JINSI YA KUCHORA NA KUTUMIA CHATI & GRAFU KWENYE MCHANGANUO WA BIASHARA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JINSI YA KUCHORA NA KUTUMIA CHATI & GRAFU KWENYE MCHANGANUO WA BIASHARA

grafu na chati katika mpango wa biashara

Huu ni mfululizo wa masomo ya utangulizi wa semina yetu  ya HESABU ZA MPANGO WA BIASHARA itakayofanyika kuanzia siku ya Jumatano tarehe 20 mpaka Ijumaa tarehe 23 mwezi huu ndani ya Group la MICHANGANUO-ONLINE kupitia njia za whatsap na Email. Ikiwa unapenda kushiriki semina hii basi wahi nafasi yako mapema kwa kutoa kiingilio shilingi elfu 10 kupitia namba zetu, 0765553030  au 0712202244 ikifuatiwa na neno, “NIUNGANISHE NA SEMINA”

Masomo haya ya utangulizi japo yanahusiana na masomo ya semina hiyo lakini siyo sehemu ya semina yenyewe, Semina itashughulika na vitu vya msingi zaidi katika masuala ya fedha hasa yale yanayowatatiza sana watu.

CHART NA GRAPH NI VITU GANI?
Chati au graph ni sawa na picha(taswira) inayowakilisha namba na maelezo kwa njia nyepesi zaidi na inayoweza kutafsiriwa kwa urahisi na msomaji wa mpango wako wa biashara. Upo usemi mmoja unaosema hivi, “ Picha hubeba maneno elfu moja” Hivyo chati moja tu inaweza kutumiwa kuelezea maneno na namba amazo zingeliweza kujaza hata ukurasa mzima.

SOMA: Jinsi ya kuandaa mchanganuo wa biashara yenye mafanikio, maeneo 6 muhimu ya kuzingatia.

Grafu husaidia kuelezea maendeleo ya kitu fulani kwenye biashara kwa mfano, mauzo, gharama za mauzo nk. na kuweza pia kulinganisha vitu hivyo na vya washindani wako au biashara nyingine kwa urahisi.

AINA ZA CHATI & GRAFU
Unapotamka chati unamaanisha grafu hizohizo ingawa grafu inaweza ikawa moja kati ya aina za chati. Kwa ujumla zipo aina nyingi za chati unazoweza ukazitumia katika mpango wako wa biashara lakini zile zilizozoeleka zaidi ni hizi zifuatazo;

SOMA: Kuandika mchanganuo wa biashara yako kwa kiswahili kuna faida nyingi.

1.Chati za mihimili iliyosimama (Column charts)
Chati hizi zina nguzo au mihimili iliyosimama na ndiyo hutumika sana katika mipango ya biashara mfano ni chati zinazowakilisha kianzio, makisio ya mauzo, makisio ya faida na hasara, na ile ya mtiririko wa fedha taslimu.

2.Pai chati (pie chart)
Hizi ni duara lililogawanywa katika vipandevipande na kila ipande huwakilisha kundi fulani la taarifa/data. Ukubwa wa kila kipande hutegemea ni asilimia ngapi ya kipande hicho huwakilisha katika duara zima.

3. Chati za mtari (line chart)
Ni zile chati au grafu zilizo na mstari unaounganisha vidoti vya data na mfano mzuri ni grafu inayopatikana katika tathmini ya mauzo yanayorudisha gharama zote(Break even analysis)

SOMA: SEMINA: Njia za uhakika za kuboresha mzunguko wako wa fdha 

4. Chati ya mihimili iliyolala (Bar chart)
Hii inafanana na ile iliyotajwa mwanzo kabisa ya mihimili iliyosimama lakini tofauti ni kwamba mihimili yake imelala upande. Mfano wake ni kama ile inayotumiwa sana kuomyesha mtiririko wa matukio katika kipengekle cha mikakati na utekelezaji

Maeneo/sehemu 7 katika mpango wa biashara unazoweza kukuta chati/grafu.

1. Punde tu mara baada ya Muhtasari tendaji. 
Kabla ya kuanza kwa Dhamira kuu, Maono na Malengo; Mara nyingi utakuta panawekwa bar chati inayoonyesha kwaufupi Mauzo, Faida ghafi na Faida halisi au chati inayoonyesha Uwekezaji, Gharama za kuanzia, Rasilimali(assets) na Mkopo.

2. Katika sura ya Maelezo ya Kampuni/Biashara kipengele kidogo cha Kianzio pana chati inayoonyesha pia Uwekezaji, Gharama za kuanzia, Rasilimali(assets) na Mkopo.

3. Kwenye Sura ya Soko kipengele kidogo cha Mgawanyo wa soko kuna Pai chati inayoonyesha mgawanyo katika vipande.

4. Katika Sura inayohusu Mikakati na utekelezaji kipengele kidogo cha Makisio ya mauzo Zipo chati mbili moja inayoonyesha makisio ya mauzo kwa miezi na nyingine ikionyesha makisio ya mauzo kwa mwaka katika miaka 3.

5. Katika Kipengele cha Fedha kipengele kidogo cha Mauzo yakurudisha gharama(breal even analysis) utaona kuna chati ya mstari inayoonyesha jinsi faida na mauzo vinavyohusiana na gharama mbalimbali.

6. Katika kipengele hichohicho cha Fedha kipengele kidogo cha Makisio ya Faida na Hasara utakutana na chati 2, au 4 moja ni ya faida halisi kwa mwaka, faida halisi kwa mwezi halafu kuna faida ghafi kwa mwaka na kwa miezi pia.

7.Tukiwa katika kipengele cha fedha hichohicho katika kipengele kidogo cha Makisio ya Mtiririko wa fedha taslimu utakutana na chati inayoonyesha makisio ya mtiririko wa fedha katika miezi yote 12.

Utaweka grafu na chati ngapi katika mchanganuo wako?
Hii hutegemea lengo lako katika uandaaji wa mchanganuo wako. Pia itategemea hadhira yako(wale watakaousoma mpango huo) Mfano ikiwa mchanganuo wako ni mrefu sana inabidi pia uweke chati za kutosha kusudi kama msomaji wako ni mvivu aweze kupata kitu cha kumrahisishia kazi ya kuelewa kile ulichokusudia. Lakini pia unaweza tu kuweka chati zinazowakilisha yale maeneo yako ya kipaumbele unayojua msomaji wako anaweza akapitia haraka haraka au hata ukaweka chati moja au mbili au usiweke chati hata moja kama mchanganuo wako ni mfupi sana.

Jinsi ya Kutengeneza Chati/Grafu katika mchanganuo wa biashara.

Chati au Grafu unaweza kutengeneza ukitumia njia mbalimbali lakini zilizozoeleka zaidi ni hizi 2

1)  Kwa kutumia program za MICROSOFT WORD au MICROSOFT EXCELL

2)  Kwa kutumia program maalumu zinazotumika katika uandaaji wa michanganuo ya biashara mfano Palo Alto Software nk.

Katika njia zote 2 utakuta mtu unatakiwa kujaza data(namba zako na maneno) halafu mambo mengine yote unaiachia programu kushughulika nayo. Inamaana kwamba itatoa matokeo kulingana na kile ulichojaza haijui kama umekosea au la.

SOMA: Huna muda wa kutosha kuandika mpango wako wa biashara? Tumia njia hizi 3 rahisi.

Njia rahisi na ya bure unayoweza kutumia ni hii ya kutumia program za Microsoft Word au Excell. Mimi hutumia zaidi WORD kutokana na kwamba inakuwa katika document ileile ninayokuwa nikifanyia kazi tofauti na excel ambayo ni lazima ukaikopi kwanza ndipo uje upaste.

1. KUTUMIA PROGRAMU YA MICROSOFT WORD KUCHORA GRAFU NA CHATI KATIKA MPANGO WA BIASHARA.

Jinsi ya kuchora Chati au Grafu hizo kwa kutumia Microsoft word ni rahisi sana na nitaonyesha somo hilo live leo usiku saa 3 katika group la Michanganuo-online kwa njia ya VIDEO na pia maandishi ya kawaida hivyo usikose tafadhali. Kama ulikuwa hujajiunga lipia kiingilio chako mapema na hii pia ndio itakayokuwa tiketi yako ya kushiriki semina Kubwa ya JINSI YA KUANDAA KIPENGELE CHA FEDHA KATIKA MPANGO WA BIASHARA siku ya tarehe 20 mpaka 23 Machi 2019.

Kiingilio ni sh. elfu 10

Namba za kulipia ni; 0765553030  au  0712202244 

Peter Augustino Tarimo

0 Response to "JINSI YA KUCHORA NA KUTUMIA CHATI & GRAFU KWENYE MCHANGANUO WA BIASHARA"

Post a Comment