Katika siri kubwa za kufanikiwa kiuchumi/kifedha au
kibiashara kwa ujumla, suala la kuweka akiba ndiyo kitu kinachochukua nafasi ya
juu kabisa tofauti na jinsi watu wengi wanavyodhania. Watu wengi tunakimbilia
kufikiri labda kitu cha msingi zaidi ni kupata kiasi kikubwa sana cha fedha
mkononi ndipo tuweze kutimiza malengo yetu ya kiuchumi na ya kifedha.
Somo letu hili ijapokuwa limeangazia suala zima la
uwekaji wa akiba lakini kipekee hasa pale mwishoni mwa somo nimeonyesha njia au
jinsi ya kuweka akiba kila mwezi kwa kutumia vyanzo usivyovitarajia kabisa kama
unaweza kuvitumia kama chanzo cha fedha za kuweka akiba. Njia hizo zinatatua
kile kitendawili cha kwanini ni vigumu sana kwa mtu kuokoa pesa kwa ajili ya
kuweka akiba?
Kuweka akiba ni tabia mtu yeyote anayoweza kujifunza na
kujizowesha maishani. Binadamu tunatakiwa katika kila kipato tunachopata
tujiwekee asilimia fulani ya kipato hicho kama akiba. Wataalamu wengi wamewahi
kupendekeza kiasi cha asilimia mtu anayopaswa kuweka kama akiba. Ingawa unaweza
ukatenga kiasi chochote kile kama akiba lakini wataalamu wengi hupendekeza kuwa
asilimi 10% au zaidi ya hapo.
Hata wanyama na wadudu wakishakula chakula
walichopata kuna wakati hukumbuka kuweka akiba mahali kwa ajili ya matumizi yao
ya baadae mfano Chui, mbwa, paka na hata nyuki. Tazama mfano mzuri myama Chui
amkamatapo swala akishakula na wanawe utamuona akikazana kupandisha mabaki ya
mzoga huo kwenye mapango ya mti kusudi akauhifadhi kama akiba kwa ajili ya
kitoweo cha siku zinazofuata.
Kwani
Kuna Umuhimu Gani WA kuweka Akiba?
Umuhimu mkubwa wa kujiwekea akiba kwanza kabisa upo
kwenye uwekezaji, hautaweza kabisa kuwekeza katika kitegauchumi chochote pale
fursa zitakapojitokeza ikiwa kama hauna akiba yeyote ile ya fedha kutokana na
vyanzo vyako vya msingi vya mapato. Na ukisema utakwenda kukopa mahali fulani
labda benki ili uwekeze, jambo hili litakuwa gumu sana kwako kwani wakopeshaji
wengi huwa hawamkopeshi mtu asiyekuwa na mradi aliouanzisha tayari kwa pesa
zake mwenyewe ukaonekana.
Na hata ikiwa utabahatika kuanzisha biashara kwa fedha za
mkopo, biashara hiyo itakuweka roho juu kiasi cha wewe kuweza hata kupatwa
magonjwa ya presha na moyo kwani hatari kidogo tu ya kupotea kwa mtaji huo
haiwezi kukupa kabisa amani akilini mwako, na hivyo kusababisha muda wote wewe
uwe ni mtu wa kuishi kwa wasiwasi na stress tu. Ukishakuwa na wasiwasi hutaweza
tena kuwa na ubunifu katika biashara au mradi wako
Umuimu mwingine wa mtu kujijengea tabia ya kuweka akiba
ni kujenga nidhamu hata katika nyanja nyinginezo za kimaisha. Nidhamu ya pesa
ni kama vile mazoezi ya kuikomaza akili yako izowee mazingira magumu na
utakaposhinda mtihani mgumu wa pesa basi na ujue umeshinda mitihani mingine
mingi ya kimaisha kwani kujinyima na kuweka akiba unajitesa kimwili sawa tu na
mtu anayekwenda gym kujifua kimazoezi.
Kumbuka siri nyingine kubwa sana ukitaka kupata pesa au
mafanikio yeyote yale maishani ni nidhamu ya kuhakikisha unatenda jambo
lilelile kila siku kwa muendelezo bila kuacha hata siku moja, ikiwa huna
nidhamu kwenye ulaji wako, utanenepa ovyo, halikadhalika ukikosa nidhamu kwenye
ratiba za masomo yako shuleni kamwe hutaweza kufaulu mtihani wako wa mwisho iwe
ni ule wa darasa la saba, kidato cha nne, kidato cha sita au hata wa chuo
kikuu.
Kutamka tu unataka kuweka akiba ni rahisi
sana kuliko utekelezaji wenyewe, changamoto kubwa hutokana na “ni wapi unakoweza ukapata fedha za ziada za
kutumbukiza katika akiba yako mbali na matumizi yako ya kila siku.” Wakati mwingine unaweza kuwaza utawekaje
akiba wakati kuna mahitaji mengine tena ya muhimu tu unashindwa kuyatimiza na
kulazimika kuyaacha.
Kisingizio kikubwa mara nyingi kimekuwa ni
watu kushindwa kuweka akiba kwa sababu tu hawana vipato kabisa au vipato vyao
ni vidogo mno kiasi kwamba hawawezi kutoa hapo asilimia fulani kwa ajili ya
kuweka akiba. Lakini jambo hili halipaswi kabisa kuwa ni sababu ya wewe
kushindwa kujiwekea akiba kwani mpaka dakika hii unapoishi bila shaka kuna aina
fulani hivi ya kipato unachopata kinachokuwezesha kuishi vinginevyo ungelikuwa
umekwisha kufa kwa njaa siku nyingi.
Tukiachana na ajira na biashara ambavyo ndivyo
vyanzo vikubwa zaidi vya kipato cha mwanadamu kuna aina vyingine za vyanzo vya
kipato kama vile, ruzuku, msaada, zawadi nk. Chochote kile unachokipata
kilichokuwa na thamani kiuchumi ni aina fulani hivi ya kipato hata kama ni
kidogo kiasi gani, hivyo unao wajibu wa kuhakikisha unaweka hapo akiba asilimia
fulani na wala siyo kujiwekea visingizio lukuki.
Hata kwa mfano, tuchukulie maisha yako wewe
ni ombaomba barabarani, kipato chako ni zile fedha unazoomba watu wanakupa, hivyo
unao wajibu wa kumega hapo sehemu fulani ya hizo pesa za msaada na kuiweka kama
akiba kabla hata hujafanya matumizi yako mengine yeyote. Fedha hizi zitakuja
siyo tu kukuwezesha kuanzisha vitegauchumi vya kukuondoa kwenye kazi ya
kuombaomba bali hata msaada mkubwa pale linapoweza kutokea janga la ghafla kama
vile ugonjwa nk.
Hatua Muhimu 5 za Uwekaji Akiba
1. Elimu
Jielimishe
kuhusiana na pesa na uwekezaji kupitia vyanzo mbalimbali mfano, vitabu,
mitandao ya kijamii kama hii, applications mbalimbali za kwenye simu za
mkononi, madarasa ya ujasiriamali na vyombo vinginevyo vya upashanaji habari
2. Kujiwekea bajeti
Bajeti
maana yake ni kupanga kabisa jinsi utakavyofanya matumizi ya fedha
utakazoingiza kabla hata haujazitia mkononi. Hii itakusaidia kuhakikisha
matumizi yako hayaendi kinyume na ulivyopanga. Unaweza kupanga bajeti yako kwa
kutumia karatasi na kalamu ama kwa kutumia apps mbalimbali za simujanja
zinazopatikana Playstore na Appstore
Bajeti
pia tunaikuta kwenye Mpango wa biashara na hivi ni vitu viwili
vinavyoshabihiana sana. Wataalamu husema mpango wako utakuwa na uzito zaidi
pale unapouandika katika karatasi. Vivyohivyo na bajeti ndivyo ilivyo.
Kumbuka
masuala haya ya Bajeti na Michanganuo ya biashara kwa ujumla wake huwa
tunajifunza kwa undani kabisa katika Group letu la MICHANGANUO-ONLINE
MASTERMIND. Bajeti kipato chako cha siku, wiki na hata mwezi kisha uhakikishe
unaiheshimu kwa kuifuata kikamilifu.
3. Kujilipa kwanza wewe
mwenyewe
Katika
kipato chochote kile utakachoingiza anza kwanza kumega utakachoweka kama akiba
kabla haujafanya matumizi mengine yeyote yale hata yale muhimu na ya msingi
kama chakula, kulipa deni, bili mbalimbali nk.
4. Badilisha tabia ya matumizi
yako ya fedha
Jifunze
kuwa bahili wa pesa zako kwa kutokununua kitu chochote kile ambacho hukukiweka
katika bajeti yako ya siku hiyo. Kubadilisha tabia kunaanzia na kubadilisha
mtazamo wa akili yako, ishi kama vile huna hela hata pale unapokuwa umepata
hela nyingi. Ukitaka kupata pesa nyingi acha kujionyesha una pesa, jishushe
chini ya kiwango chako cha pesa unazoingiza.
5. Wekeza kwenye miradi
inayolipa
Tumia
sehemu ya akiba yako kuwekeza kwenye vitegauchumi/miradi salama inayoweza
kukuingizia kipato zaidi hapo baadae. Ukishawekeza weka malengo ya muda mrefu.
Jinsi
ya kuweka akiba kila mwezi ukitumia vyanzo vya pesa usivyotarajia kabisa
Pamoja na kuona kwamba akiba unapaswa kutenga
kiasi fulani cha mapato yako lakini kuna vyanzo vya mapato vilivojificha
ambavyo ni tofauti na kipato chako ulichokizoea. Haya ni maeneo ambayo mtu
unaweza usiyatilie maanani kabisa kwamba yanaweza kukusaidia kutimiza azma yako
ya kuweka akiba pasipo kuathiri sana bajeti yako ya kawaida ya kila siku.
Maeneo hayo nitazungumzia kwa pande zote mbili, kwa Wafanyabiashara na kwa Wafanyakazi;
1)
Wafanyakazi:
.................................................................................................
ü Ndugu msomaji wangu somo hili bado
halijamalizika na somo kamili unaweza ukalipata tu kwa kujiunga na kundi letu
la masomo na semina Watsap (MICHANGANUO-ONLINE-MASTERMIND
GROUP)
ü Mwanachama anapata zawadi (OFFA) ya Vitabu na Michanganuo jumla ni
vitu 12, mara tu amalizapo kulipia ada ya mwaka mzima ambayo ni sh. 10,000/= TU
ü Kwenye group tuna masomo ya fedha adimu
na ya kipekee kabisa zaidi ya 100 na kila siku tunakuwa na somo jipya. Huwezi
kuyapata mahali pengine popote.
ü Masomo haya yanatoa mwanga mkubwa katika
ufahamu wa suala zima la pesa, jinsi inavyozunguka kwenye biashara na hata
saikolojia za watu na imani zao juu ya fedha na jinsi zinavyoathiri hali yao ya
kiuchumi.
ü Pia zipo semina za mara kwa mara za
michanganuo/Business Plans bunifu kwa biashara zinazolipa Tanzania
ü Kujiunga lipia ada kupitia namba zetu, 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo
kisha Ujumbe usemao, “NATAKA OFFA YA
VITU 12, NIUNGE PIA NA GROUP” Ikiwa hupendi kuugwa katika magroup basi acha
nebo “NIUNGE NA GROUP” kwani wapo wanaohitaji vitabu na
masomo peke yake.
VITU 12 VYA OFFA NI HIVI
VIFUATAVYO;-
1.
COURSE/SEMINA: (compiled
complete course) ya Jinsi ya
kuandika Mchanganuo wa biashara –(Ukishindwa
kuandika mchanganuo wako mwenyewe utarudishiwa pesa zako) - kwa kiswahili
2.
KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu
za BIASHARA, jinsi ya kuandaa
michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika
kila kitu. – kwa kiswahili
3.
KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri
Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili
4.
KITABU: Siri za upishi wa chapati
laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili
5.
KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 - kwa kiswahili
6.
KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN ni maarufu sana duniani na ndio
hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza
7.
MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini
Broilers - kwa
kiswahili
8.
MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza
9.
MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za
saruji- kwa
kiswahili
10. MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili
11. MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza
12. MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili
13. Kuunganishwa Group la
masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mwaka mzima ukitaka. (Mentorship group) (Ni hiyari yako lakini, usipotaka
hatukuunganishi)
Offa
hii ni ya muda mfupi!
Imeandaliwa na Peter Tarimo
Simu/Whatsap: 0765553030 au 0712202244
0 Response to "JINSI YA KUWEKA AKIBA KILA MWEZI UKITUMIA VYANZO VYA PESA USIYOTARAJIA KABISA KUIPATA"
Post a Comment