KWANINI KILA MWANAMKE ANASTAHILI KUMILIKI VYANZO VINGI VYA MAPATO? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KWANINI KILA MWANAMKE ANASTAHILI KUMILIKI VYANZO VINGI VYA MAPATO?

Mwanamke mjasiriamali
Katika masuala yote yanayohusiana na kazi, biashara na ajira, wanawake ndiyo wanaopata madhara makubwa zaidi yanayotokana na ukosefu wa vitu hivyo hasa katika uchumi wa siku hizi usioweza kutabirika kwa urahisi tofauti na zamani ambapo mtu aliweza kuishi maisha mazuri tu akiwa na ajira yake ya kawaida au biashara yake moja.



Siku hizi haiwezekani tena hata baada ya mtu kustaafu kazi aishi kwa kutegemea mafao yake ya uzeeni, ni lazima kila mtu wakiwemo wanawake kutafuta njia mbadala za kutokuwa tegemezi katika chanzo kimoja tu cha mapato iwe ni kazi, biashara, mafao ya uzeeni au fedha anazopewa na mumewe. Wanawake wanao wajibu mkubwa wa kuhakikisha wanawapunguzia waume zao mzigo katika kulea familia kwa kuhakikisha wanakuwa na vyanzo mbalimbali vya mapato.

Katika kitabu cha MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA, kitabu hicho kimezungumzia kwa undani sana mifereji saba au vyanzo mbadala 7 vya pesa ambavyo mtu yeyote yule awe mwanamke au mwanaume anaweza akaitumia mifereji hiyo na kujihakikishia uhuru kamili wa kifedha katika maisha yake yote.


Wanawake kwa asili ni watu wanaopenda kuwa na vyanzo vingi vya mapao na hii inatokana na mahitaji yao makubwa hasa ukizingatia kwamba wao ndio  watunzaji wakuu wa familia. Tatizo kubwa linalosababisha mapato yao hayo yasiweze kuonekana kama ya wenzao wanaume ni wingi wa matumizi. Mwanamke haiwezekani mtoto akose penseli wakati ana pesa kidogo kwenye pochi yake, ataitoa hata ikiwa pesa hiyo ni mtaji kwa ajili ya biashara yake.

Faida za mwanamke kuwa na vyanzo vingi vya pesa(mifereji mingi ya mapato)
·       Humwezesha mwanamke kuwa na uhuru mkubwa zaidi na urahisi katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku anapojua kwamba hategemei kwa asilimia 100% kazi yake ya msingi au biashara.

·       Humwezesha mwanamke kukaa nyumbani na familia yake-kuwa huru kifedha maana yake ni kwamba halazimiki tena kuiacha familia yake kutwa akiwa kazini, anao uwezo wa kufanya shughuli zake akiwa nyumbani na kila kitu kikaenda sawa sawa.

·       Ikiwa atafukuzwa au kuacha kazi; kitakachomtokea baada ya kuachana na ajira ni mapato yake kupungua tu na wala siyo kukatika kabisa kama vile angekuwa na chanzo kimoja tu cha mapato. Vyanzo vingine vitakuwa vikimuingizia fedha kama kawaida.

·       Uharaka katika kutimiza malengo yake. Mwanamke hatasubiri tena kwa muda mrefu ndipo aweze kupata fedha kwa ajili ya kutimiza malengo yake. Badala ya kuambiwa na mumewe, “subiri mwisho wa mwezi” anakuwa na urahisi wa kuamua muda wowote ule.

Jinsi mwanamke anavyoweza kujiwekea vyanzo vingi vya mapato.
Kuwa na mifereji mingi ya mapato maana yake ni kuanzisha miradi mbalimbali tofauti na ule mradi wako mkuu au kazi yako ya msingi. Ingawa jambo hili siyo rahisi sana kulitekeleza kama vile unavyoweza kutamka lakini kupitia mbinu na mikakati mbalimbalia kama ilivyoainishwa katika kitabu cha MIFEREJI 7 YA PESA, jambo hili linawezekana bila matatizo.


Hutakiwi kuanza mara moja kujijengea vyanzo vingi vya mapato, kinachotakiwa ni kuanza na kimoja baada ya kingine taratibu. Vile vile siyo kila mradi tu unafaa kuanzisha kama chanzo mbadala cha mapato, kuna miradi rahisi zaidi na inayofaa zaidi ya mingine. Baadhi tu ya vyanzo vya mapato au miradi mwanamke anayoweza akaanzisha kama mbadala ni hivi hapa;

1)  Biashara ndogondogo, zipo za aina nyingi kama zilivyoelezwa ndani ya kitabu chako cha MIFEREJI 7 YA PESA.
2)  Uwekezaji katika majengo na ardhi
3)  Biashara katika mtandao wa intaneti
4)  Kutumia kipaji ulichokuwa nacho katika kutatua matatizo ya watu wengine.
5)  Biashara za mtandao(Network marketing)
6)  Kutumia muda wako wa ziada baada ya kazi
7)  Kuweka akaunti ya benki inayokupa riba kila mwezi
8)  Kukodisha vitu vyako kama vile gar ink.
9)  Uandishi wa kujitegemea
10)              Kuwa na hisa katika makampuni au biashara zingine.nk.

Orodha ya vyanzo mbadala vya mapato haina mwisho, unaweza ukawa na mlolongo mkubwa sana, ni wewe mwenyewe unayeweza kuamua utumie chanzo kipi kulingana na mazingira na uwezo uliokuwa nao. Kama nilivyotangulia kusema, vyanzo vingi vya mapato siyo rahisi sana kuanzisha kama unavyoweza kufikiria lakini ni jambo linalowezekana ikiwa utakuwa tayari kufanya hivyo. Wanawake wengi wameweza na wewe pia unaweza kufanya hivyo.

.................................................................................................

Kwa elimu zaidi ya kina kuhusiana na biashara na ujasiriamali, unaweza ukajipatia vitabu vifuatavyo kutoka Self Help Books Tanzania kupitia njia za Email au vitabu vya karatasi (hardcopy).






SIMU: 0712202244  au  0765553030

Peter Augustino Tarimo.

au tembelea SMART BOOKS TANZANAIA kwa vitabu zaidi

0 Response to "KWANINI KILA MWANAMKE ANASTAHILI KUMILIKI VYANZO VINGI VYA MAPATO?"

Post a Comment