MWANAMKE ALIYEJIFANYA MWANAMUME KWA MIAKA 43 ! | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MWANAMKE ALIYEJIFANYA MWANAMUME KWA MIAKA 43 !

Mjane mwenye umri wa miaka 64, Abu Dahoo(ambaye ni mwanamke pichani juu) ameishi kwa muda wa miaka 43 akijifanya ni mwanamume kusudi  tu aweze kufanya kazi ya “Shoe shine” ili amudu kuitunza familia yake.

Baada ya serikali ya mtaa anaoishi nchini Misri kuligundua hilo iliamua kumtunukia tuzo ijulikanayo kama “Woma Breadwinner Award”. Dahoo alimpoteza mumewe miaka 43 iliyopita alipokuwa na ujauzito wa mwanawe wapekee ambaye ni wa kike.

Daooh,  Mwanamke aliyejifanya mwanaume kwa miaka 43 akipokea tuzo yake. 
Alisema aliamua kujifanya mwanamume kutokana na sababu kwamba jamii yake huwanyanyapaa wanawake wanaofanya kazi. Huvaa vazi la “Jabab” na kofia ya kiume iitwayo  “Taqiyah” pamoja na viatu vyeusi vya kiume. Alisema alichukua uamuzi wa kujifanya mwanamume kusudi aweze kufanya kazi na kujiingizia kipato kizuri kuliko kwenda kuombaomba barabarani.


“Niliamua kufanya kazi ngumu kama kubeba matofali, mifuko ya sementi na kuosha viatu kuliko kwenda kuombaomba. Na ili kujikinga na wanaume wasinitolee macho ya dharau na kutengwa nao kutokana na mila na desturi, “niliamua kuwa mwanaume….., kuvaa kama wao”  na kufanya kazi sambamba nao katika vijiji vile ambavyo  hawakuwa wakinifahamu” Alisema.


Binti yake naye aliolewa lakini mumewe  naye akawa ni mtu wa kuuma umwa, hivyo ilimbidi aendelee kujifanya mwanamume kusudi  aweze kuwatunza mwanawe na wajukuu zake.

Chanzo cha makala hii ni tovuti ya Howafrica.com

0 Response to "MWANAMKE ALIYEJIFANYA MWANAMUME KWA MIAKA 43 !"

Post a Comment