SABABU KUBWA 2 WATU HUSHINDWA KUWEKEZA PESA KWENYE BIASHARA ZINAZOLIPA SANA INGAWA WANAJUA FIKA ZINALIPA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SABABU KUBWA 2 WATU HUSHINDWA KUWEKEZA PESA KWENYE BIASHARA ZINAZOLIPA SANA INGAWA WANAJUA FIKA ZINALIPA

uwekezaji wa pesa
Kwa kawaida kila mtu anapowekeza pesa zake hutegemea kupata faida au kwa lugha nyingine unaweza ukasema anataka biashara au mradi umlipe. Biashara isiyolipa maarufu kama  “Biashara kichaa” hamna mtu atataka kuifanya hata kidogo. Faida au kulipa kwa biashara ndiyo “uchawi” wenyewe nyuma ya uwekezaji wowote ule duniani kote.

Katika Ulimwengu wa biashara kuna kitu kinachoitwa Return On Investment(ROI), tafsiri yake isiyo rasmi unaweza kuita, Malipo  katika Uwekezaji, kuna wanaoita pia Rate Of Return(ROR). ROI au ROR maneno hayo ya kitaalamu yasikutishe, siyo kitu cha ajabu sana bali tu ni KIWANGO CHA ULIPAJI wa biashara husika ambacho ni uwiano unaopimwa katika asilimia kuonyesha kiwango chake cha ufanisi (business performance) Unataka kujua ni kwa asilimia ngapi fedha utakazowekeza zinaweza kutengeneza faida katika kipindi fulani tuseme labda mwaka nk.

SOMA: Ijue sehemu ngumu kuliko zote unapoandika mchanganuo wa biashara yako.

ROI kanuni yake ni hii, Unachukua Thamani ya mradi baada ya kupata faida Unatoa Gharama zote za mradi, jibu gawa kwa Gharama za mradi kisha uzidishe mara 100. Tuchukulie mfano umeanzisha biashara ya kutengeneza juisi ya ubuyu,
Gharama zote za kuanza ni sh. 20,000
Baada ya kuuza juisi yote faida ukapata ni sh. 4,000
Hivyo ROI yako itakuwa  (4,000/20,000) X 100 = 20%

Ukiweka pesa kwenye akaunti, fixed deposit sh. Milioni 10 baada ya mwaka ukakuta imeongezeka sh. Laki 5 ina maana kwamba ROI yako ni  (500,000/10,000,000)x100 = 5%

Hivyo biashara hii ya juisi ya ukwaju kiwango chake cha ulipaji ni kizuri tu asilimia 20% ingawa hatujazingatia muda kama mwaka mmoja nk. Kuna biashara huwa na kiwango cha chini sana kwa mfano ukiwekeza pesa zako katika akaunti za kudumu katika mabenki huwezi ukapata zaidi ya asilimia 5% kwa mwaka, hisa katika makampuni ni wastani wa asilimia 10%, Majengo wastani asilimia 10% nk.

SOMA: Makisio ya fedha kwenye mpango wa biashara.

Asilimia kubwa maana yake biashara inalipa sana na asilimia ndogo biashara inalipa kidogo. Tukiwa tunaelekea  siku ya semina yetu kubwa ya HESABU ZA MCHANGANUO WA BIASHARA Machi 29 mwaka huu,  leo nimeanza kukuletea vidokezo na dondoo mbalimbali kama matayarisho ya semina hiyo.

Kipimo hiki ROI ni muhimu sana kwani unaweza ukalinganisha biashara tofauti unazofikiria kuanzisha ukachagua moja iliyo na kiwango(ROI) kikubwa zaidi. Uwiano wa ROI pamoja na vipimo vingine vingi tutakwenda kujifunza vyote kwa kina katika semina hiyo  kwa lugha rahisi kabisa mtu wa kawaida anayoweza kuelewa. Uwiano huu unakuwezesha kujua biashara inalipa vizuri kwa kiasi gani(Business Performance)

Hata hivyo katika kuchagua biashara ya mtu atakayoifanya kuna vigezo vingine mbalimbali ndio maana unaweza kukuta biashara ina ROI kubwa tu lakini bado watu wanashindwa au wanaogopa  kuzifanya na wanapoamua kuzifanya bila kuzingatia vigezo hivyo vingine huishia kupata matokeo mabaya ambayo hawakuyatarajia.

SOMA: Ni lini biashara yako itarudisha gharama zote ulizotumia?

Kuna sababu 2 kubwa zinazosababisha biashara yenye kiwango kikubwa cha kulipa faida(ROI) kutokulipa kama inavyotazamiwa na mjasiriamali ambazo ni hizi zifuatazo;

1.  Kisi cha fedha unazowekeza
2.  Kiasi cha muda uwekezaji huo utakaochukua

1.KIASI CHA PESA
Hebu fikiria uwekezaji kwa mfano wenye kulipa kwa assilimia 2% kwa mwaka, ukiweka milioni 10 maanake mwisho wa mwaka utapata shilingi laki 2 juu, lakini kwa mfano ikiwa kama utawekeza kiasi cha mtaji wa shilingi bilioni 1 kwa muda ule ule utapata shilingi milioni 20 badala ya laki 2, unaona jinsi kiasi cha fedha kinavyoweza kuleta tofauti katika wingi wa faida unayopata?

2.KIASI CHA MUDA
Hata ingelikuwa biashara ina ROI kubwa kiasi gani tuseme hata kwa kiwango cha asiliia 100%, lakini ikiwa utawekeza fedha leo mara keshokutwa umeondoa pesa zako ama kuuza uwekezaji huo, hutaweza kuona faida yeyote ile ya maana. Uwekezaji unahitaji subira ya kutosha miaka 3 mpaka 5 na kuendelea huko.

SOMA: Sababu 4 kwanini kipengele cha fedha ndio moyo wa mpango wa biashara (The heart of a business plan)



HITIMISHO.
Ili uweze kufanya uwekezaji wenye faida nzuri(tija) unatakiwa
kuchanganya vitu vyote hivi 3, kiwango kizuri cha ulipaji(ROI), Mtaji mkubwa wa kutosha na Muda mwingi wa uwekezaji wako.

...........................................................................

UJUMBE HUU NI KWA WALE TU AMBAO BADO HAWAJAJIUNGA NA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE

Ndugu msomaji wa blogu hii, ikiwa wewe bado ulikuwa hujajiunga nasi, nakukaribisha sana katika group letu la masomo ya kila siku yahusuyo pesa, liitwalo MICHANGANUO-ONLINE. Katika group hilo huwa tunakuwa na masomo kila siku pamoja na Semina za mara kwa mara. Semina kubwa tunayokwenda kufanya mwezi huu itahusu, JINSI YA KUANDAA HESABU ZA MPANGO WA BIASHARA na itaanza siku ya Jumatano ya tarehe 20 mwezi huu 2019 na kumalizika siku ya Ijumaa tarehe 22.

Kiingilio ni shilingi elfu 10 tu na unaendelea kuwa mwanachama katika group hilo ambapo utashiriki bila malipo semina nyingine zote zitakazofanyika katika group hilo kwa mwaka huu wa 2019. Pia tunakupatia vitabu, masomo na semina zote zilizopita katika group.

Hii ni ofa itakayodumu kipindi kifupi mpaka pale group litakapojaa kwani nafasi zimebakia chache mno ili idadi ya watu 250 itimie, idadi ambayo ndiyo kikomo katika magroup, hivyo ikiwa unapenda mwaka huu wote tuwe pamoja usisite wahi nafasi mapema kwa gharama hii ndogo ya sh elfu 10 ukilinganisha na vitu utakavyopata.

Ikiwa hupendi kujiunga na magroup unaweza kulipia semina na tukakurushia kila kitu kupitia email yako.

Kujiunga lipia kupitia namba zetu, 0712202244  au 0765553030 jina hutokea, Peter Augustino Tarimo kisha nitumie ujumbe wa, "NIUNGE NA SEMINA" 





0 Response to "SABABU KUBWA 2 WATU HUSHINDWA KUWEKEZA PESA KWENYE BIASHARA ZINAZOLIPA SANA INGAWA WANAJUA FIKA ZINALIPA"

Post a Comment