Biashara ya kukopesha pesa
ni moja kati ya biashara kongwe kabisa duniani, miaka kwa miaka binadamu
wamekuwa wakiazimana pesa kwa malengo mbalimbali tofauti. Hata kabla ya fedha
kuvumbuliwa watu walikuwa wakikopeshana vitu au bidhaa mbalimbali wengine
wakichaji riba (chajuu) na wengine
walikopeshana tu hivyohivyo pasipo kudai chochote toka kwa mkopaji, mkopaji
alitakiwa kurejesha kiasi kilekile alichokopa.
Ni miaka ya hivi karibuni tu
au tuseme karne chache zilizopita biashara hii ilikuja kuchukuliwa rasmi na
mabenki lakini hata pamoja na hivyo bado watu mmojammoja na vikundi kama vile
vya upatu, saccos na viccoba wanaendelea na biashara hii. Uzuri wa biashara hii
ni kwamba mtu unaweza ukaingiza kipato pasipo kufanya kazi kubwa sana endapo
utaisimamia vizuri. Biashara za kukopeshana pesa zipo za aina mbili;
· Mikopo
isiyokuwa na riba
· Mikopo
yenye riba
1.
Mikopo isiyokuwa na riba
Katika aina ya kwanza ya
mikopo ndiyo iliyokuwa kongwe zaidi na ipo ya aina nyingi mojawapo ni ile
ambayoi hufanyika zaidi baina ya watu mitaani katika vikundi visivyokuwa rasmi
maarufu kama MCHEZO, michezo ya upatu sifa yake kubwa ni kutokuwa na riba
isipokuwa mingine huwa na faini pale mkopaji anapochelewesha kulipa kwa wakati.
Lengo kubwa la mtu kucheza
mchezo ni ili kuweza kupata mtaji au fedha kwa ajili ya kutimiza lengo fulani
na kisha fedha hizo kuja kuzirejesha taratibu, lakini pia mchezo unamsaidia mtu
kujijengea nidhamu ya utunzaji wa pesa kwani anapokuwa akiwachangia wenzake ni
sawa na kuweka akiba kwa ajili ya matumizi yake ya baadae.
Kwahiyo kimsingi kabisa
upatu lengo lake ni zuri sana na wala halina shaka yeyote isipokuwa madhara
yake ambayo ndiyo tutakayokwenda kuyajadili na kuyafahamu kinagaubaga.
2.
Mikopo yenye riba
Hii ni biashara kama
zilivyokuwa biashara nyingine zozote zile, ila tu bidhaa inayouzwa ni pesa ili
ikatumike kutengeneza fedha zaidi. Biashara ya kukopesha fedha kwa riba
hufanywa na makundi yafuatayo;
1) Watu
binafsi maarufu kama, MIKOPO YA RIBA MITAANI
2) Vikundi
vilivyosajiliwa kama vile SACCOS, VICCOBA nk.
3) Mabenki
na taasisi nyinginezo kubwakubwa za kifedha zikiwemo na hata Mataifa kwa
Mataifa au nchi na nchi kukopeshana
Kabla hatujakwenda rasmi
kuona NI KWANINI MIKOPO YA RIBA MITAANI, MICHEZO YA UPATU NA BAADHI YA SACCOS
NI HATARI MTU KUJIUNGA, hebu kwanza tuone mikopo inavyofanya kazi;...............
........................................................
Ndugu msomaji wangu, somo hili kamili unaweza kulipata unapojiunga na
mastermind group letu la masomo ya kila siku ya fedha (MICHANGANUO-ONLINE). Tuna
mfululizo wa masomo yenye maudhui ya fedha zaidi ya mia moja (100+)
usiyoweza kuyapata mahali kwingine kokote nje na ndani ya mtandao.
Unapojiunga tu hivi, unapata pia OFFA ya vitu 12 ambavyo ni vitabu na
michanganuo ya biashara. Ndani ya group mbali na masomo hayo ya pesa lakini pia
tuna vitu spesho kama vile semina za kuandika michanganuo bunifu ya biashara
zinazolipa haraka Tanzania, mwanachama anayo fursa ya kuuliza swali lolote lile
kuhusiana na biashara & ujasiriamali akapatiwa majibu ya kina na wanachama
wengine akiwemo admin wenyewe wa group.
Group hili linaibua na kuchochea uwezo mkubwa wajasiriamali waliokuwa nao,
ujasiri wa kutenda na kutekeleza majukumu mbalimbali ya kiujasiriamali ili
kuleta matokeo chanya yaliyokusudiwa kwa wakati muafaka.
Kujiunga lipia kiingilio chako sh. 10,000/= kwa namba 0712202244 au 0765553030 Jina Peter
Augustino Tarimo, kisha tuma ujumbe usemao;
“NATAKA OFFA YA VITU 12 NA KUUNGWA MASTERMIND
GROUP”
SOMA
NA HIZI HAPA;
1.
Ukisoma
hapa hutahangaika kuwalamu mabenki na taasisi za fedha.
2.
Njia
za kupata mtaji wa biashara unayoipenda.
4. Ni biashara ndogo yenye mtaji mdogo faida ndogo lakini inayokua
upesi
0 Response to "KWANINI MIKOPO YA RIBA MITAANI, MICHEZO YA UPATU NA BAADHI YA VICOBA SI SALAMA KUJIUNGA?"
Post a Comment