MBINU NA MIKAKATI YA KUIKWAMUA BIASHARA YAKO KATIKA HALI NGUMU KIPESA ILI KUFANIKIWA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MBINU NA MIKAKATI YA KUIKWAMUA BIASHARA YAKO KATIKA HALI NGUMU KIPESA ILI KUFANIKIWA

Mtoto aliyebeba pesa nyingi kununua mkate baada ya hali ya kiuchumi kuwa mbaya

Habari za saa hizi mdau, karibu kwenye somo hili linalohusu mikakati mbalimbali na mbinu Mjasiriamali anazoweza akazitumia katika kuikwamua biashara yake kipindi kukiwa na hali ngumu kifedha. Na wala haijalishi unajua jinsi ya kujiwekea akiba, unapozuka mdororo wa kiuchumi ni lazima uchukue hatua hizi ndogondogo tu vinginevyo kutajiri utakusikia kwa wenzako.

Mfano mzuri wa kipindi cha hali ngumu kifedha ilikuwa ni hivi majuzi kwenye lile janga la UVIKO 19, mambo yalikuwa hayaendi kama ilivyotarajiwa na wengi hivyo kila mtu akawa ana haha kutafuta mbinu mbalimbali za kuhakikisha anafanikiwa kujitoa kwenye mkwamo ule kiuchumi  

Siri ya kufanikiwa katika kipindi kigumu kiuchumi ni vitu vidogovidogo watu wengi hupuuzia na muda hali inapokuwa ngumu siyo lazima iwe ni nchi nzima inaupitia hapana, bali wafanyabiashara mmojammoja nao kwa nyakati tofauti hukumbwa na vipindi vigumu, biashara zinatoka polepole na mzunguko wa pesa unakuwa mdogo. 

Kuna nchi ambazo hali imewahi kuwa mbaya pesa ikaporomoka thamani hadi watoto wakatumwa madukani kununua mkate mmoja tu na lundo la hela kama uonavyo pichani hapo juu

Hali inapokuwa hivyo mjasiriamali hana budi kutafuta mbinu na mikakati itakayomuwezesha kujinasua na wimbi hilo hatimaye mtiririko wake wa fedha kurudi kuwa tena chanya. Mbinu na mikakati hiyo 5 ni hii hapa chini;

1.Wekeza zaidi Kwenye Utafutaji wa Masoko

Wakati kipindi kama hicho washindani wako wanahangaika kubana matumizi kila idara ikiwemo ile idara nyeti ya masoko, wewe tafuta zaidi njia ya kuwekeza kwenye kutafuta masoko ili usonge mbele na kukamata sehemu kubwa zaidi ya soko na hivyo fedha zaidi kuingia. Kwani kuwekeza ni nini? Maana yake siyo lazima uwekeze pesa tu la hasha, uwekezaji unaweza kuwa katika muda ama rasilimali nyingine pia.

2. Wabaini Wafanyakazi Wasiokuwa na Tija Kwenye Biashara yako.

Kwa kawaida katika kipindi kigumu ni rahisi sana kumbaini mfanyakazi yule asiyekuingizia faida kutokana na sababu kwamba hata gharama unazoingia kumlipa yeye unaona kabisa mwisho wa siku haziwezi zikarudi. Ikiwa mfanyakazi wako hakuingizii faida na badala yake wewe ndiyo unaingia gharama kubwa zaidi juu yake, mpe kwanza onyo na nafasi ya mwisho ya kujirekebisha na endapo hatajirekebisha usiendelee kumlea mwache aende zake.

3.Anzisha Biashara Nyingine Inayoongeza thamani zaidi Katika hali ya Soko Iliyopo.

Itakuwa vizuri zaidi ikiwa huduma au bidhaa hiyo mpya itawalenga wateja walewale uliokuwa ukiwauzia zamani. Ili uweze kulimiliki soko vizuri zaidi wakati wa hali ngumu kipesa unaweza ukaamua kuachana na ile biashara inayosuasua ukabakia tu na ile inayotoka vizuri. Hii ni njia nyepesi ya kutajirika kwa haraka kuliko kuendelea kubana fedha ukihofia zitapotea.

4. Shikamana zaidi na Wateja wako kwa Kuwapa Matokeo Bora zaidi na Faida ya Kweli.

Chunguza ni faida zipi wateja wanazozipata kutokana na bidhaa au huduma zako kisha uangalie ni kwa jinsi gani unavyoweza ukaongeza faida hizo. Ni lazima utafakari kwa kina juu ya biashara yako kwani wakati mwingine mdororo wa kiuchumi ni matokeo ya wafanyabiashara na makampuni kujisahau wakaachana na misingi ya biashara na kukumbatia zaidi upande wao, faida, thamani na upanuzi wa biashara zao badala ya kujali faida anayoipata mteja. Jifunze njia ya kuwekeza zaidi kwa mteja kwani ndiyo msingi wa mafanikio makubwa kibiashara..................................................

.........................................

5. Mbinu moja ya 5 na muhimu sana haijatajwa hapa, unaweza kuipata kwenye somo kamili  unapojiunga na kundi letu la Michanganuo-online, mahali ambapo panapatikana masomo ya kipekee kabisa zaidi ya 100 yasiyopatikana kwingine kokote.  

Ili kujiunga na group hili ada ya mwaka ni sh. elfu 10 ambapo unatumiwa muda huohuo offa ya vitabu na michanganuo jumla vitu 14 (cheki orodha pale chini). Ndani ya group mbali na masomo ya kila siku tunakuwa pia na semina za kuandika michanganuo ya biashara bunifu zenye fursa kubwa ya kutengeneza faida haraka.

Baada ya malipo tuma ujumbe usemao; “NATAKA OFFA MPYA YA VITU 14 NA KUUNGWA MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO”

Namba zetu za malipo ni 0712202244 au 0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo

 

ORODHA YA VITU 14 VYA OFFA HII HAPA CHINI;

                           1.       KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu za BIASHARA, jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika kila kitu.kwa Kiswahili

                           2.       KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 tu - kwa kiswahili

                           3.      KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili

                           4.       KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ni maarufu sana duniani, hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza

                           5.      KITABU: Siri za upishi wa chapati laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili

                           6.       COMPILLATION: Masomo 30 ya fedha usiyoweza kuyapata popote, mengine 70 utayapata kwenye group kila siku - kwa Kiswahili

                           7.      MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili

                           8.      MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza

                           9.      MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili

                        10.    MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji- kwa kiswahili

                        11.    MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini Broilerskwa kiingereza

                        12.    MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini Broilerskwa kiswahili

                        13.    MCHANGANUO: Kiwanda cha mvinyo na juisi ya Rosella –Choya Investment – kwa kiswahili

                        14.    MCHANGANUO: Kilimo cha Tikiti maji:- Kibada Watermelon Fruits – kwa kiswahili

 

 

SOMA NA HIZI HAPA:

1.Biashara ndogo ya mtaji wa 80,000/= niuze nini kupata faida ya haraka?

2. Jinsi ya kuweka akiba kila mwezi ukitumia vyanzo vya pesa usiyotarajia kabisa kuipata

3. Siri ya kufanikiwa biashara ya kuuza vinywaji baridi vyenye faida

4. Biasharaya kuuza dagaa mchele na samaki wa maji chumvi kiubunifu: mchanganuo

 

0 Response to "MBINU NA MIKAKATI YA KUIKWAMUA BIASHARA YAKO KATIKA HALI NGUMU KIPESA ILI KUFANIKIWA"

Post a Comment