SABABU 4 KWANINI KIPENGELE CHA FEDHA NI MOYO WA MPANGO WA BIASHARA (THE HEART OF A BUSINESS PLAN) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SABABU 4 KWANINI KIPENGELE CHA FEDHA NI MOYO WA MPANGO WA BIASHARA (THE HEART OF A BUSINESS PLAN)



Katika sura au vipengele vinavyounda mchanganuo wa biashara (business plan) kipengele kinachohusu masuala ya fedha (hesabu & namba) ndio kipengele kinachochukuliwa kuwa ndio moyo wa mpango mzima wa biashara kutokana na sababu zifuatazo;

1.  Ndio  humsaidia mjasiriamali kutambua ikiwa biashara  yake italipa faida au la, na hivyo kuachana nayo au kuendelea nayo.

2.  Ndio humwezesha mjasiriamali kukisia ni kiasi gani cha mtaji kinachohitajika kuanzisha na kuendesha biashara yake kwa mafaikio makubwa.

3.  Huwezesha kubainisha mmiliki wa biashara atoe kiasi gani cha mtaji na ikiwa kiasi hicho hakitoshi basi akope kiasi gani.

4.  Sehemu nyingine zote za mpango wa biashara kama vile masoko, utawala na uendeshaji nk. ukamilifu wake hutegemea kipengele hiki cha fedha.

SOMA: Sehemu ngumu kuliko zote unapoandika mpango wa biashara.

Kipengele cha fedha  ndiyo eneo linalopaswa kutazamwa kwa umakini wa hali ya juu kabisa kutokana na umuhimu wa sababu zilizotajwa hapo juu. Ijapokuwa katika mpango wa biashara kuna kipengele mahsusi kinachohusiana na fedha lakini hesabu huanzia tokea sura za mwanzo na mfano ni kwenye kianzio wakati unapokisia mahitaji ya kuanzia katika kipengele cha Biashara/kampuni. Ukija katika kipengele cha soko utakutana na hesabu wakati wa kutathmini ukuaji wa soko, katika makisio ya mauzo kwenye kipengele cha Mikakati na utekelezaji na katika jedwali la mishahara  kwenye sura ya Utawala na nguvukazi.

SOMA: Jinsi mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanikio ya biashara yako.

Katika kipengele chenyewe mahsusi cha fedha kuna majumuisho ya hesabu hizo ndogondogo zote zilizotajwa katika aya iliyopita na majumuisho hayo huwekwa katika Taarifa au Ripoti kuu tatu ambazo ni Makisio ya Ripoti ya Faida na hasara, Makisio ya Ripoti ya mtiririko wa fedha na makisio ya ripoti ya mali na madeni(mizania ya biashara). Makisio katika taarifa hizo 3 hujengwa juu ya msingi wa utafiti au hesabu za biashara za kipindi kilichopita.

SOMA: Ni lini biashara yako itarudisha gharama zote ulizotumia?(Break Even Point)

Hesabu katika mpango wa biashara ndio kipengele watu wengi huona ni kigumu  lakini ugumu huo unatokana na kutokufahamu vyema kanuni ya kukokotoa hesabu zenyewe. Sababu hii imetufanya tuandae semina maalumu inayohusu Hesabu za mpango wa biashara.

Semina hii itaendeshwa kupitia group la whatsap la MICHANGANUO-ONLINE kuanzia tarehe 12 hadi tarehe 15 Februari 2019. Kiingilio ni shilingi elfu 10 na mwisho wa malipo ni  ni tarehe 11 siku ya Jumatatu. Dondoo zaidi kuhusiana na semina hii tutaendelea kujuzana kila siku mpaka siku ya mwisho.

Kujiunga tuma kiingilio chako kupitia namba zetu za simu ambazo ni, 0765553030 au 0712202244 jina hutokea Peter Augustino Tarimo. Kisha tuma ujumbe usemao. “NIUNGANISHE NA SEMINA YA HESABU ZA MCHANGANUO”

SOMA: Huna muda wa kutosha wa kuandika mpango wa biashara yako? Tumia njia hizi 3 rahisi.

Kwa wale watakaojiunga watapata pia offa ya masomo mengine mengi yaliyopita siku za nyuma vikiwemo vitabu 3 maarufu vya masomo ya mzunguko wa fedha 2018 na Michanganuo ya biashara hatua kwa hatua 2018. Pia mshiriki atapata fursa ya kushiriki kwenye group kwa mwaka wote wa 2019 bila kutoa malipo mengine yeyote ya ziada.

Baada ya semia hii, semina nyingine zitakazofuata zitahusiana na michanganuo ya viwanda vidogo na vya kati kama ilivyokuwa kaulimbiu yetu ya mwaka huu wa 2019,

*KWA VITABU VYA UJASIRIAMALI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI TEMBELEA;  SMARTBOOKS TANZANIA

*YALE MASOMO YA FEDHA YA KILA SIKU KATIKA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE YAMERUDI UPYA BAADA YA LIKIZO YETU YA MWEZI 1, NA KESHO  FEBRUARI 2 USIKU SAA 3 TUTAKUWA NA SOMO LIFUATALO; 

"SAIKOLOJIA YA PESA NA KANUNI YA KUFUATA ILI UWE MTU ULIYEFANIKIWA KIMAISHA" 


0 Response to "SABABU 4 KWANINI KIPENGELE CHA FEDHA NI MOYO WA MPANGO WA BIASHARA (THE HEART OF A BUSINESS PLAN)"

Post a Comment