JINSI YA KUBAJETI NA KUTUMIA VIZURI FEDHA ZA BIASHARA UFANIKIWE HARAKA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JINSI YA KUBAJETI NA KUTUMIA VIZURI FEDHA ZA BIASHARA UFANIKIWE HARAKA

jinsi ya kusimamia na kutunza hesabu za biashara

Karibu ndugu msomaji tuendelee na somo letu la elimu ya pesa. Jana sehemu ya kwanza tulijifunza Usimamizi mzuri wa fedha binafsi na leo ni fedha za biashara.  Asije kukudanganya mtu kuwa eti ipo siri ya utajiri wa haraka ama dawa ya mafanikio kwenye biashara iwe ni miti shamba au hata ramli zaidi ya uzingatiaji wa mbinu mbalimbali zinazosisitizwa na wataalamu wa biashara katika usimamiaji na matumizi bora ya fedha za biashara.

Sikushauri ufanye lakini: Ikiwa kwa sababu yeyote ile muhimu hauna muda wa kutosha kusoma kikamilifu makala zote hizi mbili hii ya leo na ile ya jana, nakushauri uzingatie tu sentensi hii moja ifuatayo;

[ Jitahidi kwa kila hali kupunguza matumizi na gharama za biashara lakini wakati huohuo ukiendelea kutoa huduma/bidhaa zenye ubora wa hali ya juu kwa wateja wako mwisho utafanikiwa ]

Unaposikia watu waliofuzu somo la jinsi ya kuondokana na umasikini haraka, basi ujue watu hao walizingatia vilivyo elimu ya usimamizi wa fedha na wakaweka katika vitendo elimu hiyo wakijua au hata wakiwa hawajui kama wanachokifanya ni usimamizi mzuri wa fedha zao. Kuna watu walifanikiwa basi tu kwa sababu ya ubahili wao huku wenzao wakiwacheka na kuwatania majina mbalimbali kama vile, “wewe bahili kama mchagga”, sijui “shilingi ikidondoka skafuni bahati mbaya ukiwa chumba cha operesheni hoi unazinduka” nk.

Unapokuwa na malengo mazuri ya kifedha katika biashara yako na kuyasimamia vizuri, biashara yako itaweza kuepukana na matatizo yatokanayo na mzunguko hasi wa fedha kwa kuhakikisha kwamba muda wote ina fedha za kutosha kujiendesha. Kama mmiliki wa biashara ikiwa utashindwa kusimamia vizuri pesa biashara yako inaweza ikakumbwa na matatizo yafuatayo;

              i)      Biashara kukosa pesa

              ii)     Kushindwa kuweka akiba

             iii)     Kuchelewesha malipo ya bili mbalimbali

            iv)    Kulipishwa faini za ucheleweshaji wa bili na madeni ya biashara

             v)     Kushindwa kukopa mahali popote pale

            vi)    Kuharibu mahusiano yako na wadau wengine wa biashara

           vii)   Kushindwa kutengeneza faida

           viii)  Na mwisho biashara kufilisika kabisa na kufa.

Kama ilivuo katika upande wa usimamizi wa fedha binafsi na kweny upande wa usimamizi wa fedha za biashara nako kuna hatua au MISAMIATI mikuu inayotumika nayo ni hii hapa chini;

              i)      Kuweka malengo ya biashara

              ii)     Kupanga bajeti inayotekelezeka

             iii)     Kurekodi na kufanya ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya biashara

            iv)    Kupunguza gharama na kuzidisha mapato

             v)     Kuweka akiba

            vi)    Uwekezaji – kufanya maamuzi mazuri katika uwekezaji wa fedha za biashara

Bajeti ni mipango, unapanga matumizi yako ya biashara au gharama ziwe vipi kulingana rasilimali zilizopo na faida inayoingia. Rais mmoja wa Marekani Benjamin Franklin aliwahi kusema hivi; “Kushindwa kupanga ni Kupanga kushindwa

 

Tofauti kati ya Usimamizi wa fedha binafsi na Ule wa fedha za Biashara

Kama tulivyoona jana kwenye utunzaji na usimamizi wa fedha binafsi za mtu mwenyewe, na kwa upande wa biashara pia kunahitajika usimamizi mzuri wa fedha ili biashara ikue na isife. Njia za kusimamia na kudhibiti matumizi ya fedha kwenye biashara zinafanana kwa kiasi kikubwa na zile za mtu binafsi isipokuwa tu kuna tofauti kadhaa hasa katika utekelezaji wake.

Kwa mfano wakati mtu binafsi yeye anaweza asimshirikishe mtu mwingine katika zoezi la usimamiaji wa fedha zake, kwa upande wa biashara mmiliki atahitajika kuwashirikisha wadau wengine mbalimbali wa biashara yake hasa wafanyakazi na wasaidizi wanaohusika kwenye utendaji wa kila siku wa shughuli za biashara. Tofauti pia ipo kwenye malengo yanayowekwa na kila upande. Malengo ya kifedha ya mtu binafsi hayawezi yakafanana na malengo ya kifedha ya biashara.

Kwenye upande wa biashara unaweza ukatumia mifumo ya usimamizi wa hesabu kwa kompyuta(accounting software) kusimamia fedha za biashara yako vizuri wakati kwa upande wa mtu binafsi mifumo hii siyo kawaida sana kutumika na mara nyingi inapotumiwa basi ni kwa kiwango kidogo na sanasana katika sura ya applications za kwenye simu za kisasa/apps za simujanja.

Tofauti nyingine pia ipo kwenye dhana hizi mbili, Kujilipa mwenyewe na kuwekeza faida katika biashara. Ingawa vitu hivi viwili kimsingi vinafanyika katika pande zote mbili lakini havina maana inayofanana kila upande. Kujilipa mwenyewe kwa upande wa mtu binafsi kunaweza kukafananishwa na kule kujiwekea akiba ya dharura asilimia 20% wakati kujilipa mwenyewe katika upande wa Biashara kunamaanisha mshahara unaojimegea kila mwezi au kila siku kutokana na faida inayoingizwa na biashara.

Kwa ujumla tofauti zipo nyingi ingawa ni ndogondogo lakini ni za msingi kabisa na hazipaswi kupuuzwa hata kidogo, ndio maana itakuwa vizuri sana ikiwa mtu atasoma masomo yote haya mawili la jana na hiili la leo kwa ukamilifu wake bila ya kuachia njiani.

 

Uhusiano mkubwa uliopo kati ya Usimamizi mzuri wa fedha Binafsi na ule wa fedha za Biashara

Ingawa tunasema Fedha za biashara na fedha binafsi zinapaswa kutenganishwa kama maji na mafuta lakini vitu hivi viwili ni kama ndugu mapacha vile, mmoja akiumwa na mwingine atanyongonyea tu hata kama hana homa.

Mara nyingi chanzo cha fedha za biashara huwa ni akiba inayowekwa kutokana na fedha binafsi za mmiliki wa hiyo biashara wakati pia fedha za mmiliki mfukoni mwake kuna wakati zinatokana na gawio la faida inayotokana na biashara.

Nasisitiza faida au kwa maneno mengine ile fedha mmiliki anayojilipa mwenyewe kutokana na faida ya biashara na wala siyo kutokana na mtaji wa biashara. Kama hamna faida ni bora kabisa ukaahirisha kujilipa mwenyewe. Hivyo AFYA NZURI ya fedha za kila upande ni jambo lenye manufaa makubwa kwa mmiliki wa biashara, biashara yenyewe na wadau wengine mbalimbali wa biashara.

Naona nisikuchoshe mno na maelezo hebu sasa moja kwa moja nikakudondolee hatua kwa hatua mbinu maridhawa za matumizi na usimamizi bora kabisa wa fedha za biashara. Zipo mbinu kubwa……………………..


 ...........................................................

Ndugu msomaji wangu, somo hili litakamilika leo katika MASTERMIND-GROUP letu la MICHANGANUO-ONLINE. Siyo masomo yote ndaniya hii blogu tunayoweka nusu, ni baadhi tu ya masomo kwa lengo la kuhamasisha wale walio na kiu ya kujifunza zaidi na kwa kina mada hizi kujiunga kwani siyo kila mtu anapenda kusoma aina ya mada zetu kwa kirefu, wengine wana interest na mada zingine tofauti.

Ndani ya group na channel yetu utapata somo hili likiwa kamili  part I & part 2, pia unaweza ukalihifadhi katika kifaa chako, simu, flash au kompyuta kwa ajili ya matumizi ya baadae.

·       Ili kujiunga na GROUP hili mshiriki analipa kiingilio cha mwaka mzima na kisha kuunganishwa na group la watsap lenye pia channel ya Telegram ya masomo mengine yote yaliyopita zaidi ya 70.

·       Ukijiunga mapema unapata zawadi ya kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI BURE  


Kujiunga na Group lipia kiingilio shilingi elfu 10 kisha tuma ujumbe watsap au SMS usemao,

“NIUNGE MASTERMIND GROUP-2022”  

Namba zetu ni; 0765553030 au  0712202244

JINA: Peter Augustino Tarimo


Ikiwa hukusoma sehemu ya kwanza ya Somo hili bonyeza hapo chini kusoma.

BAJETI: JINSI YA KUSIMAMIA, KUTUNZA NA KUTUMIA VIZURI FEDHA BINAFSI NA ZA BIASHARA YAKO (KANUNI 80/20)  


Vitabu vyetu hapo chini ukiwa popote pale nchini Tanzania na nje ya nchi tunakufikishia kwa uaminifu mkubwa, kuvipata wasiliana nasi kwa namba 0765553030 au 0712202244








SOMA PIA NA HIZI;



3. Mzunguko mzuri wa fedha ndiyo njia bora zaidi ya kufikia malengo yako ya mwaka mpya

1 Response to "JINSI YA KUBAJETI NA KUTUMIA VIZURI FEDHA ZA BIASHARA UFANIKIWE HARAKA"