NINA TATIZO KUBWA UPANDE WA MAKADIRIO YA GHARAMA NA KUJUA AINA YA MPANGO WA BIASHARA(SWALI)

ULIZA UJIBIWE
Katika safu hii ya maswali na majibu, hapa nitakwenda kulijibu swali la mdau wetu mmoja alilouliza kupitia whatsap na aliuliza kama ifuatavyo;


Mimi nna tatizo kubwa kwenye upande wa makadirio ya gharama; naambiwa kuna namna mbalimbali za kuandaa kulingana na mahitaji, mf. Kama unahitaji mkopo au unaandika kwa ajili ya kuwapa wafadhili wa biashara yako. Naomba ufafanuzi hapo kaka.

SOMA: Break Even Point: Ni lini biashara yako itarudisha gharama zote ulizotumia?

MAJIBU:
Swali lako hili lina vitu 2 tofauti,
·       namna ya kukadiria gharama mbalimbali na la pili ni
·       namna ya kuandika mpango wa biashara kwa ajili ya hadhira(wadau) tofauti mfano kuomba mkopo benki au kwa ajili ya kuwasilisha kwa wawekezaji(investors)
Nitajibu maswali yote mawili hivi;

1.Kwenye mpango wa biashara huwa tunakadiria vitu viwili ambavyo ni, Gharama mbalimbali na Mauzo(mapato). Kati ya hivyo2 gharama ndiyo rahisi zaidi kukadiria kwani kimsingi wala haukadirii bali unachukua moja kwa moja gharama halisi za vitu/bidhaa/huduma sokoni. Mauzo ndiyo unayoweza kusema kabisa kwamba tunakadiria kwani mara nyingi tunakuwa hatujajua kwa uhakika kama tutapata “exactly” wateja wangapi au tutauza kwa bei ipi. Hata hivyo ukadiriaji iwe ni gharama au mapato, vyote haupaswi kukadiria upate namba iliyo sahihi kwa asilimia mia moja kwenye mpango wa biashara, bali ni makisio tu.

SOMA: Sababu 4 kwanini kipengele cha fedha ni moyo wa mpango wa biashara(The heart of a business plan)

2.Kujibu hilo swali la pili, kwa kifupi ni hivi;
Mpango wa biashara bila kujali unaandika kwa ajili ya kupeleka Benki, kwa wawekezaji au unataka tu kwa ajili ya uendeshaji wa biashara yako, michanganuo yote huwa na sura zinazofanana(common structure). Ni lazima mchanganuo wowote ule uwe na sehemu zote muhimu kama vile muhtasari, Maelezo ya biashara, Soko, Mikakati, Sehemu ya fedha(Financials) nk.

Lakini unapoandika mfano kwa ajili ya Benki kuna vipengele(sura) ambazo utazipa kipaumbele(emphasis) zaidi kuliko viperngele vingine na maelezo yake yatakuwa pia ni mengi.

KWA AJILI YA BENKI.

·       Kwa kuwa benki huwa hawatoi mikopo kwa biashara mpya kiholela kutokana na sheria za nchi kwamba ni lazima mkopaji awe kwanza na dhamna za uhakika, benki katika mpango wako wa biashara watapenda zaidi  kuona msisitizo katika sura ya fedha umeonyesha vizuri kwanza rasilimali unazozimiliki wewe pamoja na wamiliki wengine kama wapo.

·       Historia ya mahesabu ya biashara ya siku za nyuma na uorodheshe pia dhamana zote zitakazoweza ku “back up” mkopo wako endapo utakuja kushindwa kuurejesha.

·       Msisitizo pia unatakiwa katika kipengele cha ‘Sehemu za biashara’(Business Ratios)

·       Watapenda pia kuona umeambatanisha katika mpango wako, maombi ya mkopo na ripoti zilizopita za kodi.

SOMA: Jinsi ya kuchora na kutumia chati & grafu kwenye mchanganuo wa biashara

KWA AJILI YA WAWEKEZAJI

·       Wanapenda msisitizo kwenye sura inayozungumzia Mahitaji ya fedha, unahitaji kiasi gani na kwa ajili ya nini

·       Pia orodhesha wanahisa waliopo pamoja na timu imara ya wafanyakazi

·       Wanataka pia kuona mfumo imara wa biashara unaoaminika pamoja na ushahidi wa uwezekano wa biashara kukua vizuri(Business growth)

·       Wawekezaji pia ni wavivu sana kusoma mchanganuo mrefu, hivyo tengeneza vizuri Muhtasari wako uweke mambo yote muhimu kwa kifupi ili ukiwavuta basi wakwambie upeleke mchanganuo mzima.

KWA AJILI TU YA KUENDESHEA BIASHARA YAKO.

·       Unaandika sura zote ukipenda lakini weka msisitizo tu katika zile sura au vipengele ambavyo wewe mwenyewe umepanga kuwa vitakuwa ndiyo kipaumbele chako katika kuifanikisha hiyo biashara.

·       Kwa mfano mwingine anaweza kuamua kwamba katika biashara yake suala la wafanyakazi ndio siri yake kubwa ya ushindi, hivyo sura hiyo ya ‘management’ itabidi aweke maelezo yakutosha. Ikiwa ni katika soko na mauzo basi sura ya mikakati na masoko itabidi uweke kipaumbele na maelezo ya kutosha kuliko sura zinginezo.

0 Response to "NINA TATIZO KUBWA UPANDE WA MAKADIRIO YA GHARAMA NA KUJUA AINA YA MPANGO WA BIASHARA(SWALI)"

Post a Comment