Unategemea mshahara wa mwezi au kipato kimoja? Hizi hapa mbinu za kujinasua na kuishi maisha mazuri unayotamani. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

Unategemea mshahara wa mwezi au kipato kimoja? Hizi hapa mbinu za kujinasua na kuishi maisha mazuri unayotamani.

Karibu tena rafiki na mdau wangu muhimu katika blogu hii ya jifunzeujasiriamali, baada ya likizo yangu ya mwezi Januari sasa nimerudi tena rasmi na tegemea mambo mengi mapya na mazuri mwaka huu wote huu wa 2019 niliyokuahidi mwezi Desemba.

Leo tutazungumzia juu ya hatari ya utegemezi katika mshahara au kipato kimoja tu, mtu hapaswi kuwa kama samaki kwamba akitolewa kwenye maji tu na huo unakuwa ndio mwisho wa maisha yake. Yafaa tufanane na kiboko, kwenye nchi kavu anadunda na majini pia anadunda bila wasiwasi wowote.
………………................

Siyo kila mtu unayemuona anafanya kazi ya kulipwa mshahara mwisho wa mwezi basi ni tegemezi kwa mshahara anaolipwa hapana, kuna baadhi ya watu wengine ingawa ni wachache hufanya kazi kwasababu tu wanaipenda na wanataka kukidhi hamu yao ya kuifanya hiyo kazi, wanafanya kazi ili waishi kwa furaha. Watu hawa kwa maneno mengine tunaweza kuwaita watu walio huru kifedha.

Lakini kwa upande mwingine asilimia kubwa ya watu walioajiriwa zaidi ya asilimia 95% au wale wanaofanya biashara inayowaingizia kipato kimoja tu hawawezi kuishi bila kipato hicho, maana yake ni kwamba ikiwa kipato chao cha mwezi kitasita siku moja hawana tofauti na samaki aliyetolewa nje ya maji. Kwa upande wa waliojiajiri lakini wanategemea chanzo kimoja tu cha mapato mfano biashara moja tu nao hawana tofauti na wale walioajiriwa wakitegemea mshahara wa mwezi peke yake kwani hawana njia nyingine mbadala inayoweza kuwaingizia kipato. Hata hivyo makala hii imekazia zaidi ajira.

Kwanini watu wanakuwa tegemezi kwa mshahara wa mwezi au chanzo kimoja tu cha mapato?

Sababu kubwa ya utegemezi kwenye mshahara wa mwezi ni kwamba kipato kinachotokana na mshahara ndiyo kipato kinachoweza kutabirika kwa urahisi kuliko vipato vya aina nyingine zote lakini ubaya wake ni kwamba huwafanya watu kuridhika kupita kiasi(kubweteka) kuhusiana  na hali yao ya kifedha.

Kipato cha mshahara ni cha uhakika tu pale mtu anapokuwa akifanya kazi, ikiwa atasitisha kazi leo na mshahara nao utakoma siku inayofuata. Watu hujihisi salama zaidi wawapo na ajira na hivyo kuchukulia utegemezi kwenye ajira kuwa ni jambo la kawaida tu. Lakini hali hii hubadilika ghafla kipindi usalama wa ajira unapokuwa hatarini. Kipindi hiki ndicho mtu hutambua hasara za kuwa tegemezi kwenye mshahara wa mwisho wa mwezi.

SOMA: Kwanini kama huipendi ajira yako bado unaendelea kuifanya?

Watu wengine hata inakuwa vigumu kukubali ukweli kwamba maisha ya kutegemea mshahara wa mwezi au chanzo kimoja tu cha mapato ni jambo baya na la hatari. Watu tokea utotoni tumeaminishwa aina hizi za fikra na yeyote yule anayejaribu kuhoji kasumba hizi hukumbana na upinzani mkali na kukosolewa.

Kuishi ukitegemea mshahara peke yake au chanzo kimoja tu cha mapato ni hatari iliyokuwa wazi kabisa, hebu fikiria labda umepoteza kazi yako leo kwa sababu yeyote ile, inamaana kwamba mwezi unaofuata huwezi tena kuwalipia watoto wako tuisheni wala kuwapatia hela ya matumizi shuleni. Hata chakula na matumizi mengine ya msingi nyumbani hutaweza tena kuyanunua, huwezi kuwanunulia mlo mzuri kama nyama, samaki nk wataishia tu kula mchicha na maharage ya kubangaiza  na kila kitu kitakuwa kigumu kwako.

Mtu atapunguza au kuondokana vipi na utegemezi katika mshahara wa mwezi au chanzo kimoja cha mapato?

Kabla hatujakwenda kuona njia ya kupunguza au kuondoa kabisa utegemezi katika mshahara wa mwezi, hebu kwanza tuone kwa undani nini maana ya kutegemea mshahara wa mwezi au chanzo kimoja tu cha mapato(Kuishi ukitegemea mshahara wa mwezi hadi mwezi au paycheck to paycheck). Unaweza kudhani kuwa watumwa wa mshahara wa mwezi ni watu wale wa hali ya chini tu wanaolipwa mshahara mdogo lakini utakuwa umekosea sana.

SOMA: Wafanyakazi kwenye kazi za ajira wengi  hawana fura, upo ukweli wowote au ni uzushi mtupu?  

Hata mtu anayelipwa mamilioni ya fedha ikiwa hana kipato cha ziada na nidhamu nzuri ya matumizi ya fedha hizo za mshahara hatakuwa na tofauti yeyote na mtu yule anayelipwa mshahara wa kima cha chini kabisa ambaye naye hana nidhamu na mshahara huo wala chanzo kingine cha mapato.

Kuna vitu hivi vikubwa viwili,

1.  Chanzo cha fedha
2.  Mahitaji au matumizi

Ikiwa wewe chanzo chako cha fedha ni mshahara peke yake na matumizi yako asilimia kubwa zaidi ya 95% unategemea mshahara huo basi jua kabisa kwamba upo miongoi mwa watumwa wa mshahara wa mwezi. Mtu yeyote ambaye mapato yake ni kidogo kuliko matumizi hayupo huru, ni tegemezi kwa kipato anachopata iwe ni mshahara wa kila mwezi au hata au hata faida kwenye biashara. Mtu wa aina hii hawezi kabisa kujiwekea akiba wala kuishi bila ya kipato chake hicho hata kwa miezi 2 au 3 mbele.

SOMA: Kwanini ni rahisi zaidi kutajirika ukiwa kwenye ajira kuliko kujiajiri binafsi? 

Ikiwa upo miongoni mwa watu wengi waliotegemezi kwa mshahara wa mwezi au chanzo kimoja tu cha mapato usiogope kuna habari njema kwako, unaweza kuchukua hatu za kubadili muelekeo na kuwa huru zaidi kifedha.

KIVIPI?

Ni kwa njia moja tu ya kuweka akiba  wakati huohuo ukitumia akiba hiyo kujijengea/kujinunulia rasilimali(assets) zinazoweza kuzalisha mapato zaidi. Hii ndiyo njia ya uhakika zaidi ya kupunguza na hatimaye kumaliza kabisa utegemezi kwenye mshahara au kipato kimoja tu. Huu ni mchakato unaopaswa kwenda taratibu na kwa uvumilivu mkubwa, hakuna njia ya mkato hapa.

SOMA: Ajira siyo laana bali ni mtaji wa uhakika kuliko aina nyingine zote za mitaji.

Kitu cha kwanza na muhimu zaidi kwako ni kutambua kwamba kutegemea mshahara wa mwezi au chanzo kimoja tu cha mapato maishani ni jambo baya na la hatari sana kwako. Halafu sasa anza kujinunulia asseti/rasilimali zenye uwezo wa kukuingizia kipato cha ziada. Kipato cha ziada hapa ninamaanisha kile kipato ambacho wewe hulazimiki kufanya kazi ndipo kiweze kuingia, huingia tu hata kama umelala au unaumwa.

Unaweza ukauliza swali hili, ikiwa kipato chako cha mwezi hakitoshelezi mahitaji yako yote utaweka akiba na nini kusudi uweze kuja kujinunulia rasilimali? Majibu ni haya yafuatayo;

1.Jifunze kujinyima kusudi uweze kuweka akiba zaidi.

Kuna vitu ukijinyima au ukaahirisha kuvinunua huwezi kufa, kwa mfano vitu vyote tunavyotumia ili kuridhisha  tu nafsi zetu tunaweza kuachana navyo kabisa bila madhara yeyote mfano mmojawapo ni kula mlo wa gharama ya juu kama chipsi kuku nk. wakati kuna vyakula vya gharama ndogo tu kama ugali, wali na mihogo. Kadiri utakavyoweka akiba zaidi huku ukijinunulia rasilimali ndivyo na nafasi yako ya kuondokana na utegemezi kwenye mshahara nayo itakavyoongezeka.

SOMA: Huna mtaji wa kutosha na hukopesheki? Jaribu njiia hii ya kufunga mkanda (bootstrapping)

Jitahidi kuwa mvumilivu kabla hujataka kitu au kufanya jambo linalotoa fedha mfukoni kwako. Inawezekana ni mahai pa kutembea tu kwa miguu, wewe bajaji au bodaboda ni ya nini? Ishi leo kama masikini lakini kesho uje uishi kama mfalme. Ndugu yako anayetaka leo umpe msaada wa fedha kwa mambo madogomadogo yasiyokuwa na umuhimu mkubwa kwanini usimnyime ukijua ukijakufanikiwa utampa msaada mkubwa zaidi kama kumsomeshea mwanae, hela za matibabu nk.?

2.Jijengee taswira ya uhuru wa kifedha kwenye akili yako. 
  
Oanisha na kuzizoea akilini dhana mbalimbali zinazohusiana na uhuru wa kifedha kabla hata hujaufikia uhuru wenyewe kifedha kwa mfano;

1.  Kipato cha mshahara
2.  Kuweka akiba
3.  Kujilimbikizia rasilimali(asseti) zinazowezaweza kukuzalishia kipato cha ziada
4.  Kipato cha ziada mbali na ajira
5.  Gharama/matumizi yako yote ya kila mwezi
6.  Fedha za dharura
7.  Kuwa huru na madeni
8.  Jinsi ya kuweka akiba
9.  Jinsi ya kujijengea rasilimali zinazozalisha faida. Nk.

Hakikisha unakuwa na uelewa na dhana hizi mbalimbali, kujua maana yake na jinsi unavyoweza kuzitumia katika harakati zako mbalimbali za kusaka pesa.

SOMA: Kama una biashara ndogo ya mtaji kidogo, hizi hapa njia 11 za kiboost 

Hakuna kitu kinachoweza kuizidi tabia njema ya kujiwekea akiba linapohusika suala zia la Uhuru wa mtu wa kifedha au kwa maneno mengine mafanikio kifedha. Kuweka akiba ndio mwanzo wa kila kitu pale mtu anapotaka kuanza kununua rasilimali yake ya kwanza(asset). Lakini kuweka tu akiba hakuwezi kutosha, unatakiwa pia ununue rasilimali zitakazokuingizia kipato kama hizi hapa chini;

·       Hisa
·       Akaunti ya kudumu ya benki(fixed bank account)
·       Hata tu kununua chupa ya chai(thermos) kwa ajili ya kuuzia chai nayo ni asseti, mashine mbalimnali mfano za kufyatulia tofali, kukamulia juisi ya matunda kama miwa, chungwa, embe nk. Kununua kipande cha ardhi au nyumba ingawa vitu hivi unaweza kuhitajika ushiriki wako pale kwa namna moja au nyingine siyo kama ilivyo kwa hisa au akaunti ya kudumu ya benki. Kumbuka biashara inahitaji rasilimali ili iweze kufanyika.

SOMA: Kwanini kila mwanamke anastahili kumiliki vyanzo vingi vya mapato?

Tunaweza kuondokana kabisa na utegemezi kwenye mishahara yetu ya kila mwezi au kipato kimoja tu kwa kujijengea au kujinunulia rasilimali(assets) zenye uwezo wa kuzalisha kipato cha ziada cha kutosha kukabiliana na matumizi yetu yote ya mwezi mzima bila ya kugusa mshahara wenyewe. Jambo hili linatakiwa kuwa ndio LENGO kuu la kila mtu maishani katika kuhakikisha maisha bora yaliyojaa furaha tele. Ingawaje fedha tu peke yake haiwezi kuwa ndio nyenzo kuu ya kukuletea furaha lakini ina mchango mkubwa katika kumfanya mtu aishi maisha ya UHURU.  

Xxxxxxxxxxx Mwisho wa mkala hii. Xxxxxxxxx

Ndugu  msomaji wa makala hii, huu ni mwezi wa 2 tangu mwaka huu uanze na katika email yangu ya mwisho kwako nilikuahidi moja ya malengo ya kampeni yetu ya mwaka huu tutashughulika zaidi na VIWANDA , nilisema kwamba michanganuo mingi tutakayoandika itahusiana na viwanda mbalimbali vidogo na vya kati ambapo mtu anaweza kuanzisha cha kwake kwa urahisi.

Baada ya mwezi mzima wa kwanza kumalizika ambao ndio uliokuwa mwezi wa likizo kwa upande wetu(kumbuka Desemba tulifanya kazi mwezi mzima bila ya kupumzika) sasa kampeni zetu za mwaka huu wa 2019 ndio zimeanza rasmi Februari hii. Kwa kuanzia nimegundua watu wengi katika kuandika michanganuo ya biashara tatizo kubwa lipo kwenye NAMBA au MAHESABU. Kimsingi hesabu hizi hazipaswi kuwa ngumu ikiwa utafuata kanuni inayotakiwa.

Ndio maana kabla hatujaanza rasmi Michanganuo ya viwanda mbalimbali tumeona ni vizuri kufanya semina kubwa ya jinsi ya kuandaa hesabu za mpango wa biashara. Semia hiyo itaanza tarehe 12 Februari siku ya Jumnne mpaka tarehe 15 Feb. siku ya ijumaa. Ni semina ya siku 4(Intensively) na tutahakikisha yule aliye na nia ya dhati ya kufahamu kuandaa makadirio ya hesabu za biashara anafahamu kwa uhakika kabisa.

Semina itaendeshwa kupitia group la whatsap la MICHANGANUO ONLINE, Kiingilio cha semina hii ni shilingi elfu kumi,  10,000/= na mwisho wa kulipia ni Jumatatu ya tarehe 11. Undani wa semina yenyewe tutajulishana kila siku kabla ya siku yenyewe kufika hapa katika blog na kwa njia ya email.

Vile vile masomo yetu ya kila siku katika group la WASAP la Michanganuo online yanaendelea kama kawaida kwa wale waliokwishajiunga tayari. Wale wanachama wa zamani hawatalipia tena semina hii ya Mahesabu ya mpango wa biashara, wataingia free.

Nafasi zinaweza kujaa muda wowote kuanzia sasa kutokana na idadi ya group kukaribia kufika watu 250, idadi ya mwisho, hivyo ni vizuri kama unapenda kuwa miongoni mwa group hili makini(SUPER MASTERMIND GROUP 2019) kwa mwaka mzima huu wa 2019 basi uwahi siti yako mapema kabla group halijajaa, hatutakuwa na uwezo wa kuendesha magroup mawili kwa wakati mmoja.

ASANTE SANA
Peter Augustino Tarimo
self help books Tanzania ltd

Wasap: 0765553030
Simu:    0712202244


0 Response to "Unategemea mshahara wa mwezi au kipato kimoja? Hizi hapa mbinu za kujinasua na kuishi maisha mazuri unayotamani."

Post a Comment