MTAJI WA BIASHARA YA VINYWAJI VIKALI & LAINI JUMLA NI KIASI GANI MFANO SODA, MAJI, BIA NA POMBE KALI? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MTAJI WA BIASHARA YA VINYWAJI VIKALI & LAINI JUMLA NI KIASI GANI MFANO SODA, MAJI, BIA NA POMBE KALI?

Vinywaji vya jumla na rejareja, pombe kali na laini

Kwenye kipengele chetu cha Ushauri ama Uliza ujibiwe leo tuna swali kutoka kwa msomaji wetu mmoja kutokea kule Babati Mkoani Arusha aliyetaka kufahamishwa ni kiasi gani cha mtaji kinachotosha kuanzisha duka la vinywaji mchanganyiko la jumla, soda, maji, bia, wine na pombekali. 

Nimeliweka swali lake kama alivyouliza hapo chini bila kuongeza wala kupunguza kitu chochote pamoja na majibu niliyompatia:

Kumbuka kuuliza maswali mafupumafupi ni bure kabisa, hatumtozi mtu malipo yeyote yale wala kuweka jina kamili la muulizaji swali pasipo ridhaa yake mwenyewe.

SWALI:



Habari kwema?

Nipo babati Nataka nifungue duka la jumla la vinywaji. ,,,,bia, soda, maji na pombe kali nianze na mtaji wa sh,ngapi?

Tafadhali naomba ushauri

MAJIBU:

Kwema kabisa ndugu yangu za huko Babati;

Biashara zote ikiwemo pia biashara ya kuuza vinywaji vya jumla baridi/laini na pombe kali kanuni ya kutambua kiasi cha mtaji unaohitajika kuanza ni moja tu na pia ni rahisi sana.

Kanuni hiyo huwa inatumika mara nyingi wakati mtu unapokuwa ukiandaa mchanganuo wa biashara/business plan sura ile ya maelezo ya biashara kipengele kidogo cha mahitaji ya kuanzia. Ukisoma katika kitabu changu cha, MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kimefafanua vizuri sana ukurasa ule wa 61 – 67 lakini hata hivyo hapa nitakuelekeza kwa kadri niwezavyo kwa maneno machache kusudi uweze kufahamu.

Kwanza fahamu ya kuwa biashara moja haina kiasi mahususi kimoja cha mtaji kila anayeanzisha biashara kama hiyo atalazimika kuanza nacho.Wewe duka lalo la vinywaji vya jumla unaweza kuamua uanze na mtaji wa shilingi milioni tatu (3) lakini mtu mwingine mahali pengine yeye akaamua biashara kama hiyohiyo ya vinywaji vya jumla akaianzisha kwa mtaji wa shilingi milioni 100.

Tofauti hii hutokana na tofauti pia ya kimazingira baina ya watu hao wawili nikimaanisha tofauti ya vitu kama soko, Uwezo wa rasilimali alizonazo mtu, washindani, eneo, nk. Sekta ya vinywaji kwa ujumla imejaa washiriki mbalimbali na kila mmoja hutofautiana na mwingine.

Ingawa wauzaji wa vinywaji vikali na laini vya jumla wengi ni watu walio na mitaji mikubwa hata hivyo mtu unaamua kiasi cha mtaji kulingana na mahitaji utakayoyaweka wewe kama mmiliki wa biashara husika.

Kwa mfano ikiwa unataka biashara yako iwe kubwa na uiweke eneo zuri let's say labda Kinondoni kama upo Dar es salaam utahitaji kuwa na mtaji mkubwa na ukitaka mfano kufungua biashara ndogo tu ya vinywaji vya jumla labda eneo la Chanika mtaji wako unaweza ukawa kidogo kutokana tofati za mizunguko ya watu katika maeneo hayo mawili tofauti, vipato nk.

Vilevile duka la vinywaji vya jumla Dar es salaam na duka kama hilo tuseme labda hapo Babati au Manyara utakuta kiasi cha mtaji hakiwezi kulingana. Siyo jiografia tu peke yake inayoweza kusababisha tofauti ya mitaji bali kuna vigezo vingine vingi kikiwemo uwezo wa yule mtu anayetaka kufungua biashara husika. Unaweza kuwa upo kijijini lakini kutokana na sababu kwamba upo vizuri kimtaji ukafungua bonge la duka la vinywaji vikali na vya kawaida kumzidi mtu mwingine aliyeko katikati ya mji lakini yeye uwezo wake kimtaji ni mdogo.

Sasa kanuni ni hii hapa;

Orodhesha katika daftari mahitaji yako yote kuanzia fedha kwa ajili ya kusajili biashara yako, vifaa mbalimbali mfano mizani, mashelfu, usafiri ikiwa utahitaji kuwa nao, gharama zozote zile utakazoingia iwe ni kumlipa fundi wa kukukarabatia chumba chako cha biashara (fremu), dalali wa kukutafutia fremu yennyewe na bidhaa zote unazotarajia kuuza kiasi na thamani yake.

Orodhesha bia ni kreti ngapi utataka kuanza nazo, maji katoni ngapi, soda za pepsi & cocacola creti ngapi, soda nyinginezo za chupa ya plastiki utanunua carton ngapi au chupa ngapi na pombe kali zikiwemo vodka, gin, brandy na whisky ni kiasi gani kila moja bila kusahau na mvinyo (wine) za aina mbalimbali.

Kiasi cha kila aina ya bidhaa, vinywaji na pombe kali weka makisio ya idadi ya chini kusudi mtaji usijekuwa mkubwa kupita kiasi vinginevyo labda iwe unao mtaji mkubwa usiokuwa wa mashaka.                  

 Katika listi yako hiyo orodheshea hapo pia fedha kwa ajili ya kuendesha biashara mfano mishahara, pango, umeme nk. kwa angalao miezi 3 au 6 ya mwanzo kabla hujaanza kupata faida. Usisahau na fedha za dharura.

Mwisho jumlisha kupata jumla ya vitu vyote tokea pale mwanzoni na huo ndio utakaokuwa mtaji wa kuanzishia biashara yako ya duka la vivywaji mchanganyiko, vikali na vya kawaida.

Jinsi ya kufahamu bei na idadi ya bidhaa mbalimbali itakubidi ufanye utafiti kupitia kwenda katika maduka kama unalotaka kufungua na kuulizia taarifa mbalimbali kama bei nk. Angalia usiende moja kwa moja kwenye maduka na biashara za washindani zilizokuwa karibu na mahali utakapoweka duka lako la vinywaji kwani wakijua wanaweza wasikupe taarifa zozote muhimu au kukupa taarifa za kukupotosha. Ikiwa utaenda basi chunga wasitambue kama unalenga kuwa mshindani wao. Maduka ya mbali hawana shida na wewe ukiwaeleza unatokea mbali.

.........................................................................


HUDUMA NA VITABU VYETU:

1. HUDUMA: Tunaandika mchanganuo wa biashara yeyote ile kwa gharama rafiki sana Cheki hapa baadhi wa wateja wetu tuliofanya nao kazi. Ukihitaji tuwasiliane kwa namba 0712202244 au 0765553030


2. VITABU & MICHANGANUO YA BISHARA: 








Kwa vitabu na Michanganuo zaidi tembelea, SMARTBOOKSTZ


3. DARASA (MASTERMIND GROUP MICHANGANUO-ONLINE):

Masomo ya fedha kila siku na semina za michanganuo bunifu ya biashara zinazolipa mara kwa mara. Kiingilio kwa mwaka ni sh. 10,000/= Unapata na offa ya vitu 12 vikiwemo vitabu na michanganuo ya biashara mbalimbali kama ifuatavyo; 


                 1.      COURSE/SEMINA: (compiled complete course) ya Jinsi ya kuandika Mchanganuo wa biashara –(Ukishindwa kuandika mchanganuo wako mwenyewe utarudishiwa pesa zako) - kwa kiswahili

                 2.       KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu za BIASHARA, jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika kila kitu.kwa kiswahili

                 3.      KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili

                 4.      KITABU: Siri za upishi wa chapati laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili

                 5.       KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 - kwa kiswahili

                 6.       KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ni maarufu sana duniani na ndio hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza

                 7.       MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini Broilers - kwa kiswahili

                 8.      MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza

                 9.      MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji- kwa kiswahili

              10.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili

              11.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza

              12.    MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili

              13.    Kuunganishwa Group la masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mwaka mzima ukitaka. (Mentorship group) (Ni hiyari yako lakini, usipotaka hatukuunganishi)

 

Lipia offa yako kupitia namba zetu, 0712202244  au 0765553030 jina, Peter Augustino Tarimo, kisha ujumbe watsap au sms usemao;

“NATAKA OFFA MPYA YA VITU 12

Ukihitaji kuunganishwa na group, kwenye ujumbe ongeza maneno; “NATAKA OFFA MPYA YA VITU 12 & GROUP

 

Na utapata OFFA zako ndani ya dk. 3 tu

Thamani halisi ya offa hii ni Tsh. 90,000/= lakini lipa Tsh. elfu 10 tu uokoe sh. 80,000/= !

Ukitaka kuthibitisha uaminifu wetu bonyeza hapo chini kuona baadhi ya wadau wengine waliowahi kuchangamkia offa na vitabu vyetu siku za nyuma bofya hapa>>>TESTIMONIALS



SOMA NA HIZI HAPA:

1. Biashara ya vinywaji jumla, mtaji milioni moja (1) naomba ushauri

2. Biashara ndogondogo zenye faida ya haraka tanzania ni hizi hapa, zipo nne(4)

3. Mtaji wa biashara ya duka la rejareja: nianze na shilingi ngapi ili nifanikiwe?

4. Biashara ya soda maji juisi na sigara: tumia siri hii kuongeza mauzo × 2

5. Biashara ya kutembeza bidhaa za jumla madukani, mbinu 7


0 Response to "MTAJI WA BIASHARA YA VINYWAJI VIKALI & LAINI JUMLA NI KIASI GANI MFANO SODA, MAJI, BIA NA POMBE KALI? "

Post a Comment