenyewe wewe ukiwa haupo pale. Inakubidi mwanzoni kukaza buti kwelikweli na ukomae mpaka ufike mahali mtaji umetengemaa ndipo uweze kuweka mifumo imara ikiwa ni pamoja na kuweka wasaidizi, nikimaanisha watu au mashine na mifumo mbalimbali itakayoweza kukusaidia ili mambo yaende bila wewe kuwepo pale, unaweza hata ukawa upo Dubai, UK. China, Johanesburg, New York na kwingineko lakini huku mambo yanaenda kama kawaida. Hebu mcheki Trump sasa ni rais anaendesha Marekani lakini Business zake zina ‘run’ kama kawaida. Ni kitu kama hicho.

Lakini pia kwa upande mwingine wa shilingi biashara hata ikiwa ni ndogo sana, unaweza ukatumia mifumo mbalimbali itakayokuwezesha wewe ukiwa haupo pale ijiendeshe yenyewe. Nimesema aina ya biashara ina ‘matter’ sana kwani kwa mfano biashara kama vile za mitandaoni katika Intaneti ndiyo nzuri zaidi kuweka mifumo inayoweza kuifanya biashara ijiendeshe yenyewe. Unaweza kuweka email listing, blog/website, App nk. wakati wewe unafanya ishu zako zingine huko, huku wateja wanadownload vitu na kulipia online, ukija kucheki “mpunga” umeingia kitambo wewe hata huna habari !

SOMA: Huna mtaji wa kutosha, hukopesheki?, jaribu njia hii ya kufunga mkanda(Bootstrapping).

Biashara zingine mfano mzuri duka la rejareja au duka la vyakula(Maduka ya kina mangi) ni vigumu kuweka mfumo ikiwa bado biashara ipo katika hatua za mwanzo sana. Hata hivyo nilijaribu kutengeneza mfumo mmoja na ambao kwangu uliwahi kufanya kazi vizuri sana hata katika hatua za mwanzo(TWO IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM), mfumo huo niliouweka katika kitabu changu kiitwacho, MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA unamwezesha mjasiriamali kumwachia msaidizi biashara yake pasipo mfanyakazi huyo kudokoa hata senti tano.

Kwa leo hayo ndiyo yaliyokuwa majibu kwa maswali ya wasomaji wetu wawili, naamini nimejitahidi kuyajibu kadiri ya uwezo wangu ila kama kuna ushauri au maoni mengine kutoka kwa msomaji mwingine yeyote yule yanakaribishwa kwa mikono 2, anaweza akaandika hapo katika box la maoni chini. 
ASANTE SANA.

.....................................................................


Programu zetu zote kubwa zinaendelea kama kawaida na usisite kuagiza PACKAGE inayokufaa muda wowote ule utakaohitaji zikiwa bado kwenye offa zake kwani ukifika muda muafaka bei zitabadilika na kupanda au OFFA husika kutokuwepo tena.

KIFURUSHI(PACKAGE) YA 1 (18,000/=  au 37,000/=)
Vitabu 3, softcopy kwa sh. elfu 18 vyote 3 na Hardcopy sh. elfu 37

1. MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI
2. MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA
3. MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA                KUITOA
Pamoja na kuunganishwa na grupu la wasap bure ukipenda

KIFURUSHI(PACKAGE) YA 2 (10,000/=)
Tunakutumia vitabu, michanganuo na masomo yote yafuatayo kwa gharama ya shilingi elfu 10 tu.(Vyote ni softcopy); Ukitaka pia unajiunga na group bure.1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  Kitabu kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1

3.  Kitabu kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2

4.  Kitabu kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.

5.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

6.  SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

7.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

8.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza

9.  Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.

10.              Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

11.              Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

12.              Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.


13.              Ukurasa mmoja wa mchanganuo.KIFURUSHI(PACKAGE) YA 3 (20,000/=)
Semina maalumu ya jinsi ya kufanya hesabu za mpango wa biashara(Advanced Business Plan Financials) Bei yake ni shilingi elfu 20 na tunatuma kama softcopy kwa email. 


0 Response to "NAMNA BORA ZAIDI YA KUBUNI WAZO LA BIASHARA ITAKAYOLIPA HARAKA BILA MSAADA WA MTU MWINGINE"

Post a Comment