JINSI YA KUTAMBUA THAMANI YAKO HALISI, PESA, MALI, UTAJIRI NA KILA KITU UNACHOMILIKI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JINSI YA KUTAMBUA THAMANI YAKO HALISI, PESA, MALI, UTAJIRI NA KILA KITU UNACHOMILIKI

Thamani halisi ya mtu kifedha

Thamani yako halisi kifedha, ‘Net worth’ maana yake ni kiasi cha mali zote unazomiliki baada ya kutoa madeni yote unayodaiwa. Katika Ulimwengu wa biashara unafahamu ya kwamba Biashara na Mmiliki wake ni vitu viwili tofauti kabisa, kila mmoja anajitegemea kifedha.

Hivyo tunapozungumzia hii dhana ya Thamani yako halisi kifedha na jinsi ya kutambua utajiri unaoumiliki,  tunaweza tukaizungumza tukimaanisha thamani halisi ya pesa ya vitu anavyomiliki mtu binafsi au thamani halisi biashara inayomiliki. Kwa upande wa mtu binafsi, bila kujali kama mtu huyo ni tajiri au mtu wa kawaida thamani halisi kila mtu anayo, awe anafanya kazi ya ajira, na hata ikiwa hana kazi wala biashara yeyote ni lazima tu kuna mali atakazokuwa anazimiliki, jamani akose hata nguo zake alizovaa mwilini?

SOMA: Sababu kuu 5 kwanini uandike kwanza mpango wa biashara yako kabla hujaianzisha.

Dhana kama hizi hutumika sana wakati wa kuandika mpango / mchanganuo wa biashara na kuelekea mwisho wa mwaka huu wa 2023, tutakwenda kunaandika  hatua kwa hatua michanganuo bunifu mbalimbali ya biashara zenye fursa kubwa yakutengeneza faida haraka Tanzania.

Kwahiyo ndugu msomaji wangu usione kama nakusumbua utakapoona nikichomekea mara moja moja dhana hizi za mahesabu ya ‘kihasibu’ katika makala zangu, najua kuna watu hawapendi kabisa kusikia kitu kinachoitwa hesabu lakini napenda kukuhakikishia kabisa kwamba, kwenye mpango wa biashara hesabu zake ni rahisi mno na sehemu nyingi utakuta ni kujumlisha, kutoa, kuzidisha, kugawanya na mara chache sana asilimia %.

SOMA: Sababu 4 kwanini hesabu (Kipengele cha fedha) ni moyo wa mpango wa biashara? The heart of a business plan)

Tukirudi kwenye mada yetu ya leo ni kwamba, Thamani yako halisi utaijuaje? Watu wengi hudhani kwamba ni kiasi tu cha kujumlisha mali zako zote ulizokuwa nazo, basi tayari unakuwa umejua wewe unamiliki mali kiasi gani, lakini vipi kuhusiana na madeni unayodaiwa?, vipi kuhusu mali unazomiliki kama hisa katika makampuni mengine uliyowekeza au hata biashara wakati tumeshasema biashara na mtu binafsi ni vitu viwili tofauti kabisa?

Kwa upande wa biashara huwa tunasema kwamba,

THAMANI HALISI YA BIASHARA = MALI ZOTE – MADENI YOTE

Na kwa upande wa mtu binafsi pia ni hivyohivyo isipokuwa zipo triki chache ambazo usipozitegua unaweza kuishia kupata thamani yako halisi isiyokuwa sahihi kabisa, ukadhani labda unamiliki mali za mabilioni ya shilingi kama ilivyo kwa utjiri wa Mo Dewj na Bkhresa kumbe hata maelfu ya shilingi bado hujafikisha. Hivyo ni vyema mtu ukazingatia na kujifunza elimu ya fedha na uwekezaji kama hii ili basi zitakapojitokeza fursa za utajiri uweze kuzitambua kwa urahisi.

SOMA: Njia 7 halali na nzuri za kupata mafanikio na utajiri wa haraka.

Kwenye Group la MICHANGANUO ONLINE tunadili na masuala ya pesa kwa mtu binafsi (personal financial issues) ingawa pia katika upande wa Michanganuo tunabase  zaidi na biashara, hivyo kwa ujumla tunagusa sekta ya fedha katika pande zote mbili, Mtu binafsi na Biashara kwani tunaamini ijapokuwa mtu na biashara ni vitu viwili tofauti lakini vitu hivi vina mahusiano makubwa.

Mtu binafsi anayo mahesabu yake ya fedha kama ilivyokuwa biashara na wakati mwingine mahesabu hayo huwa yanafanana au kukaribia kufanana sana mtindo wake wa ukokotoaji.

Katika mfululizo wa masomo haya ya pesa katika Group la Michanganuo-online siku zilizopita tulishawahi kujifunza somo moja muhimu sana kwa mtu binafsi lililohusiana na JINSI YA KUBAINI KITU KINACHOTAFUNA ZAIDI FEDHA ZAKO KWA SIKU NA NJIA MUAFAKA YA KUKITHIBITI. Tulitoa mifano na namna rahisi kabisa ya kukokotoa hesabu yake.

Ukijiunga na Group masomo nyeti kama hayo unayapata yote kama yalivyofundishwa, tumeyahifadhi spesho kwa ajili yako wewe ambaye bado hujajiunga mpaka pale kampeni yetu ya mwaka huu itakapomalizika. Baada ya hapo hayatapatikana tena kwa urahisi, au kuyapata itakuwa ni kwa gharama tofauti na hii ya shilingi elfu 10 kama ilivyo sasa.

SOMA: Utajuaje kama biashara yako ya ufugaji wa kuku itakupa faida?

Leo katika Group la Whatsap la MICHANGANUO-ONLINE  tutakwenda kuona mifano na njia rahisi sana ya moja kwa moja ya kutambua thamani yako kamili ni shilingi ngapi kwa upande wa mali zote unazomiliki bila kujali kama wewe ni tajiri, ni masikini au ni mtu tu wa kawaida.

Kumbuka tunakwenda kuanza msimu wa MICHANGANUO YA BIASHARA BUNIFU ZINAZOLIPA faida kubwa hatua kwa hatua. Ikiwa ulikuwa bado hujajiunga na Group hilo, huu ndio muda sahihi wewe kufanya hivyo.

Kiingilio ni shilingi elfu 10 tu (Tsh.10,000) Utapata OFFA yetu kubwa ya vitu 12, na utashiriki semina za uandishi wa Michanganuo,  masomo ya fesha zaidi ya 100 pamoja na mijadala juu ya biashara na ujasiriamali kwa ujumla kwa mwaka mzima

Kulipia tumia namba zetu; 0712202244  au  0765553030 ambapo jina hutokea Peter Augustino Tarimo. Kisha tuma namba unayotumia Whatsap au anuani yako ya email vikifuatiwa na maneno haya, “NIPE OFFA YA VITU 12 na KUNIUNGANISHA MASTERMIND GROUP.”

Masomo ya feha utayapata yote kila siku ndani ya group baada ya kujiunga, haijalishi ikiwa ulichelewa ama la, tunao utaratibu wa kuhakikisha kila mtu aliyejiunga anapata masomo yote kama wengine waliojiunga mapema, isipokuwa tu kuna muda maalumu ukifika ni basi fursa ya kupata kila somo lililopita inakuwa imekwisha. Hkikisha ukijiunga unapata masomo yote 100+


.......................................................................................


VITU 12 VYA OFFA NI HIVI VIFUATAVYO;-

                 1.      COURSE/SEMINA: (compiled complete course) ya Jinsi ya kuandika Mchanganuo wa biashara –(Ukishindwa kuandika mchanganuo wako mwenyewe utarudishiwa pesa zako) - kwa kiswahili

                 2.       KITABUMichanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu za BIASHARA, jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika kila kitu. – kwa kiswahili

                 3.      KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili

                 4.      KITABU: Siri za upishi wa chapati laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili

                 5.       KITABUNjia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 - kwa kiswahili

                 6.       KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ni maarufu sana duniani na ndio hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza

                 7.       MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini Broilers - kwa kiswahili

                 8.      MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza

                 9.      MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji- kwa kiswahili

              10.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili

              11.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza

              12.    MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado millingkwa Kiswahili

              13.    Kuunganishwa Group la masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mwaka mzima ukitaka. (Mentorship group) (Ni hiyari yako lakini, usipotaka hatukuunganishi)

 

Offa hii ni ya muda mfupi!

 

Imeandaliwa na Peter Tarimo

Simu/Whatsap: 0765553030 au 0712202244

0 Response to "JINSI YA KUTAMBUA THAMANI YAKO HALISI, PESA, MALI, UTAJIRI NA KILA KITU UNACHOMILIKI"

Post a Comment