SABABU KUBWA 9 DUNIANI KWANINI WATU HUKOPA PESA, 4 KATI YAKE NI ZA KUOGOPA KAMA UKOMA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SABABU KUBWA 9 DUNIANI KWANINI WATU HUKOPA PESA, 4 KATI YAKE NI ZA KUOGOPA KAMA UKOMA

madhara ya kulimbikiza madeni ni kuishia kufukuzwa ndani au kujiua

SEHEMU YA I
Kwa ujumla sababu moja kuu ya watu kukopa pesa duniani kutoka kwa wakopeshaji mbalimbali kama vile mabenki, taasisi za fedha na watu binafsi mbali na zile sababu mahsusi moja moja nitakazozitaja huko mbele katika somo hii ni ile ya watu hao kutaka kununua au kulipia vitu ambavyo hawana uwezo wa kuvilipia kwa fedha taslimu wakati huo. Mkopo humwezesha mtu aliye na kipato endelevu mfano ajira au biashara iliyokwishaanzisha kufanya marejesho ya mkopo aliochukua kidogokidogo katika muda waliokubaliana.

Mkopo huwanufaisha wote wawili, mkopaji na mkopeshaji, kwa mkopaji kupata kiasi chote cha pesa anachohitaji pasipo kuwa na haja ya kuweka akiba kidogokidogo hadi atimize kiasi hicho, huku mkopeshaji naye akinufaika kwa kupata riba inayotokana na marejesho ya mkopo huo. Kwa hiyo ili mtu kuweza kuiboresha na kuilinda hali yake ya kifedha wakati fulani katika maisha yake ni lazima ahitaji uwekezaji kutoka nje kama mkopo zaidi ya zile fedha anazokuwa nazo mwenyewe mkononi.

SOMA: Elimu ya fedha na umuhimu wake 2019, njoo tuunganishe nguvu tuhamishe milima.

Kuna aina mbalimbali pia za mikopo kulingana na mahitaji ya wakopaji. Aina mbalimbali za mikopo nazo huwa na masharti au vigezo tofauti tofauti kwa mfano ipo mikopo mkopaji atatakiwa kueleza bayana ataenda kufanyia kitu gani  baada ya kuupata na mingine mkopaji akishapewa huachwa aende zake akapange mwenyewe ni nini atakachokwenda kufanyia mkopo huo nk. Ipo mikopo ya muda mfupi na mikopo ya muda mrefu, mikopo ya riba na mikopo isiyokuwa na riba kabisa. Mikopo yenye dhamana na ile isiyolindwa na dhamana yeyote,  mikopo ya vikundi na mikopo ya mtu mmojammoja.

Kuna wakati mwingine kukopa hakuna maana yeyote kwa mtu na kanuni kubwa kabisa kwenye kukopa inasema hivi; “Unatakiwa kukopa tu pale kunapokuwa na uhitaji wa kufanya hivyo” Ili kunufaika na fursa zilizopo katika mikopo zingatia na ulinganishe faida na gharama za kuchukua mkopo. Kuna kitu kingine kimoja watu wengi huwa hawakijui, kwamba wakopeshaji huweka riba kubwa kwenye ile mikopo yenye hatari kubwa kusudi kuja kufidia hasara zitokanazo na mikopo chefuchefu(mikopo isiyolipika) na kuweka riba ndogo kwa mikopo ile isiyokuwa na hatari kubwa. Hatari katika mkopo ni kama vile mkopaji kutokuwa na dhamana za kutosha au bima ya mkopo nk.

SOMA: Je, Mtanzania unakopesheka na taasisi za fedha au Benki?

Unatakiwa pia kabla ya kuchukua mkopo, ujiulize maswali yafuatayo;
·       Je, Utaweza kurejesha mkopo wako?
·       Je, gharama za huo mkopo zinakubalika?
·       Ni mkopeshaji yupi(Benki, taasisi au mtu binafsi) mwenye masharti na riba nafuu zaidi ya wengine?

Kuyajibu maswali hayo na mengineyo muhimu kutakusaidia kupata mkopo unaostahili kwa ajili ya mahitaji yako. Ingawa kila mtu ni tofauti kulingana na mazingira yake mwenyewe, mifano ifuatayo inawakilisha sababu mbalimbali zinazowafanya watu wakope pesa. Baada kukuelezea sababu hizo 9, nitaenda pia kukutajia zile sababu miongoni mwa hizo 9 unazotakiwa kuziepuka kama ukoma, nikiwa namaanisha kuwa sababu hizo hazitakiwi kabisa kukusukuma ukakope vinginevyo utakuja kujutia na kusaga meno bure. Kuna watu wengi wamewahi kuuziwa majumba yao ya maana huku wakitolewa nje ya nyumba hizo mithili ya wakimbizi vile, wengine walizikimbia familia zao na hata wengine kufikia hatua ya kujitoa uhai kisa madeni yaliyotokana na sababu hizo hizo nitakazokutajia.

SOMA: Njia 7 za kupata mtaji wa biashara unayoipenda.

Hebu tuzione kwanza sababu zote 9 mchanganyiko wa zile nzuri na mbaya kabla hatujazichambua mbivu na mbichi;

1.Kukopa kwa ajili ya kununulia rasilimali(Assets) mfano nyumba, gari, kiwanja, nk.
Kumiliki nyumba ni moja ya malengo makubwa muhimu zaidi ya kiuchumi binadamu wote duniani hutamani kutimiza katika maisha yao. Lakini pia kuna ununuaji wa asseti nyingine mbalimbali kwa ajili ya biashara na hata kwa malengo mengine tu yasiyokuwa ya kibiashara. Tutakwenda kufafaua hapa vizuri kwenye kipengele cha sababu za kuepukwa kama ukoma na zile sababu zinazofaa kukumbatiwa.

SOMA: Mbinu za kubadilisha asseti mbaya zinazotafuna pesa zako kuwa asseti nzuri zitakazokupa pesa

2.Kukopa kwa ajili ya kuanzisha biashara mpya.
Mtu kwa kutumia rasilimali nyingine alizokuwa nazo kama vile kiwanja, nyumba nk. anaweza akakopa kwa dhumuni la kuanzisha biashara mpya.

3.Kukopa kwa ajili ya uendelezaji wa biashara ya zamani uliyokwishaianzisha kitambo.
Wale waliokuwa tayari na biashara zilizokwisha anzishwa kitambo huenda kukopa ili kuzipanua au kuziboresha zaidi biashara zao

SOMA: Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala

4.Kwa ajili ya kujiboresha binafsi/Mikopo ya kielimu/Vyuo vikuu nk.
Katika eneo  hili gharama za elimu au mafunzo kwa kiasi kikubwa hazina mjadala kwani faida zake kwa mkopaji ni za uhakika. Kuna mahusiano makubwa sana kati ya mafanikio ya mtu kiuchumi na elimu au mafunzo anayoyapata hivyo, ujuzi, cheti, stashahada na hata shahada vina uwezo mkubwa wa kuongeza kipato cha mtu hapo baadae.

5.Kukopa kwa ajili ya kwenda kulipia hasara mbalimbali zitokanazo na shughuli za kibiashara; Mfano mtu baada ya kufungua biashara yake mtaji ukakata sasa anaamua kwenda kukopa kusudi kurudi tena kwenye chati. Hii hufanywa sana na wale wanaofanya biashara za hisa au katika masoko ya mitaji na pia hata katika biashara ya ununuaji na uuzaji wa majumba na viwanja(Real Estate Agency)

SOMA: Unajua biashara yenye faida kubwa na ya haraka mara 2 ya mtaji utakaowekeza? 

6.Kukopa kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu na dharura mbalimbali za kimaisha.
Ugojwa haubishi hodi na unapoingia wakati mwingine unakukuta huna hata senti tano mfukoni. Sasa hebu niambie utaacha mtu wako wa karibu au hata wewe mwenyewe ufe wakati unaweza ukakopa na kuokoa maisha kisha baadae ukapiga kazi na kuzirejesha?

7.Kukopa ukalipie videni vidogovidogo vinavyokuumiza kichwa(Debt consolidation).
Kuna wakati mwingine mtu hujikuta ana madeni madogomadogo mengi kutoka kwa wakopeshaji zaidi ya mmoja, madeni hayo yana tabia ya kuwa na riba kubwa na masharti magumu kiasi kwamba kadiri muda unavyokwenda ndivyo nayo yanavyozidi kuongezeka shauri ya riba kuzaana. Wakopeshaji wengine huwa ni watu binafsi na wanakutisha hata na mapanga au visu endapo hutowalipa kwa wakati pesa zao. Wengine ni wenye nyumba na wanakutishia kila siku kukutoea vitu vyako nje tena kibabe(Kimafia) ili uadhirike mbele za watu. Kuepukana na adha zoote hizi unaamua kumtafuta mkopeshaji mstaarabu mmoja tu kama benki au taasisi yeyote ile rasmi itakayokukopesha pesa kwa masharti ya kistaarabu na kuwalipa hao ‘wahuni’ ‘wakasepa’ na kero zao huku wewe ukiendelea kulipa kila mwezi au wiki kidogokidogo.

SOMA: Mkopo wa benki au taasisi za fedha: soma hapa hutakaa uwalaumu tena.

8.Kukopa kwa ajili ya kulipia gharama mbalimbali za maisha za kila siku.
Hii  mara nyingi hutokea kwa wale wenye vipato vya uhakika. Wanakopa wakijua kesho na keshokutwa mshahara au kipato kitaingia tu penda kisipende. Wanaamini kabisa kwamba hawawezi kupanda daladala wakati tax, bodaboda na hata ndege zipo, kuna hata wengine hukopa kwa ajili ya sherehe mbalimbali kama vile za harusi nk.

9.Kukopa kwa ajili ya kuiongezea thamani rasilimali uliyokuwa nayo tayari mfano nyumba, gari, shamba nk.
Unaboresha kitu ili kipendeze zaidi kwa malengo mbalimbali
  
Nimemaliza kuzitaja na kuzielezea kidogo sababu kubwa 9 zinazowasukuma watu kukopa fedha. Pengine unaweza ukaongezea hapo nyingine, siyo mbaya kwani naamini bado zipo nyingi nyingine. Sasa nitakachokwenda kukifanya katika sehemu hii inayofuata, ni kuzigawa sababu hizo 9 katika makundi mengine makubwa 2, moja likiwa ni kundi la sababu za kuepukwa kama ukoma na kundi la pili ni la sababu zile mtu unazopaswa kutokuziogopa hata kidogo. Katika hizi 9 nilizozitaja, zipo sababu 4 za kuogopa kama ukoma na nyingine 5 ni za kukumbatia. Nitaanza kwanza na hizo 4, kisha 5 huku kila moja niikitolea ufafanuzi ni kwanini imeingia katika kundi husika.

SOAMA: Kabla ya kukoipa mkopo wa biashara yako, pambana kiume kwanza usijekuumbuka bure

Kuna sababu zingine zitakushangaza sana kwani hutoamini kabisa kama zinaweza zikaingia katika kundi la kuogopwa kama ukoma, hivyo kuwa makini sana hapa, yawezekana hapo kabla ulikuwa ukifikiri ni sababu za kukumbatiwa kumbe siyo hivyo, zitakuchoma bure, kuzikumbatia hakuna tofauti na mtu aliyekumbatia upupu.

SEHEMU YA II
SABABU 4 ZA KUKOPA PESA UNAZOTAKIWA KUZIOGOPA KAMA UKOMA VILE
1………..
………………………………………

Ndugu msomaji wangu, somo hili linaendelea hadi mwisho usiku saa 3-saa4 kwa aliyejiunga katika masomo ya kulipia. Kujiunga na group hilo(Michanganuo-online Premium group) ni bure, ila utatakiwa kununua moja ya vifurushi vifuatavyo vya masomo kwa bei rahisi kabisa ya OFFA. 

Katika Premium Group unapata mafunzo ya mwaka mzima ya fedha na jinsi ya kuandika mpango wa biashara hatua kwa hatua, toka Januari- Desemba pamoja na dondoo nyingine mbalimbali za biashara, ujasiriamali na mipango ya biashara halisi iliyokamilika kila kitu. Unapata pia fursa ya kuuliza swali lolote lile kutoka kwa wataalamu wa michanganuo(Business plan experts) na kujibiwa haraka. Aidha unaweza kujiunga na group letu jingine la bure(Michanganuo free group) kwa kiungo hiki,  https://chat.whatsapp.com/EJ3MS2MtJepEjm9GaYtT8e

Nafasi kwenye group la Premium zilizobakia ni chache ili lijae(Chini ya watu 30 tu), pia offa hii inakaribia kuisha na kila kitu kitauzwa kwa bei yake ya kawaida. Kila item hapo chini ina bei yake, jumla vyote 13 kwa bei halisi vinagharimu si chini ya sh. elfu 80. Lakini tunakupa kila kitu kwa sh. elfu 10 tu au ukipenda kuchukua kifurushi cha 2 na cha 3 elfu 18 na elfu 28

1.Kifurushi cha sh. Elfu 10 kinachojumuisha vitu vifuatavyo,

1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  Kitabu kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1

3.  Kitabu kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2

4.  Kitabu kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.

5.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

6.  SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

7.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

8.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza

9.  Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.

10.              Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

11.              Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

12.              Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.

13.              Ukurasa mmoja wa mchanganuo.

2.Kifurushi cha sh. Elfu 18 kinachojumuisha vitu vifuatavyo
Unapata Kifurushi kizima cha kwanza pamoja na vitu vingine vifuatavyo;
·       Kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA
·       Kitabu cha MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYWASIYOPENDA KUITOA

3.Kifurushi cha sh. Elfu 28 kinachojumuisha vitu vifuatavyo;
Unapata vitu vyote kutoka kifurushi cha 1 & 2 pamoja na Semina kubwa ya Hesabu za mpango wa biashara(Advanced Business Plan Financials).


KULIPIA KIFURUSHI CHCHOTE HAPO JUU, TUMIA NAMBA ZIFUATAZO,
0765553030 au 0712202244

Jina hutokea, Peter Augustino Tarimo
Kisha tuma ujumbe wasap 0765553030, usemao, NIUNGANISHE GROUP LA KULIPIA LA MICHANGANUO.
Nitakuunganisha muda huohuo pamoja na kukutumia kila kitu  

0 Response to "SABABU KUBWA 9 DUNIANI KWANINI WATU HUKOPA PESA, 4 KATI YAKE NI ZA KUOGOPA KAMA UKOMA"

Post a Comment