SHEA NA WATEJA WAKO KILA KITU LAKINI SIYO SIRI HIZI TANO(5)

MITANDAO YA KIJAMII, FACEBOOK, TWITTER NA INSTAGRAM
Ni matumaini yangu kwamba wewe unayesoma hapa ni mfanyabiashara kwa namna moja au nyingine na ndio maana upo hapa au unasoma hapa. Kama mmiliki wa biashara au kampuni bila shaka yeyote ile unapendelea kushea/kuwashirikisha wateja wako mambo mbalimbali na hili hasahasa limekuwa ni jambo la kawaida sana katika Ulimwengu wa leo wa mawasiliano ya kisasa katika mitandao ya kijamii, karibu kila mtu usipomkuta facebook, basi utamkuta Insta, Twitter au mitandao mingineyo.

Kuwashirikisha mambo mbalimbali hakuwasaidii tu wateja wako lakini pia kunakuweka wewe mwenyewe katika nafasi ya juu zaidi kama mtu wa kutegemewa. Hata hivyo wafanyabiashara na wajasiriamali wengi hulifanya jambo hili kupita kiasi na kusahau kumbe kuna hatari mbalimbali pia zinazoweza zikajitokeza endapo watawashirikisha wateja wao mambo mengi kupitiliza.

SOMA: Makosa 12 yatakayofukuza wateja dukani kwako na kudhani umelogwa.

Bila kupoteza muda wako mwingi hebu basi tukazione hizo siri 5 zikoje;

1.Maswala yako ya kifedha.
Usipende sana kulialia umasikini mbele ya wateja wako wala kujitapa kuwa una pesa nyingi(ukwasi), unapofanya mambo haya 2 kupitiliza  yanaweza kuwafanya wateja wako kukaa mbali na wewe kwani wanaweza kuhisi mambo mawili, kwanza wanaweza kufikiria biashara yako inachungulia kaburi(inafilisika) au pengine bei unayowatoza ni kubwa kupita kiasi. Hivyo utaona wakikimbia mmoja baada ya mwingine.

2. Masuala ya ndani ya biashara yako.
Wateja hawana haja ya kuyajua matatizo yako na wale wanaokusambazia mzigo, wala kujua matatizo yako na mwenye nyumba ulikopanga fremu ya ofisi/duka lako.

SOMA: Kuanzisha kiwanda rahisi cha juisi ya matunda, Tanzania ya viwanda yaja jiandae.

3.Matatizo ya wafanyakazi wako.
Kutoa malalamiko juu ya wafanyakazi wako kwa wateja wako hakuwezi kusaidia kitu, sanasana kutazidi kukufanya uonekane kama kwamba wewe ni mtu mbaya na mwenye roho mbaya. Ikiwa mfanyakazi wako ataboronga hata iiwa ni mbele ya wateja basi wewe cha kufanya kama bosi ni kuwataka radhi wateja kwa kosa hilo kisha rekebisha tatizo lililotokea halafu sasa njoo baadae ushughulike na mfanyakazi wako wakati mkiwa wenyewe wawili tu bila mtu mwingine.

4.Hali halisi ya soko ilivyo.
Kila mtu na si wewe tu hata na wateja wenyewe kuna wakati wanahisi hali ya kiuchumi kuwa ngumu. Hivyo usitegemee sana huruma toka kwao kwa kulialia kuwa ‘vyuma vimekaza, vyuma vimekaza’. Utawafanya wakushangae bure badala ya kukuonea huruma.

SOMA: Jinsi mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanikio ya biashara yako.

5.Kuhusiana na wateja wengine.
Kila mteja angependelea kujihisi kama yeye ndiyo mteja pekee, hivyo si vizuri hata kidogo kushea kupita kiasi stori za ni nani anayenunua kwako,ananunua nini,  ananunua kiasi gani na ananunua kupitia njia zipi. Sisemi ni vibaya kwa mfano kuweka ushuhuda(Testimonies) katika ukurasa au page zako lakini, fanya hivyo kimkakati na pia kwa kiasi.


…………………………………………………

LEO NINA HABARI MBILI NJEMA KWAKO,
Somo la leo lilisisitiza kutokutoa kila siri kwa wateja wako lakini mimi nitakaribia japo siyo kabisakabisa kukupa “siri zangu muhimu 2”

Habari ya kwanza kabisa;
Ni ujio wa semina yetu ya kwanza kati ya 4 tulizoazimia kuzifanya kabla ya mwaka huu kumalizika. Kumbuka Mwezi Januari niliahidi kupitia kaulimbiu yetu ya mwaka; “KIWANDA NI UTAJIRI, TUACHE MANENO MANENO TUJENGE VIWANDA KWA VITENDO”, kuwa tutaandaa michanganuo bunifu 4 kwa ajili ya uanzishaji wa viwanda(biashara za uzalishaji)  ambazo zitakuwa kama mifano kwa ajili ya mtu kuanzisha biashara ya kiwanda chochote kile kidogo na hata cha kati.

Kwa Miezi iliyobakia mwaka huu 2019 kuisha tutafanya mchanganuo mmojammoja kila mwezi, kumbuka pia kwamba hii michanganuo si ya kitoto!, na tayari nimekwishaifanyia utafiti mkubwa na kwa pamoja tena nitaomba mawazo yenu wadau mtakaojiunga na semina hizi wakati tukiandika hatua kwa hatua katika group.

Tutachambua kiwanda kimoja cha ufyatuaji wa matofali ya block kilichopo maeneo ya Kiluvya jirani na jiji la Dar es salaam, nimeshawasiliana na wahusika na tayari wameshanipatia taarifa zote muhimu kama za Mahitaji ya kuanzishia kiwanda na soko.

Bila kupoteza muda wako mwingi, niseme tu kwamba semina hii tunakwenda kuifanya kuanzia tarehe 15 katika group la MICHANGANUO-ONLINE, na kiingilio ni sh. Elfu 10 tu, fedha ambayo itakuwezesha kushiriki tena michanganuo mingine yote 3 iliyobakia bila kuchajiwa zaidi. Namba za malipo ni 0765553030 au 0712202244 jina kama kawaida ni la kwangu mwenyewe, Peter Augustino Tarimo. Unaweza ukaanza kulipia sasa hivi kujihakikishia nafasi yako mapema.

Habari ya Pili;
Ni OFFA ya “kufa mtu” inayoambatana na hiyo semina. Kusema ule ukweli hii offa naitoa tu kwa shingo upande lakini ndani kiroho kinaniuma  na nafanya hivyo ni kwa sababu tu nawapenda wadau wangu na si vinginevyo. Any way, nikuibie tu siri moja ni kwamba, kwa kukupa offa hii ni sawa na kukupa kila kitu nilichokuwa nacho katika Programu zangu zote, nakuwa sijabakiza kitu. Naamini ukiwa mjanja huwezi kuikosa offa hii hata iwe vipi. Na naitoa tu hapa na si kokote kwingineko.

IKOJE OFFA HII?
Natoa offa hii kwa watu 10 tu wa mwanzo watakaojiunga na semina hii kisha baada ya hapo itafungwa rasmi, wengine watashiriki semina na kupata tu vitu vya kawaida.

INA NINI NDANI YAKE?
Nakupatia Instatly, punde tu unapolipia, Programu zangu zote tatu zilizosheheni vitabu, michanganuo ya biashara, semina na masomo yoote ya siku zilizopita. Kumbuka vitabu ni pamoja na vitabu vyangu vikuu vya MICHANGANUO, DUKA na MIFEREJI 7 YA PESA. Hutasubiri mpaka siku ya semina ndipo ufaidike na offa yako, bali offa hii unatumiwa mara moja baada ya kulipa kiingilio chako cha sh. Elfu 10 hata kama ni sasa hivi ninapoandika hapa.

Na haijalishi kama unatumia watsap au email tu peke yake, kila kitu kipo katika mfumo wa softcopy utatumiwa hata kama huna Whatsapp kwenye simu yako. Halikadhalika semina nayo si lazima uwe katika watsap, masomo yote tunatuma pia kwa E-mail yako.

WAHI OFFA HII INGALI YA MOTOMOTO KABLA HAIJAPOA KWA KUTUMA KIINGILIO CHAKO SH. ELFU 10 KWA NAMBA, VODACOM, 0765553030 au TIGO, 0712202244 jina ni Peter Augustino Tarimo.

Dondoo za semina tutaendelea kujuzana kadiri ziku zinavyokwenda.  
Ni mimi,
Peter Augustino Tarimo
Mwalimu/kocha na mhamasishaji wako.

0 Response to "SHEA NA WATEJA WAKO KILA KITU LAKINI SIYO SIRI HIZI TANO(5)"

Post a Comment