Kwanza hebu tufahamu maana ya neno lenyewe Saikolojia
ni kitu gani, Saikolojia ni elimu ya akili au nafsi. Kwahiyo saikolojia ya
fedha ni elimu ya jinsi tunavyoichukulia fedha ndani ya akili zetu.
Saikolojia ya pesa ni kitu muhimu sana
tunapozungumzia suala zima la mali na utajiri kwa sababu fedha maana yake ni NGUVU na vilevile ni muhimu sana nguvu
hii mtu ukajifunza kuitendea matendo yaliyokuwa chanya ikiwa utataka iongezeke
na kuwa nyingi.
Ili kutambua hasa ni jinsi gani mtu
unavyoweza ukatengeneza pesa nyingi ni lazima kwanza ufahamu ni kwanini watu
hawapati pesa, kuna sababu kadhaa ni kwanini watu hukosa pesa na kumi kati yake
ni hizi zifuatazo;
1.Fedha
ni lazima ipendwe.
Mara nyingi
watu huwa hawana mapenzi na fedha, je unafahamu maana ya kuipenda fedha
na saikolojia chanya ya fedha? Hebu jaribu kufikiria kidogo kisha utoe jibu,
wengine watajibu kwamba, “mimi
ninachokipenda ni kutumia pesa” na
bila shaka hayo ndiyo mawazo ya waliokuwa wengi. Kwamba mapenzi yao kwenye pesa
yameegemea zaidi katika MATUMIZI. Watu hawapendi pesa bali wanachokipenda wao
ni kile kitu pesa inachoweza kununua na hili ni kosa kubwa sana!
Hebu jiulize tena swali jingine hili,
“Kwanini wikiendi unawatoa out watoto wako na kuwanunulia midoli na magari ya
kuchezea? Jibu rahisi unaweza ukajibu ni kwa sababu unawapenda. Kuwapeleka
matembezini na kuwanunulia watoto wako zawadi hakumaanishi kuwa unawapenda sana
bali upendo wa kweli kwao unadhihirishwa na jinsi UNAVYOWAJALI. Hivi ndio
kusema kwamba yoote yale unayowafanyia wanao lengo lake kubwa ni kuwajali na
kuwatunza na hali ni hivyohivyo ilivyo kwa pesa, pesa inahitaji matunzo na
kupendwa.
Nitatoa mfano wa watu wawili wanaokwenda
sokoni kununua pochi(wallet) ya
kutunzia fedha. Wazo la mtu wa kwanza ni kwamba yeye anahitaji tu pochi mpya
kama urembo ingawa pia ataitumia kuwekea fedha zake. Mtu wa pili yeye lengo
lake mahsusi anahitaji pochi kwa ajili
ya kuzifanya fedha zake zikae salama kwa raha mustarehe. Sasa hebu tuseme kama
wewe ndio ungelikuwa PESA, niambie
ungelichagua kuingia katika pochi ipi kati ya ya hizo pochi mbili?
Bila shaka yeyote ile wengi mngelichagua
pochi ya mtu wa pili kwa kuwa hakuna asiyependa kupendwa, usalama, starehe,
amani na kujaliwa!!! Na hii ndio saikolojia yenyewe ya pesa, ukitaka pesa iwe
rafiki kwako na kuongezeka ni lazima uipende na kuijali.
2.Kauli
hasi(-) kuhusiana na pesa.
Kuwa makini sana kuhusiana na maneno
uayotamka kama vile, Sina pesa, Vyuma
vimekaza, hali yangu kifedha ni tete sana nk. Maneno kama haya yanaweza
yakasababisha kweli ukakosa kabisa pesa. Badala ya maneno hasi kama hayo
unaweza ukatamka hivi, Pesa ipo njiani
kuja kwangu, ipo siku tu, one day yes!, pesa tayari inagonga mlangoni pangu,
pesa naziona zinanichungulia dirishani nk.
SOMA: Wanaosema nikishinda bahati na sibu milioni 100 nitafanya hiki na kile wakishinda hufanya kinyume.
Kuwa kama Dokta Shika yule jamaa aliyekwenda kununua maghorofa akiwa senti
tano mfukoni hana, unajua saikolojia aliyotumia yule jamaa ilivyomsaidia? Hata
madai ya fedha zake urusi pengine hayakuwa na mashiko kivile lakini saikolojia
ile ya kuamini pesa ilikuwa ikimchungulia dirishani, iliweza kumfanya apate
shavu la nguvu kutoka kwa makampuni kibao nchini yakiwemo ya bahati na sibu
hatimaye akapata mpunga(pesa) iliyomsaidia kuvuka mahali pagumu alipokuwa.
Katika Saikolojia ya pesa, pesa pia unaweza
ukaifananisha na mtoto mchanga, mtoto mdogo anapoanza kujifunza vitu mbalimbali
kama vile kutambaa au kutembea wazazi wake na walezi humsifia na kumpa moyo kwa
kusema, “Umekua mwanangu ee” “Kazana nitakununulia pipi” nk. hapo mtoto kweli
hukazana mpaka ameweza kabisa kile anachojifunza tena kwa muda mfupi ajabu!
SOMA: Kinamama huwabeba watoto wao kipindi kifupi lakini mioyo yao huwabeba milele.
SOMA: Kinamama huwabeba watoto wao kipindi kifupi lakini mioyo yao huwabeba milele.
Pia ASILI hututendea sisi binadamu kwa namna
kama hiyohiyo ya mtoto mdogo anavyotendewa na wazazi wake, pindi tu tunapoanza
kuchukua hatua chanya za awali katika jambo lolote lile maishani ikiwemo
kutafuta pesa, asili hutupa mara moja matokeo ya upendeleo kusudi tuweze kuwa
na uhakika na nguvu ya kuendelea mbele tukifahamu kwamba tupo katika uelekeo
sahihi na tunahitaji kufika mbali zaidi ya pale tulipokuwa. Jitahidi kubadilisha
kabisa mtazamo wako wa fedha kuwa chanya kwa maneno kama haya;
· Napenda
pesa na nazipata kwa urahisi
· Natengeneza
pesa na kuzitumia kwa urahisi
· Mara
zote naweza kuingiza pesa kiasi ninachotaka nk.
3.Wekeza
ndani yako mwenyewe
Usiache kununua kile ulichopanga kununua kwa
ajili yako mwenyewe, vinginevyo ASILI itaichukua fedha hiyo kwa namna nyingine
tofauti kabisa. Kwa mfano anaweza kuja rafiki au ndugu akajifanya kukukopa na
asijekukulipa tena kamwe au anaweza kutokea kibaka/mwizi kusikojulikana na
kuikwapua fedha hiyo hivihivi ikapotea nk.
4.Kuwa
Mkarimu na mtoaji kwa watu wengine.
Ukarimu hapa haumaanishi utapanye ovyo pesa
zako kuwaridhisha watu hapana, inamaanisha usiwe bahili kupita kiasi, kwa mfano
pale unapotakiwa kufanya malipo au kumlipa mtu chake fanya hivyo bila
manunguniko wala kisirani rohoni, unaponunua vitu vipya nk. unahitaji kuwa na
saikolojia nzuri ya fedha.
5.Woga
wa kufikwa na majanga au kufilisika.
Fedha ni aina ya NGUVU na inatakiwa kutunzwa(unapoiweka
kama akiba) ukitumia maneno chanya+ mfano;
· Akiba
hii ni kwa ajili ya safari na wala siyo “kwa ajili ya kipindi cha uzeeni”
· Kwa
ajili ya dharura na wala siyo kwa ajili ya majanga
· Kwa
ajili ya kuboresha afya na wala siyo kwa ajili ya kutibu magonjwa
6.Kuwa
makini unapomkopesha mtu
Kisaikolojia unapokopesha pesa zako inamaanisha kwamba
pesa hiyo huna kazi nayo, vinginevyo basi unatakiwa ukopeshe kwa DHAMANA. Dhamana haimaanishi kwamba
unayemkopesha hafai au hatalipa hapana, bali ni kwa sababu hamna mtu anayeweza
kuwa na uhakika na mambo yajayo, mtu anaweza baada ya kukopa akajakupata
majanga kama ya kufungwa jela, kuuguliwa nk. na pesa yako ikapotea hivihivi,
lakini kama aliweka dhamana fulani itakusaidia kurudisha fedha zako.
SOMA: Je kukopa ili ukalipe deni la zamani kunawezaje kuboresha mzunguko wa fedha kwenye biashara yako?
Ndio maana Waswahili wakasema, “Ukitakakumpoteza rafiki basi wewe mkopeshe tu pesa “ Ikiwa mtu
atakataa kukulipa deni unalomdai basi ujue amekufundisha somo kubwa ili usije
tena hapo baadae kurudia kumkopesha mtu mwingine kizembe. Saikolojia ya pesa
huwa haina tabia ya kusamehe wala kumuonea mtu huruma.
7. Hesabu
fedha zako.
Neno “Umasikini”
(Poverty) asili yake ni neno, “Usihesabu”.
Njia pekee ya kudhibiti fedha zako ni kuzihesabu. Acha mara moja kuwaachia
wasaidizi wako biashara kizembezembe bila ya mahesabu ya uhakika, wakishakuliza
saikolojia ya pesa haina cha kukusaidia zaidi ya kukuadhibu vikali na
kukucheka...............
.................Somo hili halijaishia hapa litaendelea leo hii saa 3 usiku katika Group la masomo ya kila siku la MICHANGANUO-ONLINE. Masomo haya yamerudi tena kwa kasi mpya baada ya mapumziko ya mwezi mzima wa Januari na mwaka huu yameboreshwa zaidi, badala ya kuwa na masomo ya mzunguko wa pesa na michanganuo ya biashara hatua kwa hatua tu peke yake tumeongeza pia kipengele cha SAIKOLOJIA YA PESA.
Kujiunga na kupata masomo hayo kila siku pamoja na masomo yote ya mwaka uliopita lipia kiingilio sh. elfu 10 tu. Utapata pia fursa ya kushiriki semina zetu za mara kwa mara za kuandika michanganuo kama ile tunayokwenda kuifanya tarehe 12 mpaka 15 mwezi huu wa Februari, 2019 na itakayohusu, Jinsi ya kuandaa Hesabu za mpango wa biashara(kipengele cha fedha)
Namba za malipo ni 0765553030 au 0712202244 jina ni Peter Augustino Tarimo. Ukishalipia tuma ujumbe usemao. "NIUNGANISHE NA GROUP LA SEMINA"
WASAP: 0765553030
Vitabu vyetu kwa lugha ya kiswahili pia vinapatikana vyote katika mifumo ya softcopy na hardcopy kwa maelezo zaidi tembelea; SMART BOOKS TANZANIA
0 Response to "Saikolojia ya pesa na kanuni 10 za kufuata ili uwe mtu uliyefanikiwa kimaisha."
Post a Comment