MAKOSA 12 YATAKAYOFUKUZA WATEJA DUKANI KWAKO NA KUDHANI UMELOGWA.

Kuna makosa ambayo wenye maduka wengi au biashara zingine ndogondogo huyafanya pasipo kufahamu kuwa yanawafanya wateja waondoke huku wakiwa hawajaridhika, makosa hayo yanakimbiza wateja pasipo wewe kujua, mteja aliyekasirika  siyo tu atahama duka na kwenda kununua  kwingineko, bali pia atakwenda kuwatangazia na watu wengine wengi juu ya ubaya wako na kufanya nao wakose moyo wa  kuja kununua dukani kwako. Kwa kuyafahamu makosa hayo, unaweza ukayakwepa na kuelekezea nguvu zako zaidi kwa yale matendo tu yanayoleta wateja katika biashara yako.

1.  Bei isiyofaa; kushindwa kuweka bei muafaka inayoendana na soko, wateja watakimbilia kwingine.
2.  Kutoa huduma mbaya kwa wateja, mfano ni  kauli na lugha kama  hizi hapa chini;
“Mkopo amesafiri subiri mpaka atakaporudi”

“ Njoo na bibi yako mzaa babu ndipo nikukopeshe”

“Hili siyo shirika la kukopesha  jaribu kwingine tafadhali……”

“ Sina chenji  katafute kwanza chenji ndipo uje  nikuuzie”

“ tunatoa huduma   za uuzaji wa vocha  peke yake hapa, kuingiza ni juu yako mwenyewe”

“Kakuambia nani hapa tunauza sigara; hili siyo duka la walevi hebu ondoka  hapa upesi”

“ Hatuna  vifungashio  vya bure vipo vya kununua tu”

Tafuta lugha nzuri kumfanya mteja atambue kwamba sera ya duka lako hairuhusu kukopesha na siyo kutoa lugha itakayomfanya mteja kamwe asiwe na hamu tena ya kurudi siku nyingine dukani kwako.Sikatai kwamba imani yako au hata kiafya hupendi kuuza vileo na sigara, lakini kwani walevi na wavutaji sigara huwa hawana mahitaji mengine? Na ukimjulisha kwa lugha ya upole kuwa huuzi vitu hivyo kwani hatakuelewa mpaka umuwekee mabango ya kumdhihaki?

3.  Mandhari mbaya ya duka: mpangilio wa vitu usiovutia pamoja na uchafu kama vumbi kwenye bidhaa, sakafuni na katika mazingira yote ya duka kwa ujumla.
4.  Kukopesha bila tahadhari; unaweza kudhania labda kuwakopesha wateja, bila ya kuchukua tahadhari ndiyo itasaidia wasikukimbie, kumbe ndiyo umewapa tiketi ya kubadili hata njia wanayopita kila siku na kwenda kununua wasikodaiwa.


5.  Kutokuwafahamu washindani wako vizuri, udhaifu na uwezo waliokuwa nao.
6.  Kutokuwa na uelewa wa bidhaa unazouza: inatakiwa kila bidhaa  angalao ufahamu sifa zake, ubora, tarehe ya mwisho kutumika, pamoja maelezo yake jinsi ya kuitumia ili uweze kumtoa mteja wasiwasi anapotaka kununua.
7.  Uwongo:  kuwadanganya na kuwaongopea  wateja  juu ya sifa na ubora wa bidhaa.
8.  Kutokufuata sheria za nchi na mamlaka husika: Utafuatwafutwa jambo litakalokufanya pia kila mara uwe unafunga funga  duka lako ovyo na hatimae  wateja  kukukimbia.
9.  Uaminifu; mteja kwa bahati mbaya amesahau labda chenji yake, simu au hata mwavuli aliokuja nao pale dukani, baada ya dakika kadhaa anarudi huku akihema wewe unamwambia hukuviona wakati ukweli ni kwamba umeshavificha. Hiyo siyo tabia nzuri kabisa, na mteja kama huyo umempoteza daima.

10.      Kubandika matangazo ya ajabu ajabu kama vile yanayokashifu imani na dini za watu wengine, ushabiki wa michezo n.k. usipende kuanika ovyo msimamo wako upo upande gani kwani wewe unawahitaji wateja kutoka pande zote. Kutangaza hadharani upande uliko kutasababisha wale wateja wenye   mlengo au imani tofauti na wewe wawe wazito kuja kukuungisha. Hata kama wewe ni mkereketwa wa itikadi au madhehebu fulani,  kuweka miziki au  kanda za mawaidha ya imani yako huku ukifungulia sauti ya juu sana, siyo jambo zuri labda tu duka lenyewe  liwe ni duka maalumu la kuuza  CD na  kanda za imani hiyo.11.      Kuweka msaidizi asiyefaa: Msaidizi au mfanyakazi asiyetambua wajibu wake ni kikwazo kikubwa katika biashara za aina zote, mpe mafunzo au maelekezo ya mara kwa mara juu ya huduma bora kwa mteja ukiona haelekei ni bora ukamuondoa kabla hajakufukuzia wateja wako.

12.      Jina lisilofaa: mfamo utakuta mtu kaandika bango la duka lake jina linaloelezea ama  kuwa na nembo za kutisha  kama vile,  MAFIA, ALQAEDA, PANYAROAD, nk. Jina linawakilisha picha ya biashara yako nzima hivyo ni lazima liwe zuri na lenye maana inayokubalika na kila mtu.

............................................................................

Ndugu msomaji wa makala hii, kitabu cha “MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJEREJA” kipo katika mifumo yote, softcopy na hardcopy. Kitabu hiki kimebeba uzoefu halisi wa mwandishi kwenye biashara hii kwa miaka 12, siyo simulizi za kutunga wala utafiti wa kwenye vitabu, (it’s a real experience) Maswali yote yanayopasua watu wengi vichwa na kushindwa kumudu kuifanya biashara ya duka au biashara zingine zozote za rejareja kwa ufanisi unaotakikana yamejibiwa kwa ufasaha.

HARDCOPY ni sh. Elfu 12 na utaletewa popote pale ulipo Dar es salaam. Mikoani tunatuma kwa njia ya basi lakini gharama za usafiri zitaongezeka

SOFTCOPY ni shilingi elfu 5 tu popote pale ulipo, ukishalipia, unatuma email yako na meseji uliyotuma pesa kisha tunakutumia kitabu unadownload na kusoma katika simu yako au kompyuta.

Usisahau pia semina kwenye WHATSAPP bado zinaendelea kila saa 3 - 4 usiku, karibu sana ujiunge leo.

SIMU:              0712202244
WHATSAPP:   0765553030

JINA:                Peter Augustino Tarimo

0 Response to "MAKOSA 12 YATAKAYOFUKUZA WATEJA DUKANI KWAKO NA KUDHANI UMELOGWA. "

Post a Comment