NI LINI BIASHARA YAKO ITARUDISHA GHARAMA ZOTE ULIZOTUMIA?(BREAK EVEN POINT) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NI LINI BIASHARA YAKO ITARUDISHA GHARAMA ZOTE ULIZOTUMIA?(BREAK EVEN POINT)

Kwenye mpango wa biashara kuna tathmini inayofanywa wakati unapoanza kuandaa mchanganuo wako ambapo unaangalia kwa haraka haraka hesabu na namba zako, ikiwa biashara yako kwa kipindi fulani labda tuseme wiki, mwezi au mwaka inatakiwa iuze mauzo kiasi gani kusudi iweze kurudisha ghara zote ulizotumia. Ukweli ni vigumu kutambua ikiwa biashara italeta faida au haitaleta lakini tathmini hii inasaidia kwa asilimia kubwa kutabiri uwezekano wa biashara kufanikiwa.

Ijapokuwa hiki ni kipengele kidogo kwenye sehemu ya makisio ya pesa, lakini hufanyika mwanzoni kabla ya kuandika sehemu yenyewe ya fedha ili kujiridhisha ikiwa biashara italipa au haitalipa. Hata hivyo katika michanganuo mingine watu wengine huweka tathmini hii kwenye sehemu ya fedha.


Katika ‘Break even’  unaweza kutathmini mauzo yatakayorudisha gharama au muda biashara itakaporudisha gharama zote zilizotumika. Kwa mfano tuseme umetumia jumla ya shilingi milioni moja kuanzisha biashara ya kuuza nguo, mauzo yako yatakapofika shilingi milioni moja hapo unakuwa umerejesha gharama zako zote. Ni tathmini inayotumia kanuni rahisi inayohusisha vitu vikuu vinne ambavyo ni hivi vifuatavyo;

1.  Mauzo  - A
2.  Gharama za mauzo zinazobadilika -  B
3.  Gharama za kudumu za uendeshaji - C
4.  Kiasi cha mauzo yatakayorudisha gharama  - D

Kanuni inayotumika kukokotoa Mauzo yatakayorudisha gharama ni hii hapa chini;

Ni sawa na kuchukua ;

Gharama za kudumu gawanya kwa (1- sehemu ya gharama zinazobadilika kwenye mauzo

Sehemu ya gharama zinazobadilika kwenye mauzo inakuwa katika mtindo wa sehemu au desimali, ni mauzo gawanya kwa gharama za mauzo.

Kujua muda biashara itakaporudisha gharama zote break even time kanuni yake unachukua 

Jumla ya gharama zote ulizotumia (B + C) kisha unagawanya kwa kiasi cha faida kwa mwaka, siku au mwezi kulingana na muda wako unaotafuta. Kama unataka kujua ni miaka mingapi utatumia faida ya mwaka 1, halikadhalika na ikiwa ni siku au mwezi.

Kwa mfano ikiwa mradi wa mandazi unagharimu shilingi 5,000/= kuanzisha, na kisha kwa siku unapata faida ya shilingi 1,000/= ina maana kwamba mradi huo utakuchukua siku 5 kurejesha gharama zako zote ulizotumia kuanzisha mradi wako wa mandazi; Inamaana kuwa unachukua, 5,000/1000.


Kanuni hizi hapa zimeonyeshwa kwa ufupi sana, ufafanuzi wake kwa kia unaweza kuuona katika kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI pamoja na masomo ya SEMINA YA MICHANGANUO yaliyo kwenye BLOGU YA MICHANGANUO

Baada ya kupata Kiasi cha mauzo yatakayorudisha gharama zote katika kipindi fulani, sasa hapo ndipo utakapojua ikiwa utaongeza mauzo yako kwa kiasi gani ndipo uweze kutengeneza faida nyingi zaidi.

Ikiwa utagundua kwamba mauzo yako unayokadiria yatakuwa chini ya kiasi cha mauzo ya kurudisha gharama, unaweza kuangalia uwezekano wa kuja kupunguza aidha gharama za kudumu, gharama zinazobadilika au kuangalia uwezekano wa kuongeza mauzo kusudi uweze kupita kiasi hicho na hatimaye uje upate faida.

Ila chukua tahadhari usije ukarekebisha namba tu kusudi zikupe majibu ya kukuridhisha binafsi, hapo utakuwa unajidanganya mwenyewe, hesabu zako zinatakiwa zioane na utafiti uliofanya, uhakikishe kweli zina uhalisia usikadire mauzo yasiyotekelezeka.

…………………………………………………………………….

Ndugu msomaji, Semina bado inaendelea hujachelewa kwani jinsi inavyoendeshwa siyo kama semina za kawaida, masomo yanahifadhiwa kwenye blogu maalumu ambapo mshiriki yeyote anapojiunga huyakuta masomo hayo yote na kila kitu walichojifunza washiriki wengine.


Ikiwa umeshalipia ada yako sh. 10,000/= bonyeza maneno yafuatayo ukiwa umesign in kwa email yako.BLOGU YA MASOMO YA SEMINA ITAFUNGUKA.


Soma hapa utannngulizi wa masomo 11 ya msingi ya semina.

0 Response to "NI LINI BIASHARA YAKO ITARUDISHA GHARAMA ZOTE ULIZOTUMIA?(BREAK EVEN POINT)"

Post a Comment